MWENYEKITI UVCCM MBEYA AGUSWA NA MAISHA YA KIJANA EMANUEL FEDRICK ALIYEFUNGIWA NDANI MIAKA11

July 15, 2016
Mwenyekiti wa UVCCM  Mkoa Mbeya Amani Kajuna akiwa amebeba kiti maalumu(Wheelchair)  chenye  thamani ya laki tatu na nusu (350,000) kwa ajili kumpatia msaada kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ,ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka 11 mara baada ya kuzaliwa akiwa na tatizo la ulemavu wa akili na viungo.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya (katikati )akiwa na baadhi ya wadau wakielekea mahala anapoishi kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kutokana na ulemavu wake kwa zaidi ya miaka 11 ,ambapo mwenyekiti huyo alitoa msaada wa kiti maalumu (wheelchair)  pamoja  na godoro na mahitaji mengine.

Nyumbani anakoishi kijana Emanuel Fedrick na wazazi wake mtaa wa Mwambenja Iganjo jijini Mbeya.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akimtazama Kijana Emanuel Fedrick (20) mwenye tatizo la ulemavu wa akili na viungo ambaye aligundulika akiwa amefichwa ndani na wazazi wake kutokana na tatizo lake ambapo aliishi ndani kwa zaidi ya miaka 11 bila kupata mahitaji muhimu ambapo aliwataka walezi wa kijana huyo kuhakikisha wanamtunza vymea kijana huyo nakuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki moja(100,000)kila mwezi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya Amani Kajuna akitoa maelekezo kwa wazazi wa kijana Emanuel Fedrick mara baada ya kukabidhi rasmi kiti maalum (Wheelchair)kwa kijana huyo .


Mama Mzazi wa kijana Emanuel Fedrick amwenyetatizo la ulemavu wa akili na viungo akipokea godoro ambalo limekabidhiwa na David Nyembe kwaniaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mbeya.
 
Muonekano halisi wa Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Iganzo Mbeya ambaye anatatizo la akili akiwa amelala .Picha E.Madafa,D.Nyembe



NAIBU WAZIRI TAMISEMI AUNGA MKONO JITIHADA ZA WANAWAKE KISARAWE KUSINDIKA MUHOGO

July 15, 2016

 Bi. Anna Salado, Mkurugenzi wa taasisi ya Women for Africa Foundation ya Hispania, akizungumza na akinamama wa kikundi cha Green Voices katika Kijiji cha Kitanga (hawako pichani) na kueleza jinsi alivyofurahishwa na mafanikio yao kwenye usindikaji wa zao la muhogo.


NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, ameunga mkono jitihada za wanawake wa Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe kusindika zao la muhogo.
Jaffo, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe (CCM), amesema yuko tayari kushirikiana na wanawake wa kijiji hicho pamoja na wilaya nzima ya Kisarawe kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kutokana na zao hilo.
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI NA UJUMBE WAKE, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI NA UJUMBE WAKE, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

July 15, 2016

MWG1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimsalimia Naibu Katibu Msaidizi wa Idara ya Inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji ya nchini Marekani, Catherine Wiesner wakati ujumbe huo ambao uliongozwa na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (watatu kushoto). Kikao hicho kilichofanya katika Ukumbi mdogo wa Wizara, jijini Dar es Salaam kilijadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Wapili kushoto ni Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MWG2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akizungumza na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (wa pili kulia) pamoja na ujumbe wake katika kikao kilichofanya katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Watatu kulia ni Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto na anayefuata ni Naibu Katibu Msaidizi wa Idara ya Inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji ya nchini Marekani, Catherine Wiesner. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MWG3 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akiandika maelezo ya Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (katikati) katika kikao cha kujadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Kushoto ni Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MWG4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (wa tatu kushoto) pamoja na ujumbe wake katika kikao kilichofanya katika Ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Wapili kushoto ni Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto na anayefuata na kushoto ni Naibu Katibu Msaidizi wa Idara ya Inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na Uhamiaji ya nchini Marekani, Catherine Wiesner. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, na anayefuata ni Katibu wa Waziri, Nelson Kaminyoge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MWG5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (wapili kulia) pamoja na ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyojadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika wizarani, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

JAJI MKUU WA TANZANIA, ZIARANI MAHAKAMA KANDA YA MOSHI, AZINDUA RASMI MAHAKAMA ZA MWANZO BOMANG’OMBE NA SIHA.

July 15, 2016

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akilakiwa na Mhe. Aishieli Sumari, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi alipowasili Mahakamani hapo kwa ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utendaji kazi katika Kanda hiyo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi.
 Mhe. Jaji Mkuu akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama, Kanda alipowasili mapema Julai 14, 2016 kwa ziara ya kikazi.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe iliyopo Wilayani Siha Manispaa ya Moshi. 

WAZIRI NAPE AANZA KULA SAHANI MOJA NA WAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI

July 15, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika Operesheni ya kuwasaka waharamia wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini, hali inayopelekea wasanii hao kazi zao kuzorota. Waziri Nape leo ameianza Operesheni hiyo kwa kutembelea Maduka mbalimbali yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akisimamia zoezi la ukusanyaji wa kazi zilizodurufiwa na wafanyabiashara hao katika moja ya Maduka yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimsiliza mmoja wa watuhumiwa wa kudurufu kazi za wasanii, aliekuwa na mitambo ya kufanyia kazi hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakati wa Operesheni ya kuwasaka wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.


SERIKALI YA TANZANIA YAKABIDHI MABAKI YA BAWALA LA NDEGE LILILOKOTWA PEMBA MWEZI JUNI 2016 KWA SERIKALI YA AUSTRALIA NA MALAYSIA KWA USHUNGUZI RASMI. BAWA HILO LINADHANIWA KUWA LA NDEGE YA ABIRI YA MALAYSIA MH370 ILIYOPOTEA MACHI 2014.

July 15, 2016

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati  Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi  mwandamizi wa ajali za ndege , Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati  Tanzania ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. Kutoka kushoto ni Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(katikati)  akimsikiliza kwa makini Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes (Kushoto)akizungumza na waandishi wa habari, aikiishukuru serikali ya  Tanzania wakati  ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. Kutoka kushoto ni Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(wapili kulia)  na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari  ,pamoja na  Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes (wapili kushoto) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi  mwandamizi wa ajali za ndege  wa  Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, wakati  akizungumza na waandishi wa habari,(hawapo pichani) wakati  serikali ya  Tanzania  ilipokuwa ikikabidhi bawa la ndege  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. Hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,(kulia)  akishuhudia  Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari  akisaini hati ya makabidhiano ya mabaki ya bawa la ndege  wakati  serikali ya  Tanzania  ilipokuwa ikikabidhi bawa hilo  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016.  Katika hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.Kulia ni  Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa TCAA,Vallery Chamulungu.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,( wapil kulia)  na Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari  (kulia) wakifuatilia kwa mdhamini wakati Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes (kushoto)  akisaini hati ya makabidhiano ya mabaki ya bawa la ndege , wakati  serikali ya  Tanzania  ilipokuwa ikikabidhi bawa hilo  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016.  Katika hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.aliyesimama ni  Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa TCAA,Vallery Chamulungu.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,( wanne kulia)    Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari (watano kulia) Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes (watatu kushoto), Mkurugenzi  mwandamizi wa ajali za ndege , Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Aslam Basha Khan, (wapili Kushoto) ,  Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu wa Bodi yawakurugenzi wa TCAA,Vallery Chamulungu.(kushoto) pamoja na maafisa wa kitengo cha ukaguzi wa ajari za ndege Wizara ujenzi , Uchukuzi na mawasiliano wakikabidhiana mabaki ya bawa la ndege , linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016.  Katika hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaalam.
 Mkurugenzi  mwandamizi wa ajali za ndege , Wizara ya Uchukuzi Malayasia, Basha Khan,(kushoto waliochuchuma )  na Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt leonard Chamuriho,wakikagua mabaki ya bawa la ndege,  wakati  serikali ya  Tanzania  ilipokuwa ikikabidhi bawa hilo  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari  na  Balozi wa Australia katika nchi za Afrika Mashariki, John  Feakes.
 Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari (kulia )  akisaidiana na wafanyakazi wa DHL kuingiza mabaki ya bawa la ndege  tayari kuelekea nchini Malaysia kwa uchunguzi zaidi mara baada ya  serikali ya  Tanzania  kulikabidhi bawa hilo  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari (wapili kushoto )  akitoa maelekezo kwa wafanyakazi  wa DHL jinsi ya kuingiza mabaki ya bawa la ndege  tayari kuelekea nchini Malaysia kwa uchunguzi zaidi mara baada ya  serikali ya  Tanzania  kulikabidhi bawa hilo  kwa serikali ya Malaysia, linalodhaniwa kuwa la ndege ya Malayasia MH370, iliyopotea wakati ikifanya safari kutoka malaysia kwenda China mwaka 2014. Mabaki ya bawa hilo yaliokotwa na mvuvi katika pwani ya Pemba  Chungua Hamad Chungua  (hayupo pochani)mwezi Juni 2016. ,hafala hiyo ilifanyika  Makao makuu ya TCAA Banana Ukonga  jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA ELIMU, PROF JOYCE NDALICHAKO AONGOZA HAFLA YA WASICHANA( TANZANIA GIRLS GUIDES ASSOCIATION).

