WAZIRI UMMY ATEMBELEA JENGO LA ZAHANATI MPINGI WILAYANI SONGEA VIJIJINI.

January 11, 2016
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao

Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya,  kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi



Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji

MAAMUZI YA KAMATI YA UENDESHAJI WA LIGI

MAAMUZI YA KAMATI YA UENDESHAJI WA LIGI

January 11, 2016
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi umeipa Polisi Dodoma ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mji Mkuu FC kumchezesha mchezaji Peter Ngowi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Desemba 26, 2015 mjini Dodoma.
Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mji Mkuu FC ilikuwa imeshinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.
Kamishna wa mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Polisi Tabora na Panone FC ya Moshi, Shabani Funyenge amesimamishwa kutokana na ripoti yake ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kuwa na upungufu.
Klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu yake kutoa kashfa na lugha za matusi wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Novemba 8, 2015 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Kaume jijini Dar es Salaam.
Pia imetakiwa kulipa kibendera cha kona (corner flag) pamoja ubao wa matangazo wa geti la kuingilia ndani kwenye Uwanja wa Karume ambavyo vilivunjwa na washabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi hiyo.
Mtunza vifaa wa timu ya Kimondo, Emily Nehemia, Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Idd Kibwana, Kiongozi wa Panone FC, Said watafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.
Mji Mkuu FC imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kutohudhuria kikao cha awali cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo kati yao na Polisi Dar es Salaam uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Klabu za Polisi Tabora na Panone FC kila moja imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) kugombania kuingia uwanjani kupitia mlango wa VIP badala ya ule wa kawaida kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Januari 2, 2016 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Wachezaji Ally Mwanyiro wa Rhino Rangers na Hamisi Shaban wa Lipuli wamepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kupiga wachezaji wa timu pinzani wakati wa mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kinyume na Kanuni ya 37(3) ya Ligi hiyo.
Pia Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya mshabiki wao kuingia uwanjani na kumvamia mwamuzi kwa madai maamuzi yake hayakuwa sahihi wakati wa mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Mbao FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

January 11, 2016
DSC_0063
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dkt. Rufaro Chatora
Taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini ni kama ifuatavyo; Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huu.
Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 04 hadi 10 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 615 walioripotiwa nchini kote na vifo vitatu (3). Mikoa ambayo bado imeripoti kuwa na ugonjwa huu ndani ya wiki moja iliyopita ni 11 kati ya 21 iliyokuwa imeripoti ugonjwa hapa nchini. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mikoa inayoongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wapya ndani ya wiki moja iliyopita ni pamoja na Morogoro (Manispaa ya Morogoro 87, Halmashauri ya Morogoro 66), ukifuatiwa na Arusha (Arusha Manispaa 50), Singida (Iramba 40) na Manispaa ya Dodoma ( 33).
Aidha, mikoa iliyokuwa na maambukizi lakini kwa muda wa wiki moja iliyopita hakukuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu ni pamoja na Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Lindi. Vile vile mkoa wa Dar es Salaam ambako ndiko ugonjwa ulianzia na kudumu kwa muda wa miezi minne (4) haujaripoti mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015.
Mikoa ambayo ilikwisha kuwa na ugonjwa huo lakini hapajakuwepo na wagonjwa wowote kwa muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa. Pia mikoa ambayo haijawahi kutoa taarifa ya ugonjwa wa kindupindu tangu mlipuko huu uanze hapa nchini ni Njombe, Ruvuma na Mtwara.
Bado Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea kusisitiza kuwa, ili kudhibiti ugonjwa huo na kuokoa vifo vinavyotokana na ugonjwa huu, wananchi wanasisitizwa kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka:-
-kabla na baada ya kula
- baada ya kutoka chooni
-baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia
-baada ya kumhudumia mgonjwa
Aidha, jamii inaaswa kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, maziwa na mabwawa.
Hivyo, Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja na watendaji wake kote nchini zinaagizwa kuendeleza juhudi za kuzuia kusambaa kwa mlipuko pamoja na kuchukua hatua stahiki za tahadhari kwa kusimamia utekelezaji wa yafuatayo:
*Ushirikishwaji wa viongozi ngazi mbali mbali, hasa ngazi za Halmashauri kwa kushirikisha madiwani na viongozi wa kata, vijiji, na mitaa.
*Mamlaka husika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama ikiwa ni pamoja na uwekaji wa dawa ya klorini kwenye maji na kupima usalama wa maji mara kwa mara.
*Upatikanaji wa dawa za kutibu maji (Water Guard, Aqua Tabs) katika maeneo ya mlipuko.
*Juhudi kubwa ziongezwe kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya vyoo bora kwa kila kaya.
*Uelimishwaji wa Baba na Mama Lishe, na wauzaji wengine wa vyakula kuhusu kanuni za afya.
*Kusimamia utekelezwaji wa Sheria ya Afya ya Mazingira na Sheria ndogo ndogo (By-Laws).
*Uhamasishaji wa Wananchi wanaopata ugonjwa kuwahi kutumia maji ya chumvi chumvi (ORS) na kuripoti mapema katika vituo vya huduma.
*Uboreshwaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Hitimisho
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inawashukuru wadau wote wanaoshirikiana na Serikali katika harakati za kupambana na ugonjwa huu. Aidha, Wizara inaipongeza mikoa ambayo ilikuwa na ugonjwa na sasa umetoweka au kupungua kwa kiasi kikubwa na pia kuikumbusha mikoa ambayo bado haijaathirika kuchukua hatua za tahadhari za kuzuia ili isipate mgonjwa yeyote wa Kipindupindu.

NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AZINDUA AIRTEL FURSA TUNAKUWEZESHA MSIMU WA PILI JJINI DAR ES SALAAM LEO

January 11, 2016
 Naibu Waziri  wa Kazi Vijana na Ajira, Athony Mavunde (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), na Mshauri wa mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, Mhandisi George Mulamula (kulia), wakiwa wameshika bango linaloonesha Airtel Fursa wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Airtel Fursa Tunakuwezesha uliozinduliwa leo Makao Makuu ya Artel Tanzania, Moroco  jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso, akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi.
 Mshauri wa mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, Mhandisi George Mulamula akizungumza kwa ufupi kuhusu mradi huo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha katika kipindi cha nusu mwaka na awamu ya pili.
 Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mjasiriamali Mohamed Kigumi aliyenufaika na mradi huo akielezea mafanikio aliyonayo na changamoto anazokumbana nazo baada ya kuwezeshwa na Airtel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Na Dotto Mwaibale

Kampuni ya simu ya mkononiya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha vijana ujulikanao kama "Airtel FURSA" kwa lengo kuendelea kudhihirisha kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini Mradi wa "Airtel FURSA" ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA"  umewawezesha vijana zaidi ya 2500 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa zaidi kwa jamii inayowazunguka.
 

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel  Sunil Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake  kuwawezesha vijana na kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania
 

" Mradi huu wa "Airtel FURSA"  unadhihirisha dhamira yetu ya kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA" umetoa matokeo mazuri sana na  tumefanikiwa  kugusa maisha ya  maelfu ya vijana wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,"
 

"Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani  shilingi  billion moja ili  kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za mkononi" alisema Colaso
 

Akizindua rasmi mradi wa "Airtel FURSA" Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha  na kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ili kuboresha maisha yao. alisema Mh Mavunde
 

"Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali, zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya"Airtel FURSA" ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:"
 

"Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza  uchumi wa nchi" aliongeza Mavunde"

Airtel FURSA"  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. 
Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. Or tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com<http://www.airtel.com>  naujaze fomu yako ya maombi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KIWIA AONDOA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA BAADA YA KUSHINDWA KULIPA GHARAMA ZA MAHAKAMA

January 11, 2016
Agrey Laban ambae ni Katibu wa Highness Kiwia akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Haighness Kiwia.

Katika kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka 2015 iliyofunguliwa Novemba 25 mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga ushindi wa mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kutokana na madai ambayo ni pamoja na kuendesha kampeni za ubaguzi wa kikabila sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Kesi hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa mwanasheria wake Paul Kipeja kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai ya kwamba mteja wake ameshindwa kulipia gharama za Mahakama ambazo ni Shilingi Milioni 10 na kwamba washtakiwa walikuwa ni Angelina Mabula pamoja na Mwanasheria wa Serikali ambapo gharama ya kufungua kesi hiyo kwa kila mlalamikiwa ilikuwa ni shilingi Milioni Tano.

