MASHIRIKA 40 YAUNGANA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI JIJINI DAR ES SALAAM

December 17, 2017

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), akizungumza na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia katika mkutano wa pamoja uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Pugu Poverty Alleviation and Development Agency (PPADA), Abraham Silumbu, akitoa taarifa ya utafiti walioufanya katika Soko la Tandale na Magomeni.
 Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
 Ofisa Ufutiliaji na Tathmini wa Shirika la Eguality for Growth (EfG), Shabani Lulimbeye, akitoa mada kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wadau wakisikiliza mada 
 Mkurugenzi wa Shirika la Esscreative and Legal Foundation, Erick Mukiza akimuelekeza jambo Mwanasheria mwenzake, Mchala Hamisi kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Wodevota, Catherine Mhagama kutoka mkoani Ruvuma akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Nurget Development in Tanzania (NDT), Hemed Ngochele akichangia jambo. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania (Tamwa), Neema Bishubo.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi wa EfG, Susan Sita, akiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa Programu wa Shirika la Tanzania Network of Women, Kennedy Godwin akichangia jambo.

Na Dotto Mwaibale

Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali yameungana na Shirika la Equality for Growth (EfG) katika kukabiliana na ukatiti wa kijinsia masokoni dhidi ya wanawake.

Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa wadau kutoka katika mashirika hayo, Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi wa EfG, Susan Sita alisema shirika hilo liliona ni vizuri kupanua wigo wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni kwa kuyashirikisha mashirika mengine.

"Tuliona ni vizuri kuyashirikisha mashirika mengine katika mapambano haya ambapo mashirika 40 kutoka Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni yalikubali kati ya hayo manne yameanza kufanya kazi hiyo rasmi kwenye masoko ya Magomeni na Tandale wilayani Kinondoni," alisema Sita.

Aliongeza kuwa, mkutano huo malengo yake ni kuelezea mradi wa mfano kwa wadau na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuaya la utoaji haki ili kupanua wigo wa utoaji wa taarifa juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye masoko.

Alitaja malengo mengine ni kuona mashirika mengine yanavyoweza kutumia mradi wa mfano wa sokoni na kuusambaza katika masoko mengine Tanzania ikiwa ni pamoja na kuandaa mikakati ya pamoja na namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Jane Magigita alisema ushirikishaji wa mashirika hayo ulianza mwaka 2015 na kazi kubwa ya mashirika hayo ni kuwakomboa wanawake masokoni kwa kupinga ukatili wa kijinsia.

Alitaja kazi nyingine ni kuboresha uhusiano kati ya wanawake wafanyabiashara na maofisa wa masoko katika kujenga uwajibikaji pamoja na kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wanafanya shughuli zao kwenye mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kiuchumi, kimwili, matusi na  kisiasa huku wakipewa heshima kama binadamu wengine na kujipatia kipato chao bila ya vikwazo.

"Tunahitaji kuona tunafanikisha ushirikiano kati ya watekeleza sheria, kamati za masoko, viongozi na maofisa wa Manispaa,  Polisi na wafanyabiashara wote katika kudhibiti ukatili wa wanawake katika masoko," alisema Magigita.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Pugu Poverty Alleviation and Development Agency (PPADA), Abraham Silumbu alisema ushirikiano huo umewapa mori wa kazi kwani utasaidia kupunguza vitendo hivyo vya kikatili masokoni nchini.

"Kwa kweli tumeanza kuona matunda ya ushirikiano huu tumepanga mapambano haya kuyapeleka katika masoko yote hapa nchini," alisema Silumbu. 


Tigo Yatoa Mamilioni kwa Washindi wa Promosheni ya Msimu wa Sikukuu

December 17, 2017



Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza na baadhi ya washindi wa  promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo wateja 11 wamejishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 44 wakijishindia zawadi za kila siku za shilingi 500,000  kila mmoja. Pamoja na zawadi hizo za kila siku, zawadi kubwa katika promosheni hiyo inayoendelea ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5. 

Baadhi ya washindi wa  promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' wakimsikiliza Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia zawadi za kila siku za kati ya shilingi laki tano na shilingi milioni moja katika promosheni hiyo inayoendelea ambapo pamoja na zawadi za kila sikiu, zawadi kubwa zinazoshindaniwa ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5. 

Mmoja wa washindi wa promosheni inayoendelea ya  'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' akizungumza na waandishi wa habari. Wateja wa Tigo wanaofanya miamala  kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa

Mmoja wa washindi wa promosheni inayoendelea ya  'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Rehema Juma Ramadhani, mkaazi wa Pugu Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia donge nono katika promosehni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaofanya miamala  kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa. 

  • Wateja 20 wapokea zawadi kemkem za pesa kwa kufanya miamala kupitia Tigo Pesa


Dar es Salaam, 8 Novemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa leo imewatangaza na kuwazawadia washindi 20 wa promosheni yake ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’ inayoendelea katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka mpya ambapo wateja wanajishindia mamilioni ya pesa.


Washindi wanne (4) wamepata bahatiya kushinda zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 16 wakijaza mifuko yao na donge nono la shilingi laki tano (TZS 500,000) kila mmoja.  each. Jumla ya shilingi milioni 12 zimetolewa kama zawadi kwa wiki  hii.


Washindi wa zawadi za TZS 1 milioni ni wafanyabiashara Neema Fredrick Mosha, Fredrick Joseli Mponzi , Sefu Athumani Sefu na Hadija Mohamed Lukulumbale ambaye ni mama nitilie.


Washindi  wa zawadi za TZS 500,000 ni Michael Joseph Moshi, Moses Muhonga Amuli, Saidi Khatib Kiko, Sylvester Michael Madaga, Aziza Ramadhani Ngozi, Evelyne Gwamaka Mwakyembe, Tumsifu Harold Temu na Sikudhani Constantine Mwenda. Wengine walioshinda TZS 500,000 ni Queentina Msafiri Mbwambo, Hilary Andrew Massawe, Ashura Ally Salim, Halima Saidi Shaabani, Fatuma Ally Makumbo, Halima Saidi Sangiwa, Jenifer Samuel Apolinale na James John Mkanula.


‘Tunatarajia kupata jumla ya washindi 153 katika kipindi cha mwezi mmoja wa promosheni hii. Bado tuna zawadi za thamani ya TZS 108 milioni kutoa kwa washindi 133,’ Meneja wa Wateja wa Tigo, Mary Rutta alisema wakati akikabidi zawadi kwa washindi Dar es Salaam leo.


Alibainisha kuwa pamoja na zawadi za kila siku, promosheni hiyo ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde,’  itakuwa na zawadi kubwa za mwezi  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni.


‘Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa ambao wanahitaji kutumia huduma ya Tigo Pesa kwenye simu zao ili kupata nafasi ya kushinda. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda,’ alisema.

Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

DK. KIGWANGALLA AFUNGA MAFUNZO YA 15 YA JESHI USU KWA MAAFISA WANYAMAPORI WA TAWA, TANAPA NA NGORONGORO MKOANI KATAVI

December 17, 2017

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaongoza Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kupiga gwaride la ukakamavu muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi. 

Na Hamza Temba-  Mlele, Katavi
...........................................................................

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wahifadhi wote nchini kushirikiana na wadau wengine hasa mamlaka za Mikoa na Wilaya katika maeneo yenye uvamizi wa mifugo na migogoro ya mipaka ya hifadhi ili kutatua changamoto hizo kwa namna shirikishi ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo jana Disemba, 16, 2017 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya 15 ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

“Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tutaiendeleza, Falsafa yetu ni kuwashirikisha wadau wote, kama kuna taasisi za kiraia kwenye eneo lako la kazi, taasisi za kijamii, mamlaka za mikoa na wilaya, wananchi, halmashauri husika mshirikiane nao ili kupunguza madhara ya operesheni zetu, na zoezi hili la uhifadhi liwe endelevu,” alisema Dk. Kigwangalla.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.

Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.

Alisema katika kuelekea mfumo huo, Jeshi hilo litakuwa moja bila kubagua taasisi yeyote ambayo ipo chini ya Wizara yake. “Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 inampa Waziri mamlaka ya kuunda Jeshi Usu, haikusema jeshi la TAWA, TFS, TANAPA au NGORONGORO na kwa vile hili jeshi ni langu nataka liwe moja, na tunakimbiza mchakato huu kwa haraka ukamilike kwa mujibu wa Sheria.

