Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ashauri wajumbe kufanya kazi kwa ushirikiano

Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ashauri wajumbe kufanya kazi kwa ushirikiano

December 04, 2014


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi Mwenye suti ya Bluu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mikutano mjini Mpanda muda mfupi baada ya kutoka kwenye Kikao  cha Tano cha Bodi ya  Barabara kilichofanyika leo mjini Mpanda. unnamed4 
Wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi wakifuatilia mjadala wa kikao hicho mbele ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomhn Chang’ah mwenye suti ya kahawia na Selemani Lukanga Mkurugenzi wa Mji Mpanda. unnamed5Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye kikao cha bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi.
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi
Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt Ibrahim Msengi ameshauri wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha barabara za Mkoa huo zinajengwa kwa kiwangokinachokubaliki kuliko kukaa kinywa kusubiria hadi kikao kiitishwe ndiyo waseme mapungufu yaliyojitokeza.
Dkt Msengi alitoa kauli hiyo wakati akifungua Kikao cha tano cha Bodi ya Barabarakilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mji Mpanda Mkoani Katavi na kuzungumzia changamoto mablimbali zinazoikabili sekta ya miundo mbinu Mkoani humo hasa sekta ya Barabara.
Alisema kikao cha Bodi ni cha kisheria hivyo Wajumbe wake wanawajibu na jukumu la kusimamia na kufuatilia kazi zote zinazofanyika katika Mkoa kwa kufuata taratibu zinazotakiwa bila kuingilia mchakato mingine ya kisheria kama mambo ya zabuni na masuala ya Kifedha lakini kubwa zaidi ni ushirikiano wa karibu miongoni mwao taasisi nyingine kwa kuwa kila kitu kinahitaji ushirikiano na mawasiliano ya karibu.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema haitakuwa busara barabara zinajengwa chini ya kiwango na wajumbe wa bodi wapo waaona na kuacha kushauri hadi  kazi inakamilika ndipo wanaanza kuhojii wakati ungeweza kusimamia mapema na kusaidia kuondoa kasoro hizo kwa kutoa ushauri mapema.
Akashauri kuwa ni vyema ufuatiliaji uwepo tangu mwanzo ili kuhakikisha taratibu zote zinafuatiliwa kwa kufuata utaratibu na sheria na kuona  barabara kama zinajengwa kwa wakati,akaeleza kuwa hiyo ni moja ya kazi ya bodi ya barabara.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo alieleza  Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi ilizinduliwa mwaka 2012 wakati linazinduliwa Mkoa ulikwa na mtandoa wa barabara  zinazohudumiwa  zikiwa katika hali mbaya lakini bodi imefanya jitihada mbalimbali na   kazi mbalimbali  zimeendelea kufanyika chini ya uongozi wa Bodi hii.
AIisema kazi mbalimbali zimefanyika na zinaendelea kufanyika akataja  barabara ya Mpanda – Uvinza,iko katika hali ya usanifu pia barabara ya Mpanda – Ugalla hadi Kaliua undyankulu Kahama, Mpanda –Inyonga, shughuli zinaendelea katika kuhakikisha Mkoa unafunguka.
Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara na Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye amehamia Mkoa wa Tanga Dkt Rajabu Rutengwe akimkaribisha Mwenyeiti Mpaya wa Bodi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa mpya wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi ni moja ya Mkoa ambao uko nyuma kwa maendeleo ya Barabara za lami nchini hadi wakati unaanzishwa mwaka 2012 ulikuwa na kilometa (2)mbili za lami tofauti na maeneo mengine nchini lakini sasa unamtandao wa barabara za lami kilometa 34 hayo ni maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili tu juhudi zimefanyika.
Amesema Mkoa una sura ya Samaki ya Pweza ili uende sehemu nyingine kutoka makao makuu ya mkoa lazima uende moja kwa moja halafu lazima urudi ulikoanzia safari  hivyo ameshauri wajumbe wa bodi ya Barabara na wananchi kwa ujumla kutoaushirikiano wa karibu kwa Mkuu wa Mkoa Mpya kama waliompatia wakati yeye alipokuwa mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa Bodi ya Barabara hivyo na mwenzake apewe ushirikianokam aliokuwa akipewa ilikuleta maendeleo katika Mkoa huo.

MBUNGE WA CHALINZE ATOA WITO KWA MAKAMBUNI YA MAWASILIANO KUSAMBAZA HUDUMA KWA WATEJA WAKE

December 04, 2014

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,(kulia)Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wapili kutoka kulia ,akigonganisha glasi za mvinyo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania ikiwa ni ishara ya kusherehekea uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo alilolizindua lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto)akimfafanulia jambo Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofika kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kulia kwa Mheshimiwa ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa wa Pwani.
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wanne toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Chalinze mjini Mkoani humo.

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani  Mh. Ridhiwani Kikwete,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano  kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo  Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya Ruvu,Miono,Gwata  wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imefungua duka jipya  katika  eneo la Chalinze.

Chalinze  ni moja ya kituo maarufu katika  mkoa wa Pwani ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Chalinze na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa  mballimbali na nje ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard   wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka  85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa pwani
MBUNIFU WA MAVAZI SHERIA NGOWI AKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA

MBUNIFU WA MAVAZI SHERIA NGOWI AKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA

December 04, 2014

1
WaziriMkuu, MizengoPinda akisalimiana na Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi alipotembelewa jana nyumbani kwake Masaki jijini Dar esSalaam. (Picha Zote: AtuzaNkurlu-SheriaNgowi Brand).
2
Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi akimuonesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baadhi ya vitambaa vya kisasa vya suti ambavyo vitatuka Kumtengenezea Waziri Mkuu jana jijini Dar es Salaam.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia na kuchagua aina ya vitambaa vya suti amabvyo vitatumika kutengenza baadhi ya Suti Zake alipotembelewa na Mbunifu wa Kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi jana jijini Dar es Salaam.(Picha Zote: Atuza Nkurlu-Sheria Ngowi Brand).
Forum CC yakabidhi mapendekezo ya Asasi za kiraia kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi

Forum CC yakabidhi mapendekezo ya Asasi za kiraia kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi

December 04, 2014

IMG_6881
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Sanato Mhenge (kusshoto) akipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi wa Forum CC Euster Kibona ofisini kwake jijini Dar es salaam.
IMG_6880
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Naibu wake Ummy Ali Mwalimu wakimsikiliza meneja mwezeshaji wa Taasisi ya Forum CC Rebeca Muna wakati wakipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa kimataifa wa Tabia Nchi unaoendelea kufanyika Lima nchini Peru.
IMG_6883

Ujumbe wa Forum CC ukiongozwa na meneja mwezeshaji wake Rebeca Muna( kushoto), katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Binilith Mahenge(wapili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wake Ummy Mwalimu(katikati), pamoja na mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster Kibona (wa pili kutoka kulia) na ofisa maendeleo wa Forum CC Adam Anthony. wakati wa makabidhiano ya mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano mkuu wa kimataifa wa TabiaNchi.
Akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya waziri mwenye dhamana na Mazingira Mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema serikali inapaswa kubainisha mapendekezo ya kupunguza makali ya uharibifu wa mazingira kwa nchi zilizoendelea. Pia nchi zilizoendelea zikubali kuwepo na makubaliano ya kisheria na kuheshimu kanuni juu ya masuala yote ya mazingira.
Kibona ametoa wito kwa viongozi wa dunia na Afrika kuwashirikisha wadau wengine katika mchakato wa mikataba ya kimataifa ili kupunguza manung’uniko ya kutoshirikishwa kwa wadau. Pia amesema nchi zilizoendelea zinapaswa kutoa fedha ,teknolojia na kujenga uwezo juu ya kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira.
Saudia yasaidia kuboresha huduma za jamii nchini.

Saudia yasaidia kuboresha huduma za jamii nchini.

December 04, 2014

unnamed 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas. unnamed3Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
…………………………………………………………………….
Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imesainiana mkataba wa mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 45.21 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.
Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas
Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.
Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.
Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.