Kufuatia ombi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Eugenia Gerald Rujwauka alitoa maamuzi ya kuifuta kesi hiyo kama ambavyo mlalamikaji alivyoomba.

Baada ya kesi hiyo kufutwa, Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea mlalamikiwa, amebainisha kuwa baada ya maamuzi hayo anatarajia kukutana na mteja wake ili kujadiliana hatua za kuchukua na huenda akafungua kesi ya madai dhidi ya Kiwia kutokana na kufungua kesi na kisha kuiondoa mwenyewe na hivyo kumuingiza mteja wake katika gharama zisizo za lazima.

Ifahamike kwamba Angelina Mabula pamoja na Highness Kiwia hawakuhudhuria Mahakamani hapo na hakukuwa na wafuasi wengi wa vyama vya siasa kama ilivyozoeleka ambapo nje ya Mahakama hiyo, Agrey Laban ambae ni Katibu wa Kiwia ameilalamikia Mahakama kutokana na kushindwa kupunguza gharama za kesi hiyo jambo ambalo limepelekea haki kupotea.

Wakati hali ikiwa hivyo, Kheri James ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula, amepongeza maamuzi ya kesi hiyo kufutwa na kuongeza kuwa hatua hiyo inatoa wigo wa mbunge huyo kuwatumikia wananchi.

Akiwa ofisini kwake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akapata fursa ya kuzungumzia Maamuzi ya Mahakama juu ya kesi hiyo ambapo amempongeza Mabula kwa uvumilivu wake kwa kuwa kiongozi akiwa na kesi Mahakamani anakosa uimara wa kuwatumikia wananchi.

Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana, Angelina Mabula (CCM) aliibuka mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kupata ushindi wa kura 85,425 na hivyo kumshinda mpinzani wake wakaribu kutoka Chadema Highness Kiwia aliekuwa akitetea jimbo hilo ambae alipata kura 61,679.
Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea  Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama
Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea  Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama
Katibu wa Mbunge wa Ilemela Kheri James (mwenye miwani) akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya Mahakama
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akieleza namna alivyopokea maamuzi ya Mahakama.

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI YASHTUSHWA NA KASI YA DAWASCO.

January 11, 2016
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) Mhakndisi Cypian Luhemeja akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Mbogo Mfutakamba ,wakielekea katika kikao cha Unongozi na wafanyakazi wa DAWASCO kilichofanyika makao makuu y a shirika hilo. 
Mkurugenzi wa Rasilimali watu w Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam,DAWASCO,Bi,Joy Chidosa akifanya utamburisho katika kikao hicho.
Baadhi ya Mameneja wa vitengo mbalimbali katika Shirika la Maji safi na Maji taka jijini Dar es Salaam DAWASCO ,wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasco wakionekana wenye nyuso za furaha wakati wa kikao hicho.
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliai Mhandisi ,Mbogo Mfutakamba.
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi kilicho fanyika makao makuu ya ofisi za Dawasco.
Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza na wafanyakazi wa DAWASCO wakati wa kikao kilichofanyika makao makuu ya shirika hilo .
Mwakilishi wa wafanyakazi wa DAWASCO,Abdalah Jongo akiongea kwa niaba yao wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO wakiliombea dua shirika hilo ili liweze kutimiza malengo yake ya kutoa huduma ya maji safi na maji taka kwa usalama kwa wakazi wa miji ya Dar es Salaam,Kibaha na Bagamoyo.


Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa jijini Dar es Salaam.(0755659929).

WIZARA ya maji na umwagiliaji, imesema inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mipango ya usambazaji wa huduma za maji, inayofanywa na shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) na kutoa rai kwa watumishi wa shirika hilo kushirikiana ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yalisemwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mbogo Futakamba, alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa DAWASCO, katika makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Futakamba, alisema kasi ya utoaji wa huduma bora za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, imepunguza malalamiko mengi ya wananchi, na kwamba serikali imeanza kupata matumaini makubwa na kujenga imani kwa shirika hilo kwa kufanikisha malengo makuu ya usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Aidha alisema kwa kiwango kikubwa wizara ya maji na umwagiliaji kwa sasa inajivunia kwa kazi nzuri iliyofanywa na shirika hilo, hasa kwa kuzingatia kuwa DAWASCO ndio jicho la wizara kutokana na wingi wa wananchi wanaohitaji huduma za maji zinazosambazwa na shirika hilo.

