Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda akiwa ameubeba mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Raymond Mushi (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda baada ya kumaliza mbio zake wilayani humo Dar es
Salaam leo leo asubuhi. Mwenge huo ulianza mbio zake Wilaya ya Ilala na
kuzindua miradi mbalimbali.
Kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (kulia), akisalimia na Meya wa
Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
Viongozi mbalimbali wa Wilaya
ya Kinondoni wakiwa wamejipanga foleni wakisubiri kuupokea mwenge wa
Uhuru kabla ya kuanza mbio zake wilayani humo.
Wakimbiza mwenge kitaifa.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa
jiwe la msingi ya mradi wa maji Mburahati Barafu na Kisiwani
uliofadhiliwa na Jumuia ya Ulaya, Serikali ya Ubelgiji na Serikali ya
Tanzania wakati wa ukimbizaji wa mwenge huo Wilaya ya Kinondoni humo.
Kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa
jiwe la msingi ya baabara tatu katika Shule ya Sekondari ya Makulumla.
Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Beatrice Mhina.
Mwanafunzi Noel Mwita wa Shule
ya Sekondari ya Makulumla, akiekeza namna ya kuchanganya madawa wakati
kiongozi huyo wa mwenge, Juma Chum (wa nne kushoto), alipoweka jiwe la
msingi za maabara katika shule hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa shule
hiyo, Beatrice Mhina, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius
Wambura na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
Wananchi wa Mburahati wakiupokea mwenge huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo hilo.
Vijana wa hamasa wakipamba hafla hiyo kwa kuonesha matukio mbalimbali.
Mwanamuziki Rehema Chalamila
‘Ray C’ akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoacha matumzizi ya dawa ya kulevya
mbe ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum
(hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa
na dawa hizo katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum, akimkabidhi Amina Mshana
chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Wakimbiza mwenge wa Uhuru
kitaifa, Delina Simfukwe (kushoto) na Bakia Abdallah wakiteta jambo na
mwanamuziki RehemaChalamila ‘Ray C baada ya kutoa ushuhuda kuhusu
matumizi ya dawa za kulevya.
…………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda ametoa ajira ya moja kwa moja kwa kijana Yusuf Mzitto
mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa ameathiriwa na matumizi
ya dawa za kulevya wa wilaya hiyo.
Makonda alitoa ajira kwa kijana
huyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu. Juma
Khatibu Mchum wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na
matumizi ya dawa za kulevya kilichozinduliwa na kiongozi huyo wa mbio za
mwenge katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi.
“Kijana huyu mwenye elimu ya
juu ya masuala ya kompyuta alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za
kulevya hivyo baada ya kuacha kutumia dawa hizo tumempa ajira katika
ofisi yangu ili aweze kufanyakazi badala ya ujuzi wake kupotea bure”
alisema Makonda.
Makonda alisema kuwa katika
kuwawezesha vijana walioathiriwa na dawa hizo wamepatana na viongozi wa
manispaa hiyo kuwa kila kampuni inayofanya shughuli za kijamii katika
wilaya hiyo ili iweze kupata tenda ya kufanya kazi yoyote ni lazima itoe
mchanganuo kwanza wa utoaji wa nafasi ya ajira kwa vijana wa wilaya
hiyo.
Alisema wamechukua hatua hiyo
ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana waliohamua kuachana na matumzi ya
dawa za kulevya ambao hawana kazi hivyo kupitia kakampuni hizo ziweze
kuwasaidia vijana hao baada ya kupatiwa tenda na manispaa hiyo.
Alisema ili kuunga jitihada za
Rais Jakaya Kikwete za kupambana na uingizaji wa dawa za kulevya
ameanzisha mpango wa kukutana mara moja kila mwezi na vijana
walioathiriwa na dawa hizo ili kubadilishana mawazo badala ya kuwatenga.
Makonda alisema vijana hao
wengi wao ni wataalamu wa masula mbalimbali akimtolea mfano kijana
aliyepewa ajira katika ofisi yake ambaye atawasaidia katika mambo
mengine.
Akizungumzia mbio za mwenge
katika wilaya yake kwa mwaka huu alisema umezindua na kuweka mawe ya
msingi kwenye miradi saba yenye jumla ya sh.5,079,153,972 ambapo kati ya
fedha hizo sh.14,802,200 ni fedha kutoka serikali kuu, sh.2,672,992
kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, sh.913,800,780 ni
mchango wa wahisani na sh.1,477,978,000 ni michango ya wananchi.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni
pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa baabara, ujenzi
wa shule za Sekondari, ujenzi wa jengo la wazazi, ujenzi wa ofisi ya
Kata na ujenzi wa nyumba ya walimu.
Alisema mwenge huo ulipata
fursa ya kukagua miradi endelevu wa ugawaji wa vyandarua, mradi wa
wanawake wajasiriamali, mradi wa vijana wajasiriamali watunzaji wa
mazingira na mradi wa huduma za ukimwi.
Kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka watanzania wote bila ya kujali
itikadi za vyama vyao kudumisha amani na utulivu wa nchi hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema amani ya nchi tusipo
kuwa makini inaweza kuharibiwa kwa siku moja wakati imetafutwa kwa miaka
mingi na aliwata vijana kuacha kutumia dawa za kulevya na kujikinga ma
malaria ambayo yame kuwa yakiua watu wengi kuliko ukimwi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)