WAZIRI BERNARD MEMBE AHANI MSIBA WA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN MJINI UNGUJA

June 14, 2015
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimpa mkono wa pole Bi. Mwaka Mohamed ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akitoa mkono kwa familia ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akitoa ubani kwa Bi. Mwaka Mohamed ambaye ni mjane wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM), marehemu Salmin Awadh Salmin aliyefariki mapema Februari mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwake, Mkoa wa Mjini Unguja, Zanzibar.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MAELFU YA WANANCHI WA HALMASHAURI TATU ZA MKOA WA MORO WANUFAIKA NAMPANGO WA MKURABITA

June 14, 2015

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.Rajabu Rutengwe kushoto akifurahia jambo na Mratibu wa Mkurabita Saraphia Mgembe.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.Rajabu Rutengwe mwenye suti nyeusi akiongoza kucheza ngoma ya Sangula ya wapogolo baada ya kuzindua utoaji wa hati miliki za kimila chini ya Mkurabita wilayani Kilombero.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wa wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wakimsiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro .
 Furaha ya hati ya miliki za kimila na Mkurabita.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali wa wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja.
Na John Nditi, Morogoro
WAKUU wa wilaya  , Wakurugenzi  na Wenyeviti wa halmashauri ambazo  zimenufaikana Mpango  wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA), wametakiwa kuitumia  fursa hiyo adhimu kuwapatia wananchi wao maendeleo kwa kutumia rasilimali ardhi katika kukuza uchumi wa taifa letu. 
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkuratiba nchini, Saraphia Mgembe, Juni 10, mwaka huu mjini Ifakara wakati  wa uzinduzi wa kimkoa wa utoaji wa hati miliki za kimila kwa baadhi ya wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero,  ambao mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa huo, Dk Rajab Rutengwe.
Pamoja na hayo  alisema ,katika kupambana na upungufu wa fedha, Mkurabita imejiandaa kufanya majaribio ya kuunda Mfuko wa Urasimishaji utakaoendeshwa kwa mfumo wa dhamana.
Kwa mujibu wa Mratibu hiyo kuwa, utekelezaji wa urasimishaji ardhi mijini uliofanyika katika  Manispaa ya Morogoro umetoa  hamasa ya kuujaribu mfuko wa urasimishaji kutokana na uzoefu uliopatikana katika  Manispaa hiyo.
Hata hivyo alisema katika mpango huo kwa mkoa wa Morogoro ni  halmashauri  wilaya tatu  ya Kilosa, Mvomero na Kilombero  zimenufaika kwa urasimishaji wa ardhi vijijini na  jumla mashamba  9,180 yamepimwa na yameandaliwa hati za hatimiliki za kimila  7,837.
Pia alisema , Mkurabita umeendesha zoezi la urasimishaji ardhi mijini katika Manispaa ya Morogoro kwenye  Kata ya Mbuyuni, Mlimani, Lukobe na Kihonda  ambapo idadi ya wamiliki 222 walichangia uzalishaji wa viwanja 1,122 na hati 72 zimeandaliwa ambapo Manispaa itaendelea kurasimisha mitaa mingine na kuzalisha viwanja vingine 5,660.
Hivyo alitoa rai  kwa wananchi walionufaika na mpango huo wazitumie  hati hizo katika kujikwamua na umaskini kwa kupata mikopo na mitaji kutoka taasisi zetu za fedha na mabenki.
Mbali na hayo, aliwataka Wakurugenzi wa halmashauri ambazo kazi ya urasimishaji imefanyika sasa waiendeleze kazi hoyo kwa kuhakikisha watendaji wao wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa .
“ Tunapofika hatua hii watu wengi hawatofaitishi maofisa wa Mkurabita na wale wa halmashauri wanapokosa uadilifu ‘vitendo vya rushwa’ wananchi husema ni Mkurabita , wananchi mnapoona utata wowote toeni taarifa ili maamuzi stahiki kwa watumishi wasiowaadilifu “ alisema Mratibu huyo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rutengwe, katika hotuba yake ya uzinduzi alisema hati hizo hazina ukomo wake,  ni dhamana ambayo taasisi za fedha zinazitambua na hivyo wananchi walirasimishwa wanapata  fursa ya mikopo na mitaji ya kujiendeleza.
Hata hivyo alisema, hati za kimika zina manufaa makubwa kwa wananchi kwa kusaidia  kuinua uchumi wao , kuimarisha usalama wa miliki ya ardhi na dhamana ya kupata mitaji ya mikipo itakayoongeza uboreshaji wa shughuli za uzalishaji ili kujiongezea kipato.
“  Nawasihi wananchi wote mliopokea hati hizi mzitumie kwa manufaa yenu na kuboresha maisha na si nyaraka za kuficha na kuhifadhi tu” alisema Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo pamoja na kuupongeza Mkurabita , mkuu huyo wa mkoa aliomba mpango huo uendeleze kujenga uwezo katika halmashauri zilizobakia ya Gairo, Ulanga na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma-JUNI 16-23,2015

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma-JUNI 16-23,2015

June 14, 2015

TANGAZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
index
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
inawakaribisha wananchi na wadau wote katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Tarehe 16-23 Juni, 2015
Mahali: Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
Kaulimbiu: “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni Chachu ya Kuwawezesha Wanawake, Kuongeza Ubunifu na Kuboresha Utoaji Huduma kwa Umma”. Ushauri na Huduma mbalimbali zitatolewa na wataalamu kutoka katika Taasisi za umma bila malipo. Ufunguzi utafanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb), na siku ya kilele Tuzo zitatolewa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi.
Tarehe 17 Juni, 2015 Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na ufunguzi utaongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue, na Msemaji Mkuu atakua Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Hakuna kiingilio katika maadhimisho haya, wananchi wote mnakaribishwa.
………………………..
Limetolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini K.n.y; KAIMU KATIBU MKUU (UTUMISHI)