“Tunafarajika Mhe. Rais ameshaunga mkono na ameshatupa maelekezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi naye ameshasaini, ni sisi sasa tuendelee kujipanga vizuri ndani ya wizara, tuanze kuishi kwenye mfumo huo, kuanzia kwenye sare, uratibu wa mafunzo, uongozi na mfumo wa utawala,” alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema mfumo huo wa Jeshi Usu utakuwa na mnyororo mmoja wa mamlaka (chain of comand) na kwamba utahusisha taasisi zote za uhifadhi zilizopo chini ya wizara yake kwenye sekta ya wanyamapori, misitu na mali kale. “Sijawaona watu wa misitu hapa au mambo ya kale, wote hawa ni ni muhimu, rasilimali za mali kale nazo ni muhimu sana kulindwa kwani zikiharibika hazitengenezeki tena” alisema.

Katika hatua nyingine amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa mafunzo yote ya Jeshi Usu ambayo yanaendelea katika kituo cha Mlele, Mkoani Katavi yanaratibiwa moja kwa moja na Wizara tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo uratibu unafanywa na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Akizungumzia mafanikio ya vita dhidi ya ujangili na matunda ya mafunzo hayo alisema, “Katika siku za hivi karibuni tumepiga hatua kubwa ya kupambana na ujangili hasa wa tembo, Kwa dhati napongeza jitihada zinazofanywa na zinazoendelea kufanywa na wahifadhi, maaskari watumishi wengine na wadau wetu wote kwa ujumla ambazo zimeimarisha hali ya uhifadhi wa maliasili zetu”. 

Alisema kwa kiasi kikubwa matukio ya ujangili yamepungua na kwamba nyara nyingi zinazokamatwa katika kipindi hiki ni za zamani ambazo zilikuwa zimefichwa na majangili kwa ajili ya kuzitafutia masoko au kukimbia mikono ya sheria.

Alisema Wizara yake itaendelea kutumia mbinu za kisasa za kiitelijensia za kukabiliana na ujangili ikiwemo kutumia ndege zisizo na rubani kwa ajili ya doria na kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano ambayo haitaweza kuingiliwa na majangili au watu wengine wenye nia ovu na uhifadhi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Dk. Nebo Mwina akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa mafunzo hayo ya Jeshi Usu, aliwataka kuishi kwenye viapo vyao kwa kudumu katika ukakamavu, uhifadhi, maadili mema na nidhamu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Dk. James Wakibara aliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyopewa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali, kujiepusha na rushwa na kudhibiti vitendo vya ujangili.

Mhifadhi Gloria Bidebeli kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA akisoma risala ya wahitimu hao alisema mafunzo hayo yatawawezesha kuboresha ufanisi wa shughuli za uhifadhi kwa kutii amri na kutekeleza maagizo kwa wakati.

Mafunzo hayo ya wiki nne ambayo yalianza Novemba, 20 mwaka huu yalihusisha Mameneja wa Mapori ya Akiba na Tengefu 20, Wakuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili wanane, Maafisa Wanyamapori 29 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Wahifadhi Wanyamapori watano kutoka TANAPA na Wahifadhi Wanyamapori 26 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Mafunzo hayo yalihusisha matumizi sahihi ya silaha, mbinu mbalimbali za kupambana na uhalifu, huduma ya kwanza, ukakamavu, sheria mbalimbali zinazosimamia maliasili, ukamataji na upekuzi wa wahalifu na jinsi ya kuwafungulia hati za mashtaka.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MT. PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA LEO

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MT. PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA LEO

December 17, 2017
d (1)
:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana na Mapadri baada ya ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (2)
Kwaya ikitumbuza wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (3)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (4) d (5) d (6)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (7)
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiwa na waumini wengine kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (8)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (9) d (10)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (11) d (12)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (13) d (14) d (15) d (16)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  waumini baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Matakatifu Paulo wa Msalaba la Jimbo Kuu la Katoliki la Dodoma leo Desemba 17, 2017
d (17) d (18) d (19) d (20)

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM (NEC) MJINI DODOMA

December 17, 2017

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman  Kinana pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiimba mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi  (White House) mjini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim akiwaaga wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) mara baada ya kumaliza muda wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye amemaliza muda wake Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim. Picha na IKULU