MIUNDOMBINU YA BANDARI YA KIGOMA KUBORESHWA NA KUPANULIWA

December 11, 2014


Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo kuanza kufanya upanuzi wa Bandari ya Kigoma  na kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika Bandari ya Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku katika bandari hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kigoma.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini nchini ipo kwenye mkakati wa kuiendeleza bandari hiyo ili iwe ya kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa bandari hiyo.
“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka huu wa fedha ilipanga kuiendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini na anga ili kuongeza ufanisi wa sekta hizi, ambapo Bandari ya Kigoma ni mojawapo ya bandari zilizopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, upanuzi wa bandari hiyo upo kwenye hatua za upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma na kutwaa maeneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Mkuu wa Bandari hiyo Bw. Athuman Malibamba alisema kuwa mpaka kufikia Juni 2014 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya uthamini wa mali eneo la Kibirizi lenye hekta 10 kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. “Pia, Mamlaka imempata Mtaalam Mshauri (M/S Royal Haskoning H.D.V Nederland, B.V) atakaefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kazi ya uthamini wa mali imekamilika kwa eneo la Katosho lenye hekta 69 kwa ajili ya kujenga bandari kavu,” alisema.
Kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika nchi za jirani kunatoa fursa ya kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kigoma ili kuwa na uwezo wa kuhudumia shehena inayoongezeka na kukuza uchumi katika mkoa na Taifa kwa ujumla. Aidha kuanzishwa kwa Eneo Maalum la Kiuchumi, katika mkoa wa Kigoma ni kichocheo muhimu kwa Mamlaka ya Bandari (TPA) kuimarisha huduma katika bandari ya Kigoma na hivyo kuweza kuzitumia fursa zitakazojitokeza mara baada ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuanzishwa. 

 Sehemu ya chelezo zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya meli na boti katika Bandari ya Kigoma.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Katikati mbele) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
 Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni (Wapili kushoto) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) walipofanya ziara bandarini hapo.
 Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Aliyenyanyua mkono) akionesha kufurahia jambo wakati walipofanya ziara katika Bandari ya Kigoma.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo
 Afisa utekelezaji wa Bandari Kigoma, Bw. Teophil Luoga (Kulia aliyechuchumaa) akiwaonesha eneo la upanuzi wajumbe wa timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) mara alipofika kujionea maendeleo ya bandari hiyo.


PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI YAFANYIKA MKOANI DODOMA

December 11, 2014

 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Amina Mfafaki akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea wakati wa kufunga maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto katika ukumbi wa Bwalo la polisi Dodoma.(Picha na John Banda)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime akiongea jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto yaliyofanyika Bwalo la polisi Dodoma.
 Kamanda wa polisi wilaya ya Dodoma mjini Malingumu akizungumza akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Staff Sajent Mwanajuma Mtuli wa polisi Dodoma akisisitiza jambo kwenye ufungaji huo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto.
 Baadhi ya Askari wakifuatilia jambo kwenye kilele hicho.

Wakina mama wajawazito wa wodi ya chikande walioalikwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto uliofanyika katika Bwalo la polisi Dodoma.
PICHA YA ZARI WA DIAMOND NA WANAWE WAKILA BATA

PICHA YA ZARI WA DIAMOND NA WANAWE WAKILA BATA

December 11, 2014

Kuvuja kwa mkanda wake wa ngono hakujamzuia Zari ‘the Bosslady’ Tlale kufurahia muda bora na wanae wakati huu wa likizo za sikukuu za Christmass. Zari mwenye watoto watatu, ameonesha kutoyumbishwa na kusambaa kwa mkanda huo na leo amepost picha akiwa na wanae wakifurahia chakula pamoja.
“Current situation…… school is closed most offices are closed, time to spend more quality times togther ‪#‎HolidayModeActivated‬,” ameandika Zari kwenye picha alizoweka kwenye ukurasa wa Facebook.

KATIBU MKUU WA COASTAL UNION AKIWAONYESHA KIWANGO CHAKE CHA SOKA WACHEZAJI WA U-20 WA TIMU HIYO

December 11, 2014



KATIKA KUSHEREKEA 9 DISEMBA BASI MAARUFU NCHINI LASOMBELEA WAHAMIAJI KUWAINGIZA DAR

December 11, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
KATIKA KUSHEREKEA 9 DISEMBA BASI MAARUFU NCHINI LASOMBELEA WAHAMIAJI KUWAINGIZA DAR
WAKATI Taifa likisherekea siku kuu ya TISA DESEMBA Gari yenye namba za usajili T.131 AZZ SCANIA mali ya kampuni ya Saibaba limekamatwa likiwa na  raia 12 wa  Ethiopia likiwasafirisha kutokea Arusha kuelekea jijini Dar es salaam.

