Mfalme Mohammed
VI wa Morocco akishuka kwenye ndege iliyomleta akiwa ameongozana na
ujumbe wake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es salaam leo Oktoba
23, 2016
Mfalme huyo
amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Dk. John Pombe Magufuli jioni hii, Mfalme Mohammed VI atakuwa nchini
kwa ziara rasmi ya siku tatu.
(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA leo jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili
kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam jioni hii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akielekea karibu na ndege iliyomleta mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam.
Mfalme Mohammed VI wa Morocco
akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis
Mwamunyange akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.