MBUNGE SALIM AWAPA TAHADHARI WANAOZIMEZEA MATE FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

January 17, 2023
















“Hamtazila kizembe”


Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham amesema hatamfumbia macho mtu yoyote atakekuwa kikwazo cha kukwamisha mradi wowote unaosimamiwa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.


Mbunge salim ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa shule ya sekondari mwaya kata ya Ruaha kwa lengo la kuwaomba wananchi kujitolea kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ili iweze kukamilika kwa wakati na ianze kutoa huduma.


Mbunge Salim pia amesema kwa mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Rais Dkt.Samia Sulluhu Hassan jimbo la Ulanga limepata kiasi cha shilingi Milioni themanini na tisa laki moja na arobaini elfu kama fedha za mfuko wa jimbo (89,140,000/=) ikiwa ni fedha nyingi kupatiwa tangu aingie madarakani.


Mbunge salim amesema kiasi cha Mil 50 amekielekeza kukamilisha bweni la wasichana  Shule ya sekondari mwaya kata ya ruaha kwa lengo la kupunguza mimba za utotoni na kuinua kiwango cha elimu katika jimbo la Ulanga.


Aidha Mbunge Salim amemtaka mhandisi wa halmashauri hiyo ndugu Amir Athumani kuhakikisha wanazitumia vyema fedha hizo na zinakamilisha mradi huo wa bweni kwa wakati bila kikwazo chochote ili watoto wa kike waanze kulitumia.


Mbali na mkutano huo mbuge salim pia amefanya ziara ya kukagua miradi yote iliyopata fedha za mfuko wa jimbo kwa mwaka 2021/22 ili kujiridhisha kama fedha hizo zimefanya kazi vyema kama ilivyoelekezwa na kamati ya mfuko wa jimbo katika vikao vyao.


Mbunge salim amemshukru Rais Dkt Samia sulluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka wilaya ya Ulanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya,elimu,miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo.

MABONDIA ZAIDI YA 20 KUPANDA ULINGONI JANUARI 18 NA 28 JIJINI TANGA KUONYESHANA UMWAMBA

January 17, 2023

 



MASHABIKI wa ngumi mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushuhudia pambano la ngumi la kufungua mwaka 2023 wakati w mabondia Mustafa Doto kutoka Dar es Salaam atakapopambana na Said Mundi kutoka Tanga katika mnyukano wa round 10 kesho Januari 18, 2023. 


Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa leo, Promota maarufu  nchini, Ali Mwazoa na ambaye pia mtayarishaji wa pambano hilo alieleza kutakuwa na mengine ya utangulizi  9.


Mapambano hayo yatakuwa kati ya Jay Jay atakayepambana na Peter Julius wakati Jonas Mtafya atapigana na Patrick Kimweri.  Wengne ni Hamis Mwambashi dhdi ya Haji Juma, wote kutoka Tanga.


Mtoto wa bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla, Snake Junior atapambana na Ali Reli wote kutoka  Tanga..


Haya ni mapambano ya utangulizi kwa ajili ya mabondia chipukizi kuelekea pambano kubwa la aina yake mkoani na nchini Tanzania kati ya mabondia wawili wanaogopwa, Ibrahim Classic atakayemkabili bondia mwenye mikwara na ngumi nzito, Ndondande Harmer, wa nchini Zimbabwe. Pambano hilo litakuwa la round 10.


Promota Mwazoa alitoa wito kwa mashabiki wa jijini Tanga na nje ya  mkoa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mabambano hayo mawili yatakayofanyika 18 na 28 Januari ambayo yatautangaza mkoa katika fursa za biashara na ajira.


Pia Mwazoa aliahidi kuandaa mapambano mengine ya ngumi ambayo yatatoa zaidi fursa kwa vijana wanaochipukia katika ulingo wa michezo ya ngumi nchini.