MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA NA UWEKEZAJI YAFANA DAR

October 06, 2017
 Sehemu ya wananchi wakitoka kwenye semina ya ufugaji bora wa samaki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Taasisi ya NUEBRAND EC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Joachim Komba wa Taasisi ya Eden Agri, akitoa elimu ya ufugaji bora wa samaki na faida zake wakati wa semina iliyofanyika  wakati wa wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji
 Wajasiriamali wakiata maelezo kuhusu ufugaji bora wa samaki aina ya kambare  waliokuwa wakioneshwa katika banda hilo la Eden Agri
 Wananci wakiwa banda la NSSF
 Wajasiriamali wakipata maelezo ya jinsi ya kunufaia na Benki ya NMB kuhusu mikopo mbalimbali
 Ofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar,Aisha Ali Mohammed akimpatia maelezo mkazi wa Jiji kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo
 Maofisa wa Taasisi ya Nuru wakitoa maelezo  kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo
 Wajasiriamali wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), Neema Fredrick (kushoto) na Godfrey Mshomari kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wanachama wa mtandao huo. Aliyekaa ni Happiness Mshana.
 Ofisa Mkuu wa Elimu kwa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, James Mtalika (Kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo wakati wa maonesho hayo

BENKI YA AZANIA YAENDELEA NA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTEMBELEA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)

October 06, 2017
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya Azania jana imeendelea na Maadhimisho ya  Wiki ya huduma kwa Wateja kutembelea Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ambapo imekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba.

Akizungumza ofisini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe amesema kuwa wameitembelea TCRA kutokana na kuwa Wateja wao wakubwa wanaowathamini.

Itembe amesema kuwa wanaendelea kutembelea Wateja wao Bega kwa Bega ili kuwahudumia vizuri, pia kusikiliza maoni yao juu ya huduma zinazotolewa na Benki hiyo zikiwemo changamoto pamoja na ushauri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba ameshukuru kutembelewa na Benki ya Azania, ambapo amesema kuwa wamefurahi kutokana na kuwa Wateja wa Benki hiyo. Mhandisi Kilaba amesema kuwa wao kama TCRA hawajakosa pa kwenda isipokuwa huduma zilizopo kwenye benki hiyo zinawafaa. Pia ameiomba Benki ya Azania kuwekeza kwenye viwanda ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Pia amesema Watumishi wa Malamka hiyo hawajapata vikwazo kupata huduma kama Taasisi katika Tawi hilo lililopo Mawasiliano.

Hata hivyo, Mhandisi Kilaba ameishauri Benki hiyo kuwa na ubunifu zaidi katika sehemu nyingi, kuboresha mambo kama ya Mobile Bank ili kuwafikia wateja wengi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba(wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(Wa pili kulia), Meneja wa Tawi la Benki la Azania la Mawasiliano, Valentina Chamasa, Meneja Mkuu wa Benki ya Azania, Nyansaho Rhimo( wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Alinanuswe Kabungo(wa tatu kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati(kushoto).

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimshukuru mkurugenzi kwa niaba ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuwa wateja wao wa muda mrefu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuwa wateja wa benki hiyo ili kupunguza adha kwa wafanyakazi hao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akizungumza kuhusu namna benki ya Azania inavyoweza kujikita kusaidia kukuza viwanda hasa vidogo vidogo na vikubwa ili kuendana na kazi ya Rais Magufili kufikia kwenye malengo waliyojiwekea kama taifa pamoja na kuwashauri kupanua huduma hasa kupitia njia ya simu ili kuwafikia wateja wengi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
Meneja Mkuu wa Benki ya Azania, Nyansaho Rhimo(kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Alinanuswe Kabungo(wa pili kushoto) wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi alipokuwa anakabidhiwa hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) kuhusu namna wanavyofanya kazi bega kwa bega na wafanyabiasha wa Kariakoo kwenye moja ya duka la wateja wa Benki ya Azania  walipowatembelea leo.

WAZIRI UMMY AIBEBA AFRICAN SPORTS YA JIJINI TANGA

October 06, 2017

 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezaji


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo

 Mmoja kati ya viongozi wa timu ya African Sports wakimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania.
Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia aliwalipia kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka Tanzania Bara.
“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi  katika Jiji la Tanga.
“Sambamba na hilo lakini pia tumepokea mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili “Alisema.
Aidha pia Waziri Ummy aliitaka timu hiyo wahakikishe wanafanya vizuri katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa nchini.
“Ndugu zangu wana African Sports msituangushe hakikisheni mnatumia misaada hii mnayoipata iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya kufanya vizuri “Alisema.
Hata hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia akaunti ya fedha wachezaji wote wa timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao kulipwa moja kwa moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

MWENYEKITI MPYA CCM, KAMATI YA SIASA YACHAGULIWA KWA KISHINDO WILAYA YA SINGIDA VIJIJINI

October 06, 2017
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.

Na Mathias canal, Singida

Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida  Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa CCM Wilaya lakini pia nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi Ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya  ambapo Richard Niangusha Kwimba aliibuka mshindi kwa kupata kura  6, nafasi ya pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi aliyepata kura 3.

Nyingini ni nafasi ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa waliomba ridhaa katika nafasi hiyo ni watu 14 ambapo kati yao washindi ni Sabasaba Manase, Zainabu Abdaleah na Khadija Kisuda Lesso.

Nafasi ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham, Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi, Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba Nyaland.

Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba  walikuwa watano lakini washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na  Sada Njiku. Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na Edward Jared Ihonde.

Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Singida Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

WASTAAFU WAIPONGEZA PSPF KWA KUPOKEA MALIPO YA PENSHENI YA MWEZI KWA WAKATI

October 06, 2017
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin  Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.
“Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.
Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.
“Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.
Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.
Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.

 Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye  ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
 Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma.
  Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
 Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
 Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017.
Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe.
 Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.
Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF.
Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki.
 Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.
 Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.

MWENYEKITI WA CHADEMA MTAA WA KIHESA KILOLO B AMPIGIA MAGOTI MBUNGE RITTA KABATI

October 06, 2017
 Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
 Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo miundombinu yake imeharibika.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo amemuomba mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuwasaidia kukarabati shule ya msingi Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake imeharibika na sio rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Akizungumza na blog bwana Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo shule hiyo haijawahi kufanyiwa ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.

“Mwandishi ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili” alisema Madembo

Madembo alisema kuwa shule nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea zinamiundombinu ilichoka hivyo serikali na viongozi wa kisiasa kuanza kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili kuboresha taaluma kwa watoto wetu kuendana na karne ya sasa.

“Hebu angalia hapo juu hili paa muda wowote kuanzia sasa hili paa la darasa linaweza kuleta maafa kwa wanafunzi lakini viongozi wetu hawaliangalii hili swala ndio maana nimemuaomba huyu mbunge Ritta Kabati kusaidia kuarabati” alisema Madembo

Aidha Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa anafanyakazi na wenyeviti wote wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kuijenga manispaa na kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Nimekuwa navikao vya mara kwa mara kwa wenyeviti wa mitaa ya hapa manispaa hivyo wenyeviti wa CHADEMA wamekuwa wa kwanza kuniita kila wakati kusaidia kuleta maendeleo katika maeneo husika ndio maana leo unaniona nipo na mwenyekiti wa CHADEMA kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto za hii shule ya Igeleke” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi mbalimbali kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo wananchi nsio kuangalia vyama vinafanya nini.

“Mimi ni kada wa chama cha mapinduzi lakini nimekuwa nikifanya kazi vizuri na viongozi mbalimbali wa kiasa kwa lengo la kuleta maendeleo tu ndio sababu inayosababishwa wapinzani kuniona mimi bora wakati wa kufanya shughuri za kuleta maendeleo” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa ataendelea kufanya ziara kwenye shule zote zenye matatizo ili kuzisaidia kuyatatua matatizo hayo na leo amefanya ziara katika shule ya msingi Igeleke kwa kuziona changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuzitafutia ufumbuzi.

Naye mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.