NSSF YAWANUFAISHA YATIMA NA WAHUDUMU WA WAGONJWA MAHOSPITALINI

June 14, 2015


Mhasibu Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdulkarim Kisuguru akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vyakula pamoja na vifaa vya shule katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu cha, Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam akizungumza wakati hafla ya kupokea misaada kutoka NSSF.
Baadhi ya watoto wanaolelea katika kituo cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es salaam wakiwa katika haflaya kupokea msaada wa vyakula na vifaa vya shule vilivyotolewa na NSSF. 
Maofisa wa NSSF wakiwa katikahafla hiyo.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (wa pili kulia) akiwa na baadhiya maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke walipofikakutoa msaada katika kituo cha Darul-Arqam.
 Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke.
  Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika hafla hiyo.
Kijana aliyewahi kuishi na kusoma katika katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira cha Darul-Arqam, Idd Abasi  akitoa ushuhuda wake kwa viongozi wa NSSF mkoa wa Temeke. Kijana Idd kwa sasa anasoma Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam akichukua masomo ya BSC, LMV.
Baadhi ya vyakula vilivyotolewa na NSSF kwa kituo hicho.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha, Darul-Arqam, Ustaadh Hemed Jaffar. Hafla hiyo ilifanyika Tandika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario na kushoto ni Ofisa wa Huduma kwa Wateja, Carolyne Newa.

Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa madaftari kwa mtoto, Ally Abdallah.
Ofisa Mkaguzi wa NSSF mkoa wa Temeke, Ummy Kimario (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa madaftari kwa mtoto, Ally Abdallah.
Viongozi wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Darul-Arqam cha Tandika jijini Dar es Salaam.  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam (J.A.I), ya jijini Dar es Salaam akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kusaidia taasisi hiyo ambayo inatoa huduma za kijamii pamoja na kuwahudumia wagonjwa bila kujali imani wala jinsia. 
 Baadhi ya maofisa wa NSSF mkoawa Temeke.
Maofisa wa NSSF mkoa wa Temeke wakiwa katika ofisi za JAI muda mfupikabla ya kutoa msaada wa vifaa tiba.

Mhasibu Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdulkarim
Kisuguru akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa tiba katika Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam ya jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mafao ya Matibabu NSSF, Dokta Zakia Mohamed akifafanua jambo kuhusu vifaa tiba walivyokabidhi katika taasisi hiyo.
Sehemu ya msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na NSSFkwa taasisi ya JAI.Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mwenyekiti Kamati ya Utendaji ya Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam, Ahmed Hassan Bakar (wa pili kushoto) na Naibu Mwenyekiti, Aman Soud Aman.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Jumiiyatul Akhlaaqul Islaam ya jijini Dar es Salaam akiagana kwa furaha na Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kulia) baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.
RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA 25 WA UMOJA WA AFRIKA

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA 25 WA UMOJA WA AFRIKA

June 14, 2015

01
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika.
02
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba   mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika.
03
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa wa Ubalozi  wa Tanzania  nchini Afrika Kusini mara walipowasili katika hoteli ya Sun Internatioal Maslow Hotel, Sandton, Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 25 wa kawaidavwa Umojanwa Afrika.
PICHA ZOTE NA IKULU
04

LOWASSA APATA WADHAMINI MIKOA YA KATAVI – RUKWA

June 14, 2015

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah (shati la kitenge) akizungumza machache wakati wa kumkaribisha, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa, wakati alipofika kwenye ofisi za Chama hicho, Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Baadhi ya wananchi wa Mji wa Mpanda wakionekana ni wenye furaha nyingi pindi walipomuona Mh. Edward Lowassa akipita kwenye maeneo yao wakati akielekea Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015.
 Mapokezi ya Mh. Lowassa mjini Mpanda, Katavi leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia wananchi wa mji wa Mpanda, Mkoani Katavi waliojitokeza kumlaki, wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi, alikofika leo Juni 14, 2015 kwa ajili ya kutafuta udhamini wa wanaCCM ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. alie mbele yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa kuingia kwenye Ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Katavi leo Juni 14, 2015, waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Bi. Elizabert Kashira. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akizungumza machache mara baada ya Mh. Lowassa (pili kulia) kukabidhiwa fomu za wadhamini wa CCM za kumuwezesha kutata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaburou pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Beda Katani.
 
Wana Mpanda haoo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa ili aweze kuwashukuru wanaCCM wa Mpanda kwa kumdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Mpanda, waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi leo Juni 14, 2015.Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi. 
Umati wa watu nje ya Ofisi za CCM Mpanda.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Rukwa, leo Juni 14, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wanaCCM na wananchi wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa leo Juni 14, 2015.
 
Mjumbe wa NEC ya CCM kutoka Mlele, Bw. Kampala akiwasalimia wanaCCM wa mji wa Sumbawanga.
“Salaam wanaCCM wenzangu.
 
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wanaCCM wa Mji wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa wakati alipofika kutafuta udhamini wa kupewa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya wanCCM 4045 wamemdhamini.