WADAU WAKUTANA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI

April 12, 2018
MkurugenziwaTathmini ya Athari kwa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhina Usimamiziwa Mazingira Dkt. Fadhila Khatib akifungu awarsha ya wadau kuhusu usimamizi jumuishi wamasuala yamabadiliko ya tabia nchi maeneo ya Pwani, warsha hiyo inaendelea katika Ukumbiwa NIMR Dar es Salaam.

Washiriki wa warsha jumuishi ya usimamizi wamasuala ya mabadiliko ya tabianchi maeneo ya Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi MkurugenziwaTathmini ya Athari kwa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na UsimamiziwaMazingiraDkt. Bi. Fadhila Khatib.


Sehemu ya washiriki wa warsha jumuishi ya usimamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi maeneo ya Pwani wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi (hayupopichani).


Imeelezwa kuwa mabadiliko ya Tabia ya nchi yanasababisha athari mbalimbali kama vile ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, kumezwa kwa visiwa na kuongezeka kwa ujazo wa maji yabahari unaosababishwa na kuyeyuka kwa barafu katika ncha za Dunia.

Hayo yamesemwa leo na KatibuMkuu Ofisiya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na MkurugenziwaTathminiya Atharik wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la HifadhinaUsimamiziwaMazingiraDkt. Fadhila Khatib wa kati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu usimamizi jumuishi wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi maeneo yaPwani.

Mhandisi Malongo amesema kuwa hasara za athari hizonikubwazaidikatika bara la Afrika kwakuwauchumi wake nitegemezikwahaliyahewana pia uwezo mdogo wakuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na umaskini.
Hatahivyoripotiyawataalamuiliyotolewamwaka 2011 kuhusu gharama za kiuchumi zitokanazonamabadilikoyatabianchizinawezakufikiaasilimiambili 2% yaPato la Taifakwamwakaifikapomwaka 2030.

“WadauwamwambaowaPwanikatikamtandaowenumliouanzishachiniyamradihuumnaowajibuwakuwekakipaumbelekwenyekutafutamikakatiyakukabiliananachangamotozamabadilikoyatabianchi” Malongo alisisitiza.

Kwa upandemwingineMsimamiziwaMradihuoDkt. Kanizius Manyika amesema kuwa mradi umekamilika kwa asilimia 99 na umefanikiwakuvukamalengoyaliyokusudiwakwakutoamajikobanifuzaidiya 3000 katikaHalmashauriza Jiji la Dar es Salaam, Ujenziwamtaro Ilala BungoniwenyeurefuwaMita 475 naMtoni-MtonganiMita 550. Pia ujenziwaukutawawenyeurefuwamita 920 barabaraya Barack Obama naMita 380 katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni.

Mradi huo ambao shughuli zake zimekamilika umechangia kutatua baadhi ya changamoto zinazosababibishwa nakuongezeka kwa usawa wamajiya bahari ikiwani pamoja nakutoa elimu kwa ummajuuyamabadilikoyatabiachinaatharizakenaupandajiwaMikokokatikajiji la Dar es Salaam.


WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA MJINI DODOMA LEO

April 12, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS uliofanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki na Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akihutubia baraza hilo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akihutubia baraza hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania waliohitimu mafunzo ya Jeshi Usu hivi karibuni wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala huyo uliofanyika leo mjini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki muda mfupi baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo.
HOTUBA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA

April 12, 2018


Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuhusu mikakati wa bandari hiyo kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike
PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huo
Mwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huo
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga

MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa yaliyofanyika.

Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji .

Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo kusafirisha bidhaa zao.

“Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama.

Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika.

“Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia shehena inayowasili “Alisema.

Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika kufanya kazi hizo kwa wakati.

DC ILALA AWATAKA WAJASIRIAMALI WANAWAKE KUJIUNGA NA JUKWAA LA WANAWAKE

April 12, 2018

Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, Juliana Richard, Mwenyekiti, Anjela Mwamakula na aliyevaa miwani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.


Wanachama wa Kikundi cha Mshikamano Mchikichini Sokoni wakiwa kwenye uzinduzi wa kikundi chao.


Hapa wakiserebuka.


Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza kwenye uzinduzi huo.


Uzinduzi ukiendelea.

Wakiimba na kucheza katika uzinduzi huo.


Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Anjela Mwamakula akisoma taarifa ya kikundi mbele ya mgeni rasmi.

Makofi yakipigwa.
Umakini katika uzinduzi huo.

Katibu wa Kikundi, Juliana Richard akimkabidhi mgeni rasmi risala yao.
Mkurugenzi wa Shirika la EfG, Jane Magigita akizungumza katika uzinduzi huo.
Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akihutubia wakati akizindua kikundi hicho.



Mkurugenzi wa Shirika la EfG, Jane Magigita akionesha cheti cha kikundi hicho baada ya kuzinduliwa.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Anjela Mwamakula na Katibu wake Juliana Richard (kulia), wakionesha cheti.
Mwakilishi wa Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilala, Regina Ng'ongolo, akizungumza.

Ofisa Ushirika Manispaa ya Ilala, Donald Kibhuti akizungumza machache kwenye uzinduzi huo.

Ofisa kutoka ofisi ya Sheria na Msajili Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Geofrey Mlagala, akizungumza.

Mlezi wa Kikundi hicho, Betty Mtewele akizungumza.


Zawadi zikitolewa kwa mgeni rasmi.








Mjasiriamali Godliver Massawe (kulia), akimuonesha mgeni rasmi bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanawake hao.


Picha ya pamoja na mgeni rasmi

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE Wajasiriamali wametakiwa kujiunga na Jukwaa la Wanawake ili kujiinua kiuchumi.

Mwito huo umetolewa na Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati akizindua kikundi cha wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Kalekezi amewataka wanawake hao kuacha unafiki na kupendana jambo litakalowasaidia kusonga mbele kwenye umoja wao huo.

Alisema Dunia imeanzisha Jukwaa la Wanawake ambapo wanawake watakuwa wakukutana kujadili changamoto walizo nazo na jinsi ya kuzikabili pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za maendeleo.

"Jukwaa ili na sisi linatuhusu hivyo hatuna budi kujiunga nalo kwani huko tutapata wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali pamoja na biashara hivyo ni vizuri tukalichangamkia" alisema Kalekezi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG) Jane Magigita alisema wakati huu si wakulala bali ni wakuangalia fursa nyingine ili kujikomboa kiuchumi.

Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kupambana vilivyo ili kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi.

Mkurugenzi huyo ambaye kupitia shirika analoliongoza la EfG amekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wanawake alisema hivi sasa kwa Dar es Salaam semina zimekwisha badala yake wanakwenda katika mikoa nane ambapo wataanzisha kampeni ya uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia masokoni ambapo wasaidizi wa kisheria waliopata mafunzo kutoka shirika hilo ndio watakao kuwa wahamasishaji wakubwa.

"Sasa hatutakuwa tena na semina tunakwenda kufanya uhamasishaji mkubwa mkoani tutakuwa na basi letu maalumu katika kampeni hiyo" alisema Magigita.

Katibu wa kikundi hicho, Juliana Richard wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema changamoto yao kubwa ni miundombinu mibovu katika soko lao la mchikichini na mikopo wanayokopa kuwa na riba kubwa.

Alisema kikundi hicho kwa sasa kinamtaji wa sh.milioni 11 lakini lengo lao kwa kiasi cha chini kuwa na sh.milioni 70.

Ofisa kutoka ofisi ya Sheria na Msajili Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Geofrey Mlagala alisema wanawake ambao wapo tayari kuanzisha vikundi vyao milango ipo wazi na watasaidiwa kuelekezwa namna ya kuvifungua.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)



UNDP YAISAIDIA TANZANIA MFUMO BORA WA KUKUSANYA NA KUHIFADHI TAARIFA ZA HEWA YA UKAWA

April 12, 2018
Calvin Edward Gwabara, Morogoro.

SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linaisaidia Tanzania kuwa na mfumo bora wa kukusanya na kuhifadhi taarifa za hewa ya ukaa nchini ili taarifa hizo ziweze kutumika katika mipango mbalimbali ya kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuwa na taarifa sahihi za mchango wan chi katika kukabiliana na tatizo hilo.
Baadhi ya washiriki mafunzo hayo kutoka wizara mbalimbali na vyuo vikuu wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa wadau wakuu wa mpango huo na namna ya kutumia mfumo huo katika kukusanya taarifa hizo mtaalamu wa miradi inayohusu nishati na mabadiliko ya tabia nchi kutoka UNDP tawi la Tanzania Bwana Abbas Kitogo amesema mfumo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na takwimu sahihi za hali ya hewa ya ukaa na namna tunavyopambana katika kuipunguza .

Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania hatuna taarifa sahihi na rasmi sana pale inapotakiwa kueleza mchango wetu kama taifa katika kutatua changamoto hiyo na hivyo kushindwa kujua kama nchi tufanye tuongeze nguvu wapi au tufanye nini katika kusaidia jitihada hizo za dunia.

Aidha amebainisha kuwa kupitia mradi huo wa kujenga uwezo wa serikali katika kujenga mifumo ya jinsi ya kuzia hewa ukaa Tanzania wameamua kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kama vile wizara na vyuo vikuu lengo likuwa ni kuwawezesha wataalamu wa serikali kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuzitolea taarifa kule zinakotakiwa.

‘’Tunatakiwa kutoa taarifa kwa umoja wa mataifa ule mpango maalumu wa hewa ukaa na mbadiliko ya tabia ya nchi tunazalisha hewa kiasi gani na mipango yetu ya kupunguza ni kiasi gani na namna ambavyo kama nchi tunaweza kupambana na tatizo hilo hivyo ni muhimu mfumo huu wa taarifa uwepo maana kwa sasa hatuna’’ Alisema Kitogo.



Amesema kuwa Wataalamu wametungenezea mfumo GG inventory System ambao utakuwa katika hali ya taarifa lakini pia kama tovuti maalumu ambayo itakuwa inasimamiwa ofisi ya makamu raisi lakini watakaokuwa wanaifanyia kazi ni kituo cha kitaifa cha kufuatilia kaboni kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA maana wao ndio wana utaalamu wa kufanya kazi hii.

Ameongeza kuwa kwa kuweka mfumo huo SUA utawezesha wanafunzi pia wanaosoma hapo kuweza kujifunza na kuwa na uwezo kuutumia mfumo lakini pia kuona namna unavyofanya kazi pale ambapo watakutana nao.

‘’Tumepitisha mkataba wa Paris wa kuungamkono juhudi za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika hewa ya ukaa hivyo ni muhimu kuwa na mfumo huo ambao utatuwezesha Tanzania kujitathimini na kuona jitihada zinazofanyika pale tunapotakiwa kutoa taarifa ya nchi kwenye umoja wa mataifa’’ Aliongeza Kitogo.

Amesema kupitia UNDP wameweza kutafuta wataalamu hao na kuwapa kazi ya kutengeneza mfumo huo na baada ya kuutengeneza sasa wameuleta na kuwafonyesha unavyofanya kazi na kuwafundisha namna ya kuutumia maana ni mfumo ambao unabadilika hivyo unahitaji kuboreshwa.


Kwa upande wake mratibu wa kituo cha kitaifa cha kufuatilia hewa ya kaboni kilichopo SUA Prof. Zahabu Eliakimu amesema kuwa mwanzoni wakati walipoanzsha kituo hicho cha kitaifa walikuwa wamejikita kwenye kufuatilia hewa chafu zinazosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi walikuwa wanaiangalia zaidi hewa moja ya kabondayoksidi lakini kupitia mfumo huu watahusisha hewa zote saba zinazohusika katika kusababisha mabariliki ya tabia nchi.

Amezitaja hewa hizo ambazo mfumo huu utahusika katika kuzifuatilia ukiachia mbali ile ya carbondioxide ya awali ambazo zitaangaliwa katika kila sekta kuwa ni Green house,Methane,Chlorofluorcarbon,Hydrofluorcarbon,Nitrous Oxide,Walter Vapor pamoja na Ozone.

‘’Tunavyoenda na kuzingalia hewa zote hizi tunabaki kuona kuwa hewa ambayo ndio inaongoza zaidi katika kuchangaia mabadiliko hayo ya tabia ya nchi kuwa ni Carbondioxide lakini hizo nyingine zinachangia kwa kiasi kidogo lakini sekta inayohusika zaidi ni sekta ya matumizi ya ardhi kwenye mistu,kilimo makazi ya watu ndiyo kupitia madaliko hayo’’ Alisema Prof. Eliakimu.

Kwa upande wake Mataalamu mwandamizi wa mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais Bi. Adelaida Tillya amesema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwa taifa kwani utaisaidia nchi kuweka mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwakuwa sayansi imeonyesha vitu vinavyoweza kuachangia mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana nayo kama nchi na mtu mmojammoja.

‘’Tanzania inaonekana haichangii kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi kama ambavyo zinachangia nchi zingine, lakini ni lazima kuangalia maendeleo ya nchi kama tunapunguza au tunaongeza uzalishaji wa hewa ukaa’’ Alisema Bi. Tillya.

Ameongeza kuwa kwa nchi zinazoendelea zimejiwekea mikakati ya kitaifa katika kuangalia malengo ambayo nchi imejiwekea kama imefikiwa au la na kuweza kutoa ripoti kwa mamlaka husika kila baada ya miaka miwili kama unavyotutaka Mkataba wa kimataifa tuliousaini wa kuungana na nchi zingine duniani katika kupunguza tatizo hili.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAAFISA MBALIMBALI WA JWTZ

April 12, 2018

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza majina ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU