BERNARD MEMBE ATUA TANGA KUTAFUTA WADHAMINI KUANZA SAFARI YA IKULU
Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, akiwahutubia wanachama wa CCM Mkoa wa Tanga waliojitokeza makao makuu ya chama hicho kumdhamini katika fomu zake za kuomba ridhaa ya kugombea urais.
MAHAFALI YA TATU YA SHULE YA AWALI YA CHEKECHEA YA OJAYS KIDDIES ZONE YAFANYIKA LEO JIJINI DAR
Wahitimu wa shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone, Bi Usia Nkoma Ledama akizungumza jambo wakati wa mahafali ya tatu ya shule hiyo
Mwalimu Debby Ndulla(wa kwanza kushoto) akiwatambulisha walimu wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone ambao ni Mwalimu Tatu(wa pili kutoka kushoto) akifuatiwa na Mwalimu Revina(katikati), Mwalimu Doroth(wa pili kutoka kulia) pamoja na Mwalimu Aika(kulia)
Mwalimu Debby Ndulla(wa kwanza kushoto) akiwatambulisha wadada wanaowalea watoto wadogo wa shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone
Mwalimu Debby Ndulla(kushoto) akimtambulisha Kaka Tobi mbele ya wazazi pamoja na walezi wa watoto waliofika kwenye mahafari ya Tatu ya shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone
Kaka Tobi akiwapungia mikono wazazi pamoja na walezi wa watoto(hawapo pichani)
Wanafunzi wa dalasa la Lantana katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
Wanafunzi wa dalasa la Lilies katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
Wanafunzi wa dalasa la Lavender katika shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone wakitoa burudani wakati wa mahafari ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika leo
Bwana na Bibi Seyvunde wakizungumzia maendeleo ya mtoto wao ambaye alikuwa ni mmoja wa wahitimu leo.
Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Ojays Kiddies Zone, Bi Usia Nkoma Ledama(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Gerald Hando(katikati) pamoja na Mwalimu Debby Ndulla(kushoto)
Baadhi ya wazazi pamoja na walezi waliofika katika mahafari ya watoto wao wakifuatilia yanayoendelea.
Picha hizi chini ni wakati wa kukabidhiwa vyeti kwa wanafunzi hao waliohitimu leo
Wazazi pamoja na walezi wakichukua matukio
UN KUSAFISHA KILIMANJARO
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkaribisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo.
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez, alikutana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na kufanya naye mazungumzo.
Miongoni mwa mambo waliyojadili ni maandalizi ya shughuli na matukio kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa (UN@70 ).
Katika mazungumzo yao walikubaliana kufanya shughuli ya upandaji miti kuzunguka Mlima Kilimanjaro na kusafisha sehemu ya mji kabla ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa mkoa alikubaliana na wazo hilo na kusema shughuli hiyo inafaa kufanyika katikati ya mwezi wa Agosti.
Wawili hao wakipiga picha ya pamoja.
Wakiagana.
MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MJINI BUKOBA
Sehemu ya Wakazi wa mji wa Bukoba Mkoani Kagera wakiwa nje ya Uwanja wa
Ndege wa Bukoba, wakimsubiri kumlaki Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, tayari kwa kupokea
fomu ya wanaCCM wa kumdhamini.
Wadau wa CCM wakijadiliana jambo.
Ndege iliyombeba Mh. Edward Lowassa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM
Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze wakati alipowasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mh. Lowassa katika tabasamu.
Umati
wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa
umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye
ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, leo Juni 15, 2015.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Katibu wa UWT wilaya ya Bukoba
Vijijini, Agness Bashemu alipokuwa akitoa taarifa fupi ya namna ya
kumkabidhi fomu hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini,
Yussuf Ngaiza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoba, Dkt. Aman Kaborou akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC) Bukoba, Nazir Karamagi akuzungumza machache mbele ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze akizungumza mbele ya umati wa wanaCCM
pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, na
kutangaza kwamba yeye pia ni mmoja ya wana Safari ya Matumaini.
Shangwe kila kona.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara
baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate
ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye
Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye
majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi
Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, Wakati akitoa shukrani zake kwa kumdhamini ili
apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania,
kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya
wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wanaCCM
pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015,
mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili
apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania,
kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Subscribe to:
Posts (Atom)