July 15, 2016

 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Maraki wa Tanzania Girl Guides waliohudhuria katika sherehe ya kuwapokea washiriki wa Mradi wa YESS-Girl Guides iliyofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mabinti walioshiriki Mradi wa Matembezi ya YESS- Girls hapa nchini wapili kulia ni Lydia Omondi kutoka Kenya, Florence Kwizera kutoka Burundi na Avengiline Du Toit kutoka Afrika kusini wakiwa na Girl Guide wa Tanzania wakitoa burudani katika sherehe ya kuwapokea washiriki wa Mradi wa YESS-irl Guide jijini Dar es Salaam.
 Mabinti walioshiriki Mradi wa Matembezi ya YESS- Girls  wakiwa katika picha ya Pamoja.
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi Binti Rose Ipyana Mwambete aliyewakilisha TanzaniaGirl Guide katika mradi wa YESS-Girls Movement 2016 huko Rwanda wakati wa sherehe iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti Happyness Mshana aliyewakilisha Tanzania huko Madagaska katika Mradi wa YESS-Girls Movement.
Baadhi ya washiriki wakipokea vyeti katika sherehe iliyofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
WANANCHI SASA WANAWEZA KULIPA KODI ZA TRA POPOTE KWA KUTUMIA NMB.

WANANCHI SASA WANAWEZA KULIPA KODI ZA TRA POPOTE KWA KUTUMIA NMB.

July 15, 2016

Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure (kulia) akipeana mkono na Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati mara baada ya kuingia makubaliano leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB 'NMB Mobile' au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote. Kushoto ni Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akishuhudia. Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure (kulia) akipeana mkono na Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati mara baada ya kuingia makubaliano leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB 'NMB Mobile' au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote. Kushoto ni Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akishuhudia.Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato (TRA) na NMB kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure pamoja na Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kushoto) wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato (TRA) na NMB kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure pamoja na Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kushoto) wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Viongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Benki ya NMB (kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano kati ya TRA na Benki ya NMB kushirikiana katika ukusanyaji kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB. Viongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Benki ya NMB (kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano kati ya TRA na Benki ya NMB kushirikiana katika ukusanyaji kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB.Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo leo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo leo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati akishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB 'NMB Mobile' au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote. Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati akishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB 'NMB Mobile' au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote.Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo leo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo leo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.

  WANANCHI sasa wanaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kutumia Benki ya NMB. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati TRA na NMB walipokuwa wakiingia makubaliano, Mkuu wa Kitengo cha Miamala wa Benki ya NMB, Michael Mungure alisema ushirikiano huo umelenga kuwarahisishia raia ulipaji kodi.

 Alisema mwananchi anaweza kulipa kodi mbalimbali za TRA popote alipo kwa kutumia simu iliyosajiliwa na huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi (NMB Mobile) na kulipa kodi anayoitaji na kama sio mteja pia anauwezo wa kulipa kodi hiyo kwenye tawi lolote la NMB nchini kote bila kujali alipo. Alisema makubaliano hayo yanaendelea kurahisisha hali ya ulipaji kodi kwani.

Benki ya NMB ina matawi mengi na karibu wilaya zote za Tanzania. Alisema mtandao wa matawi ya nchi nchini ni mkubwa na imesambaa kwa asilimia 95 katika wilaya zote huku ikiwa na wateja milioni 1.3 wanaotumia mtandao wa NMB kupitia simu za mkononi 'NMB Mobile' jambo ambalo litawarahisishia wananchi ulipaji kodi mbalimbali za TRA. Alisema mteja wa NMB aliyejiunga atatakiwa kupiga *150*66# kisha kuchagua huduma ya ulipaji kodi kabla ya kufuata maelekezo mengine yatakayomuongoza kufanikisha malipo ya kodi anayoitaji kulipa.

 Imeingia ubia na TRA kulipa miamala ya kodi popote walipo. Popote alipo usiku au mchana kulipa kodi zote na ushuru anayoitaka. Sio mpya tumekuwa tukifanya kipya ni mfumo wa ulipaji sasa kutumia mtandao wetu moja kwa moja...mfumo wetu utaweza kumuunganisha mteja moja kwa moja na mfumo wa TRA na kufanya malipo yake. Kwa upande wa TRA, Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi, Ramadhan Sengati alisema kwa ushirikiano huo na benki ya NMB sasa mifumo ya NMB inazungumza na mifumo ya TRA moja kwa moja bila usumbufu wowote na kumuwezesha mwananchi kulipa kodi yake popote alipo. 

Aidha alisema hatua hiyo inaleta unafuu kwa kutosumbuka sana kwa walipaji wa kodi mbalimbali na kusaidia kuondoa usumbufu. Alisema hatua hiyo pia ni inaleta usalama wa mtu kutozunguka na fedha mkononi bila sababu jambo ambalo si salama kwa muhusika. ".

..Hii itachangia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi na mfumo bora wa ulipaji, kwani mteja anaweza kulipa kodi yoyote na hata ushuru na hata wa kimataifa kwa kutumia mfumo huu popote alipo," alisema Sengati na kuongeza kuwa; "Malengo yetu ni kurahisisha ulipaji wa kodi ili kujenga maisha bora, huku ndio tunako enda hivyo tunawashauri wananchi watumie mfumo huu kulipa kodi mbalimbali za TRA.

ASKOFU DK. CHARLES GADI KUONGOZA MKUTANO MKUBWA WA KUOMBEA TAIFA VIWANJA VYA BIAFRA JIJINI DAR ES SALAAM

July 15, 2016
 Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkubwa wa kuombea Taifa kila Jumanne kwa siku 1001 utakaofanyika kuanzia Julai 19, 2016 viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mchungaji James Manyama, Palemo Massawe na Mchungaji Leonard Kajuna.
 Mchungaji Palemo Massawe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askofu Dk. Charles Gadi (wa pili kushoto), na wachungaji wenzake wakiomba baada ya kuzungumza na wanahabari.


Na Dotto Mwaibale

Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi anatarajiwa kuongoza mkutano mkubwa wa kuliombea Taifa utakaofanyika kuanzia Julai 19 katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametajwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.


Makonda anatarajiwa kuzindua mkutano huo wa maombi hayo ya siku 1,001 ambayo  yataendelea kufanyika siku ya Jumanne ya kila wiki.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo 
Dar es Salaam leo, Askofu Dk. Charles Gadi alisema maandalizi ya  maombi hayo yamekwisha kamilika na kuwa yanakuja kufuatia mengine ya siku elfu moja na moja ya kuliombea taifa yaliyokwisha kufanyika  mwaka 2012 na kukamilika mwaka 2015.

Alisema "Tunakumbuka tulianza maombi ya siku elfu moja mwaka 2012 ambapo yalitimiza mwaka 2015, tunashukuru Mungu kwamba yote tuliyoyaorodhesha katika mahitaji ya siku hizo 1,001 yametimizwa na mengi yako mbioni kutimizwa". 

Alisema katika siku 1,001 wanakusudia kuombea mambo 16 yakiwemo kuombea wananchi wawe na utayari wa  kulipa kodi, kuhamasisha wanachi kujiunga na mifuko ya jamii, watunze na kulinda miundombinu ya taifa, matumizi endelevu ya ardhi, kuhamasisha utalii wa ndani, wananchi kupenda kupima afya zao mara kwa mara na wawe na tabia ya kujiwekea kumbukumbu ya hesabu ya shughuli zao.


"kuhamasisha  wananchi kulinda maadili ya taifa, kuhamasisha usafi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla, kuhamasisha wanachi kupenda vitu vya hapa nchini, kuiomba serekali iwalinde na kuwawezesha wawekezaji wa ndani na kuiombea serekali iweze kununua vifaa vya kutomsha kwa ajili ya hospitali zetu " Alisema

Askofu Dk. Gadi alitumia muda huo kuwaomba wananchi na waumini wengine kutoka madhehebu na dini mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambao ni muhimu wa kuliombea taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani ili watu wake waweze kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)