MTANDAO WA WANAWAKE WAZINDUA ILANI YA UCHAGUZI JIJINI DAR

September 01, 2015

 Mkurungenzi Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Edda Sanga akizungumza na wananchi juu ya uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba na uchumi leo jijini Dar es Salaam.
Mkurungenzi Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Edda Sanga akizidua ilani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba na uchumi leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi (katikati) akiwa na wanawake walioshika mabango ya ujumbe mbalimbali katika uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba na uchumi leo jijini Dar es Salaam.
Mgombea uraisi kupitia chama cha ACT Wazalendo, Anna Ng’hwira akishangiliwa na wanawake walifika katika uziduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari juu ya wanawake wapiga kura wakatae kuuza haki zao kwa kurubuniwa na vyama, viongozi au watu wenye uchu wa madaraka na tabia ya kuzalilisha wapiga kura wao leo jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nainokanoka Arusha akizungumza na waandishi wa habari juu ya matumizi ya lugha ya kashfa hasa zenye kudhalilisha wagombea wa kike wenye ulemavu na changamoto nyingine.
Sehemu ya wananchi walihudhulia uzinduzi huo leo Jiji Dar es Salaam( Picha na Emmanuel Massaka)

AFRIKA KUZINGATIA VIPAUMBELE VYAKE WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MALENGO MAPYA YA MAENDELEO

September 01, 2015

 Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza siku ya Jumanne, wakati  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio linalowasilisha kwa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali  Malengo na Ajenda mpya za Maendeleo Endelevu ( Ajenda 2030)   Anaonekana pia Rais wa Baraza Kuu la 69, Bw. Sam Kutessa .
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akiwa na Afisa Mkuu Siongelael Shilla wakati wa upitishaji wa Azimio  namba A/69/L.85   kuhusu Ajenda 2030  ambapo baada ya kupitishwa  kwa kauli moja azimio hilo wazungumzaji  wanaowakilisha  makundi ya kikanda walipata fursa ya kuelezea misimamo yao juu ya  baadhi ya   mambo ambayo walikuwa wakitofautiana kimtizamo na kimsimamo.
Na Mwandishi Maalum,   New York
AFRIKA,  imesisitiza  na kubainisha kwamba  itatekeleza malengo mapya ya maendeleo endelevu kwa  kuzingatia  maslahi, vipaumbele, sera,   mila na tamaduni ambazo nchi za Afrika  zimejiwekea.

Aidha  Afrika inasema kuwa,  utekelezaji wa  malengo hayo    pia utazingatia  sheria za kimataifa  na ambazo nchi  za Afrika  zimeridhia na si vinginevyo.

 Hayo yameelezwa na  Balozi Fode Seek,  Mwakilishi wa Kudumu  wa Senegal katika Umoja wa Mataifa ambaye ni  Mwenyekiti wa    nchi za Afrika   kwa mwezi Septemba.

  Alikuwa  akizungumza  kwa  niaba ya  nchi   za Afrika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana  siku ya jumanne, kupitisha Azimio namba A/69/L.85  ambalo linawasilisha  ajenda ya  Maendeleo Endelevu (ajenda 2030) itakayotekelezwa kwa miaka   15 ijayo.
Ajenda 2030 inachukua nafasi ya   Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayofikia ukingoni  mwishoni mwa  mwaka huu.

Kupitishwa kwa  azimio hilo  la ajenda 2030, inayojumuisgha  malengo 17 na ambalo sasa litawasilishwa  baadaye mwezi huu wa Septemba   kwa Viongozi Wakuu wa  Nchi na Serikali tayari kwa kuridhiwa na  kuanza utekelezaji wake mwakani, kunakamilisha mchakato  uliodumu kwa  zaidi ya miaka miwili ya majadiliano yaliyozaa malengo mapya na ajenda mpya.
“Afrika  itashirikiana na  wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa malengo haya  yanayolenga  katika kuondoa umaskini, kuboresha huduma za jamii,  upatikanaji wa fursa za maendeleo na ajira  na bila ya  kumwacha yoyote nyuma. Lakini  tutatekeleza kwa kuzingatia  mipango yetu, vipaumbele vyetu, sera  zetu na kwa  maslahi ambayo  ambayo kila  nchi itaona inafaa  kutoka na mazingira na uwezo wa nchi  yenyewe” akasema Balozi. Seek

Baadhi ya mambo ambayo Afrika inasema  kimsingi haikubaliani katika ujumla wake na ambayo kwayo utekelezaji wake utazingatia utashi wa kila nchi,   kuzingatia Imani za kidini,  mila na tamaduni na  sheria  za nchi husika ni pamoja na  tafsri sahihi ya neno familia ambalo  Afrika na baadhi ya  nchi nyingine  inasema  familia ni  Baba, Mama na  watoto na si  tafsili ile inayopigiwa chapuo na baadhi ya nchi za  magharibi.

Jambo  jingine ambalo   Afrika na   Nchi nyingine   imetoa msimamo ,   linahusu tafsiri ya  jinsia ambayo kwa Afrika inaamini kwamba jinsia ni ya kike na kiume.

  Utolewaji   na upatikanaji wa   huduma za afya, elimu na mafunzo yanayoambatana na eneo hilo  na  hususani uzazi wa mpango, ni eneo jingine ambalo Afrika na mataifa mengine yanayoendelea  yanasisitizia kuwa utekelezaji wake usiwe wa shurutisho na ufanyike kwa kuzingatia mila na desturi za nchi husika.

Mbali ya  msemaji huyo kwa niaba ya nchi za Afrika kuanisha baadhi ya maeneo ambayo  Afrika itayatekeleza  pasipo kushurutishwa.  Wazungumzaji   zaidi ya 30 wakiwakilisha  makundi ya  kikanda  na baadhi wakizungumza kwa niaba  ya nchi zao walichangia maoni yao   kuhusu ajenda 2030.

