KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YAKE KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

June 23, 2015

Afisa wa Jeshi la Magereza nchini, Nsajigwa Mwankenja akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kuhusu shughuli zinazofanywa na Jeshi hilo, wakati Katibu Mkuu alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Uhamiaji kuhusu shughuli zinazofanywa na Idara hiyo, wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisoma vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Jeshi la Magereza (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, aina ya mbegu bora ya muhugo inayolimwa na Jeshi hilo katika mashamba yake, wakati alipotembelea banda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Israel Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Rose Mdami, ya jinsi ya kujaza fomu ya kuomba Kitambulisho cha Taifa, wakati Mkurugenzi Kamuzora alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
NHC LAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MKOA WA LINDI NA MTWARA

NHC LAFANYA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA KATIKA MKOA WA LINDI NA MTWARA

June 23, 2015

Uhakiki wa vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri na kusaidia wananchi kupata matofali ya kujengea nyumba bora umeanza katika Mikoa mbalimbali ukianzia na Mkoa wa Lindi na Mtwara. Katika hali isiyotarajiwa Mkoa wa Mtwara ambao kwa muda mrefu umekuwa ukililia kuletewa maendeleo umeshindwa kutumia fursa ya msaada wa mashine kwa vijana waliyopewa na NHC hali iliyolifanya Shirika kutwaa baadhi ya mashine ili zipewe vikundi vingine vinavyofanya vizuri Fuatilia kupitia habari picha hizi ili ufahamu kilichojiri katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania. Leo uhakiki huo unaendelea Mkoani Ruvuma.
New Picture
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Nicholous Kombe akimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akimshukuru kwa Halmashauri hiyo kusaidia kikundi cha vijana kwa kuwawezesha fedha na udongo kwa ajili ya kutengeneza matofaliya kufungamana. Katikati ni Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu.
New Picture (2)
Jengo la Ofisi ya kikundi cha vijana cha Narunye(hakuna kutegeana) katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini likiwa limeonwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana. Kikundi hiki kimeshaanza kupata maombi mengi ya matofali kutoka kwa wananchi wanaohitaji.
New Picture (1)
Kikundi cha vijana cha Ruangwa Materials Group katika Halmashauri ya Wilaya Ruangwa kimeshatengeneza matrofali kwa kutumia mashine ya msaada kutoka NHC. Halmashauri ya Wilaya hiyo imeamua kuyatumia matofali ya vijana hawa kujengea zahanati na majengo mengine yanayohitajika katika Halmashauri zikiwemo nyumba za Waalimu.
New Picture (3)
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa mawaidha kwa kikundi cha vijana cha Narunye kilichopo katika Wilaya ya Lindi vijijini baada ya kutembelea kikundi hicho kukagua kazi zake.Vijana hawa wanajihusisha pia na utunzaji mazingira.
New Picture (4)
Baada ya Wakurugezi wa Halmashauri za Kilwa na Lindi Vijijini kutokuwa karibu na vikundi vya vijana, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC na Meneja wa Mkoa wa Lindi waliweza kufanya mazungumzo nao ya kina na hatimaye wamekubali kuwasaidia vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC katika Halmashauri zao ili waweze kujiajiri. Kulia ni Bi. Oliver Vavunge ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilwa Bi. Maimuna Mtanda.
New Picture (5)
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Bw. Daniel Kaluse hakuwa nyuma kutembelea kikundi cha Vijana na Maendeleo kilichopo eneo la Mitwero nje kidogo ya Manispaa hiyo ili kuwapa moyo na kufahamu maendeleo yao akiwa ameandamana na ujumbe wa NHC.
New Picture (6)
Meneja wa NHC Mkoa wa Mtwara Bw. Joseph John akitoa taarifa ya Mkoa kwa Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ya maendeleo ya vikundi vya vijana waliosaidiwa mashine na NHC . Katika taarifa yake Meneja huyo alisikitishwa na vijana wa Mkoa wa Mtwara kushindwa kutumia kikamilifu msaada huo na akalaumu Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kushiriki kikamilifu katika programu hiyo ya kusaidia vijana.
New Picture (7)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akikemea na hatimaye kukinyanganya mashine kikundi cha Likonde katika Manispaa ya Mtwara kwa kuifungia stoo mashine waliyopewa msaada na NHC bila kufanya kazi iliyokusudiwa ya kufyatua matofali. Mashine hiyo itapewa kikundi kingine ili itumike kikamilifu.
New Picture (8)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akiwa Wilayani Tandahimba akikagua matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Maendeleo Group kilichopewa msaada wa mashine na NHC. Kikundi hiki kinasubiri kulipwa na Halmashauri matofali hayo yanayotarajiwa kujengea nyumba za waalimu.
New Picture (9)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Bw Dennis Mwaitete akielezea mkakati wa Halmashauri yake wa kusaidia vijana ulivyo alipotembelewa na ujumbe wa NHC uliokuwa ukihakiki vikundi vya vijana Mkoani Mtwara.
New Picture (10)
Kikundi cha vijana cha Umoja Lekanelo kilichopo Wilaya ya Newala kilichoshindwa kutumia kikamilifu mashine ya msaada kilichopewa na NHC kiliweza kupokonywa mashine hiyo jana. Wilaya ya Newala ina shughuli za madini na kilimo cha korosho kiasi cha kuwafanya vijana kushindwa kujihusisha kikamilifu na mradi wa kufyatua matofali.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Marx Kamaoni akizungumza na ujumbe wa NHC uliofika Ofisini kwake kuhamasisha Halmashauri za Wilaya kusaidia vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali na NHC.
New Picture (12)
Vyombo vya habari vimehusishwa katika uhakiki huu na hapa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Newala Bw. Marx Kamaoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa Halmashauri yake kusaidia vijana.
New Picture (13)
Kikundi cha Vijana cha For Energy Group kilichopo Wilayani Masasi kilitembelewa na baada ya kuridhishwa na utendaji wake NHC ilikiongezea mashine mbili zilizopokonywa vikundi vingine vilivyoshindwa kuzitumia Wilayani Newala na Masasi Vijijini. Hii ni nyumba iliyojengwa na kikundi hicho Wilayani Masasi.
New Picture (14)
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akivionya vikundi vya vijana vya Nayoden na Mangaka Wilayani Nanyumbu waliokula fedha ya mtaji waliopewa na NHC ambapo aliamuru kuchukuliwa kwa mashine zao na kuwapa muda wa kujiandaa. Aliwataka kuziomba mashine hizo kwa maandishi watakapokuwa tayari kuzitumia. Mashine hizo zilifungiwa Ofisi ya Kata ya Mangaka kwa muda wa miezi nane wakisubiri kupata fedha nyingine kutoka NHC.
New Picture (15)
Mashine iliyopokonywa vijana wazembe Wilayani Nanyumbu ikipandishwa katika gari baada ya vijana hao kuzembea kuitumia na kuifungia Ofisi kwa muda mrefu.

