WAZIRI WA FEDHA AKAGUA NA KUTOA MAAGIZO KUHUSU MADINI YA ALMASI YALIYOKAMATWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

September 09, 2017

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.
Dare es Salaam, 09 Septemba, 2017: Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ameviagiza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Williamson Diamond Ltd na wote waliohusika kuidhinisha usafirishaji wa madini ya almasi kutoka migodi ya kampuni hiyo na kudanganya thamani halisi ya madini hayo kwa lengo la kuisababishia hasara Serikali.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 09 Septemba, 2017 baada ya kukagua madini ya almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam yakisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji.

Miongoni mwa hatua za kisheria ni pamoja na kutaifisha madini yote ya almasi yaliyokamatwa baada ya kubainika udanganyifu wa thamani yake halisi, kuwakamata na kuwachunguza wote waliohusika katika udanganyifu huo wakiwemo wajumbe wa bodi zilizomaliza muda wake na wafanyakazi waliopo na waliostaafu.

Almasi hiyo ilikamatwa tarehe 31 Agosti, 2017 muda mfupi kabla ya kupakizwa kwenye ndege ili isafirishwe kwenda nchini Ubelgiji, na ilipochunguzwa ilibainika kuwa nyaraka za kampuni ya Williamson Diamond Ltd zimeonesha kuwa almasi hiyo ina thamani ya Dola za Marekani Milioni 14.798 sawa na Shilingi Bilioni 33 za Tanzania wakati thamani yake halisi ni Dola za Marekani Milioni 29.5 sawa na Shilingi Bilioni 65 za Tanzania.

Kabla ya kukagua almasi hiyo Waziri Mpango amepokea taarifa ya timu ya wataalamu iliyofanya tathmini ya thamani halisi ya madini hayo ambapo kiongozi wa timu hiyo Prof. Abdulkarim Mruma amesema pamoja na kubaini upotevu mkubwa wa fedha, kuna dosari nyingine zikiwemo kukosekana kwa vifaa ya kupimia madini hayo, almasi kusafirishwa na kuuzwa sokoni bila uwepo wa mwakilishi wa Serikali na ameshauri hatua za udhibiti huo zifanyike katika madini yote yanayochimbwa hapa nchini.

Pamoja na kuipongeza timu iliyofanya tathmini hiyo na vyombo vya dola vilivyokamata madini hayo Waziri Mpango amesema Serikali itatekeleza ushauri wote uliotolewa na timu ya Prof. Mruma na kwamba kuanzia sasa almasi inayozalishwa hapa nchini itasindikizwa na maafisa wa Serikali hadi sokoni na inataka kuanza kupokea gawio halali kutoka mgodi huo.

Waziri Mpango ametoa maagizo hayo mbele ya viongozi wa vyombo mbalimbli wakiwemo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP - Lazaro Mambosasa.



Benny Mwaipaja
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
TPSF yamwaga Balozi wa China anayemaliza muda wake nchini

TPSF yamwaga Balozi wa China anayemaliza muda wake nchini

September 09, 2017
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing katika hafla fupi ambayo imefanyika katika hoteli ya Serena iliyopo Dar es Salaam. 

Akizungumza katika hafla ya kumuaga, Mwenyekiti wa TPSF, Dk. Reginald Mengi alimshukuru Dk. Youqing kwa mambo yote ambayo ameyafanya akiwa balozi wa China nchini na kumuomba kuendelea kushirikiana na Tanzania hata atakaporejea China. 

“Muda mwingine nashindwa kujua kama unaiwakilisha China au Tanzania umekuwa na matendo mema kwa Tanzania kwa kipindi chote ambacho umefanya kazi nchini umekuwa daraja kubwa la kuunganisha China na Tanzania,  

“Wote tunajua umuhimu wa biashara ya Tanzanania na China ilivyo kubwa na mambo mambo mengi uliyoyafanya yalifanikiwa, jambo ambalo tunaweza kusema ni tutakukumbuka sana,” alisema Dk. Mengi. 

Kwa upande wa Dkt. Lu Youqing aliishukuru (TPSF kwa ushirikiano waliomba kwa kipindi chote ambacho alikuwa akifanyakazi nchini na kuahidi kuwa hata atakaporudi China ataendelea kushirikiana nao. “Tumeishi vizuri kwa kipindi nilichokuwa hapa niwaahidi kuwa nitarudi tena Tanzania nikiwa kama mfanyabiashara na siku moja ninapenda kuwa mwanachama wa TPSF, kuweni huru kuja hata China kujifunza namna China tunafanya biashara,”alisema Dkt. Youqing. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akisalimia na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Kivukoni uliopo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza katika hafla ya kumuaga Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing. Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla ya kumuaga baada ya muda wake wa kufanya kazi nchini kuisha. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa na viongozi wengine wa TPSF walioshiriki hafla ya kumuaga Balozi Youqing. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa TPSF.

Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi Yafikia tamati leo nchini nzima

September 09, 2017
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi  , Brigitta  Mbuya, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu  nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.


Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi  , Ibrahim Hassan mkazi wa Goga, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu  nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi  , Cecilia Paul mkazi wa Kimara, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu  nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam jana.

Shule ya Sekondary Mugabe yapokea msaada wa Vitabu Kutoka kwa Mkurugenzi Ubungo

September 09, 2017
 Mkuu wa shule ya Sekondary Mugabe Madam Kayumbu  akikabidhiwa vitabu hivyo na afisa elimu Neema Maghembe mara baada ya kukabidhiwa na mkurugenzi wa manispaa ya ubungo ndugu  John Lipesi Kayombo 

Msaada huo wa vitabu umetolewa Taasisi ambayo ni asasi ya Wazalendo na maendeleo na watoto ni Amana
iliyowakilishwa na Mohamed Shaban aliyeambatana na  Ally Six NurdinKatika makabidhiano hayo mbali na mkurugenzi wa Ubungo kukabidhi vitabu hivyo pia aliahidi kutoa matofali 1000 Pamoja na mifuko 50 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule jambo lililoungwa mkono na Taasisi kwa kutoa matofali 200.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Kayombo akiwa katika Picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondary  Mugabe,walimu na wageni waliohuduria katika hafla hiyo ya kukabidhi vitabu hivyo
Aidha Mkurugenzi kayombo ametoa agizo shule ya Sekondari Mugabe itumike kama Library ya wilaya ili kila shule walimu na wanafunzi waweze kwenda pale kujisomea