Mwakilishi wa  Kudumu wa Afrika ya Kusini  Balozi Kingsley Mamabolo ambaye ni   Mwenyekiti wa  Kundi la G77& China. Akizungumza kwa niaba ya kundi hilo anasema.  

  Haikuwa kazi nyepesi   kufikia makubaliano    yaliyopelekea kupitishwa kwa kauli moja  Malengo   na Ajenda  2030
“   Ajenda hii  ambayo tumeipitisha kwa kauli moja,  hatuwezi kusema kwamba haina mapungufu.  lakini tumefika hapa tulipo baada ya  majadilliano marefu na magumu na kukubaliana kuto kukubaliana”.

  Na   akaongeza  Ajenda 2030 ina mambo mengi yakiwamo malengo    17  na viashiria  169. Lakini jambo   moja la msingi na muhimu  ni kwamba, utekelezaji wake  utategemea  kila nchi inavyopanga vipaumbele vyake na sera zake” akasema Balozi Mamabolo.

Awali akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo, Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban   Ki   Moon,   amesema. Agenda 2030   ni makubaliano ambayo kila   nchi inapashwa kujivunia na kwamba utekelezaji wake utahitaji ushirikiano wa karibu baina ya wadau mbalimbali.
Akasema   Agenda   2030 itapitishwa na Viongozi Wakuu wa   Nchi na Serikali kutoka  Mataifa mbalimbali duniani akiwamo Baba Mtakatifu Francis.

DR. MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI WA MASASI

September 01, 2015


1
 Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akbiaihutu wakazi wa mji wa Masasi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Bomani mjini Masasi ambapo amewaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili aweze kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo na mabadiliko Bora na siyo bora mabadiliko.
2
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo hutubia wakazi Masasi.
 Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hiyo ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha Dk. Emmanuel Nchimbi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Namtumbo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara wakati akiwa njiani kuelekea Masasi kwa ajili ya kampeni.
????????????????????????????????????
Lazima tumuona Magufuli  hapa.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoani Mtwara Ndugu Mohamed Sinan wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wakazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara.
????????????????????????????????????
Wananchi wa kijiji cha Michiga wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao kijijini hapo.
????????????????????????????????????
Wakazi wa Mangaka wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia akiwa njiani kuelekea Masasi.
????????????????????????????????????
Dr. Magufuli akiwahutubia Wakazi wa Mangaka
????????????????????????????????????
Baadhi ya wazee wa kijiji cha Majimaji wakimsikiliza Dr. Magufuli.
????????????????????????????????????
Akina mama hawa wakionyesha furaha yao mara baada ya kumuona Mgombea Urais Kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Dr John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kijiji cha Majimaji wilayani Nanyumbu.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akipokea kadi za waliokuwa wanachama wa CUF mara baada ya kujiunga na CCM kwenye mkutano wa kampeni mjini Tunduru.
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana waliojiunga na CCM mjini Tunduru baada ya kurejesha kadi zao kwa Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakipiga picha ya pamoja.
????????????????????????????????????
Wana CCM wakifurahia hotuba ya Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati akihutubia  mjini Tunduru.
????????????????????????????????????
Wakazi wa mji wa Tunduru wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akihutbia wananchi wa mji wa Tunduru.
????????????????????????????????????
Wana CCM wakifurahia hotuba ya Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mama huyu akimbeba mtoto wake kuhakikisha mtoto wake naye anamuona Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Vijana wa kata ya Matemanga wakifuatilia hotuba ya Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungana  ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akiwanadi wagombea Ubunge na Udiwania Katika mji wa Namtumbo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wana CCM wakiwa wamevalia sare zao zenye picha ya Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Wana CCM ni Shangwe tu kwa Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA JUMA DUNI HAJI AFANYA KAMPENI MIKOA YA KUSINI

September 01, 2015

Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa
amembeba motto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Kikundi cha Kwaya ya Tujikomboe kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kamapeni uliofanyikakatika uwanja wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chadema, Juma Duni Haji akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa
amembeba mtoto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar Said Issa Mohamed (kushoto) akimtambulisha mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  kupitia Chadema, Juma Duni Haji wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
 
Wafuasi wa Ukawa wakisukuma gari la mgombea Mwenza wa Ukawa kupia Chadema, Juma Duni Haji baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba motto, Mohamed Mchokonole wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Mgombea
Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea wa
ubunge  jimbo la Lindi mjini ikupitia
CUF, Salum Barwani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili
mkoani Lindi 
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kupitia Chadema, Juma Duni Haji (kulia), akimtambulisha mgombea wa ubunge wa jimbo la Liwale kupitia CUF, Zubery Kuchauka wakati wa mkutano wa kampeni ulifanyika kwenye uwanja wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kupitia Chadema, Juma Duni Haji (katikati) akiwaaga wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar Said Issa Mohamed (kushoto) akimtambulisha mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  kupitia Chadema, Juma Duni Haji wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Maulidi Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akipokea kadi ya CCM kutoka kwa bibi, Razina Mwandachi baada ya kujiunga na Ukawa na kukabidhiwa kadi ya CUF wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akipokea kadi ya CCM kutoka kwa bibi, Razina Mwandachi baada ya kujiunga na Ukawa na kukabidhiwa kadi ya CUF wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.
Wafusi wa Ukawa wakiwa katika mkutano wa kampeni zamgombea mwenza wa urais wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji uliofanyika katika uwanja wa Maulidi uliopo wilayani Nachingwea.
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwaaga wafuasi wa Ukawa mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili mkoani Lindi.