CCM VITI MAALUMU UDIWANI TANGA KUMEKUCHA

July 22, 2015


 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT) Wilaya ya Tanga wakifuatilia mkutano wa kuwapitisha wagombea nafasi za Udiwani Viti Maalumu kwa halmashari ya jiji la Tanga ambalo liko na viti 27 vya Udiwani.

  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu, akifungua mkutano wa uteuzi wa wagombea nafasi za Udiwani viti Maalumu kwa halmashauri ya jiji la Tanga ambayo iko na jumla ya viti 27 vya Udiwani.





Hapa baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wakichagua viongozi ambao watawapendekeza kuchaguliwa Udiwani viti maalumu uchaguzi mkuu mwaka huu

NJAMA ZA MAKABURU KUMG’OA MKURUGENZI WA KONYAGI MGWASSA ZAGUNDULIKA

July 22, 2015

 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), maarufu kwa jina la Konyagi . David Mgwassa Kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MKAKATI wa kumng’oa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi (TDL) David Mgwassa umebainika kutokana na kuwepo kwa njama zinazoendeshwa kwa siri na makaburu.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kiongozi huyo amekuwa akipigwa vita kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mafanikio yanayopatikana chini ya uongozi wake.
Makaburu hao wamekuwa wakifanya njama mbalimbali za kumng’oa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutaka kushika wadhifa wa mkurugenzi huyo kwa kutoa taarifa ambazo si za kweli kwa uongozi wa ngazi za juu nchini Afrika Kusini na Uingereza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kukabidhi ofisi ifikapo Julai 30, mwaka huu.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa tayari taarifa za kuondolewa kwa kiongozi huyo zimezagaa katika viwanda vya TDL na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) pia tangazo la kumbadilisha limetolewa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kutangaza Kenya na Uganda.
Kutokana na taarifa hizo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TDL wameazimia kugoma ili kushinikiza mkurugenzi huyo kuendelea na madaraka yake.
“Tumesikia taarifa kuwa mkurugenzi wetu anaondolewa madarakani kwani tumeshangazwa sana kutokana na kuishi naye vizuri na kupatikana kwa mafanikio mengi tangu ashike wadhifa huo na pia ameboresha maisha yetu kwa kutuongezea mishahara,” alisema mfanyakazi mmoja ambaye hakutaja jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa wafanyakazi.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa Bw. Michael Benjamin anatarajia kushika wadhifa wa Bw. Mgwassa.
Mtandao huu ulimtafuta Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Steve Kilindo ili kuzungumzia taarifa hilo alikiri kuwepo kwa mabadiliko hayo lakini hana taarifa zaidi kuhusiana na sakata hilo.
“Kweli kuna mabadiliko hayo ya uongozi lakini taarifa za ndani sina,” alisema.
                         Mike Benjamin kutoka Afrika Kusini anayetarajia kurithi cheo hicho

HIVI NDIVYO WANANCHI WA JIJI LA TANGA WALIVYOSHEHEREKEA SIKUKUU YA IDDI HOTEL YA TANGA BEACH RESORT

July 22, 2015





DIAMOND PLATNUMZ AWASHUKURU WADAU WALIOFANIKISHA USHINDI WA TUZO YA (MTV MAMA)

DIAMOND PLATNUMZ AWASHUKURU WADAU WALIOFANIKISHA USHINDI WA TUZO YA (MTV MAMA)

July 22, 2015

????????????????????????????????????
Salam Sharaf  Meneja wa Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  katika shughuli za kimataifa akizungumza na waandishi wa habari  huku mwaamuziki huyo mwenye miwani  akifuatilia wakati wa  mazungumzo na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwashukuru wadau wote wa muziki na mashabiki wake kwa mchango wao kutokana na ushindi wake alioupata katika tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards. 2015 zilizofanyika katika  jiji la Durban  Kwazulu -Natal nchini Afrika Kusini Mwishoni mwa wiki iliyopita na kumfanya mwanamuziki huyo alishinda alishinda  katika kipengere cha Mtumbuizaji Bora (Besta Live Act)  katika tuzo hizo za MTV MAMA. Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya Tansoma Kariakoo jijini Dar es salaam.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Salam Sharaf  Meneja wa Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  katika shughuli za kimataifa akizungumza na waandishi wa habari  huku mwaamuziki huyo mwenye miwani  akifuatilia alipozungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya kuwashukuru wadau wote wa muziki na mashabiki wake kutokana na ushindi wake alioupata katika tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards. 2015 zilizofanyika katika  jiji la Durban  Kwazulu -Natal nchini Afrika Kusini Mwishoni
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  akizungumza na waandishi wa habari  huku akiwana tuzo yake aliyoipata nchini Afrika Kusini.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari  huku katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  akipozi kwa picha mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo. wa pili kutoka kulia ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz Bw. Said Fella.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  akipozi kwa picha  na mameneja wake mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.  kulia ni  Bw. Said Fella  na kutoka kushoto ni Babu Tale na Sallam Sharaf.
????????????????????????????????????

Mwanamuziki Nassib Abdull (Diamond Platnumz)  akipozi kwa picha  na mameneja wake mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.  kulia ni  Bw. Said Fella  na kutoka kushoto ni Babu Tale na Sallam Sharaf.
CHADEMA WANAHUTUBIA MWANZA LEO,JAMES LEMBELI NA ESTHER BULAYA NDANI

CHADEMA WANAHUTUBIA MWANZA LEO,JAMES LEMBELI NA ESTHER BULAYA NDANI

July 22, 2015

mw1
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibroad Slaa akiwa kwenye gari katika msafara wa mapokezi kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya waliohamia Chadema wakitokea CCM jana jijini Mwanza.
unnamed (4)
Aliyekuwa Mbunge wa CCM jime la Kahama James Lembeli kulia akiwa na aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Vijana  CCM mkoa wa Mara Esther Bulaya ambao wote wamehamia CHADEMA wakiwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Mwanza.
mw2
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibroad Slaa akiwa kwenye gari katika msafara wa mapokezi kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya waliohamia Chadema wakitokea CCM jana jijini Mwanza.
mw3
Mbunge wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, James Lembeli (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika, wakiwapungia wananchi mikono walipokuwa kwenye msafara wa mapokezi ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho wakiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara.

UZINDUZI WA KAMPENI YA AWAMU YA PILI YA WAZAZI NIPENDENI WAFANYIKA DAR ES SALAAM LEO

July 22, 2015

 Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo na Mshauri wa Kiufundi wa Malaria kutoka  Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)
 Ofisa Uzazi Salama,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Masuala ya Afya ya Uzazi wa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University, Dk,.Rosemarie Madinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Taasisi hiyo ndiyo inayoendesha kampeni hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mwongozaji wa uzinduzi huo akiendelea na kazi.
 Wanahabari wakiwa kwenye shughuli hiyo.
  Ofisa Uzazi Salama,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kushoto), akimpongeza  Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali, baada ya kutoa tamko la Wizara hiyo katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki Nyoshi Al-Saadat wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia “Wana wa Ngwasuma” itakayotoa burudani katika maonyesho mbalimbali yatakayokwenda sanjari na uzinduzi huo yatakayofanyika kuanzia kesho viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam kuanzia kesho, akizungumza katika uzinduzi huo utakaopambwa na burudani za kumwaga.
…………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
SERIKALI imesema imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano toka 157 mwaka 1990 hadi kufikia 54 kwa mwaka 2013.
 
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam leo
 
Alisema kati yua watoto hai 1,000 wanaozaliwa na kufikia lengo la Melenia (MDG) 4 waliojiwekea kufikia mwisho wa mwaka huu Disemba 2015.
 
“Pamoja na mafanikio hayo bado hari si shwari kwa upande wa vifo vinavyotokana na uzazi kwani vimepungua kutoka 770 mwaka 1990 na kufikia 410 kwa mwaka 2014 kwa kila vizazi hai 100,000 tofauti na lengo tulilojiwekea kufikia Disema 2015 kuwa vipungue kufikia 193 kwa kila vizazi hai 100,000″ alisema Dk.Ali.
 
Alisema Kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya kwanza ilitengenezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na msaada toka watu wa Marekani kupitia taasisi ya USAID, Mfuko wa Malaria wa Rais wa Marekani na taasisi ya Kukinga na kuzuia Magonjwa.
 
Dk. Ali alisema programu hiyo ilihusisha kutuma ujumbe uliolenga kuimarisha afya ya mjamzito na mtoto na kuwa ilizinduliwa hapa nchini jijini Mwanza kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2012.
 
Alisema katika kampeni hiyo ya masuala ya afya na ustawi wa jamii vyombo vyote vya habari ni muhimu zaidi kuhabarisha na kuwa ujumbe mfupi wa simu za kiganjani wenye taarifa anwai zitakuwa zinatumwa wakati wowote wa ujauzito mpaka mwaka mmoja baada ya kujifungua.
 
Aliongeza kuwa ili kujiunga mhusika, ndugu, jirani au rafiki atatuma ujumbe “mtoto” kwenda namba 15001 jambo litakalosaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, mtoto mchanga na mtoto alie chini ya miaka mitano.
 
Alisema uzinduzi wa kampeni hiyo unakwenda sanjari na maonyesho mbalimbali, upimaji wa damu, masuala ya huduma ya VVU na Ukimwi yatakayoanza leo asubuhi viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Dk. Ali alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mingine hasa wanaume na wanawake kufika kwenye maonyesho hayo kupata huduma za afya ya uzazi ambayo yataambatana na burudani za muziki kutoka bendi za Wanaume Familia, Ngwasuma, Wanaume Halisi na nyingine nyingi.

YANGA YAICHAPA TELECOM 3 -0

July 22, 2015

Mabingwa mara tano wa michuano ya Kombe la Kagame timu ya Young Africans (Yanga SC) leo imeibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka nchini Djibout, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili, na Geofrey Mwashiuya  aliyefunga bao la tatu kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.

Katika mchezo wa leo Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake Amissi Tambwe na Saimon Msuva zilizookolewa na mlinda mlango wa Telecom Nzokira Jeef.

Baada ya ushindi huo wa leo kocha mkuu wa Yanga, mholanzi Hans Van der Pluijm amesema vijana wake leo wamecheza vizuri na ndio manaa wameweza kuibuka na ushindi huo wa mabao 3- 0.

Aidha kocha huyo amesema kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya KMKM utakochezwa saa 10 kamili ijumaa, ukitanguliwa na mchezo kati ya Gor Mahia dhidi ya Khartoum utakoanza saa 8 kamili mchana.

Katika mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.

KAGAME KUENDELEA KESHO
Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam itaendelea kesho siku ya alhamis katika uwanja wa Taifa, ambapo Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR SC watacheza dhidi ya LLB ya Burundi, mechi itakayoanza majira ya saa 10 kamili jioni.


Mchezo wa kwanza utazikutanisha timu ya Heegan FC ya Somalia itakayocheza dhidi ya Al Shandy ya Sudan.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


--
Best Regards,

 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania 

MAGUFULI AENEDELEA KUJITAMBULISHA NA KUWASHUKURU WANACHI WA CHATO MPAKA DODOMA KWA KISHINDO.

July 22, 2015
   Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya ofisi ya CCM juu ya gari ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita alipopita kuwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji Bukombe mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita mchana huu alipokuwa akipita njiani kuwashukuru na kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
    Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi  alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Kahama mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
   Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya ofisi ya CCM juu ya gari ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita alipopita kuwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji Bukombe mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita mchana huu alipokuwa akipita njiani kuwashukuru na kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
    Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi  alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Kahama mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-DODOMA

“NAMNA FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI ULIVYOPANIA KUIPA JAMII UELEWA JUU YA ATHARI ZA UCHAFUZI WA VYANZO VYA MAJI MKOANI TANGA

July 22, 2015
*Filamu nyingi hapa nchini zimekuwa zikibebea maudhui mbalimbali ambayo yanasaidia kuibadilisha jamii tabia au kuiepuesha na madhara yanayoweza kuwakuta endapo hawatazingatia uhalisi ya jambo ambalo linazungumziwa.*
*Ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa vitu ambayo vimekuwa vikichangia kwa asilimia kubwa uchafuzi wa Mazingira hapa nchini ni pamoja na uchomaji wa misitu,ulimaji ,uvunaji ,ufugaji na ukataji wa miti hasa katika vyanzo vya maji yamekuwa yakipigia kelele na serikali pamoja na wadau binafsi hasa
kwenye vyanzo vya maji.*


*Kwa kuona umihimu wa kutekeleza jambo hilo kwa vitendo,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) iliamua kuandaa filamu ya Mamba wa Mto Zigi iliyotengenezwa na watengenezaji wa filamu za kichunguzi na historia (National Documentary Film (NadoF) ambapo mamlaka hiyo ndio mmiliki wake ambayo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi uliopita na Makamu wa Rais,Dkt Ghalibu Bilal kwenye viwanja wa Tangamano mjini hapa.*

*Akizungumza na mwandishi wa Makala hii,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa),Mhandisi Joshua Mgeyekwa anasema kuwa utengezaji wa filamu hiyo ulianza mwaka 2009 na kukamilika mwaka 2012.*

*Anasema kuwa matayarisho ya filamu ya “Mamba wa Mto Zigi” yalisukumwa na ongezeko la uchafuzi pamoja na uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji vya mto zigi vinavyoanzia katika milima ya usambara mashariki ambayo ni sehemu muhimu kwa utajiri wa bayoanuai katika Afrika.*

*Anaeleza kuwa kugundulika kwa dhahabu katika milima ya usambara mashariki miaka ya mwanzoni ya 2000 kulisababisha wimbi kubwa la uchimbaji holela wa madini na kuongeza shughuli za kibinadamu katika eneo la bonde la Zigi.*

*Vile vile kwa kiasi kikubwa kumekuwa na kilimo kisichozingatia hifadhi ya ardhi katika maeneo ya vyanzo vya mto Zigi ,Ufugaji karibu na mto ,uchomaji wa moto,ukataji wa miti kwa ajili ya nishati ya mkaa,uvunaji wa miti katika shamba la miti la Lunguza ambao ulisababisha udongo kuingia mtoni na kupunguza kina cha bwawa la Mabayani la kuhifadhia maji yanayotumiwa na
wakazi wa Jiji la Tanga.*

*Anasema kutokana na hali hiyo kumejitokeza athari kubwa ikiwemo kupungua kina cha bwawa la mabayani kutoka wastani wa mita 8.7 hadi kufikia mita 5.4 sawa na asilimia 38 ndani ya miaka 32 tangu kujengwa kwake.*

*Anaeleza hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2000 ikiwemo kuongezeka kwa viwango vya hali ya tope kwenye maji kunakohitaji fedha zaidi ya kununua madawa ya kusafisha,kuota kwa magugu maji na metete kunakosababisha maji kuwa na rangi .*

*Anasema hali hiyo inapunguza eneo la bwawa pamoja na kuhama kwa wanyama waliokuwa wakiishi katika eneo la bonde zigi na kuwafanya mamba kuwinda watu badala ya wanyama waliotoweka kutokana na uharibifu wa misitu.*

* “Huu mto zigi unategemewa na watu wasiopungua 350,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo,ufugaji na matumizi ya maji ya binadamu hivyo uharibifu huo unaweza kuleta changamoto kubwa kwa watumiaji wake “Anasema Mkurugenzi huyo.*

*Aidha anasema mto huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo unapokuwa ukipita na hali ilivyo kwa sasa idadi ya watu inaongezeka na kiasi cha maji kinapungua ambapo hilo ni janga linalotakiwa kudhibitiwa sasa.*

*Anaelezea malengo makuu ya kutayarisha filamu hiyo ni kubainisha hali ya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mto zigi ili kutoa elimu na kushirikisha jamii inayozunguka bonde la mto huo na wadau wengine nje ya bonde hilo ili kulinda mazingira kwa faida ya vizazi vijavyo.*

*Mkurugenzi huyo wa mamlaka anasema filamu hiyo inalenga kutoa fursa ya utafiti wa kisayansi juu ya tatizo la ongezeko la magugu maji katika bwawa la mabayani na mto zigi ili kupata jibu la kisayansi namna ya kuweza kukabiliana na hali hiyo.*

*Anasema katika utekelezaji huo lengo kuu ni baada ya uzinduzi wa filamu hiyo itatumika kufauta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya uhifadhi wa bwawa la mabayani,mto zigi na vyanzo vyake.*

*Hata hiyo anasema mpango huo unalenga kuihusisha jamii katika hifadhi ya mto Zigi ikiwa ni pamoja na kuwapatia maji watu waishio karibu na mto huo,kuanzisha miradi kama ufugaji wa nyuki ili kulinda misitu na kuwaongezea kipato wananchi karibu na bwawa la mabayani na mto zigi.*

*Anasema jambo jengine ni kupanda miti inayofaa katika bonde la mto zigi na kutumia utafiti katika kulinda mamzingira hasa uondoaji wa magugu maji na matete pamoja na kupunguza ujaaji wa tope kwenye bwawa hilo.*

*Mgeyekwa anasema kukamilika kabla ya kukamilika kwa filamu hiyo walikumbwa na misukosuko mikubwa nay a kusikitisha na kukatisha tama ikiwemo  kufariki waandaaji wenzao wakati wa kuiandaa filamu hiyo ambao ni muongozaji Dkt Meena,Dereva wa gari Kibabu na Muongozaji wa filamu ,Proffesa Edward Mgema
na Meneja wa Filamu Iluminata Gerald.*

*Anasema vifo hivyo viliwapa simamanzi kubwa na vilichangia sana kuchelewa kukamilika kwa filamu hiyo kwani watu hao walikuwa ni kiunganishi kikubwa kwenye kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri kuanzia hatua ya maandalizi mpaka mwisho kwa uzalendo.*

*  “Watu hawa walifanya kazi kubwa sana kwa uzalendo wa hali ya juu maana hawakuweka mbele maslahi yao binafsi bali waliangalia maslahi ya Taifa na umuhimu wa jambo hilo kwa ajili ya maendeleo “Anasema.*

*Anasema hali ya uharibifu iliyoonekana wakati wa maandalizi ya filamu hiyo imeiwezesha Tanga Uwasa kwa kushirikiana na WWF katika kuanzisha kikundi kazi kijulikanacho UWAMAKIZI ambacho kimeanza kazi kwa mafanikio makubwa
katika Tarafa ya Amani Tanga Juni 2014 na sasa kuna vijiji jirani wanaomba kujiunga na kikundi hicho.*

*Hata hivyo anaeleza mamlaka hiyo inashirikiana na Chama cha Watumiaji Maji Zigi-Mkulumuzi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira katika mto Zigi na Mkulumuzi ambapo mamlaka sasa imeimarisha kamati shirikishi ya mazingira inayoundwa na uongozi wa vijiji vinavyozunguka bwawa la mabayani.*

*Vijiji hivyo ni kutoka wilaya za Tanga,Muheza na Mkinga ambapo kwa sasa wanaweka mizinga ya nyuki 40 ikiwa ni jitihada za ulinzi na rasilimaji  na kuongeza vipato kwa wadao hao muhimu katika kulinda vyanzo hivyo.*

*Mkurugenzi huyo anamalizia kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika filamu hiyo ambao ni watengenezaji wa filamu hiyo Nado F,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,GIZ,Benki ya CRDB,Amani Nature Reserve,Wizara ya Maji,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Serikali ya wilaya ya Muheza,Wizara
ya Maliasili na Utalii-Idara ya Misitu na Nyuki.*

*Anahitimisha kwa kuwashukuu wafanyakazi wote wa Tanga Uwasa na uongozi wa Mkoa wa Tanga na kueleza kuwa filamu hiyo itakuwa ni kichocheo cha uhifadhi za mazingira sio tu katika mto zigi bali pia katika maeneo mbalimbali hapa nchini.*

*Mwisho.*