NYALANDU APATA WADHAMINI MKOANI KILIMANJARO

June 23, 2015

Katibu wa Jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi,UVCCM wilaya ya Moshi mjini ,Joel Makwaia akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu alipowasili ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kutafuta wadhamini .
Nyalandu akisalimiana na vijana waliofika kumdhamini.
Kundi la vijana waliofika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro waliofika kwa ajili ya kumdhamini ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu katika harakati zake za kuwania nafasi ya kugombea urais wa Tanzania.
Baadhi ya vijana hao waliojitokeza kumdhamini Nyalandu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini ,Loth Ole Nesele akizungumza wakati akimkaribisha Nyalandu kuzungumza na iajana hao.
Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii,LAzaro Nyalandu,Faraja Nyalandu  akisalimia wananchi waliofika kumdhamni mumewe.
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi hao ambao wengi wao ni viajana waliofika kwa ajili ya kumdhamini.
Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini,Loth Ole Nesele akimkabidhi Waziri Nyalandu fomu ya majina ya wanachama wa chama chama mapinduzi waliojitokeza kumdhamini.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwashukuru vijana hao waliojitokeza kwa wingi kumdhamini.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI/HLANGANANI–(WORLD TOURISM EXPO) ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA

MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI/HLANGANANI–(WORLD TOURISM EXPO) ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA

June 23, 2015
IMG_4145
Pichani juu na chini ni Afisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IMG_4137 IMG_4168
Afisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
IMG_4185
Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa AfAfisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.
IMG_4229
Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii zinazofanywa na kampuni yake kwa wageni waliofika katika banda la Tanzania wakati wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare.
IMG_4241
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (wa pili kulia) akitoa maelezo yaliyomo kwenye vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho nane ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4191
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel ya nchini Tanzania, Joseph Waryoba (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Zambia, Felix Chaila aliyembelea banda la Tanzania wakati wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers ambayo yamemalizika juzi.
IMG_4195
Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tanzania Travel Company ambayo pia imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare.
IMG_4205
Timu kutoka Tanzania ambayo imeshiriki maonyesho ya utalii nane ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare ikiongozwa naAfisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Wakala wa utalii kutoka kampuni ya Cordial Tours and Travel nchini Tanzania, Joseph Waryoba, Meneja Masoko na Tehama wa kampuni ya Best Northern Tours and safaris nchini Tanzania, Mary Joel pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Samwel Diah (kulia).
Na Modewjiblog team, Harare
TIMU ya watanzania walioenda kuhudhuria maonesho ya utalii nchini Zimbabwe wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza uendeshaji wa sekta ya utalii.
Walisema katika ziara yao hiyo wamegundua kwamba Wazimbabwe kuanzia wanapompokea mgeni hadi anapofika hotelini wanaonesha kujali hali ambayo mgeni hawezi kusahau hata kidogo.
Aidha amesema kwamba hata mipangilio ya kwenda kwenye vivutio inafanyika katika hali ambayo huwezi kusahau hata kidogo.
Kutokana na mazingira hayo, wamesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza namna ya kupokea na kuishi na wageni na kuwatengenezea taswira ambayo hawatakaa wakisahau.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari za Utalii Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog yaliyofanyika mjini Harare siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya siku tatu ya utalii ya Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers jijini Harare.
Solomon amesema ingawa hali ya Tanzania si mbaya, watendaji katika viwanja vya ndege na mahotelini wanaweza kuangalia namna Wazimbabwe wanavyojali kazi zao na tabasamu zao nyakati zote kwa wageni .
“Si kwamba kwetu kuna shida lakini unaona watu wanavyojituma hapa” alisema Esther Solomon na kuongeza kuwa aliona jinsi walivyojipanga vizuri na wafanyakazi walikuwa na uelewa wa hali ya juu.
Esther aliongoza kundi la watu watano wa Kitanzania walioalikwa na mamlaka ya utalii Zimbabwe (ZTA) kuhudhuria maonesho hayo.Tanzania iliweka banda lake pia katika maonesho hayo ya siku tatu yaliyomalizika juzi.
Makampuni ya mawakala wa utalii aliyoambatana nayo katika safari hiyo ni pamoja na Tanzania Travel Company, Cordial Tours and Travel, Mberesero Tented Camp na Best Northern Tours and safaris .
Alisema safari yao Zimbabwe pamoja na ushiriki wao katika maonesho pia walifika katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini yakiwemo maporomoko ya Victoria.
Aidha walipewa nafasi ya kukagua sehemu za malazi kwa ajili ya wageni.
Alisema katika maonesho hayo wamefanikiwa kupata wageni wengi wanaoulizia namna ya kufika Tanzania na pia ushirikiano wa makampuni katika sekta ya utalii.
“ Watu wengi wamekuja kututembelea. Na wengi ni watu weusi. Mwamko wao wa kutembelea vivutio ni mkubwa.” Alisema Esther na kuongeza kuwa wamebaini kwamba ipo haja ya watanzania kuhimizwa kutembelea vivutio kwani hata nchini Zimbabwe wanaotembelea vivutio ni wananchi wenyewe.
Alisema wengi waliofika katika banda la Tanzania waliulizia namna ya kufika visiwa vya Zanzibar na pia mbuga za Tanzania.
Aidha mawakala wengi waliulizia namna ya kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utalii katika bara la Afrika.
Asilimia 80 ya watalii nchini Zimbabwe wanatoka bara la Afrika na waliobaki ndio wanatoka nje ya bara hili.