Raia hao wamekamatwa majira ya saa 10:30 jioni maeneo ya Mbwiko Kata ya Mbwiko Tarafa ya Mombo barabara kuu ya Mombo –Segera Wilayani Korogwe.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Frasser kashai amewataja raia hao kuwa ni Kashoma Bayen umri wa miaka 24,Berchano Gamada umri wa miaka 32, Awal Jamal  umri wa miaka 23  ,Yanis Gatiso umri wa miaka 28, Metson Sipril  umri wa miaka 21,Tashona Hayalis umri wa miaka 30.

Wengine ni Adino Samiru umri wa miaka 20, Kengeny  Siyun umri wa miak 22 ,Charnes Egesa umri wa miaka 20, Abdi Bandru umri wa miaka 21, Siumanda Siumanda umri wa miaka 26 na Na Malako Abuu umri wa miaka 23.Watuhumiwa wote watakishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.

MTOTO NAE KINAWA WA BIASHARA

Hawa walikamatwa siku za nyuma nchini
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mbukuzi mwenye umri wa miaka 17 mkulima na mkazi wa Putini kata ya Chongoleani Wilaya ya Tanga kwa kosa la kuwaasafirisha wahamiaji haramu wapatao sita (6) ambao ni Raia wa Ethiopia.

kamanda Kashai amesema kuwa mnamo tarehe 8 Disemba mwaka huu majira ya saa saba 13:00 mchana, huko katika  kisiwa cha Jambe Kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe Wilaya Tanga wamekamatwa Dolec Dalalo umri wa miaka 28, Alaleus  Tesame umri wa miaka 21, Hashinavia Shamibu umri wa miaka 23, Taken Ndasalh umri wa miaka 20,Tamesgen Kisfon umri wa miaka 20, Mihon Eriamin umri wa miaka 22.

Aidha mtuhumiwa amekiri kufanya kufanya biashara hiyo ya usafirishaji wa wahamiaji haramu na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

ONYO KALI
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linatoa onyo kali kwa watu wanaovunja Sheria ya Kuingiza wahamaiaji haramu kinyemela ndani ya nchi kinyume cha sheria. Jeshi la polisi litawafuatilia watu hao na kuhakikisha kwamba wanakamatwa pamoja  hamaiaji hao haramu ambao wanawasafirisha.

Aidha amewashaukuru wananchi kwa juhudi za kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuwapa ushirikiano juu ya uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao wanayoishi.

Pamoja na hayo aliwasisitizia wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao wanayoishi ili kuweza kuzuia na kukabiliana na uhalifu mkoani hapa.
chanzo:Mwanamke makini Blog.
TANGA BADO NJIA MUHIMU YA WAHAMIAJI HARAMU "18 WAKAMATWA" Matukio ya kumatwa kwa Wahamiaji Mkoani Tanga yamezidi kushamiri ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mbukuzi mwenye umri wa miaka 17 mkulima na mkazi wa Putini kata ya Chongoleani Wilaya ya Tanga kwa kosa la kuwaasafirisha wahamiaji haramu wapatao sita (6) ambao ni Raia wa Ethiopia. Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Frasser Kashai amesema kuwa mnamo tarehe 8 Disemba mwaka huu majira ya saa saba 13:00 mchana, huko katika kisiwa cha Jambe Kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe Wilaya Tanga wamekamatwa wahamiaji hao ambao wametambulika kwa majina ya Dolec Dalalo umri wa miaka 28, Alaleus Tesame umri wa miaka 21, Hashinavia Shamibu umri wa miaka 23, Taken Ndasalh umri wa miaka 20,Tamesgen Kisfon umri wa miaka 20, Mihon Eriamin umri wa miaka 22. Aidha mtuhumiwa amekiri kufanya kufanya biashara hiyo ya usafirishaji wa wahamiaji haramu hivyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika. Katika tukio jingine Gari yenye namba za usajili T.131 AZZ SCANIA mali ya kampuni ya Saibaba limekamatwa likiwa na Raia 12 wa Ethiopia likiwasafirisha kutokea Arusha kuelekea jijini Dar es salaam Raia hao wamekamatwa majira ya saa 10:30 jioni maeneo ya Mbwiko Kata ya Mbwiko Tarafa ya Mombo barabara kuu ya Mombo –Segera Wilayani Korogwe. Kamanda kashai amewataja Raia hao kuwa ni Kashoma Bayen umri wa miaka 24,Berchano Gamada umri wa miaka 32, Awal Jamal umri wa miaka 23 ,Yanis Gatiso umri wa miaka 28, Metson Sipril umri wa miaka 21,Tashona Hayalis umri wa miaka 30. Wengine ni Adino Samiru umri wa miaka 20, Kengeny Siyun umri wa miak 22 ,Charnes Egesa umri wa miaka 20, Abdi Bandru umri wa miaka 21, Siumanda Siumanda umri wa miaka 26 na Na Malako Abuu umri wa miaka 23. Watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili pale upepelezi wa awali utakapo kamilika.

Make Money at : http://bit.ly/copy_win