YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO NOVEMBA 10,2017

November 10, 2017

 Wabunge wakiwa wamesimama wakati wa dua ya kuiombea nchi na bunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Capt(Mst) George Mkuchika akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati  wa Mkutano wa Tisa wa kikao cha nne cha Bunge hilo leo Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe.Stanslaus Nyongo akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati Mhe.Subira Mgalu akitoa maelezo ya maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Dk.Mary Mwanjelwa akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO UGANDA, PIA AZUNGUMZA NA WANAHABARI MBALIMBALI MASAKA NCHINI UGANDA

November 10, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watanzania waishio nchini Uganda katika eneo la Masaka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakizungumza na wanahabari mara baada kumaliza ya kufanya mazungumzo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha umahiri wa kupiga ngoma pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika eneo la Kyotera nchini Uganda. PICHA NA IKULU
 RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA MASAKA NCHINI UGANDA

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA MASAKA NCHINI UGANDA

November 10, 2017

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
4
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la mkutano baina ya wajumbe wa nchi mbili za Tanzania na Uganda katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja aliombatana nao katika Mazungumzo na ujumbe wa Uganda uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa pamoja na ujumbe wa Uganda.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za Asili cha Cranes Performance mara baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
10
Kikundi Cranes performance kikitumbuiza katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Masaka Uganda.
PICHA NA IKULU

MHISPANIA AWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA BAISKELI

November 10, 2017
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) walipofika katika kituo cha kupumziki cha Horombo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiendesha baiskeli katika eneo la Saddle wakati wa kuekelea kituo cha Kibo .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akikokota baiskeli yake  katika eneo lenye mawe wakati akiekelea kituo cha Kibo 
Muongoza Watalii,Ally Chuwa akitoa msaada wa kufunga viatu kwa Ramon Abecia wakati akielekea kituo cha Kibo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli  ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto)  na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MPANDA milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Shelutete anaeleza namna ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa mstari wa mbele katika kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.
Kwa upande wake Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayowakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila mara.
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.
Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa wageni watakaofanya aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake kwa kuwa na taahadhari sambamba na waongoza wageni waliobobea katika kazi ya Utalii.

PROMOSHENI YA NUNUA NA USHINDE YAFIKIA TAMATI KWA KUTOA ZAWADI KWA WASHINIDI WA TIGO-MASASI MTWARA

November 10, 2017


    
Meneja  Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo  akitoa maelezo kwa mteja wa Simu aina ya Tecno R6 kwa Faraji Said Lembe Mkazi wa Masasi katika Duka la Huduma kwa Wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara Simu ya Tecno R6 inauzwa shilingi laki moja na tisini na Tano kama Promotion.

Meneja  Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo  akikabidhi simu aina ya Tecno S1 kwa mteja Faraji said Lembe mara baada ya kupata maelezo katika Duka la Huduma kwa wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara.
Meneja  Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo  Akikabidhi Kofia Ngumu na Funguo ya pikipiki kwa mshindi wa shindano la Nunua Ushinde Saudi Chimatilo Mkazi wa Chiungutwa,Masasi Mkaoni Mtwara Shindano hilo ni kwa wanunuzi wa Sim aina ya Tecno R6 na Tecno S1 ambapo washindi walikabidhiwa Seti za Television pamja na Pikipiki.

WCS WAIPIGA MSASA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAGA

November 10, 2017
 Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuzitunza rasilimali za wanyama pori kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo kama wao walivyotunziwa na wananchi waliokuwepo miaka ya huko nyuma
Mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii katika shirika lisilo la kiserikali (WCS) Anna Kimambo alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha jamii zinasimamia vilivyo rasilimali za wanyama pori,misiti na vyanzo vya maji ili baadae weweze kuona faida ya vitu wanavyo vitunza.


Na Fredy Mgunda,Mbalali

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifandhi shirikishi wa wanayama pori (WCS) limeipiga msasa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawalinda wanyama pori na kunufaika na uwepo wa wanyama pori hao.
 
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuyatumia vizuri mafunzo waliyopata kulinda rasilimali za wanyama pori.

“Nawaombeni tumieni vizuri mafunzo haya kwa kuwa yatawasidia katika swala zima la uhifadhi ambalo ndio jukumu lenu la kwanza kabla hamjaangalia nini mnapata kama faida kwa kufanya hivyo WAGA itakuja kuwa jumuiya kubwa sana” alisema William

William aliwaomba jumuiya hiyo kutojihusisha na ujangili kwa kuwa wanaelimu ya uhifadhi na kuhakikisha wanyama pori wanalindwa kwa faida za taifa.

“Kuna jumuiya nyingi zimekuwa na migogoro kutokana na baadhi ya wajumbe kujihusisha na ujangili na kusababisha wanyamapori wengi kukimbia katika maeneneo ya hifadhi na kuwapunguzia kipato kwa wanajumiya hivyo nendeni mkatoe elimu kwa wananchi wengine kwa kuwa nyinyi mshapata elimu hiyo” alisema William

Aidha William alisema kuwa jumuiya ya WAGA bado ni changa hivyo wanatakiwa kuheshimu utawala bora ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa kunufaika na pori ambalo serikali imewapatia kwa ajili ya kufanya maendeleo ya vijiji.

“Najua kuwa mmeenda kujifunza kwenye jumuiya nyingine na mmeona kuna jumuiya zinamigogoro mingi hadi serikali huwa inaingilia kati na kuna jumuiya ambazo zinaendeshwa kwa kufuata utawala bora hivyo nawaomba mjifunze kufanya kazi kwa kufuata utawala bora” alisema William