MH DC WA KILOMBERO DUSTAN KYOBYA AMEIFUNGUA RASMI SHULE MPYA YA SEKONDARY LIPANGALALA

January 15, 2024


Na Mwl. Kassim Mandwanga
Kidatu Kilombero

Asubuhi ya jumatatu sawa na tarehe 15 january 2024, Mh Dustan Kyobya* Mkuu wa wilaya ya Kilombero na mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Kilombero, ameambatana na viongozi kadhaa wa halmashauri katika zoezi la ufunguzi wa shule mpya ya sekondari Lipangalala.

Mh DC Kyobya alikuwa ameongozana na Mkurugenzi wa halmashauri comrade Zahra Michuzi, Mh Kassim Faya Nakapala mwenyekiti wa halmashauri, Comrade Mwambeleko katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya pamoja na afisa elimu sekondari ndugu Godwin Samson Mukaruka.

Sambamba na ufunguzi huo Mh Kyobya alipanda mti wa kumbukumbu na kusisitiza mambo yafuatayo:

Mh mkuu wa wilaya amesisitiza kutunzwa kwa miundombinu ya shule hiyo kwa kuwa ndoto ya wana Kilombero ni kuona shule hiyo inakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita.

Katika swala la lishe mkuu wa wilaya amewakumbusha wazazi kizingatia muongozo wa elimu bila malipo kwamba mzazi ana jukumu la kumpatia chakula mtoto, hivyo basi amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni hapo.

Mh DC, ambaye ni mtu wa vitendo sana, akasisitiza pia majengo yaliyosalia yakamilishwe kabla ya tarehe 22 January 2024.

Sambamba na hilo mwenyekiti wa halmashauri cde Kassim Faya Nakapala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lipangalala amemshukuru sana Mh DC na Mkurugenzi kwa utendaji wao wa kazi wa viwango vya juu na kwamba utendaji huo umekuwa chachu ya ukamilikaji wa shule hiyo uliokwama kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu.

Mwenyekiti huyo pia amewashukuru wananchi na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilombero cde Mwambeleko amewataka wananchi kuwa na imani na Mh Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake, pia amewapongeza Mh DC na Mkurugenzi Kwa utendaji wao mzuri pamoja na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii.

Uzalendo ni vitendo.







ELIMU YA FEDHA KUPELEKWA VIJIJINI KWA NJIA YA WASANII

January 15, 2024

 Na. Peter Haule, WF, Morogoro


Wananchi wametakiwa kukopa kwenye taasisi za fedha zilizosajiliwa na kutambulika na Benki Kuu ya Tanzania au Mamlaka Kasimishwa kwa kuwa itasaidia kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwa mkopaji kwa kuwa taasisi hizo zinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria.

Rai hiyo imetolewa mkoani Morogoro na Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, wakati akifungua Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI)

Alisema kuwa mkopaji anapaswa kuwa na elimu sahihi kuhusu huduma za fedha na kusoma na kuelewa vyema mikataba ya mikopo ili kufahamu gharama halisi za mkopo na kuziafiki kabla ya kuchukua husika mkopo ili kuepuka kuingia hasara kwa kudhulumiwa.

“Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha, umeelekeza kutoa elimu ya fedha kwa umma kwa njia mbalimbali, hivyo mafunzo kwa wasanii yatawezesha kupeleka elimu ya fedha vijijini ambako kumekuwa na uelewa mdogo wa masuala hayo na kusababisha uwepo na mikopo umiza”, alisema Kimaro.

Alisema kuwa mwananchi anapokopa ni lazima ajue riba, ada na gharama zingine lakini pia mkopaji anapaswa kujua kiasi ambacho anatakiwa kulipa kwa kipindi chote cha mkopo.

Alisema kuwa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha ni Mpango uliowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha katika kuhakikisha huduma za fedha zinaimarika, mitaji inapatikana na kunakuwa na Sekta ya fedha himlivu inayochangia ipasavyo kwenye pato la Taifa.

Bw. Kimaro, alisema kuwa program ya elimu kwa umma inatekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2020/2021 hadi 2025/2026 ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa miaka 10 kuanzia 2020/2021 hadi 2029/2030.

Alieleza kuwa baada ya hapo Mpango Mkuu utafanyiwa tathmini ili kuona mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wake na kuja na maboresho iwapo changamoto zitajitoeza.

Bw. Kimaro, alisema kuwa Sanaa ni eneo muhimu la kufikisha ujumbe kwa umma kwa kuwa ni rahisi kuwafikia wananchi na njia yenye mafanikio makubwa si tu kwa Tanzania lakini pia duniani kwa ujumla.

Alibainisha kuwa maeneo muhimu ambayo yataangaziwa wakati wa kutoa elimu ya fedha ni pamoja na usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji wa akiba, mikopo, uwekezaji, bima, bima ya amana, mpango wa kujiandaa na maisha ya uzeeni, kodi, mifumo ya malipo na kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha.

“Tutaenda vijijini na tutachagua maeneo ambayo elimu ya fedha ipo chini baada ya wasanii kupata uelewa ili kupeleka elimu sahii kwa wananchi”, aliongeza Bw. Kimaro.

Aidha, alisema kuwa mkopaji anashauriwa kukopa kwa ajili ya uwekezaji unaozalisha kama vile kununua sehemu ya ardhi ambapo ataweza kuzalisha mazao au kupanua biashara itakayomwezesha mkopaji kurejesha mkopo kwa wakati na kuweza kukopa zaidi baadae kama atahitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), Bi. Aline Augustin, alisema kuwa upekee katika kuelimisha jamii ni matumizi ya Sanaa za maonesho jukwaani kwa ajili ya maendeleo ya jamii, kwa kutumia pia ngoma bila maneno na maigizo kwa njia ya redio.

‘’Kwa njia ya redio na ngoma TACCI, inakuwa na nafasi kubwa ya kuifikia jamii na kupenyeza elimu na kuvutia watu wa makundi tofauti kwa kuwaleta pamoja na kuchochea mazungumzo na majadiliano katika elimu inayotolewa’’, alisema Bi. Augustin

Aidha, alisema kuwa mafunzo ya elimu ya fedha yanayoendelea kutolewa yanawapa uelewa na wigo mpana wa kuandaa elimu kwa njia ya sanaa itakayokidhi matakwa ya Wizara ya Fedha katika kufikisha ujumbe stahiki kwa wananchi hususani waishio vijijini.

Bi. Augustine, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuamua kutumia sanaa kufikisha elimu vijijini na ameahidi kutumia mafunzo wanayopata kuongeza ujuzi na kuhakikisha elimu ya fedha kwa njia ya sanaa inawasilishwa kwa ufanisi na kwa tija.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akifungua mafunzo ya elimu ya fedha kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), yanayofanyika mkoani Morogoro, kushoto ni Mkurugenzi wa TACCI, Bi. Aline Augustin na kulia ni mtaalamu wa masuala ya fedha wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akitoa mada kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa wasanii hao, mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia TACCI, Bi. Aline Augustin, akieleza kuhusu umuhimu wa utoaji elimu kwa njia ya sanaa ili kuwafikia wananchi kwa urahisi, wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii kutoka Shirika hilo, mkoani Morogoro.

Mtaalamu wa Masuala ya Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Msumule, akitoa mada kuhusu Sera na Sheria za Huduma Ndogo za Fedha, wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) yanayofanyika mkoani Morogoro.

Afisa Msimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI), Bi. Aline Augustin, wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii kutoka Shirika hilo, mkoani Morogoro.

Baadhi ya Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) wakisikiliza kwa makini mada kuhusu Sera na Sheria za Huduma Ndogo za Fedha, wakati wa mafunzo kwa wasanii hao, Mkoani Morogoro.

Baadhi ya Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) wakipata mafunzo ya elimu ya fedha ili waweze kutoa elimu hiyo kwa wananchi hususani wa vijijini, mafunzo hayo yanatolewa na Wizara ya Fedha mkoani Morogoro.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Morogoro)

NAIBU WAZIRI DAVID KIHENZILE ATEMBELEA BANDA LA TASAC MAONESHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI

January 15, 2024

 

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile  akizungumza na watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) alipofika kwenye banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Sheria Mkuu kutoka TASAC Devotha Mandanda alipotembelea banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Ukaguzi wa Meli kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kapt. Ghadaf  Chambo kuhusu namna ya kusajiliwa kuwa kapteni wa meli alipotembelea banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Sheria Mkuu kutoka TASAC Devotha Mandanda pamoja na kupiga picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Banda la Shirika hilo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

DKT. EMMANUEL NCHIMBI KATIBU MKUU WA CCM

January 15, 2024

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

***

Dkt. Emmanuel Nchimbi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu.


Uteuzi wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake mpya umefanyika leo Jumatatu Januari 15, 2024 wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kisha kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyofanyika mjini Unguja, Zanzibar

TAASISI WATEMBELEA BANDA LA TCAA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

January 15, 2024

 Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari na Masoko Mwandamizi Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Ally Changwila katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.


***

Viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi wameendelea kufurika ndani banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) na kujipatia elimu ya Usafiri wa Anga pamoja na huduma mbalimbali zinapatikana katika Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC)ndani ya maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba Nyamanzi, Zanzibar kuanzia Januari 08-21,2024.


Wageni hao wameongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Ki uchumi wa TCAA Bw. Daniel Malanga, Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mikeli Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Dkt. Zainabu Mshana, Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO, Christine Mwakatobe.


