MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MABALOZI WA NORWAY NA MALAWI

December 11, 2015

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10, 2015 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,jana Dec 10, 2015.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 11, 2015.
Picha na OMR

BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA 'TUMA PESA NA SIMBANKING SHINDA PASSO'

December 11, 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi  wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja mku, Tulli mwambapa akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika hafla hiyo.
Wageni.
Zawadi za washindi.
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi akikabidhiwa zawadi ya Solar Panel
Martin Mmari akimkabidhi Deo Ndejembi funguo ya gari aina ya Passo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari (katikati), akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Maria Minde, wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akimkabidhi funguo ya gari mshindi wa shindano la ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Hellen Solomon.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari.
Deo Ndejembi akiwa ndani ya gari aina ya Passo.

Dar es Salaam, Tanzania
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Bunge, Sera, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ni miongoni mwa washindi watatu wa magari aina ya Toyota Passo yaliyotolewa na Benki ya CRDB.


Kuanzia Februari, 2015 benki hiyo ilianzisha shindano la Tuma pesa na simubanking, shinda Passo ili kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kwa simu za kiganjani ambapo kila mwezi kwa mwaka mmoja, mteja mmoja wa benki hiyo alishinda gari.

Jana Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei aliwaongoza watendaji wengine wa benki hiyo kugawa zawadi kwa washindi watatu wa Septemba, Oktoba na Novemba.
Pamoja na Mavunde aliyeshinda gari hilo Septemba, washindi wengine na miezi yao kwenye mabano ni Maria Minde (Oktoba) na Hellen Achimponta (Novemba).
Akizungumzia mafanikio ya Tuma pesa na simu banking, shinda Passo, Dk. Kimei alisema wateja wa huduma hiyo wameongezeka kutoka 830,000 mwaka 2013 hadi 1,200,000 mwaka 2015 ambapo jumla ya miamala 10,152,605 imefanyika na kuiingizia benki Sh. milioni 695.
“Matumizi ya huduma za simbanking yanamuweka mteja karibu zaidi na benki… anaweza kufanya huduma yoyote akiwa popote wakati wowote bila kufika benki.
MKUTANO WA TPLB JUMAPILI

MKUTANO WA TPLB JUMAPILI

December 11, 2015
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) itafanya Mkutano wake wa Pili wa Baraza Kuu (Governing Council) jijini Dar es Salaam, Jumapili, Desemba 13 mwaka huu.

Mkutano huo utahudhuriwa na Marais/Wenyeviti wa klabu zote 40, ambapo 16 ni za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine 24 za Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes na kutoa mwelekeo wa Bodi kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ndiye anayetarajiwa kufungua Mkutano huo utakaofanyika kuanzia saa 10 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Taifa.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB MOSHI WAJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA USAFI .

December 11, 2015

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Moshi,Emanuel Kishosha akishiriki na wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya uwanja wa michezo wa King George.
Waganyakazi wa Benki ya NMB wa matawi ya Mandela na Mawenzi wakishiriki zoezi la usafi .
Wafanyakazi wa NMB wakihakikisha hakuna uchafu unasalia katika uwanja wa michezo wa King George.
Kazi ya ukusanyaji taka ikiendelea.
Kila mfanyakazi alishiriki zoezi la usafi bila ya kuchoka.
Meneja wa NMB,Emanuel Kishosha akisukuma tololi kuzoa taka.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini (kushoto) mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika uwanja wa michezo wa King George .
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha akiwashukuru wafanyakazi wenzake wa benki hiyo kwa kujitokeza katika zoezi la kufanya usafi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755659929)