AZAM BINGWA LIGI KUU, YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE

April 13, 2014

Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya
AZAM FC ndiye bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine mjini hapa, huku waliokuwa wapinzani wao katika mbio za taji hilo, Yanga SC wakishinda 2-1 dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha leo. 
Azam imefikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote baada ya mechi za mwisho Aprili 19, mwaka huu.
Gaudence Mwaikimba akishangilia baada ya kuifungia Azam bao la kwanza, Kulia ni Kipre Tchetche

Yanga SC yenye pointi 55 sasa ikiifunga Simba SC Aprili wiki ijayo itafikisha 58.
Mabao ya Azam leo yamefungwa na Gaudence Mwaikimba na John Bocco, wakati la Mbeya City limefungwa na Mwagane Yeya. 
Mchezo ulikuwa mkali na ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu, na sifa ziwaendee makipa wa timu zote mbili, David Burhan wa Mbeya City na Aishi Manula wa Azam FC kwa kazi nzuri ya kuokoa hatari langoni mwao.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 43, mfungaji Gaudence Mwakimba aliyemalizia pasi nzuri ya beki wa kulia Erasto Nyoni.
Baada ya bao hilo, Mbeya City walicharuka na kufanya mashambulizi mawili hatari langoni mwa Azam, lakini hawakuweza kupata bao hadi kipyenga cha kuhitimisha kipindi cha kwanza kinapulizwa.
Kipindi cha pili, Azam waliingia na mfumo wa kucheza kwa kujihami ili kulinda bao lao, mbele wakimuacha Mwaikimbe pekee na John Bocco akashuka katikati huku Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akimsaidia Kipre Balou kukaba kiungo cha chini.
Mfumo huo ulikabirisha mashambulizi mengi langoni mwa Azam na haikuwa ajabu Mbeya City walipokomboa bao dakika ya 70 kupitia kwa Mwagane Yeya baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa na kipa Aishi Manula kufuatia shuti la Deus Kaseke.
Bao hilo kidogo liliwachanganya Azam FC na Mbeya City wakauteka mchezo kwa dakika kadhaa, kabla ya shambulizi la kushitukiza kuipa ushindi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa dakika ya 86, baadaa ya John Bocco kukutana na mpira uliorudishwa.
Wachezaji wa Mbeya City walimzonga refa Nathan Lazaro wa Kilimanjaro baada ya bao hilo na kusababisha mchezo kusimama kwa zaidi ya dakika tatu.
Refa huyo alitoa kadi nyekundu kwa Mwagane Yeya baada ya vurugu hizo. Askari wa jeshi la Polisi walilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya mechi kwa kuwadhibiti mashabiki wa Mbeya City waliotaka kufanya vurugu na pia kuusindikiza msafara wa Azam FC.
Pamoja na kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wake leo, Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo
Azam inakuwa timu ya sita nje ya Simba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.
Kikosi cha Mbeya City leo kilikuwa; David Burhan, Aziz Sibo/Hamad Kibopile dk50, Hassan Mwasapili, Yussuf Abdallah, Yohana Morris, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga, Saad Kipanga/Alex Sethi dk68 na Deus Kaseke. 
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar, Gaudence Mwaikimba, John Bocco na Kipre Tchetche/Kevin Friday dk51.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Ashanti United imeilaza Simba SC 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la Mohamed Nampaka dakika ya 17, Yanga SC imeifunga JKT Oljoro 2-1 mabao yake yakifungwa na Rajab Zahir dakika ya 70 na Mrisho Ngassa dakika ya 73 huku la wenyeji likifungwa na Jacob Masawe dakika ya 68.
Bao pekee la Elias Maguri dakika ya 36 limeizamisha Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, wakati Mgambo JKT imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
BREAKING NEWS MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA SASA HIVI LIVE

BREAKING NEWS MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA SASA HIVI LIVE

