WIZARA YA AFYA YAITAKA MSD KUTAMBUA NAFASI YAKE KATIKA MATUMIZI BIMA YA AFYA WA WOTE

December 11, 2023

   Na MWANDISHI WETU


WIZARA ya Afya imeitaka Bohari ya Dawa (MSD) kutambua nafasi yake katika matumizi ya bima ya afya kwa wote na kuzingatia upatikanaji wa bidhaa za afya, ubora na bei zilizo katika muongozo wa matibabu wa serikali.

Pia , amezitaka taasisi za afya kuangalia upya mifumo ya utoaji huduma lengo ni kuona namna gani inavyoweza kubadilika ili kukidhi mahitaji ya bima ya afya kwa wote.

Maagizo hayo yalitolewa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe wakati akifungua kikao cha MSD na wateja wake wakubwa.

Katika kikao kazi hicho Dk.Grace amesisitiza MSD kuhudumia wananchi kutokana na mahitaji na taasisi zote za afy kuangalia mifumo ya utoaji huduma inavyoweza kubadilika kukidhi mahitaji ya bima ya afya kwa wote.

“Tuangalie upya mifumo yetu ya utoaji huduma namna inavyoweza kubadilika ili kukidhi mahitaji ya bima ya afya kwa wote.Tusisumbue wananchi muwasiliane wenyewe wao wanataka hudum,”alisema

Kwa mujibu wa Dk.Grace alifafanua kuwa muswada wa bima ya afya umepitishwa kinachoendelea sasa ni kufanyia kazi kanuni kwakushirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya Fedha,Ikulu na wadau wengine.

Kwa upande wake Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi alisema, kikao hicho kitajadili changamoto na kutafuta suluhuhisho ili MSD aweze kuwahudumia wateja wakubwa kwa bidhaa wanazozihitaji.

“Tumeshiriki kikao cha MSD ambacho kinaunganisha wateja wake wakubwa kutoka katika hospitali kubwa lengo ni kuboresha huduma za kuwahudumia na kupata bidhaa wanazohitaji kwa ajili ya kutoa huduma.

Aliongeza kuwa :”Changamoto ambayo ipo inatokana na utendaji ni kwamba wateja hawa wanapokosa bidhaa MSD huagiza bidhaa zao nje ya nchi ambapo ni kinyume na sheria .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai alisema, lengo la kuwakutanisha wateja wakubwa ni kwasababu mahitaji yao ya dawa ni makubwa tofauti na hospitali nyingine.

Alitaja wateja ambao wamekutana nao kuwa ni Hospitali ya Kibong’oto, Muhimbili, Ocean road, Benjamini mkapa na Hospitali ya Mirembe.

“MSD tuna mkakati wa kuwa na wateja wakubwa ambao sio mpya lakini tumeamua kuweka katika uhusiano wa kibiashara.Tunachokifanya hapa leo kuangalia wapi tulipo sasa kuja na malengo ya pamoja ili kutengeneza mpango mkakati namna tunavyoweza kuyafikia malengo hayo.

Aliongeza kuwa “Tunakaa leo na kutengeneza mkakati wa pamoja na kuanza utekelezaji wake.Lengo tutembee pamoja katika kuhakikisha waanchi wanapata huduma.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga alisema, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesaini sheria ya Bima ya afya kwa wote na utekelezaji wake unaanza hivi karibuni.


“Leo tumeshiriki katika kikao kilichoandaliwa na MSD ambapo unalengo la kutafuta suruhu ya pamoja kuhusu suala zima la upatikanaji wa dawa nchini.

Aliongeza kuwa :“Ili kutimiza adhma ya serikali ya Awamu ya Sita ya bima ya afya kwa wote lazima tukae pamoja kuwa na mikakati ambayo itafanya adhma hiyo itimie pasipo vikwazo vyovyote,”alisema

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke Dk. Joseph Kimaro alisema kumekuwa na maendeleo makubwa kwa MSD hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa serikali ya Awamu ya Sita.

“Lengo la kikao hiki ni kuimarisha ushirikiano katika utoaji huduma za afya ambapo inaenda sambamba na uwepo wa dawa na vifaa tiba ambapo kazi hiyo imepewa MSD ,”alisema



BENKI YA CRDB YAPATA CHETI CHA VIWANGO VYA KIMATAIFA CHA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA TEHAMA ISO 20000-1:2018

December 11, 2023

 

Dar es Salaam 11 Desemba 2023 – Benki ya CRDB leo imekabidhiwa cheti cha viwango vya Usimamizi wa Huduma za TEHAMA cha ISO 20000-1:2018 kilichotolewa na Shirika la Viwango la Uingereza (BSI). Cheti hicho kimekabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Benki yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Akipokea cheti hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi, na Mkuu wa Sera za Biashara na Uwekezaji Ubalozi wa Uingereza, Afisa Uendeshaji Mkuu wa Benki ya CRDB amesema cheti hicho ni ishara ya dhamira ya dhati ya Benki ya CRDB katika kuhakikisha mifumo, taratibu, na huduma za TEHAMA za benki hiyo zinakidhi ubora wa kimataifa.
Mwile alisema Benki ya CRDB imekuwa ikiwekeza katika mifumo ya kisasa na hivyo kupelekea mabadiliko makubwa katika huduma zake za TEHAMA kufikia viwango vya kimataifa. Hata hivyo mazingira ya biashara yamekuwa yakibalika kwa kasi kutokana na ukuaji wa teknolijia jambo ambalo limepelekea benki hiyo kufanya mchakato wa kuboresha viwango vyake.

“Tukitambua umuhimu wa kuwa na mifumo ya utoaji huduma iliyo na viwango bora, Benki ilifanya mchakato wa kupata cheti cha ubora wa ISO 20000 cha usimamizi wa huduma. Tulipitia mchakato mrefu uliohusisha uboreshaji wa michakato yetu ya usimamizi wa huduma za TEHAMA,” alisema Mwile.
Mwile aliongezea kuwa benki hiyo pia iliwekeza mipango ya kina ya mafunzo na uhamasishaji ili kuhakikisha wafanyakazi wanaelewa mahitaji ya viwango vya ISO 20000 na kutambua majukumu yao muhimu katika michakato ya usimamizi wa huduma za TEHAMA. Hii ilienda sambamba na kuanzishwa kwa utamaduni wa kuboreha mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.

Akielezea faida za kupata uthibitisho wa kiwango hicho cha kimataifa cha ISO 2000, Mwile alisema kunasaidia kuchochea michakato na taratibu zinazohakikisha huduma za TEHAMA zinatolewa kwa ufanisi na kukidhi viwango vya kimataifa, hivyo kutoa uzoefu uliobora kwa wateja.

“ISO 20000 pia inakuza utamaduni wa kuboresha mara kwa mara. Cheti hiki kinatuhimiza kutathmini na kurekebisha mara kwa mara michakato yetu ya usimamizi wa huduma za TEHAMA, kuhakikisha tunaendana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja na maendeleo ya teknolojia,” aliongezea.
Akikabidhi cheti hicho Mkurugenzi Mkaazi, na Mkuu wa Sera za Biashara na Uwekezaji Ubalozi wa Uingereza, Anna-Maria Mbwette ameipongeza Benki ya CRDB kwa cheti hicho cha ubora wa kimataifa na kusema kunaonyesha dhamira yake katika ubora, usalama na usimamizi madhubuti.

Anna-Maria alisema kupata ISO 20000 katika huduma za TEHAMA kutasaidia benki hiyo kujenga imani sit u kwa wateja wake, bali pia wawekezaji na washirika wa kimataifa kwani viwango hivyo vinatambulika na kutumika kote duniani.

Kiwango cha ubora wa ISO 2000O katika usimamizi wa huduma za TEHAMA ni mwendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kufikia viwango vya kimataifa kwani benki hiyo tayari imepata vyeti vya ubora vya ISO/IEC 27001:2013 cha usimamizi wa usalama wa taarifa, na ISO 22301:2019 cha mipango, mifumo, na michakato ya uendeshaji biashara yenye ufanisi.
Afisa Uendeshaji Mkuu Benki ya CRDB, Bruce Mwile, akipokea Cheti cha Ubora cha Usimamizi wa Huduma za TEHAMA cha ISO 20000-1:2018 kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi, na Mkuu wa Sera za Biashara na Uwekezaji, British High Commission, Anna-Maria Mbwette ambaye amekabidhi kwa niaba ya Shirika la Viwango la Uingereza (BSI) katika hafla fupi iliyofanyika leo 11 Desemba 2023 Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza wakati hafla fupi ya kupokea Cheti cha Ubora cha Usimamizi wa Huduma za TEHAMA cha ISO 20000-1:2018 kilichotolewa na Shirika la Viwango la Uingereza (BSI) kwa Benki ya CRDBBenki ya CRDB. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Benki ya CRDB, Mwanaisha Kejo.






RC Chalamila apongeza Jeshi la polisi na Barrick kwa kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa vitendo

December 11, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akiongea katika hafla hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila (katikati) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Afisa Mawasiliano wa Barrick,Abella Mutiganzi na Meneja Mawasiliano (Corporate Communications and Country Liaison Manager) wa Barrick, Georgia Mutagahywa (Kulia) kutokana na kampuni hiyo kufadhili mafunzo ya utambuzi wa masuala ya jinsia yaliyoendeshwa na Jeshi la Polisi katika katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia iliyofanyika katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (kushoto) ni Mkuu wa Chuo hicho, SACP Dk.Lazaro Mambosasa
Meneja Mawasiliano (Corporate Communications and Country Liaison Manager) wa Barrick, Georgia Mutagahywa, akiongea katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi cha Dar es Salaam.Mwaka huu Barrick ilishirikiana na Jeshi la Polisi katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akikabidhi cheti kwa Mratibu wa madawati ya kijinsia kwenye vyuo vya kati na vya juu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Gift Msowoya,
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo
Wanafunzi wa shule ya msingi Mgulani wakiimba wimbo kuhusu ukatili wa kijinsia katika hafla hiyo

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Barrick kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili kwa kijinsia kwa vitendo, ambapo limeweza kutoa elimu ya utambuzi wa vitendo hivyo na hatua za kuchukua wahanga wa vitendo hivyo katika shule za msingi,sekondari , kwenye maeneo ya biashara jijini Dar es Salaam.

Chalamila, alitoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kufunga maadhimisho hayo iliyofanyika katika Chuo Cha Polisi cha Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za kupinga vitendo hivyo.

Alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika siku 16 kwa kufikisha elimu ya utambuzi wa vitendo hivyo bado kunahitajika nguvu ya pamoja kuendeleakuongeza ushawishi,kuhamasisha,kukemea na kuelimisha jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo matatizo ya kisaikolojia yanaopelekea wananchi wengi kuelewa tatizo hilo na kujikuta vitendo hivi vinaongezeka kwa kasi hususani katika miji mikubwa kama Dar es Salaam.

“Natoa Pongezi kwa Jeshi la Polisi na Barrick, kwa kuungana pamoja kuhakikisha mnapeleka elimu ya utambuzi wa elimu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.Natoa wito kuwa muendeleze ushirikiano huu katika kampeni mbalimbali zenye lengo la kuleta mabadiliko chanya kama ambavyo mmefanya katika maadhimisho haya.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Polisi cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam,SACP Dk.Lazaro Mambosasa,alisema kuwa jeshi la polisi kwa kutumia wataalamu wake waliopo katika madawati ya kijinsia yaliyosambaa katika mtandao mkubwa wa vituo vyake litaendelea kutoa elimu na kusaidia wahanga wa vitendo sambamba ba kuhakikisha wanaofanya vitendo hivyo wanafikishwa haraka kwenye vyombo vya sheria.

Naye Meneja Mawasiliano (Corporate Communications and Country Liaison Manager) wa Barrick, Georgia Mutagahywa, alisema kuwa,Barrick Imekuwa mstari wa mbele kukabiliana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hivyo siku zote itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika vita vya kupambana kutokomeza vitendo hivi vya ukatili wa kijinsia chini.

Awali akitoa taarifa ya kampeni hiyo kwa mgeni rasmi, Mratibu wa madawati ya kijinsia kwenye vyuo vya kati na vya juu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Gift Msowoya, alisema kuwa katika kipindi cha kampeni wameweza kufikia shule zaidi ya 10 za msingi na sekondari katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam,Kwenye masoko na mikusanyiko ya watu pia kupitia vipindi vya televisheni na vyombo vingine vya habari, elimu hiyo imeweza kuwafikia watanzania wengi.

Msowoya, pia alisema kuwa katika kipindi hicho cha kampeni waliweza kutembelea gereza la Segerea kupeleka elimu hiyo sambamba na kufanya matendo ya huruma ambapo waliweza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika gereza hilo.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambayo huadhimishwa duniani kote na hapa nchini kuadhimishwa na taasisis mbalimbali na wadau wa masuala ya kijinsia mwaka huu yalianza tarehe 25 Novemba na kuhitimishwa tarehe 10,mwezi huu.
--