TANGA YAWATAKA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI INDIA KUWEKEZA ILI KUWEZA KUNUFAIKA KUTOKANA NA UWEPO WA RASILIMALI NYINGI ZILIZOPO

November 27, 2016
Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.
Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye
Balozi wa India nchini Sandeep Arya kushoto akiteta
jambo na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye katikati wakati wa kongamano la wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga uliofanyika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini India na
Tanga wakimfuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara juzi kwenye ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka nchini India kuwekeza mkoani hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo kilimo,utalii,elimu na Afya ili kuweza kunufaika nazo.

Mwilapwa alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na Mkoa wa Tanga.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza kuleta tija ya kimaendeleo.

Alisema kuwa India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya ukuaji wa maendeleo.

   “India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo “Alisema.

Awali akizungumza Balozi wa India nchini, Sandeep Arya alisema ujio wa Waziri Mkuu wa India Tanzania umeongeza ari kwa Taifa ilo kuona haja ya kuendelea kuwekeza na kusaidia katika masuala mbalimbali ya afya, Elimu Bishara na Kilimo.

Alisema kuwa soko la India linahitaj bidhaa zenye ubora na rahisi hivyo anaamini kutokana na ushirikiano wa nchi hizi mbili kufanana mahitaji kutakuwepo na fursa kubwa ya muingiliano wa kibiashara ambao utaleta tija na faida kwa pande zote mbili.

Hata hivyo alisema licha kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, matibabu ya kansa lakini wanatoa nafasi 350 za mafunzo nchini india kila mwaka ili kuwapatia nafasi watu kujifunza jinsi India inavyofanya kazi katika shughuli zake za uzalishaji.

Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikaribishwa kuzungumza alisema moja kati ya mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ni kuhakikisha inakuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi wa hali ya nchi hivyo hakuna haja ya wananchi kukata tamaa.

Nape alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuzitumia fursa zilizopo hapa nchini ili kuhakikisha zinaleta manufaa kwa wananchi kwa kukuza vipato vyao na hata kuongeza pato la Taifa.

WANAOWABEZA MAWAZIRI WA MAGUFULI KUWA HAWAMSHAURI NA WANAMUOGOPA WAMECHEMSHA – MPINA.

November 27, 2016


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akivalishwa Scarf na Kijana Mussa Sulumbi baada ya kuwasili katika viwanja vya makao makuu ya Jimbo vilivyopo katika mji mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu.


Pichani, sehemu ya Hadhara iliyokuwepo katika mkutano wa Chama Cha Mapinduzi jimboni Kisesa.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akihutubia wananchi wa Jimbo lake hawapo pichani katika mkutano wa kuelezea mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya CCM na utatuzi wa changamoto za jimbo la Kisesa. (Picha, Habari na Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais)



Diwani wa Kata ya Lugeka (CHADEMA) Mhe. Zakayo Sarya akiongea mbela ya Hadhara haipo Pichani, akisimama pamoja na madiwani wa Jimbo la Kisesa katika mkutano wa CCM jimboni humo.