April 13, 2014
Screen Shot 2014-04-13 at 5.10.14 PM
Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki Tanzania ambae aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata muziki aliokua anaufanya.
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili
zimesema Mzee huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13 2014 saa nane mchana baada ya kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo na taratibu za mazishi blogu ya wananchi itaendelea kuzitoa 
HABARI ZA KWANZA KUHUSU KOMBE LA KAGAME CUP KUFANYIKA DAR

HABARI ZA KWANZA KUHUSU KOMBE LA KAGAME CUP KUFANYIKA DAR

April 13, 2014

\

 

Dar es Salaam. Michuano ya Kombe la Kagame imepangwa kufanyika nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Juni huku Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) likiwa kwenye mazungumzo ya mwisho na wadhamini wa michuano hiyo.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye
alisema   jana kuwa kesho Jumatatu wanatarajia kumtangaza mdhamini wa michuano hiyo kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kumalizana naye.
“Tupo kwenye mazungumzo ya mwisho na wadhamini wetu, nakuja huko Dar es Salaam kumalizana na wadhamini wetu, kila kitu tutaweka wazi Jumatatu, ngoja kwanza tumalizane nao,”alisema Musonye.
Cecafa imekuwa ikihaha kusaka wadhamini wa kuandaa michuano hiyo, ambapo awali walitangaza itafanyika Rwanda, lakini Rwanda ikawatolea nje kubeba gharama hizo, ambapo Cecafa wameamua sasa michuano ifanyike kwenye ardhi ya Tanzania.
Habari ambazo gazeti limezipata zinasema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lipo tayari kuisaidia Cecafa kubeba michuano hiyo kwa kuziingiza timu nne za Tanzania bara ambazo ni Simba, Yanga, Azam, na Mbeya City.
“Michuano hiyo inagharimu dola za Marekani 600,000 (Dola 1= Sh 1,594.90) na Cecafa haina kitu, TFF imezishauri iingize timu nne za Tanzania bara kwa vile zina mashabiki kwani Mbeya City ikicheza na Yanga au Simba zote zina mashabiki hivyo zitaingiza fedha za kutosha kuendesha mashindano hayo,”alisema kiongozi mmoja ndani ya TFF.
Katika michuano ya mwaka jana ambayo ilifanyika Darfur, Sudan, timu ya Vital ‘O’ ya Burundi ilinyakua ubingwa huku timu za Tanzania zikiwa zimejitoa.
Hata hivyo, kutokana na ukata unaoikabili Cecafa imebidi ikubali timu za Tanzania, Simba na Yanga kushiriki kwani zilijitoa kwenye michuano hiyo mwaka jana kutokana na kuzuiwa na Serikali kwa kile kilichoelezwa kuwa hali ya usalama katika miji ya El- Fasher na Kadugli huko Darfur siyo nzuri na kuzikataza timu za Simba na Yanga kwenda kushiriki michuano hiyo inayodhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa jumla ya dola za Marekani 60,000.

SOURCE: MWANANCHI

*TBL YAZINDUA RASMI MASHINDANO YA CASTLE LAGER PERFECT 6, JIJINI DAR MSHINDI KUWASHUHUDIA BARCELONA LIVE CAMP NOU

April 13, 2014


Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindao ya Castle Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi jijini. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo.
Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika jana kwenye ufukwe wa Mbalamwezi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah.
************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Dar
Timu ya Soka ya Puyo chini ya Nahodha wake Majuto Omary jana jioni iliibuka kidedea katika mashindao ya Castle Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi jijini.

Mashindano hayo ambayo yalijumuisha timu sita za waandishi wa habari za Michezo yamezinduliwa juzi ambapo timu hiyo ya Puyo ambayo ilikuwa na wachezaji wengi wazee, imetinga moja kwa moja kwenye fainali za Taifa zitakazofanyika mwishoni mwa mwezi Julai.

Puyo ilinyakua zawadi ya Kombe na Medali kutoka kwa wadhamini wa mashindano ya hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle baada ya kuzisambaratisha timu za Xavi, Mess, Neymer na Masherano.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo alisema mashindano hayo yatashirika wachezaji wa baa mbali mbali ambao wanatumia kinywaji cha Castle na kwamba yataanza kwa ngazi ya baa, Kanda hadi Taifa ambapo timu sita zitapatikana na kuungana na ile ya Taswa ambapo zitacheza fainali na timu itakayoibuka kidedea katika shindano hilo la Perfect Six watapata fursa ya kutembelea uwanja wa Camp Nou na kujionea timu ya FC Barcelona ikicheza katika ziara ambayo itagharamiwa na Castle.

"Shindano hili litadumu kwa miezi mitano, litafanyika nchi nzima, ambapo timu mbali mbali katika Kanda saba zitasajiliwa na kucheza katika hatua ya mtoano kenye maeneo mbali mbali ambayo yatachaguliwa na kutangazwa mapema.

"Kila kanda itatoa timu moja na kufanya kuwa jumla ya timu saba ambazo zitawakilisha kanda hizo huku timu ya nane ikiwa ni Puyo ambayo inaundwa na waandishi wa habari, timu hizo zitachuana kwa mtoano kwenye robo fainali, nusu fainali na hatimaye fainali.

Naye Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah akifafanua zaidi alisema "Sio kwa wachezaji tu kutakuwa pia na droo maalum kwa wanywaji wa Castle na wateja wawili nao watapata fursa ya kwenda Hispania kujionea Barcelona inavyocheza  na pia kila wiki kuna zawadi ya Sh100,000 itatolewa kwa washindi sita.

Hata hivyo Fimbo alionya kuwa shindano hilo la Perfect Six halitawahusisha wachezaji wa zamani ambao wameshachezea timu mbali mbali za Ligi Kuu, na kwamba litahusisha wale tu ambao hawajawahi kucheza mpira kabisa katika ngazi yoyote inayotambulika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

BREAK NEWS !LINEX ATUA TANGA,SASA KUFANYA SHOW KALI LACASACHIKA LEO

April 13, 2014
MSANII WA MZIKI WA BONGOFLEVA HAPA NCHINI,SUNDAY MJEDA 'LINEX"AKIWA NA MAMA YAKE MARTIN AKA TIN DADY KUSHOTO  LEO MARA BAADA YA KUMTEMBELEA NYUMBANI KWAO MAGOMENI JIJINI TANGA.


HAPA LINEX ALIAMUA KUPIGA PICHA NA MTOTO BAADA YA KUPENDA KUZUNGUMZA NA MAMA YAKE TIN DADY LEO ENEO LA TANGASISI JIJINI TANGA.,PICHA ZOTE NA RAISA SAID.

MADRID YAIKONG'OTA ALMERIA 4-0 NA KUIVUKA BARCELONA

April 13, 2014



Real Madrid: Lopez, Nacho, Fabio Coentrao (Llorente 73), Illarramendi, Pepe, Varane, Modric, Isco, Benzema, Di Maria (Casemiro 64), Bale (Morata 70). Subs not used: Casillas, Casemiro, Morata, Vazquez Iglesias, Mascarell, Llorente, Da Silva.
Goals: Di Maria 28, Bale 53, Isco 56, Morata 85.

Almeria: Andres Suarez, Tomar Marcos, Jimenez Ortiz, Tebar, Martinez, Torsiglieri, Garcia Rabasco, Garcia Perez-Roldan (Soriano 72), Rios Lozano (Vidal Parreu 57), Sundy Zongo (Diaz Gonzalez 69), Rodrigues Barbosa. Subs not used: Silva Fernandez, Vidal Parreu, Diaz Gonzalez, Fernandez Saez, Soriano, Cuesta Diaz, Azeez.
Referee: Juan Martinez Munuera

Attendance: 65,896.




MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA VYUO VIKUU NA SEKONDARI HUKO DODOMA

April 13, 2014


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupokewa na Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rehema Nchimbi tarehe 11.4.2014.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwa shamrashamra za kwaya na matarumbeta wakati alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.