Katibu wa NEC, Irikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Mzee
Mangula baada ya kuhutubia katika kongamano hilo. Kulia ni Katibu
Mtendaji Mkuu wa CCM mkoa wa Vyuo Vikuu, Christopher Ngubiagai
Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika Kongangamano hilo la Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere. Nape amewataka wasomi kutofumbia macho matatizo ndani
ya CCM, badala yake wakati wakisifu mema wawe mstari wa mbele
kuyafichua na kuyakemea mapungufu ili chama kiende na wakati
Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM mkoa
wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Christopher Ngubiagai akizungumza wakati wa
kongamano hilo la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,, Theodora Malata akizungumza mwanzoni mwa kongamano hilo
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akizingumza kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Philip Mangula na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa na
viongozi wengine meza kuu baada ya kuwasili ukumbini.(Picha na Bashir
Nkoromo)