“Nimeona jitihada zenu, nimependa jinsi mnavyofanya kazi kama timu, naomba muwe na uaminifu mkubwa sana katika kazi, kuweni wawajibikaji ili wananchi wapate huduma ya maji”, alisema mhandisi Futakamba.

Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na shirika hilo za kupunguza kiwango cha upotevu wa maji pamoja na kudhibiti wizi wa maji, ambavyo vimekuwa kikwazo kinachochochea malalamiko ya wananchi kwa shirika hilo.

Awali akitoa taarifa ya shirika hilo, afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema shirika hilo limefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji, baada ya kuongeza uzalishaji kutoka mita za ujazo 7,834,234 hadi mita za ujazo 8,421,370 kati ya mwezi Mei hadi Novemba 2015.

Alizitaja sababu za mafanikio ya ongezeko la kiwango cha maji ni pamoja na udhibiti wa upotevu wa maji katika bomba kubwa, kufanya matengenezo ya tahadhari, maboresho ya maslahi ya wafanyakazi na kuboreshwa kwa kitengo cha upotevu wa maji.

Mhandisi Luhemeja alibainisha kuwa DAWASCO, imefanikiwa kufunga dira katika maungio ya maji, kuziba maeneo yanayovujisha maji kwa wakati, kupambana na wezi wa maji, kuhakiki ufanisi wa dira za maji, kusajili maboza ya wauzaji maji na kuboresha usomaji wa dira, ambavyo viliwezesha kupunguza kiwango cha maji yanayopotea kutoka asilimia 62 hadi 45, kati ya mwezi Mei mpaka Novemba 2015.

Aliongeza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya uboreshaji wa huduma za maji yaliwezesha shirika hilo la DAWASCO, kuongeza makusanyo ya mapato kutoka shilingi bilioni 2.9 hadi kufikia bilioni 6.2 kati ya mwezi Mei hadi Novemba 2015.

Wakati huo huo shirika hilo limeanza kutekeleza agizo la serikali linaloitaka DAWASCO, kuongeza idadi ya wateja wake hadi kufikia milioni moja, katika jiji la Dar es Salaam, miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani, hadi kufikia mwezi Juni 2016.

Katika utekelezaji wa agizo hilo DAWASCO iko katika utekelezaji wa Maagizo ya serikali ya kuhakikisha wananchi waishio katika Jiji la Dar s salaam, Miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani wanaunganishiwa Maji ifikapo Julai 2016. Katika kutekeleza agizo hilo Dawasco imejipanga katika awamu kuu NNE (4)

1.      Awamu ya kwanza itawahusu wateja wote walioko katika maeneo ambayo kwa sasa yanapata maji na kuna miundo mbinu ya mabomba karibu.

2.      Awamu ya Pili itahusu maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba makubwa ya Maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu ya kukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.

3.      Awamu ya Tatu itahusisha maeneo yote yaliyopitiwa na mradi maarufu wa Mabomba ya Kichina, Maunganisho katika awamu hii yataanza baada ya kukamilika kwa Miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu,

4.      Awamu ya  Nne itaanza katika maeneo yote ambayo kwa sasa hakuna miundo mbinu ya Maji na yako mbali kutoka katika mabomba makubwa .

Gharama ya kuunganishiwa huduma ya Majisafi ni Tsh 200,000 kwa wateja wadogo (Domestic Customers)na Tsh 400,000 kwa wateja wakubwa (Corporate Customers) Mwisho.


TATIZO LA MAJI JIMBO LA NYAMAGANA MKOANI MWANZA LAMTESA MABULA.

January 11, 2016
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akifafanua jambo ofisini kwake.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula amesikitishwa na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo kukabiliwa na ukosefu wa Maji safi na salama huku baadhi ya miradhi ya maji ikichukua muda mrefu bila utekelezaji wake kukamilika kwa wakati.

Mabula ameelezea masikitiko yake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa jimbo la Nyamagana, juu ya kukosa huduma ya maji ya bomba licha ya jimbo hili kuzungukwa na ziwa Victoria.

Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana, amebainisha kuwa ipo miradi ya maji ambayo bado haijatekelezwa kutokana na serikali kushindwa kutoa pesa kwa wakati jambo ambalo amesema kuwa atalisemea mara kwa mara katika vikao vya bunge lijalo ili kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza