MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA WATENDAJI WAKE WA MAZINGIRA

August 21, 2016

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha kazi kilichodumu kwa siku mbili ambao alipokea na kujadili masuala mbali mbali yanayohusu mazingira, kulia ni Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
 Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha Idara ya Mazingira kilichoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira na Wakuu wa Vitengo, waliokaa pamoja na Makamu wa Rais kushoto ni  Waziri Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais  Ndugu Mbaraka Abdulwakil.
                                                             ...........................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa Idara ya Mazingira katika ofisi yake wajipange vizuri kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari za kimazingira mjini Dodoma wakati serikali ikijiandaa kuhamia kwenye mji huo.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 21-Aug-16 alipokuwa akifunga mkutano wa kazi wa siku mbili na watendaji wa Idara ya Mazingira ambapo walijadili namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kote nchini.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuuweka mji wa Dodoma salama kimazingira ikiwemo ubora wa miundombinu za maji taka.

Makamu wa Rais amesema kutokana na idadi kubwa ya watu hasa watumishi ambao watahamia Dodoma bila miundombinu imara hali ya uchafuzi wa mazingira itakuwa si nzuri hivyo ni muhimu kwa watendaji hao kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kuhakikisha mji wa Dodoma hautaathirika kimazingira.
Kuhusu utendaji kazi wa watumishi wa ofisi yake amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa uwazi katika matumizi ya fedha za miradi na hasa  inayohusika na uhifadhi wa mazingira jambo ambalo litaondoa manung'uniko miongoni mwa watumishi na wananchi kwa ujumla.

Amesema ushirikiano huo miongoni mwa watumishi utasaidia kwa kiasi kikubwa ufanisi katika kazi za kila siku ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Makamu wa Rais amesema ataendelea na utaratibu wa kukutana na watumishi kila baada ya miezi 4 katika ngazi ya viongozi kama hatua ya kujitathmini katika mipango ya kazi waliyojiwekea.
SERENGETI BOYS YAITANDIKA AFRIKA KUSINI MAGOLI 3-1 UWANJA WA AZAM CHAMAZI, NA KUIFURUSHA KWENYE MICHUANO

SERENGETI BOYS YAITANDIKA AFRIKA KUSINI MAGOLI 3-1 UWANJA WA AZAM CHAMAZI, NA KUIFURUSHA KWENYE MICHUANO

August 21, 2016

1
Mchezaji Asad Ali Juma wa timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys akikokota mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Vijana ya Afrika Kusini  katika mchezo wa kufuzu katika fainali za Mataifa ya Afrika zitakayofanyika nchini Madagascar uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
  Katika kipindi cha pili mchezaji Ibrahim Abdallah ameifungia goli la pili timu ya  Serengeti Boys ,  Wakati kipindi cha kwanza  mchezaji  wa Serengeti Boys  Rashid Abdalla alifunga goli la kwanza.
Kwa matokeo  hayo Serengeti Boys inasonga mbele katika michuano hiyo  ya vijana baada ya kuitoa timu ya Afrika Kusini kwa magoli 3-1 kufuatia sare ya magoli 1-1 nchini Afrika Kusini, Ambapo inatarajiwa kukutana na timu kati ya Namibia au Congo Brazaville.
1n
Mchezaji Ibrahim Abdallah kushoto akisahangilia na wenzake mara baada ya kuifungia  goli la pili timu ya  Serengeti Boys kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi
n2
Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwa furaha mara baada ya timu ya Serengeti Boys kuifunga timu ya Afrika Kusini kwenye uwanja wa Azam Chamazi magoli 3-1
2
Vikosi vya timu hizo vikiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
3
Kikosi cha timu ya vijana ya Afrika Kusini
4
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Serengeti Boys kikiwa katika picha ya pamoja.
5
Viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania wakiwa katika jukwaa kuu kulia ni Celestin Mwesigwa nakushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania Jamal Malinzi  pamoja na viongozi wengine.
6
Benchi la Ufundi la Serengeti Boys.
7
Benchi la Ufundi la timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Majaliwa awasili Mpanda

Majaliwa awasili Mpanda

August 21, 2016


KS1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwapungia wananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kikazi mkoani humo Agosti 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KS2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Vijana wa CCM baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara  ya kazi mkoani Katavi Agosti 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KS3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya  wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo Agosti 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KS4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya  wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo Agosti 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

GHALA LA KAMPUNI YA BOSS SHOPPING CENTRE LTD LIKITEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM

August 21, 2016

 Askari wa Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto wakizima moto uliokuwa ukiteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd zilimo kuwa zikihifadhiwa bidhaa mbalimbali eneo la Viwanda Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo mchana.
 wananchi wakijadiliana jambo eneo la tukio.
 Kazi ya uokoaji ikiendelea.

 Askari wa uokoaji wakiwa kazini.
 Mmoja wa wamiliki wa ghala hilo akisaini fomu  ya uzimaji wa moto huo.
 Moto ukiendelea kuwaka

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Na Dotto Mwaibale

MOTO mkubwa umeteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd lililokuwa likitumika kuhifadhia bidhaa mbalimbali maeneo ya viwandani Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio mmoja wa wamiliki wa ghala hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa hakuwa msemaji alisema moto huo ulianza saa 9 mchana.

"Tumepata hasara kubwa katika ghala hili tulikuwa tukihifadhi friji, TV, sabufa kwa ujumla ni Boss Bland Home" alisema.

Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Baadhi ya waokoaji walikuwepo eneo la tukio walilalamikia Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto kwa kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji ya kutosha hivyo kushindwa kuhudhibiti moto huo kwa wakati ambapo ilizuka taharuki na kwa wamiliki wa viwanda vilivyokuwa jirani na ghala hilo.

Jitihada za gazeti hili kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ili kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda baada ya kumpigia simu ambayo ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa. 


TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUTANGAZA HIFADHI ZAKE.

August 21, 2016



 Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha,Kitulo na Katavi.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete  alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanao tarajia kufika nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.

“ Wataaam na wanasayansi wa kitaifa na kimataifa wathibitisha kuwa  eneo pekee ambalo tukio hilo litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya nyanda za juu kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Katavi.Kitulo na Ruaha”alisema Shelutete .

“Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii”aliongeza Shelutete.
 
Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la rujewa wilaya ya mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.

Kwa upande wake mhifadhi wa idara ya  utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya tarifa za tukio hilo kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.

JK AONGOZA MAMIA MAZISHI YA BI SHAKILA MBAGALA CHARAMBE JIJINI DAR.

August 21, 2016


s Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar .
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar,wa pili kushoto akishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar,kushoto ni  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
 Mke wa Rais Mstaafu awamu ya nne,Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.

Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Makamu wa Rais Mh,Samia Suluhu akijadiliana jambo na mmoja wa waombolezaji nyumbani kwa marehemu,kabla ya maziko kufanyika.Bi Shakila,amefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiwa na baadhi ya waombolezaji wengine wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wanamuziki wakongwe wakiwa kwenye mazishi ya Bi Shakila,hukko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe. 
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe. 
Mwili wa marehemu Bi Shakila ukiswaliwa tayari kwa maziko 
Waombelezaji wakiwa wamebeba Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Bi Shakila wakielekea mazikoni,jioni ya leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar. 
Mwili ya Bi Shakila tayari umeishapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele
Safari ya mwisho ya Bi Shakila Said .
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akijalidiliana jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto).
 Baadhi ya wanamuziki wakongwe na bongofleva wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki mazishi ya Bi Shakila huko nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar
 Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na waombolezaji.
Katibu MKuu wa Shirikisho la Wanamuziki nchini,John Kitime akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwa marehemu Mbagala Charambe,jijini Dar.