Benki ya CRDB yawahakikishia dhamana ya kazi na mikopo Wakandarasi

November 07, 2017
Mkurugenzi wa benki ya CRDB, huduma kwa wateja wakubwa, Goodluck Nkini akizungumza kwenye semina kwa Wakandarasi iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanroad pamoja na kampuni ya uuzaji mitambo ya Mantrac.
Semina hiyo ilifanyika jana Jijini Mwanza na kuwakutanisha Wahandisi na Wakandarasi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza.

Na Binagi Media Group
Benki ya CRDB imewahakikishia Wakandarasi upatikanaji wa mikopo pamoja na dhamana ya kazi, itakayowawezesha kuwa na vigezo vya kupata tenda na hatimaye kutimiza vyema shughuli zao.

Mkurugenzi wa CRDB mkoani Mwanza, Wambura Calystus alitoa ahadi hiyo jana kwenye semina kwa wakandarasi wa barabara, iliyoandaliwa na beki hiyo kwa kushirikiana na wakala wa barabara Tanroad mkoa wa Mwanza pamoja na kampuni ya uuzaji na ukodishaji wa mitambo ya Mantrac.

“Miradi ya ujenzi na miundombinu imekuwa mingi katika nchi yetu hivyo tumeona ni bora benki yetu ya CRDB iweze kukaa na wakandarasi ili tuone namna bora ya kuwafikishia huduma waweze kujenga miundombinu hiyo bila tatizo”. Alisema Calystus.

Naye Mkurugenzi wa CRDB huduma kwa wateja wakubwa, Goodluck Nkini alisema ushirikiano baina ya benki hiyo, Tanroad pamoja na kampuni ya Mantrac utawasaidia wakandarasi hususani wadogo kupata mitambo bora ya kufanyia kazi na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.

“CRDB itawezesha wakandarasi kupata mitambo na kuondoa kero iliyokuwepo awali ya wakandarasi kukosa kazi kwa sababu ya kutokuwa na mitambo”. Alisema Meneja Mauzo kutoka kampuni ya Mantrac Kanda ya Ziwa, Eutachius Katiti.

Awali Kaimu Meneja wa Tanroad mkoani Mwanza, Joseph Mwami alikiri kwamba wakandarasi wengi walikuwa wakikumbana na changamoto ya kupata kazi kutokana na kukosa dhamana ya kazi hivyo imani yake ni wakandarasi kutumia vyema fursa hiyo.

Kwa upande wake Mhandisi Emmanuel Mapigano ambaye ni mmoja wa wakandarasi waliohudhuria semina hiyo kutoka kampuni ya MP Investment Ltd, alitoa rai kwa benki ya CRDB, Tanroad pamoja na kampuni ya Mantrac kuendeleza ushirikiano huo ili kuwawezesha wakandarasi kukua na kulijenga taifa kwa umoja.
Wakandarasi waliohudhuria semina hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Mwanza, Wambura Calystus.
Mkurugenzi wa CRDB, wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuke (kushoto), akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Mwanza, Wambura Calystus.

SERIKALI IMETOA BURE MBEGU NA VIUATILIFU KWA AJILI YA KILIMO CHA PAMBA KWA MKOA WA SINGIDA.

November 07, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi mmoja kati ya wa wakulima wa Pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama kilo kumi za mbegu za zao la pamba zilizotolewa bure na Serikali kwa wakulima hao. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga.
 Mkulima wa Pamba Bi Johari kutoka kijiji cha Kinyagiri Wilayani Mkalama akibeba mbegu za Pamba kilo kumi alizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, mbegu hizo zimetolewa bure kwa wakulima wa Pamba Mkoa wa Singida.
 Mama Devid Mkulima wa Pamba wa Kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama akijifunza kwa vitendo namna ya kuandaa kamba inayotumika kuonyesha vipimo vya upana na urefu katika kupanda pamba badala ya kilimo cha mazoea cha kumwaga mbegu bila kufuata kipimo chochote.
 Wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Lyelembo Wilayani Mkalama wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga (hawapo pichani) kabla ya kupewa mbegu za pamba zilizotolewz bure.

Wakulima wa pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama wakimfuatilia kwa makini mtaalam kutoka Bodi ya Pamba Nchini akiwaelekeza namna ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu waharibifu wa pamba, viuatilifu hivyo vitatolewa bure na serikali kwa wakulima wote wa pamba Mkoani Singida.

Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao la pamba mkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kufufua kilimo hicho mkoani hapa.  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katika vijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewa jukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pamba bure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali. 
Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulima mashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba. 
Amesema kuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifu wataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora. 
“Mmepewa upendeleo maalum, kazi yenu sasa ni kulima tu, malipo ya mbegu na viuatilifu vyote italipwa na Serikali. Hapa hakuna kisingizio cha kushindwa kulima”, amesema Mtunga na kuongeza;
“Pandeni vizuri ili wakati mnatumia dawa, kiwango kikubwa cha dawa kisipotee bure maana kama hukupanda kwa mstari lazima kutakuwa na ugumu wa kupulizia mimea yako. Jengeni utamaduni wa kuwatumia wataalamu wa kilimo kama ilivyo kwa wafugaji mifugo yao inapopatwa na maradhi”.  
Aidha, amewataka wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanang'oa masalia yote ya misitu ya pamba na kuichoma moto kwa kuwa, kwa kuacha kufanya hivyo wanaruhusu wadudu waliomo kwenye masalia kuendelea kunenepeana na hivyo kuhatarisha mazao mapya yanayopandwa.  
Mkurugenzi huyo amewasihi wakulima kuacha kuchanganya kilimo cha pamba na mazao mengine akisema kuwa tafiti zinaonesha pamba iliyochanganywa na mazao mengine hutoa vitumba vitatu tu ikilinganishwa na vitumba 10 kwa kilimo cha pamba iliyolimwa peke yake. 

MHE MWANJELWA: UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA UMEONGEZEKA KWA KASI

November 07, 2017
Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali imesema kuwa utekelezaji wa mpango wa Kilimo Kwanza umekuwa na mafanikio katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara nchini ambapo uzalishaji wa jumla wa mazao ya biashara katika msimu wa mwaka 2016/2017 umeongezeka kufikia Tani 881,583 ukilinganisha na Tani 796,562 katika msimu wa mwaka 2015/2016.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amebainisha hayo Leo Novemba 7, 2017 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mkoani Singida Mhe Yahaya Omary Masare aliyetaka kufahamu Kuna mafanikio kiasi gani kwa mazao ya biashara na chakula kwani Katika mpango wa kilimo Kwanza serikali ilihamasisha watanzania kuongeza uzalishaji katika kilimo ili serikali itoe mikopo ya matrekta. 
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa mafanikio ya mpango huo ni makubwa kwani Katika Wilaya ya Manyoni uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kufikia Tani 42,554 katika msimu wa mwaka 2015/2016 ambapo uzalishaji wa mpunga umeongezeka kutoka Tani 1342 mwaka 2011/2012 hadi kufikia Tani 6212 mwaka 2015/2016.
Alisema kwa upande wa Zao la Alizeti uzalishaji umeongezeka kutoka Tani 4464 mwaka 2010/2011 hadi kufikia Tani 21,871 mwaka 2016/2017 wakati huo huo zao la Ufuta uzalishaji umeongezeka kutoka Tani 2285 mwaka 2010/2011 hadi kufikia Tani 8874 katika msimu wa mwaka 2015/2016.
Aliongeza kuwa katika Mkoa wa Singida uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka Tani 453,297 mwaka 2013/2014 hadi Tani 481,452 mwaka 2015/2016.
Uzalishaji wa mazao ya biashara umeongezeka kutoka Tani 184,066 mwaka 2012/2013 hadi kufikia Tani 293,873 katika msimu wa mwaka 2015/2016.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa Jumla ya Matreka yanayofanya kazi nchini ni 18,774 ambapo kati yake Matrekta makubwa ni 11,500 na matrekta madogo ya mkono ni 7274.

VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA

November 07, 2017
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya Wema, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniface Magiri wakati wa uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazi lishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga wilayani humo jana.
 Wanakikundi cha Aliselema wakishusha mbegu ya mihogo tayari uzinduzi wa shamba darasa.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo katika Kijiji cha Isunda kilichopo Kata ya Nkolye.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Isunda.
 Wanakikundi cha Aliselema wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akielekeza namna ya kupanda mihogo.


  Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda mbegu ya mihogo mkuu wa wilaya hiyo.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akipanda mbegu ya mihogo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa akipanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto waliyokuwa nayo ya kupata mazao kiduchu kwa kutumia mbegu zisiso bora.

 Wakulima wakisubiri kuelekezwa namna ya upandaji wa mbegu hizo za mihogo.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Kisanga kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la viazilishe.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda mbegu ya viazilishe katika kijiji cha Kisanga.
 Wanawake wa Kijiji cha Kisanga wakiwa kwenye uzinduzi huo wa shamba darasa la mbegu ya viazilishe.
 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru mkoani Mwanza, Mariana akielekeza namna ya upandaji wa viazilishe.
 Mkuu wa Wilaya, Peres Magiri akipanda mbegu ya viazilishe wakati wa uzinduzi wa shamba hilo.
 Mwalimu wa Baraka Kita wa Shule ya Msingi Sogea B, akipanda mbegu hiyo ya viazilishe.
 Mkulima, Mariam Said akipanda mbegu ya viazilishe 
Mwalimu George Adamu Mwalwizi, akizungumzia mbegu mpya ya viazi lishe walioletewa kuwa itakuwa ni mkombozi kwao na wanafunzi.

Na Dotto Mwaibale, Sikonge Tabora

WANAFUNZI wilayani Sikonge mkoani Tabora wataanza kunufaika na viazi lishe baada ya kupokea mbegu bora ya viazi hivyo, mihogo na mahindi ya Wema kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

Hayo yameelezwa katika Kijiji cha Kisanga na Mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface Magiri wakati akizungumza na wakulima kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazilishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga.

Magiri alisema baada ya kuotesha mbegu hiyo ya viazilishe kwa wingi kitakachofuata ni kuanzisha utaratibu wa wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kupata chakula cha mchana badala ya kwenda nyumbani.

Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa na kutoa mrejesho.

Aliongeza kuwa shule mbalimbali zitaanzisha mashamba ya viazilishe hivyo ili kumaliza tatizo la kukosa chakula kama sio kulipunguza.

"Tunahitaji matokeo chanya ya mashamba darasa hayo yawasaidie wakulima wengine katika wilaya hiyo na kuwa atahakikisha anatembelea mara kwa mara yalipo mashamba hayo" alisema Magiri.

UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUAGIZA CHAKULA UKIWA HAPO ULIPO?

November 07, 2017
Na Jumia Food Tanzania

Katika maisha ya sasa yenye pilikapilika takribani siku nzima, muda umekuwa ni bidhaa adimu na kitu ambacho kinazingatiwa sana. Si jambo la kushangaza kujikuta unapitiwa mpaka kufika saa kumi za jioni haujatia kitu chochote tumboni huku muda ukiwa hauko upande wako tena.

Lazima tukubaliane na uhalisia kwamba kuna wakati muda unakuwa sio rafiki ili kuendana na majukumu tuliyonayo, ukizingatia wengi wetu tukifanya kazi kwa waajiriwa ambao hutulipa kulingana na muda tunaotumia kazini. Ili kukabiliana na changamoto kama hii unahitaji mbadala wa kukufanya uendelee na shughuli zako za siku bila ya kuhofia kupoteza muda na kuhatarisha kazi yako.

Kutokana na maendeleo ya tekinolojia duniani hususani mtandao wa intaneti, hivi sasa kuna mfumo unaokuwezesha ukaagiza chakula na kukufikia papo hapo ulipo. Hii inamaanisha kwamba kama vile unavyokwenda kwenye mgahawa unaoupenda au kuuzoea, ukatazama orodha ya vyakula vilivyopo, bei zake na kuagiza chakula ukipendacho ndivyo Jumia Food inavyofanya.

Ikiwa na orodha ya takribani migahawa 70 tofauti yenye aina ya vyakula mbalimbali jijini Dar es Salaam, Jumia Food inawakutanisha wateja na watoa huduma kwa kuwarahisishia kuagiza chakula kwa urahisi na kuwafikia ndani ya muda mfupi popote pale walipo. Mtu anaweza kuwa anajiuliza kwamba atakuwa na uhakika gani kuwa chakula atachokiagiza kitakuja kama vile alivyotarajia?
Jibu ni rahisi. Tunafahamu kwamba kwa watanzania walio wengi bado ni wageni na huduma za mitandaoni kwa sababu huwa tunapenda kufanya maamuzi ya kufanya manunuzi juu ya bidhaa fulani mpaka tuione, kuigusa pengine kuijaribu. Lakini linapokuja suala la chakula watu wengi huwa wanafahamu mahali wanapopendelea kula, chakula wanachokipendelea, ladha pamoja na bei yake.

SERIKALI YALIPA MADAI YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA TTCL SH. BILIONI 12.7

November 07, 2017
Benny Mwaipaja, Dodoma
SERIKALI imewalipa pensheni wafanyakazi 245 wa iliyokuwa Kampuni ya Simu ya TTCL, chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kiasi cha shilingi bilioni 12.7.

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Ngalawa, aliyetaka kufahamu, lini Serikali ingewalipa wafanyakazi wa TTCL wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki madai ya pensheni yao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa malipo hayo yamefanyika kwa wafanyakazi 245 ambao wamelipwa fedha zao kwa mkupuo ambapo kati yao wastaafu 54 walifariki dunia na malipo yao kulipwa warithi wao.
“Wastaafu 198 wanaendelea kulipwa malipo ya nyongeza ya pensheni ya kila mwezi” alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa malipo hayo yanafuatia uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi namba 69/2005 ambapo wafanyakazi hao 254 waliishitaki Serikali kupinga uamuzi wa kusitisha mfuko uliojulikana kama East Africa Non Contributory Pension Scheme.

 “Katika Shauri hilo, Mahakama Kuu iliamua kuwa, uamuzi wa Serikali kusitisha mfuko huo haukuwa sahihi kisheria na hivyo kuamua wafanyakazi 254 waliokuwa katika shauri hilo walipwe madai yao ambayo yalijumuisha malipo ya mkupuo, riba pamoja na pensheni yao ya kila mwezi” aliongeza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa baada ya uamuzi huo wafanyakazi wengine 324 nao walifungua kesi Makahama Kuu wakitaka walipwe pensheni kama wenzao walivyolipwa wakati hawakuwa sehemu ya wafanyakazi waliofungua na kushinda kesi hapo awali.

“Mahakama Kuu iliamua kuwa, wafanyakazi waliofungua kesi ya awali ndio walipwe madai yao, na kwamba deed of settlement iliyosajiliwa Mahakamani ilihusisha wafanyakazi hao pekee” alifafanua Dkt. Kijaji.

Alisema wafanyakazi wengine ambao hawakuwa sehemu ya kesi hiyo hawawezi kulipwa kwa kutumia hukumu na tuzo ya kesi ambayo hawakuwa sehemu yake na kusisitiza kuwa, Serikali haiwezi kulipa madai mengine ambayo hayakuthibitika kisheria.

TFF YASIMAMISHA MCHEZO WA FORODHANI v AMBASSODOR

November 07, 2017


Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Wakati mchezo wa TFF ikisimamisha mchezo wa Azam Sports Federation Cup kati ya Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama, Mchezo wa Bulyanhulu na Area C, sasa utafanyika kesho Jumatano Novemba 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Mchezo kati ya Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama, umesimamishwa kusubiri uamuzi wa Kamati ya Mashindano baada ya Baruti ambayo imelete malalamiko kuhusu nafasi yake.
Michezo mingine inayochezwa leo Jumanne ni Msange na Mirambo kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi; Pepsi na Kilimanjaro Heroes kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga; Mji Mkuu na Nyundo kwenye Uwanja wa Mpwapwa mkoani Dodoma.
Eleven Stars itacheza na Ndovu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, Changanyikeni itacheza na Reha Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam wakati Bodaboda itacheza  na Kitayosce Uwanja wa Nyerere, Mbulu mkoani Manyara.
Mbali ya mchezo kati ya Bulyanhulu na Area C, mechi nyingine za kesho Jumatano, Novemba 8 zitakuwa ni kati ya Cosmopolitan na Abajalo kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati makumba Rangers watacheza na Green Warriors kwenye Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam.
AFC ya Arusha itaikaribisha Nyanza FC kwenye Uwanja wa Ushirika; Boma Fc na African Sports watacheza kwenye Uwanja wa Ushirika; huku Motochini ikicheza na Ihefu wakati Stand Misuna watacheza na Madini ilihali Burkina FC itaialika Mbinga United kadhalika Mkamba Rangers itacheza na Makambako FC kwenye Uwanja wa Sabasaba.

KATIBU MWENEZI CCM EDWIN BASHIR WAPINZANI ACHENI SIASA ZA MAJI TAKA

November 07, 2017
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru katika uchaguzi mdogo wa kumpata diwani atakayekuwa kiongozi wa kata hiyo huku CCM wakimuombea kura mgombea wao Baraka Kimata 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Kitwiru

Na Fredy Mgunda,Iringa

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kufanya siasa safi kwa kutoa hoja za msingi wakati wanaomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru unaoendelea hivi sasa.
 
Akizungumza na blog hii Bashir alisema kuwa wapinzani wamekuwa wakitoa lugha za matusi kwa wananchi wakati wakiomba kura majukwaani.

“Kila wakisimama jukwaani ni matusi tu utafikiri ndio kura zenye mimi naomba watumie lugha za kistaarabu kuomba kura kwa wapiga kura kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na kuwafanya wananchi kumchagua kiongozi wanaemtaka” alisema Bashir

Bashir alisema kukitukana chama chama mpinduzi ni kukikosea heshima kwa kuwa chama hicho kimekuwa kikifanya kampeni za kistaarabu bila kutoa maneno ya machafu kwa wapinzani na kuendelea kuwaaminisha wananchi kuwa CCM inafanya kampeni za kistaarab.

“Yaani saizi wakisimama kwenye majukwa kazi yao ni kutoa lugha chafu dhidi ya chama chetu hivyo mimi nawaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watulivu na kuhakikisha mgombea wa chama cha mapinduzi anashinda kwa kishindo” alisema Bashir

Aidha Bashir aliwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura mgombea wa chama cha mpinduzi (CCM) ambae atawaletea maendeleo kwa kufuata na kutekeleza vilivyo ilani ya chama hicho kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayofanya.

“Huku CCM kuna mfumo ambao unawaongoza viongozi wetu na mambo mengi yanafanywa kwa kufuata utaratibu hivyo wananchi wanatakiwa kumwamini Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata ya Kitwiru” alisema Bashir

Bashir amewataka viongozi wa CCM kutumia lugha nzuri wakati wa kuomba kura na matusi kuwaachia wapinzani na kutengeneza utofauti baina ya CCM na vyama vingine.

“Niwaombe wanakitwiru kuhakikisha tarehe ishirini na sita mwezi huu Baraka Kimata anaibuka mshindi katika uchazi huu mdogo wa kata hiyo” alisema Bashir

Lakini Bashir amewahakikishia wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watashinda kwa kishindo kutokana na mikakati ya chama hicho ambayo ipo imara na dhabiti kwa ajili ya kushinda kata hiyo.

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2018/19 NA MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2018/19

November 07, 2017


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

  
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI  MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2018/19 NA MWONGOZO
WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI
KWA MWAKA 2018/19


                                                            

1.          Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likae kama Kamati ya Mipango ili kupokea na kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2018/19 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2018/19.

2.          Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya. Aidha, tunamshukuru sana kwa kuendelea kulijalia Taifa letu amani na utulivu na kutuwezesha kukutana katika mkutano huu wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujadili namna ya kuharakisha maendeleo ya nchi yetu.

3.          Mheshimiwa Spika, kipekee napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini kuongoza Wizara ya Fedha na Mipango kufuatia mabadiliko aliyoyafanya hivi karibuni katika Baraza lake la Mawaziri na safu ya uongozi wa Mikoa. Aidha, ninawapongeza Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wakuu wa Mikoa waliobakia katika nafsi zao na wale waliobadilishwa vituo vya kazi. Vile vile, ninawapongeza kwa dhati wote walioteuliwa kuwa Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wakuu wa Mikoa wapya.

4.          Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hii adhimu kutambua na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri na makini katika kusimamia rasilimali za Taifa, kupambana na rushwa, kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma na zaidi ya yote, kwa moyo wake adili katika kupatia majibu kero za wanyonge. Hakika uongozi wake umezidi kuijengea heshima kubwa nchi yetu.

5.          Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kumpongeza Mhe. Janeth Masaburi (Mb) aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge katika Bunge lako Tukufu hivi karibuni kutoka Chama Tawala cha CCM. Aidha, nawapongeza kwa pamoja Waheshimiwa Alfredina Apolinary Kahigi, Kiza Hussein Mayeye, Nuru Awadh Bafadhili, Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Mtamba, Sonia Jumaa Magogo, Rehema Juma Migilla na Zainab Mndolwa Amir walioteuliwa na Chama cha Wananchi - CUF kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninapenda kuwakaribisha na kuwashauri watumie jukwaa hili kikamilifu katika kuishauri Serikali na kuwatumikia wananchi. Napenda pia kumpongeza Bw. Stephen Kagaigai kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

6.          Mheshimiwa Spika, ninawiwa pia kutoa shukrani za dhati kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb) na watendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu, Bw. Doto Mgosha James kwa ushirikiano walionipa katika maandalizi ya hotuba hii na vitabu vya Mapendekezo ya Mpango na Mwongozo. Aidha, ninawashukuru sana Wizara, Taasisi, Idara za Serikali, Sekta Binafsi na wadau mbalimbali waliotoa maoni na michango yao katika kukamilisha Mapendekezo ya Mpango na Mwongozo.

VIDEO.........."SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA". DK. KIGWANGALLA

November 07, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuaza ziara ya kukagua maeneo hayo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana, pamoja na mambo mengine alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa kwa tuhuma za rushwa na kuhujumu jitihada halali za Serikali za kumaliza mgogoro huo. Aliagiza Mkurugenzi huyo afikishwe TAKUKURU kwa uchunguzi wa tuhuma hizo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa  mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari. 

AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI

November 07, 2017
 mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za   kupandisha ngazi ya  rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika ya uzee (habari picha  na  woindeshizza blog )


 mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika  la Nyangulo   
RC MRISHO GAMBO: NAJIVUNIA KUWA MTEJA WA NMB

RC MRISHO GAMBO: NAJIVUNIA KUWA MTEJA WA NMB

November 07, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta (kati kati) akisoma jiwe la msingi mara baada ya ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mto wa Mbu lililopo katika Wilaya ya Monduli. Hafla hii ya Uzinduzi imefanyika mwishoni mwa wiki. Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini –Salie Mlay pamoja akishuhudia. 
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta (kati kati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mto wa Mbu lililopo katika wilaya ya Monduli . Hafla hii ya Uzinduzi imefanyika mwishoni mwa wiki. Kwanza kulia ni Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini –Salie Mlay pamoja na Meneja wa NMB Tawi la mto wa Mbu wakishuhudia uzinduzi huo.
RC MRISHO GAMBO; NAJIVUNIA KUWA MTEJA WA NMB "Nawapongeza sana NMB wamefanya huduma za kipenki kuwa rahisi kuliko kitu chochote kwangu. Nikihesabu nimara ngapi nimekwenda benki kwa mwaka mzima haitofika hata mara tano. Lakini natumia huduma za kibenki kila siku. Ninajivunia kuwa mteja wa NMB. Natumia simu yangu kufanya miamala tofauti tofauti na inanisaidia kutumia muda wangu vizuri..NMB Mobile imekua mkombozi wangu na hata kwa wengine pia. Kwa kweli NMB mnastahili pongezi juu hili kwa kua NMB Mobile imekua mkombozi wa Muda pia…." Alisema Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipozindua Tawi la NMB Ngaramtoni. NMB imezindua matawi mengine mapya matatu katika mikoa ya kaskazini ikiwapo Moshi na Arusha. Hii ni moja ya jitiahada zinazofanywa na uongozi wa benki ya NMB ili kuhakikisha kwamba huduma za benki zinamfikia kila mwananchi kwa ukaribu na uharaka wa huduma za kibenki. Wiki iliyopita kwa mfululizo benki imezindua tawi la NMB Mbuyuni lililopo katika Manispaa ya Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Anna Mghwira alizinua tawi hili, Tawi la NMB Ngaramtoni lilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo. Tawi hili lipo katika Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arumeru pamoja na Tawi la NMB Mto wa Mbu tawi hili lipo ndani ya mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Monduli na Mgeni rasmi alikua Mhe. Iddy Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Monduli. Matawi haya yote ni mapya kabisa na yatatoa huduma za kibenki kama Matawi mengine ya NMB Matawi haya yote matatu yamekua neema kubwa sana kwa wakazi wa wilaya hizi kutokana na adha waliyokua wakiipata awali ya kwenda katika wilaya nyingine za jirani ili kupata Huduma za kibenki. Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wateja wa NMB walisema kwamba haikua kazi rahisi kwao kusafiri mwendo mrefu wakiwa wamebeba pesa nyingi baada ya kuwa wameuza mifugo na mazao yao kwenye minada mbalimbali. Kuna mfanyabishara mwenzetu wiki iliyopita alinusurika kuibiwa fedha zake karibu kabisa na dukani kwakwe. Tatizo lake alikuwa anaweka mauzo yake ya zaidi ya wiki anaweka kwenye ndoo ndani ya duka lake. Inapofika wiki mbili ndipo anapeleka fedha zake benki. Sasa hivi NMB wapo hapa karibu halafu pale pale karibu Sokoni kuna wakala wa NMB. Imekua rahisi sana kwetu hatutarajii kusikia tena habari za wafanyabiashar akuibiwa tena. Tunawashukuru sana NMB kwa kujua hitaji letu la muda mrefu….Alisema Elibariki Kimario Mkazi wa Moshi mjini. Uzinduzi wa matawi haya matatu katika mkoa wa kilimnajaro na Mkoa wa Arusha unafanya NMB kua na matawi zaidi ya 2012 nchi nzima pamoja na Mashine za kutolea fedha zaidi ya 800 Mawakala 4100 nchi nzima. Ni kusudio letu kwamba tuweze kuwafikia wateja wetu kila mahali walipo na wasipoteze muda mwingi kupata huduma za Kibenki. Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB Ngaramtoni.  
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba mbali mbali zilizokua zinaendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Mto wa Mbu lililopo katika Wilaya ya Monduli. Hafla hii ya Uzinduzi rasmi imefanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya tawi la NMB Mto wa Mbu.