Na Evelyn Mkokoi – Mwandoya Meatu
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye Pia ni Mbunge wa jimbo la Kisesa Wilayani Meatu, amesema waowabeza Mawaziri wa Rais Magufuli na kusema kuwa wanamuogopa na kuwa hawawezi kumshauri wamechemsha na wanajidanganya.
Naibu Waziri Mpina (MB) ameyasema hayo leo jimboni Kisesa alipokuwa katika Mkutano na Jimbo wenye lengo la kuelezea mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utatuzi wa Changamoto za Jimbo Hilo.
Mpina alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano wamekuwa wakibezwa kwa kile kinachonadaiwa wanamuogopa Mheshimiwa Rais na hawawezi kumsogelea na kumpa ushauri.
“Naenda kinyume na kauli hiyo kwani hao wanaosema hivyo hawaoni tunachokifanya kuzunguka usiku na mchana kutatua kero za wananchi hii ni katika kutekeleza azma ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla ya kuwafikia wanachi na kusikiliza na matatizo yao, juzi nilikuwa Kahama, nikaenda Geita na Singida na leo nipo Hapa Mwandoya ningefika vipi huko bila wananchi kuleta shida zao”. Alisisita Mpina.
“Serikali imeweza kurudisha Hekta nyingi za ardhi zilizokuwa zikimilikiwa na watu binafsi kama Sumaye na zitarudishwa kwa wananchi, leo mnasema vipi Mawaziri wa Magufuli hawamshauri”. Aliuliza Mpina.
Akiendelea kuongea na wana Kisesa Mbunge wa Jimbo Hilo Naibu waziri Mpina, aliongeza kwa kusema kuwa, Pia Ndege aina ya Bombardier Q400 zilizonunuliwa na serikali pamoja na upanuzi wa barabara akitolea mfano wa Barabara ya Mwenge Jijini Dar es Salaam na Barabara ya Airport ya Mwanza, vyote vimefanyika na bado watu wanabeza bila kuona kama Mawaziri wana Mchango na wanamsaidia Mhe. Rais Magufuli.
Akiendelea kusikiliza changamoto za wanakisesa ikiwa ni pamoja na changamoto ya eneo la makaburi na standi ya Mwandoya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu Bw. Mussa Isaac Mpina alilitoea ufafanuzi na kusema kuwa jambo hilo lipo katika mpango wa fedha wa mwaka unaokuja hivyo linasubiri utekelezaji.
Akizitaja baadhi ya changamoto zilizotatuliwa Jimboni Kisesa ikiwa ni pamoja na Barabara, Mitandao ya simu, upatikanaji wa maji safi na salama, na kuwepo kwa Zahanati katika mji mdogo wa Mwandoya, Mhe Mpina alisema kuwa ndani ya muda Mfupi zahanati hiyo itapata vifaa vya kisasa vya Ultra-Sound, X-Ray na Fridge la kuhifadhia Damu kwani Zahanati hiyo imeshakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kutoa huduma ya uzazi.
Akiongea kabla ya kuanza kwa Mkutano huo Diwani wa kata ya Lugeka CHADEMA mhe.Zakayo Sarya Maarufu kwa jina la Trump, alisema uchaguzi uliisha wakati alipotangazwa mshindi, kazi inayofuata ni utekelezaji wa masuala ya maendeleo bila kujali itikadi za vyama vyetu.
“ Nawashangaa sana wapinzani wenzangu wa wanaobeza mambo mazuri anayofanya Mhe, Rais mimi Binafsi nampongeza sana kwa jitihada zake za kuleta maendeleo bila kubagua vyama, rangi, dini wala kabila.
Awali akihutubia Mkutano huo Naibu waziri Mpina aliwashuru wana Kisesa kwa kumuamini na kumuweka madarakani tangu 2005 akiwa kijana mdogo na kuhaidi kuwatumikia bila ubaguzi wa aina yoyote kwa manufaa ya taifa.

AMIRI JESHI MKUURAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 59/15 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 27, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipatiwa maelezo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mondululi kuhusu zoezi la   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipatiwa maelezo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mondululi kuhusu zoezi la   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinti wakielekea kwenye uwanjani tayari kushuhudia  zoezi la   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Sehemu ya  Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Kikosi cha Fanfare kikiwa tayari kwa  zoezi la   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akielekea kugagua gwaride kabla ya kutunuku   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua kikosi cha Brass band wakati wa zoezi la   kutunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimzawadia mmoja wa  Maafisa Wanafunzi bora wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa zawadi kwa mmoja wa  Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa zawadi kwa  mmoja wa  Wanafunzi bora wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi bora wa kike wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni  kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  wakila kiapo cha Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) wakivishana vyeo baada ya kutunukiwa kamisheni  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  wakivishana vyeo baada ya kutunukiwa kamisheni Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  wakivishana vyeo Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Kikosi cha Fanfare wakati wa  zoezi la   kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016



Kwisha kwa zoezi la   kutunukiwa kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016 kunafuatiwa na maonesho mbalimbali

Brass Band ya JWTZ likisindikiza maafisa wapya
Maafisa waandamizi wa jeshi wakishuhudia  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Maafisa waandamizi wa jeshi wakishuhudia  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Wageni waalikwa na maafisa waandamizi wa jeshi wakishuhudia  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Wageni waalikwa wakishuhudia  zoezi la kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Wageni waalikwa na maafisa waandamizi wakishuhudia  zoezi la kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Wageni waalikwa na maafisa waandamizi wakishuhudia  zoezi la kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Meza kuu
Meza kuu
Wakuu wa majeshi wastaafu