MICHEZO YA LIGI KUU MWISHONI MWA WIKI

MICHEZO YA LIGI KUU MWISHONI MWA WIKI

October 28, 2016
Wakati Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiendelea leo Ijumaa Oktoba 28, 2016 kwa mchezo mmoja, kwa siku ya kesho Jumamosi Oktoba 29, mwaka huu kutakuwa na michezo mitano wakati kwa siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili—michezo yote ikiwa ni ya raundi ya 13, ligi ikielekea ukiongoni mwa mzunguko wa kwanza.
Leo Kagera Sugar inacheza dhidi ya Azam FC katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati kesho itakuwa ni zamu ya Toto Africans ya Mwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Keshokutwa Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

ILIVYOKUWA KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA OMAR KOPA JIJINI MWANZA.

October 28, 2016
Malikia wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Na BMG
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Wananzengo wakifurahia burudani iliyotolewa kwenye Usiku wa Mshike Mshike na 102.5 Lake Fm
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Wananzengo kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ikijitambulisha kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Madjz wa 102.5 Lake Fm, Dj Hcue (katikati), Dj KFlip (kushoto) na Dj Dhifa (kulia)
Dj Dhifa
Dj KFlip (kushoto) na Dj Hcue
Khadija Omar Kopa akihojiwa na wanahabari baada ya show
Hakika 102.5 Lake Fm Mwanza ni Raha ya Rock City na ni Redio ya Wananzengo. Kaa tayari kwa show ijayo.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YAONGEZA VYANZO VIWILI VYA MAJI

October 28, 2016
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Prof Faustine Bee (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge kuelekea katika chanz cha Mkashilingi kilichopo wilyani Hai kwa ajili ya uzinduzi, kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).Joyce Msiru.
Waziri wa Maji na Uwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanzo cha maji cha Mkashilingi kilichopo  wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wakimsilikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa chanzo cha Mkashilingi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kujionea chanzo cha maji cha Mkashilingi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwasili atika chanzo kingine cha Kaloleni kwa ajili ya uzinduzi rasmi ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru.
Chanzo cha Maji cha Kaloleni.
Chumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya maji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji cha Kaloleni.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizindua mradi wa maji wa Kaloleni.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Gerson Lwenge akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.
Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee akiotesha mti katika chanzo hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA JANE GOODALL INSTITUTE

WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA JANE GOODALL INSTITUTE

October 28, 2016
kima1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Jane Goodall, mara baada ya Mhe. Waziri Makamba kutembelea Ofisi zao Kigoma Mjini. Wa kwanza kulia ni Bi. Mary Mavanza Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa kuhifadhi mfumo wa Ikolojia Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Samson Anga
kima2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa katika boti Maalumu kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe
kima3
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Bw. Donatus Bayona (kulia) na Bi.Happy Kiyemi Mkuu wa Idara ya Utalii wakimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kutembelea Hifadhi ya Gombe
………………………………………………………
Na Lulu Mussa- Kigoma
Shirika lisilo la Kiserikali la Jane Goodall linalojishughulisha na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori wengine limepongezwa kwa jitihada zake za kutunza mazingira na kusaidia jamii kuhifadhi mfumo wa ikolojia ukanda wa Magharibi mwa Tanzania.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba mara baada ya kutembele Ofisi zao Mkoani Kigoma. Waziri Makamba amesema kuwa Shirikal hilo la Jane  Goodall limekuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi ambayo inagusa jamii moja kwa moja.
Akitoa maelezo ya shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo kwasasa, Naibu Mkurugenzi wa Bi. Mary Mavanza amesema kuwa wanatekeleza miradi mitatu ikiwa ni pamoja na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori, Mradi wa Mizizi na chipukizi ambao unatekelezwa nchi nzima katika shule  zote na mradi wa uhifadhi unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Mpanda, Nsimbo kwa Mkoa wa Katavi na Uvinza kwa Mkoa wa Kigoma.
Aidha, Shirika hili pia limefanikiwa kuhamasisha wanajamii 42 kufanya shughuli za kukuza kipato ambazo ni rafiki kwa mazingira kupitia ufugaji nyuki na  huduma za ki ikolojia. Pamoja na mafanikio hayo shirikali hili limewasilisha hoja ya kwa Waziri Makamba kusaidia kukamilika kwa Mchakato wa kupandisha hadhi ya ardhi jumla kuwa misitu ya Hifadhi ya Wilaya ili kudhibiti idadi kubwa ya sokwe waliobaki Tanzania ambao kwa sasa hawana ulinzi thabiti.
Taasisi ya Jane Goodall liliasisiwa miaka 56 iliyopita na mtafifiti Dr. Jane Goodall kwa lengo la kufanya shughuli za kitafiti, kurejesha uoto wa asili uliopotea na kuhakikisha wanajamii wanaboresha uchumi wao kwa kutumia maliasili zinazowazunguka.
Waziri Makamba pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kufuatilia changamoto za kimazingira Hifadhini hapo.

Bia ya Serengeti yasherehekea kutimiza miaka 20

October 28, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari  ambapo alitangaza maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Anayefuatia ni Meneja masoko wa SBL  Anitha Msangi na kulia  mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka  .Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam

Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL  Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.

Mpishi Mkuu mtanzania  Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchini kupata  kinywaji hiki  cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.


 Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko  Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema leo katika hotel ya Hyatt Regency
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema leo

  • SBL yaizindua bia hiyo katika muonekano mpya

  • Yashinda zaidi ya medali 10 za ubora wa kimataifa

Dar es Salaam  Oktoba 27, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo  imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja  wake na umma wa Watanzania  kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.

 “Tunawashukuru  wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote  ambao kimsingi wametusaidia  na kuwa nasi  katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.

Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa  ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.

Aidha Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.

“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager  katika  ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa  na wateja wetu wa ndani  pamoja na medali  zaidi ya 10  za kutambulika kimataifa  ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager  katika ubora wa hali ya juu  kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema Weesie.

Uzinduzi wa muonekano mpya wa  bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.


MPIGIE KURA KARIM MICHUZI KWENYE SHINDANO LA AIRTEL VIDEO CHALLENGE

October 28, 2016

MPIGIE KURA KIJANA WETU KARIM MICHUZI ILI KUWEZESHA SHORT FILM YAKE YA "KA MBU" KUSHINDA SHINDANO LA AIRTEL VIDEO CHALLENGE. BONYEZA HAPA ILI UPIGE KURA...

BENKI YA POSTA YAJENGA CHOO CHA SH.MILIONI 14.5 SHULE YA MSINGI PANDE JIJINI TANGA

October 28, 2016
 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses katika akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Vyoo katika shule ya msingi Pande ambavyo limegharimu kiasi cha sh.milioni 14.5 kushoto ni Afisa Kilimo na Mazingira Jiji la Tanga,Ened Mzava na kulia ni Afisa Elimu Sayansi Kimu, Rukia Magogo 


 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses akizundua Jengo jipya la Choo cha Shule ya Msingi Pande ambalo wamelijenga.
 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses pamoja na wageni wengine wakipiga makofi mara baada ya kulizundua jengo hilo
 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses kulia akipongezwa na mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pande,Mathias Anthony mara baada ya kuzindua Jengo la Choo


 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses katikati akielekea kuzindua Jengo hilo
Afisa Elimu Msingi wilaya ya Mkinga,Zakayo Mlenduka akizungumza kwenye halfa hiyo

 Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses wa tatu kutoka kushoto akionyeshwa choo za zamani ambacho kilibomoka na Afisa Kilimo na Mazingira Jiji la Tanga,Ened Mzava wa tatu kulia wakati alipotembelea eneo hilo
Choo cha zamani ambacho kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi wa shule hiyo ambacho kilianguka