RC GAMBO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUACHA DHANA YA KUOGOPA KUSTAAFU

May 29, 2017



Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF jijini Arusha juzi ,wakati akifunga mkutano huo ambapo aliwataka wastaafu watarajiwa kujiandaa kustaafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya kuongeza kipato hali itakayosaidia wao kujiendeleza kimaisha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema watumishi wakajianda mapema wakiwemo wa umma na sekta binafsi .
Mkurugenzi wa mfuko wa GEPF Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa bodi Ya wadhamini,wa mfuko huo Joyce shaidi akizungumza katika mkutano huo.
Kulia ni mkuu wa kitengo cha kusimamia amana za wawekezaji katika benki ya CRDB Bw.Masumai Ahmed.

Wadau wa mkutano wakiwa wamesimama kuashiria kumalizika kwa mkutano huo
KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO

KIFAA CHA DIJITALI KUWAWEZESHA WAKULIMA WADOGO TANZANIA KUPATA FEDHA, PEMBEJEO NA MAFUNZO

May 29, 2017
Wakulima wadogo nchini Tanzania hivi karibuni wataweza kupata taarifa mbalimbali za kijiditali kuhusu masuala ya pembejeo, ukiwemo ushauri utakaosaidia kutatua matatizo yanayowakabili kama vile upatikanaji wa fedha, pembejeo na mafunzo. 

Mradi huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali, wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu, wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na biashara za mazao ya sekta ya kilimo. Kifaa hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu. Pia kifaa hicho kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya pembejeo hizo. “Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA). “Kifaa hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni ufumbuzi wa kipekee. 

Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.

” Wakulima wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo. 

Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo. Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.

Badala yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo. Isitoshe, wakulima wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha kisasa wanashindwa kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa vile ni asilimia 6 tu ya mikopo ya benki ndio imetengwa kusaidia sekta ya kilimo. 

DKT.KIGWANGALLA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA MKURANGA

May 29, 2017
Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani. Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo. Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya. Awali wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa uangalifu wa hali juu huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika kusaidia wananchi wake. “Nimesikia kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine ya X-Ray na na vifaa vingine muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na tunawaomba muwe na imani na Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya jambo hilo. Hospitali ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa vifaa ikiwemo mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali katika tukio hilo. Tazama hapa kuona tukio hilo:
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amsikiliza Mbunge wa Mkuranga Mh. Abdallah Ulega katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Baadhi ya wazee wa Mkuranga
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga akisoma taarifa
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga

UNESCO KWA KUSHIRIKIANA NA GPF TANZANIA WAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA ,CHUO KIKUU CHA MWALIMU NYERERE

May 29, 2017
Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere  na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Bw. Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi  Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
 Mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

May 29, 2017
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya  biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akisalimiana na mmoja wa watumishi Tanapa wakati wakati alipotembelea banda lao kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiendelea na shughuli ya kukagua mabanda ya Maonyesho
Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao

 Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga katika Banda lao lililopo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunapofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tano kutoka kushoto ni Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo katikati ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu na kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens
 kulia ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens wakimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alifika kwenye banda lao kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo
 Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens kulia akisitiza jambo kwa mkazi wa Jiji la Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali muhimu ikiwemo za matibabu kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu katikati ni  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia kwake ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Sabrina Komba

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa tayari kutoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga kuhusu namna wanavyoweza kunufaika kupitia mfuko huo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kuhusu faida za wakazi wa Jiji la Tanga kujiunga na mfuko huo lakini pia namna walivyojiandaa na ujio wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga

HOSPITALI YA MKURANGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO-DK.KIGWANGALA

May 29, 2017
Na Chalila Kibuda ,Globu ya  Jamii
Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana kuanzishwa kwake kulianzia katika zahanati.
Hayo ameyasema na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya  Mkuranga,  amesema Hospitali ya Mkuranga kuanzia majengo kuwa mbalimbali tofauti na inavyotakiwa.
Amesema katika ziara hiyo amesema hata mfumo wa kuhifadhi taka katika hospitali hiyo hauko sawa pamoja  na hali ya usafi katika wodi ya wazazi.
Dk.Kigwangala amesema kutokana na mazingira yaliyopo katika hospitali itachukua hatua katika kuiweka hospitali hiyo kwenye .ubora mzuri.
Aidha amesema Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amekuwa bega kwa bega na hospitali ya  Mkuranga  ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau katika kusaidia hospitali katika maeneo mbalimbali.
Dk. Kigwangala amesema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali  kujitoa katika kufanya masuala mengine bila kusubiri serikali kuu ikiwa ni pamoja na kutenga siku ya kufanaya  usafi katika hospitali hiyo.
Nae Mbunge wa  Mkuranga , Abdallah Ulega amesema ziara ya Naibu Waziri huyo itazaa matunda kwa hospitali ya Mkuranga kuwa na sifa ya hospitali ya Wilaya.
Amesema  watakuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwa mara moja kwa wiki hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri wakati ziara yake katika Hospitali hiyo. .(picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri katika ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala.

“MRADI WA BOMBA LA MAFUTA WAIVA”

May 29, 2017


 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
 Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo


MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.


Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya nchi na nchi (Iga) kukamilika.


Hayo yalisemwa leo na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.


Alisema tayari wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka 100.


Awali akizungumza kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za kudumu na muda mfupi.


Alizitaja fursa ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga kiuchumi.


“Hivyo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP) SIMON SIRRO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP) SIMON SIRRO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

May 29, 2017
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akisaini Hati ya Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba,IGP mpya Simon Sirro,  IGP wa zamani Ernest Mangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro pamoja na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba mara baada ya tukio la uapisho wa IGP Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU