DED MNASI: AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA HALMASHAURI YA ILEJE MKOANI SONGWE

August 13, 2017
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Haji Mnasi akiwa anakagua mradi wa mfereji mkubwa wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na wananchi wakati wa ukaguzi.
Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.


Na fredy Mgunda, Ileje

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Leo amefanya ziara ya kushitukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ila ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015 kwenda 2020 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi  wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6  wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawanugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

"Mradi huu ni mkubwa sana naomba wananchi wautumie vizuri na kuutunza kwa kuwa unamanufaa ya muda mrefu kutokana na ujenzi wake kuwa mkubwa na wagharama kubwa na unaubora unaokidhi vigezo vyote kuwa mradi wa kutumu"alisema Mnasi

Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mreji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo wa halmashauri ya wilaya ya Ileje.

"Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wametegemea Kilimo katika kuendesha maisha yao hivyo uwepo wa mradi huu utakuwa na tija ya kimaendeleo kwa wakulima na wafanyabiasha mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika halmashauri hii" alisema Mnasi

Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yako.

"Wananchi wangu itumieni vizuri fulsa hii kuleta maendeleo katika halmashauri hii sihitaji kusikia malumbano yoyote juu ya matumizi ya mradi huu wa umwagiliaji ambao unatija sana kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla"alisema Mnasi

Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo ,alimwagiza mtendaji wa kata mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

"Unajua huu mfereji utaongeza ajira kutokana na Kilimo kinacholimwa katika wilaya hii hivyo ni lazima wananchi kuutunza na kuuthamini mradi huu" alisema mkude

Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo mlipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

"Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

WILAYA YA NEWALA INAHITAJI TEKNOLOJIA YA KISASA KUINUA KILIMO

August 13, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Mtafiti, Bestina Daniel kutoka COSTECH na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama. 
MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE

MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE

August 13, 2017
DSC_0026
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akiongea jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, baada ya mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaan Leo.
DSC_0034
Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0043
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0047
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
DSC_0052
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland  akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.
DSC_0060
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. AshaRose Migiro baada ya kumaliza mazungumzo yaliyoohusu masuala ya mazingira.
………………………………………………………………..
Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland  amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.
Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa  kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.
Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika oparasheni zake za viwandani, na Balozi Migiro; Mpina alisema kuwa  viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam Mpina lisema mfumo wa majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.
Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Uingerea  Mhe. Asharose Migiro akitolea mfano wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya ufukwe ya ocean road ambayo imelika, alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonyesha ushirikiano katika suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Amefanya mazungumzo hayo leo na Naibu waziri Mpina na Team ya wataalam baada ya kutembelea kisiwa cha Zanzibar.

MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA AKAGUA BARABARA YA MAKOKA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI MMOJAMMOJA

August 13, 2017
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Mmoja wa Madereva wa Daladala ambao ufanya safari zao kituo cha River Side kwenda Makoka mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo 

  Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, akizungumza na Dereva wa Bodaboda katika barabara ya Riverside Makoka mara baada ya kukagua barabara hiyo iliyochongwa kwa fedha za Mfuko wa jimbo
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na  Wakazi wa eneo la Ubungo Makoka mara alipo fika katika kituo cha Daladala eneo la Riverside kupata maoni yao nini kifanyike kuboresha barabara hiyo hili iweze kupitika muda wote 
Mjumbe wa shina Makoka Phinias  akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea  juu ya barabara ya Makoka River side   mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo