AGNESS MASOGANGE AHOJIWA UWANJA WA NDEGE DAR KWA ZAIDI YA MASAA 10

AGNESS MASOGANGE AHOJIWA UWANJA WA NDEGE DAR KWA ZAIDI YA MASAA 10

August 06, 2014



Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini.

RAIS KIKWETE AJIUNGA NA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA AFRIKA NA MAREKANI JIJINI WASHINGTON DC LEO

August 06, 2014

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Ikulu ya Marekani (White House) jijini Washington DC kwa dhifa ya Kitaifa waliyoandaliwa viongozi wa Afrika na mwenyeji wao Rais Barak Obama Julai 5, 2014.
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Afrika katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani  ambao umefunguliwa na Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC  leo Julai 6, 2014.
 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry anaelekeza namna ya kutumia kipaza sauti baada ya Rais Obama kufungua mkutano huo, wakati  mwenyekiti wa Umoja wa Afrika  Rais  Mohamed Ould Abdel Aziz alipoongea kwa niaba ya Viongozi wa Afrika.PICHA NA IKULU.

TUKIO KATIKA PICHA: KUMEKUCHA NANE NANE MBEYA KUMEKUCHA YAWAVUTA WENGI !

August 06, 2014


Hapatoshi Nane nane .... Full mamia ya watu .. 
 Kila mtu na lake...
 Madogo nao hawapo nyuma.... kila mtu lake...

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI KWA NCHI ZA AFRIKA NA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA, JIJINI ARUSHA.

August 06, 2014


 Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. 
  Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. 
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. 
 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. 
********************************************
Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha jana Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara. 
Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.
Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.
Elimu duni chanzo cha wanawake wengi kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi

Elimu duni chanzo cha wanawake wengi kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi

August 06, 2014

IMG_0130 
Na Anna Nkinda – Washington
Imeelezwa kwamba kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi, upungufu wa upatikanaji wa huduma za afya, na vitendea kazi, utungaji wa sera zisizo rafiki, pamoja na ukosefu wa takwimu za magonjwa ni moja ya sababu zinazosababisha wanawake wengi kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wake wa marais wa Afrika waliohudhuria hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na kituo cha Marais wa Afrika (African Presidential Centre) cha chuo kikuu cha Boston iliyofanyika mjini Washington.
Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwa kiasi kikubwa kuna mahusiano kati ya ugonjwa wa Ukimwi na Saratani ya mlango wa kizazi ambao kama mgonjwa atapata matibabu mapema atapona lakini kutokana na uelewa mdogo baadhi ya wanawake wanapoteza maisha.
“Kutokana na utaalamu uliopo sasa ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi unazuilika na kutibika lakini bado kuna uelewa mdogo katika jamii kuhusu uhusiano uliopo kati ya ugonjwa huu na ule wa Ukimwi; kama zitapatikana fedha za kutosha asasi zisizo za kiserikali ambao ni wawezeshashi wataweza kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na magonjwa haya”, alisema Mama Kikwete.
Akiongelea kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi Mama Kikwete alisema ugonjwa huo unasababisha vifo vya watu wengi lakini bado kuna magonjwa mengine ambayo ni tishio nchini kama Malaria na Kifua kikuu ambayo nayo yanaua watu wengi.
Alisema, “Ugonjwa wa Ukimwi unasababisha vifo vya wanawake wengi nchini kwa upande wa vijana watoto wa kike wanaathirika zaidi ukilinganisha na watoto wa kiume na kwa watu wazima wanawake wengi wanapata maambukizi zaidi ukilinganisha na wanaume.
“Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi yamepungua kutoka asilimia 7 kwa mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2012 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar maambukizi ni asilimia 0.6% kwa miaka yote hiyo”
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema vituo vya kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vimeongezeka kwa sababu vituo vilivyokuwa vinatoa huduma ya uzazi na watoto wachanga hivi sasa vinatoa huduma ya upimaji wa maambukizi ya VVU lakini bado jitihada kubwa zaidi zinahitajika kufanyika ili kuwe na vituo vingi vya kutoa huduma hiyo.
Kwa upande wa vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 147 kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwaka 1999 hadi kufikia vifo 81 kwa mwaka 2010. Vifo vya watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka 99 na kufikia 51 kwa kila vizazi hai 1000 ingawa tatizo limepungua hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuimarisha afya ya watoto.
Kuhusu vifo vya kina mama wajawazito alisema vimepungua kutoka 578 kati ya vizazi hai 100,000 mwaka 1996 hadi kufikia 454 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2010 hii inatokana na jamii kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa mwanamke kuhudhuria kliniki mapema pindi apatapo ujauzito na kujifungulia katika vituo vya afya .
Mama Kikwete alisema, “Vifo vingi vya kina mama wajawazito vinatokana na kutofuata uzazi wa mpango na uchumi mdogo wa wanawake, utoaji wa mimba usio salama, kuvunja damu nyingi wakati wa kujifungua, kifafa cha mimba, kushindwa kujifungua, uhaba wa huduma za haraka za uzazi na huduma za mtoto mchanga na uhaba wa watoa huduma za afya waliobobea,”.
Aliendelea kusema vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua vinahusiana na afya ya mama wakati wa ujauzito, hali ya kujifungua na jinsi ya kumjali mtoto wakati wa kujifungua. Mwanamke atakayejifungua mtoto akiwa na umri mdogo atakuwa na watoto wengi ambao umri wao haujapishana hayo yote yana madhara kwa afya ya mama na mtoto .
“Ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga, ugonjwa wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi na Ukimwi hasa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Taasisi ya WAMA inafanya kazi ya uraghibishi kwa kutoa vifaa tiba na elimu ya uzazi kwa vijana. Tunawakaribisha ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wa Tanzania”, alisisitiza Mama Kikwete.
Akiwakaribisha wake hao wa Marais Mkurugenzi wa Kituo cha Marais wa Afrika Balozi Charles Stith aliwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika nchi zao ya kujali afya ya mama na mtoto na kuwataka waendee na kazi hiyo bila ya kukata tamaa kwani wao kama viongozi wanahitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii inayowazunguka.
Balozi Stith alisema kituo chake kinatambua mchango wao na kazi wanayoifanya hasa katika kushughulikia afya ya mama na mtoto na upatikanaji wa elimu ya mtoto wa kike na kuhahidi kuwa kituo hicho kitaendelea kushirikiana nao ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Mama Kikwete anauhudhuria mkutano wa wake wa Marais wa Afrika ulioandaliwa na Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama kwa kushirikiana na Taasisi ya George W. Bush ambao unajadili matatizo ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto, ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti na elimu ya mtoto wa kike.
BENKI YA POSTA YADHAMINI KLABU YA WAANDISHI, TASWA SC

BENKI YA POSTA YADHAMINI KLABU YA WAANDISHI, TASWA SC

August 06, 2014

1
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akikabidhi  mfano w hundi kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary (wa kwanza kulia)ikiwa sehemu ya benki hiyo kusaidia michezo nchini.  Katikati ni Afisa Mawasiliano wa wa benki hiyo, Chichi Hilda Banda.
2
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ya benki hiyo kuisaidia timu ya waandishi wa habari za michezo nchini Taswa SC. Benki hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2 na pia itasaidia jezi kwa timu ya mpira wa miguu na netiboli. Kwa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa TPB, Chichi Banda na wa kwanza  kulia ni  Taswa SC, Majuto Omary.
3 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ya benki hiyo kuisaidia timu ya waandishi wa habari za michezo nchini Taswa SC. Benki hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2 na pia itasaidia jezi kwa timu ya mpira wa miguu na netiboli
……………………………………………………………………………….
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeidhamini klabu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC), kufuatia juhudi zake za kuhamasisha na kuendeleza michezo nchini.
Benki hiyo imeisaidia klabu hiyo fedha taslims sh. Milioni 2 na inatarajia kuwapa jezi seti moja moja kwa timu ya mpira wa miguu na mpira wa pete (netiboli) ikiwa ni kuthamini mchango wao Taswa SC katika sekta ya michezo nchini.
Kaimu Afisa Mteandaji Mkuu wa TPB, Moses Manyatta alisema kuwa wanafuraha kubwa kusikia kuwa waandishi wa habari za michezo wameamua kufanyakazi kwa vitendo kwa kuanzisha timu ya mpira wa miguu ambayo kwa sasa ina miaka zaidi ya 20 na timu ya mpira wa pete (netiboli) ambayo ina mwaka mmoja na nusu.
“Tumefarijika kutokana na ukweli kuwa mbali ya kuandika, mmeamua kufanya michezo kwa vitendo na kuwa mfano wa kuigwa, TPB ipo bega kwa bega nanyi na tutaendelea kushirikiana katika sekta mbali mbali tofauti na michezo,” alisema Manyatta.
Alisema kuwa TPB ni benki halisi ya Kitanzania yenye kutoa huduma bora kwa wateja wake na kwa sasa imeingia katika sekta ya michezo ambapo kwa sasa inashirikiana na timu kongwe nchini, Yanga na Simba katika zoezi la kuandikisha upya wanachama na mashabiki wa timu hizo.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza TPB kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa wadau wakubwa wa benki hiyo katika shughuli zake mbalimabli.
Majuto alisema kuwa wameomba udhamini kwa makampuni mengi kutokana na ukweli kuwa timu yao inachangamoto nyingi pamoja na kuwa na mafanikio makubwa.
“Tunawapa pongezi kubwa sana TPB, mmeonyesha kuwa ni benki halisi ya Kitanzania yenye kutoa huduma bora hapa nchini, Taswa SC ipo bega kwa bega nanyi katika kuendeleza gurudumu la maendeleo la nchi hii,” alisema Majuto.
Majuto pia aliwaomba wanachama wa timu ya Taswa SC kuwa mstari wambele katika shughuli za TPB kwani wameonyesha kuwajali katika shughuli za kila siku.
Wanamichezo wa Tanzania warejea huku wakiijengea nchi heshima ya kuwa na nidhamu

Wanamichezo wa Tanzania warejea huku wakiijengea nchi heshima ya kuwa na nidhamu

August 06, 2014

JM1A
Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akisalimiana na baadhi ya Wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
JM1B
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda akiwaelekeza jambo baadhi ya Wanamichezo waliwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
JM1C
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia jambo na baadhi ya wanamichezo walikuwa wamewakilisha nchini katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
JM2A
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko Akizungumza kwa niaba ya Serikali na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jan.Kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi.
JM2B
Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akizungumza na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika jana katika Ukumbi uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda na Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Rish Urio
JM3
Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Kapteni wa Timu ya Taifa iliyoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw. Seleman Kidunda, mara baada ya kurejea nchini jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda, Meneja wa Timu hiyo Muharami Mchume na Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi
JM4
Baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland, wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini jana jijini Dar es Salaam.
JM5
Baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland, wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali (hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya mapokezi na kuwakaribisha iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA
Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniI
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

MSICHANA ALIYEPIGWA NA MTOTO WA RAIS OBAMA ATOA KAULI YA KUSHANGAZA

August 06, 2014




Mtoto wa rais wa kike wa Marekani, Malia Obama mwenye umri wa miaka 16 alimpiga/alimgonga kwa bahati mbaya msichana aliyefahamika kwa jina la Bridget Truskey walipokuwa katika tamasha kubwa la muziki la Lollapalooza nchini Marekani. 
 
Msichana huyo amewashangaza watu baada ya kuonesha kufurahishwa sana na tukio hilo  kutokana na umaarufu wa Malia Obama.