MKUTANO WA TAKWIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

April 03, 2015

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kutokaTanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwi mu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari kikuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Takwimu Kenya Bw.Zachary Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri akichangia wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afriki Mashariki uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
TBN WAMUAOMBA RAIS JUU YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO

TBN WAMUAOMBA RAIS JUU YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO

April 03, 2015

000 
Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni.
Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015
Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika.
Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari.
Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu.
Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa sahihi?
Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari.
Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia.
Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013.
Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’
Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini.
Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
IMETOLEWA NA;
Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN)

ASILIMIA 100 YA TANZANIA SASA IMEKUWA NI DIJITALI

April 03, 2015

 Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa Televisheni kwa mfumo wa Analojia kwenda Dijitali ambapo asilimia 100 ya nchi sasa imekuwa Dijitali. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala na Ofisa wa Masafa, Christopher Asenga.
  Ofisa wa Masafa wa TCRA, Christopher Asenga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.  
 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
MGAWAHAWA WA KWANZA MKUBWA WA KIAFRIKA WAFUNGULIWA ULAYA

MGAWAHAWA WA KWANZA MKUBWA WA KIAFRIKA WAFUNGULIWA ULAYA

April 03, 2015
IMG_1562
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi Maalumu, Trollhattan-Sweden
MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.
Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
IMG_1477
Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
IMG_1567
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.
Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.
Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
"Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."
Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.
IMG_1577
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia) wakielekea eneo la tukio.
Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.
Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013.
"Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.
Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.
IMG_1587
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto), Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (katikati).
Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.
IMG_1590
IMG_1592
IMG_1598
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiongozana na Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande kwenye sehemu maalum aliyoandaliwa.
IMG_1484
Pichani juu na chini ni wadau kutoka kila kona ya dunia waishio nchini Sweden walihudhuria.
IMG_1551
IMG_1487
IMG_1538
IMG_1495
IMG_1512
IMG_1625
Bw. Per R. Bostrom akisalimiana na Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (aliyeketi). Kulia ni Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
IMG_1627
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund wakiwa meza kuu.
IMG_1875
Meza kuu.
IMG_1629
Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (katikati) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mgahawa huo.
IMG_1647
Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande akizungumza machache na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa risala ya ufunguzi.
IMG_1656
IMG_1926
Meza kuu wakifuatilia historia ya Chef Issa Kapande (hayupo pichani) wakati akizungumza na wageni waalikwa.
IMG_1980
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akisoma risala mara baada ya kuzindua mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande.
IMG_1951
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago akitambulishwa kwa wageni waalikwa.
IMG_1650
Baadhi wageni waalikwa wakisikiliza historia ya Chef Issa Kapande kabla ya mgeni rasmi kusoma risala ya ufunguzi.
IMG_1669
Ukumbi mzima ulionekana kuvutiwa na historia ya maisha na mafanikio ya Mtanzania Chef Issa Kapande (hayupo pichani).
IMG_1685
Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Chef Issa Kapande ambapo alimuomba aitafutie nafasi ndani ya mgahawa wake kama kumbukumbu.
IMG_1699
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (kushoto) na mwenyeji wake Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund pamoja na Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (kulia) wakiongoza wageni waalikwa 300 kushiriki chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mmiliki wa mgahawa huo Chef, Issa Kapande.
IMG_1700
IMG_1708
Chef Issa Kapande akikata nyama ya Mbuzi kwa ajili ya mgeni rasmi, Mh, Balozi Dora Msechu.
IMG_1712
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akifurahi jambo na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Khamis Mwinjuma Simba (kushoto).
IMG_1715
Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund akijisevia minofu ya nyama ya Mbuzi wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo.
IMG_1742
Wageni wakiendelea kupakua chakula.
IMG_1769
IMG_1775
IMG_1798
IMG_1816
IMG_1821
IMG_1756
Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (kulia) na mkewe wakishiriki chakula cha jioni kwenye mgahawa wa Mtanzania mwezao.
IMG_1824
Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kushoto) pamoja na Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu ni miongoni kati ya wageni waalikwa 300 waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_1835
IMG_1838
Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kulia), Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu (kushoto) pamoja na mtoto wa Mwenyekiti wa chama hicho, Grace Saulli wakijichana msosi uliondaliwa na Chef Issa Kapande.
IMG_1866
Wageni waalikwa wakiendelea kupiga msosi uliofurahiwa na wengi ambao utakuwa unapatikana kwa chakula cha mchana kwa kipindi cha mwezi mmoja na hapo baadae itakuwa mpaka chakula cha usiku ndani ya mgahawa wa "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food).
IMG_1869
Mh. Balozi Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund.
IMG_2028
Mgeni rasmi Mh. Balozi Dora Msechu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
IMG_2080
Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Daniel Saulli (kushoto), Mhasibu wa chama hicho, Emmanuel Ntundu (kulia), Katibu wa chama hicho, Mathias Pembe (wa pili kulia) pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
IMG_2265
Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kulia) na Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja kikundi cha burudani.........
IMG_2216
Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya kumbukumbu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
IMG_2237
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja na timu yake kwenye mgahawa huo.
IMG_2041
Mdau Abraham Juma Ndwatta wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden akiwa na Grace Saulli kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
IMG_2074
Wadau wakiendelea kupiga picha na Mh. Balozi Dora Msechu.
IMG_2125
Mh. Balozi Dora Msechu akisakata rhumba kwenye uzinduzi huo.
IMG_2093
Chef Issa Kapande akicheza muziki na wageni waalikwa.
IMG_2119
IMG_2106 _________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa Thehabari.com na Mwenyekiti wa TBN. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com