Pia Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi-Wizara ya Uchukuzi, Biseko Chiganga, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango -Wizara ya Uchukuzi Maseke Mabiki, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mohamed Malick Salum, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha Mussa Mandia na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Profesa Ulingeta Mbamba


CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Habari na Masoko Mwandamizi Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Ally Changwila katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Mussa Mbura akizungumza jambo mara baada ya kupata maelezo katika Banda la Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Omary Haji Kaimu Meneja wa TCAA Kituo Cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Mussa Mbura pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mikeli Mbossa wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid walipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mikeli Mbossa akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mikeli Mbossa akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Meneja wa TCAA Kituo Cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Omary Hajimara baada ya kutembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Mussa Mbura akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Meneja wa TCAA Kituo Cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Omary Hajimara baada ya kutembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi alipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha Mussa Mandia akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid alipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Dkt. Zainabu Mshana akizungumza jambo mara ya kupata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) Dkt. Zainabu Mshana akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu utendaji wa shughuli za Mamlaka Pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO, Christine Mwakatobe akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Habari na Masoko Mwandamizi Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Ally Changwila baada ya kutembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi-Wizara ya Uchukuzi, Biseko Chiganga akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa TCAA Kituo Cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Omary Hajimara alipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi-Wizara ya Uchukuzi, Biseko Chiganga akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid mara baada ya kutembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid alipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango -Wizara ya Uchukuzi Maseke Mabiki akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango -Wizara ya Uchukuzi Maseke Mabiki akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu utendaji wa shughuli za Mamlaka Pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mohamed Malick Salum akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi alipotembelea katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Profesa Ulingeta Mbamba akisaini Kitabu katika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Profesa Ulingeta Mbamba akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu utendaji wa shughuli za Mamlaka Pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA ZAWADI KWA GOLIKIPA BORA WA MASHINDANO YA LIGI YA MAPINDUZI CUP VISIWANI ZANZIBAR

January 15, 2024

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi cheti maalum kwa Mkurugenzi Mtendajiwa Tanzania Commercial Bank TCB Adam Mihayo mmoja ya wadhamini wa mashindano ya ligi ya Mapinduzi Cup Kwa ikiwa nikutabua na kuthamini uwepo wa wadhamini mbalimbali na wadau wa michezo.
Mkurugenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank PLC(TCB), Adam Mihayo (kushoto), akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/- kwa Mlinda Mlango bora wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024, kutoka Timu ya Mlandege Athuman Hassan, mara baada ya Timu hiyo kuibuka kidedea kwa kuikanda timu ya Simba Sc kwa bao 1-0 wakati wa mchezo wa fainali wa kombe hilo. Mchezo huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya New Amani vilivyopo visiwani Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Hussen Mwinyi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo (kuila) akifuiraha jabo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, kuila kwake na wadaui wiengne wakati wakitazama mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi Cup kati ya Timu ya Simba SC na Mlandege FC mchezo uliyofanyika visiwani Zanzibar viwanja vya New Amaani

Baadhi ya Maofisa wa Tanzania Commercial Bank TCB wakiwa na watazamaji wengine visiwani Zanzibar katika kufuatilia mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi Cup yanayofanyika visiwani vya New Amaani Zanzibar


Tanzania Commercial Bank PLC (TCB) ambae ni Moja ya wadhamini wa mashindano ya ligi ya Mapinduzi Cup yanayofanyika visiwani Zanzibar kila mwaka jumamosi iliyopita iyopita Benki hiyo ilikabidhi zawadi ya pesa kiasi cha shilingi milioni Moja kwa golikila bora wa ligi hiyo Athuman Hassan kutoka klabu ya Mlandege Fc Makabidhiano ya zawadi hiyo yalifanyika muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali baina ya Mlandege Fc na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa New Amani Visiwani Zanzibar ambapo mchezo ulikamilika kwa timu ya Mlandege kuibuka na ushindi wa Goli 1-0.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank TCB Adam Mihayo amesema TCB itaendelea kutoa hamasa kwenye michezo mbalimbali hapa Nchini kwani michezo imekuwa ikiwakutanisha watu karibu pia michezo ni ajira.


“Zawadi hii tunazitoa kwa kuleta hamasa kwa wachezaji ili wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa ,pia kusaidia kuboresha mchezo huu mwanzo tu Kwa Tanzania Commercial Bank kushiriki katika michezo wa soka hapa nchini”amesema Mihayo.


Tanzania Commercial Bank tumekuwa na utaratibu wakujitolea sana katika jamii kwakufauata misingi ya Benki yetu tumeweza kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania bara pamoja na visiwani katika sekta mbalimbali ikiwepo elimu, Afya, michezo, na Biashara na kutoa elimu ya kifedha.

Hapa visiwani Zanzibar tumeshafanya mambo kadhaa ikiwepo kuwasaidia vikundi vya wanawake wajasiliamali kwa kuwapa vitendea kazi vikiwemo vyerehani na kuwawezesha vikundi vya kinamama wa Jimbo la Paje wanaolima zao la mwani kwa kuwajengea kisima Cha furahia ili kuwarahisishia shughuli zao za kilimo wa zao hilo ”

“ Kwa upande wake Golikila wa Mlandege Athuman Hassan alishukuru kupata zawadi hiyo na kuahidi kuwa atazidi kuongeza bidii kuwa kinara na kusaidia timu yake kupta ushindi wa kila mechi. “Napenda kuwashukuru TCB kwa kunipa zawadi hii kwani itakwenda kuongeza sana hamasa upande wangu na wa wachezaji wote na makocha pia.