Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya
Gymkana mjini Bukoba leo akiomba kura za ndiyo kwa wananchi wa mkoa huo
kumpigia kura za ndiyo kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzaniaifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili aweze kuwatumikia watanzania.
Mgombea urais huyo Dk. John Pombe
Magufuli amesema mara atakapochaguliwa na watanzania na kuunda baraza
lake la mawaziri , Kazi ya kwanza ya waziri wake wa kilimo ni
kuhakikisha anatatua tatizo la bei ya zao la kahawa ambapo ameahidi kuwa
serikali yake itapunguza kodi mbalimbali zaidi ya 27 zinazotozwa kwa
wakulima wakati wa uuzaji wa zao la kahawa ili kuipandisha bei ya zao
hilo na kuwafaidisha wakulima ambao ndiyo wanaoteseka katika kilimo cha
zao hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-BUKOBA)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimnadi mbunge na madiwani wa jimbo la Bukoba mjini hawapo mpichani
wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Bukoba.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Bukoba
mjini Mh. Balozi Khamis Kagasheki akimuombea kura Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John
Pombe Magufuli na kujipigia debe yeye mwenyewe.
Mwanamuziki Diamond Platnumz na
kundi lake wakitumbuiza katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika kwenye
viwanja vya Gymkana mjini Bukoba.
Mwanamuziki Diamond Platnumz akitumbuiza katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkana mjini Bukoba.
Mgombea udiwani kata ya Chanji
mjini Sumbawanga akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea ubunge kupitia vijana mkoa wa Kagera Halima Bulembo akizungumza katika mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiwa amekaa na Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh. Balozi
Khamis Kagasheki.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Muleba
Kaskazini Mh. Charles Mwijage akizungumza katika mkutano huo na
kuwapigia debe wabunge wa viti maalum mkoa wa Kagera kulia ni Halima
Bulembo na kushoto ni Oliver Semguruka.
Kada wa CCM Amon Mpanju akimpigia
debe Dk John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata
ya Maruku Bukoba Vijijini.
Mmoja wa wananchi akiwa
amejikinga na jua kwa bango lenye picha ya Dr. John Pombe Magufuli
katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Maruku Bukoba vijijini.
Wasanii Mh. Temba kulia na Chege wakikamua jukwaani.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Gymkana Bukoba mjini.
Msanii Fid Q akiwapa mistari wananchi wa Bukoba mjini.
Baba na Mwana! Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza jambo na
mwanaye Halima Bulembo ambaye ni Mgombea Ubunge viti maalum vijana Mkoa
wa Kagera.
Jasson Samson Rweikiza mgombea
ubunge Bukoba vijijini akiomba kura kwa wananchi katika mkutano wa
kampeni uliofanyika kata ya Maruku Bukoba vijijini.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akizungu za na mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba vijijini Jasson Samson
Rweikiza.
Hapa ni CCM tu!
Hapa ni Kijani Tu mjini Biharamulo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi katika kata ya Nshamba Muleba Kusini wakati akiwa
njiani kuelekea Kamachumu mkoani Kagera.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiteta jambo na Mgombea ubunge jimbo la Muleba Kaskazini Mh. Charles
Mwijage na Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa Abdallah Bulembo mjini
Kamachumu.
Mgombea ubunge jimbo la Muleba
Kaskazini Mh. Charles Mwijage akiwahutubia wananchi wa Kamachumu katika
mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Muleba Kaskazini.
Watu wa Muleba na rangi ya kijani Kamachumu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimfariji Jojia Osward mke wa Marehemu Osward Lwakabwa aliyekuwa
mgombea udiwani kata ya Muleba aliyefariki kwa ajali jana mjini Muleba
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akimfariji kaka wa marehemu Osward Lwakabwa Mzee Elias Lwakabwa wakati
alipohani msiba wa mwana CCM huyo aliyefaiki kwa ajali jana.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akizungumza na watoto wa Marehemu Osward Lwakabwa aliyefariki kwa ajali
ya pikipiki kulia ni Fratenus Osward na Adelitus Osward.
CCM hoyee kijana akiwa ameshika mabango ya picha yenye picha za Dk. John Magufuli.
Diamond Platnumz na kundi lake wakitumbuiza mjini Bukoba wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Bukoba.
Diamond Platnumz akifanya vitu vyake.
Nyomi ya Bukoba hiyo.
Yamoto Bandi kama kawa jukwaani.