RAIS DKT MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA MKOA WA PWANI

June 21, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kunawa na kisha kuchukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017  katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha  yatima mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (wa pili kulia) akichukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017 katika futali aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani futari katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akichukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017 katika futali aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani futari katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
 Kina mama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaya Mhe. Asumpta Mshama wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
 Kina mama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaya Mhe. Asumpta Mshama wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa neno la shukrani leo Jumatano Juni 21, 2017  wa waliohudhuria  futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha
 Mmoja wa waze Maarufu wa Kibaha ambaye ni Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu Mzee Jumanne Mangara (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Bagamoyo Sober House Bw. Alkareem Bhanji (kati) na Mdau Oshiro
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwa na Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. sylvester Koka na wadau 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya kuzungumza machache wakati wa  futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa akitoa neno la shukurani kwa futari aliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa  wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha
   Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Pwani Sheikh Hamisi Mtupa   baada ya kuzungumza machache wakati wa  futari aliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa  wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha

 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  akizungumza machache na kuomba dua baada ya futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Sehemu ya waalikwa wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya   futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Sehemu ya waalikwa wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya   futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Sehemu ya waalikwa wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya   futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Ndekilo, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali, Kaimu Shehe wa Mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa na Padri R. Mukandara
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizunguka meza hadi meza kupeana mikono na kuwashukuru waalikwa kwa kufika katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizunguka meza hadi meza kupeana mikono na waalikwa katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.

WANAWAKE WA KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA WAFANYA KONGAMANO LA TATU JIJINI DAR ES SALAAM

June 21, 2017
 Askofu Saldonie Simon Sinde akiwasalimia Wakina mama katika Kongamano la Tatu la Wanawake wa Muungano wa Makani ya Pentekoste Tanzania (UW-MMPT), lililoanza Katika Kanisa hilo Sinza Afrika Sana Dar es Salaam jana. Askofu Sinde pia alivitambulisha vitabu vyake viwili alivyoviandika.

WANAWAKE VIONGOZI KATIKA MASOKO WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUTEMBELEA KATIKA MASOKO AONE MIUNDOMBINU ILIVYO

June 21, 2017
Ofisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Suzan Sita (kulia), akitoa mada katika Warsha ya Siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa Umoja wa Wanawake Masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na shirika hilo inayoendelea katika Hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam jana.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO

June 21, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kuzindua rasmi Mradi wa huo wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa  mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga kabla ya kudua Mradi huo wa maji.
 Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAS AKUTANA NA WATUMISHI WA KITUO CHA DAR ES SALAAM.

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAS AKUTANA NA WATUMISHI WA KITUO CHA DAR ES SALAAM.

June 21, 2017
ZOR1
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashamba akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ili azungumze na Watumishi wa Ofisi ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
ZOR2
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongea wakati wa mkutano wake na Watumishi wa Ofisi yake walioko Dar Es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
ZOR3
Mmoja wa Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Aidan Mtuhi akichangia maoni yake wakati wa Mkutano huo.
ZOR4
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (hayupo pichani)
Naipenda Tanzania Yangu, Nasimama na Rais Wangu!-Dk. Hamisi Kigwangalla

Naipenda Tanzania Yangu, Nasimama na Rais Wangu!-Dk. Hamisi Kigwangalla

June 21, 2017
Naipenda Tanzania Yangu, Nasimama na Rais Wangu!-Dk. Hamisi Kigwangalla Kila siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema na mimi sasa nipo kwenye Serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'Naibu Waziri'. Lakini kiukweli nina hamu na shauku ya kuzungumza na wananchi wenzangu. Nami nitoe yangu ya moyoni. Kama mwananchi mwingine yeyote yule tu. Nina haki hiyo. Na mimi haki yangu inalindwa na katiba na sheria za nchi yetu. Leo nimeona acha nipumue kidogo. Niseme. Niuvue userikali wangu. Niseme kama mwananchi mwingine yeyote yule. Nianze kwa kuweka wazi kabisa hapa, kwamba; haya ni yangu. Si ya Serikali. Serikali ni ya Rais Magufuli, tumempa dhamana, ndiyo. Hili halibishaniwi. Tumempa kazi, ndiyo. Hili pia halibishaniwi. Lakini kazi hii anaifanyaje? Tunazijua changamoto anazokumbana nazo? Je, ana nia ya kuzitatua? Ni maswali ambayo yanastahili majibu. Kwenye makala hii nitajaribu kuyafafanua kidogo kwa mtazamo wangu kadri nitakavyojaaliwa. Pamoja na kumpa dhamana Rais wetu, ni lazima tufahamu kuwa na sisi tuna wajibu wa kutimiza kwa Taifa letu. Tuna kazi ya kufanya kumsaidia Rais wetu kubeba mzigo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwenye Taifa letu. Tusimuachie huu mzigo peke yake. Tuubebe sote. Nchi ina changamoto nyingi sana, siyo kwamba Rais ama Serikali yake haizifahamu ama haina nia ya kuzitatua, ama Rais Magufuli amesinzia, ama anastarehe; kila siku anahangaika kukuna kichwa, usiku na mchana kuzitafutia ufumbuzi. Nadhani hili halina ubishani sana kwa mpenda kweli. Binafsi, sina shaka kabisa juu ya uwepo wa nia thabiti ya kuleta mapinduzi. Sina. Kwenye biashara ya kujenga nchi changamoto haziishi siku moja. Ukimaliza moja, nyingine inaibuka, na nyingine zinazaliwa kutokana na majawabu ya changamoto uliyoitatua. Juzi juzi hapa nilisema kuhusu mfumo wa afya wa nchi kubwa kama ya Marekani kuwa na changamoto ya kuwabagua watu maskini na wale wa tabaka la kati na kwamba unajenga matabaka makubwa sana yanayowanyima fursa sawa baadhi ya watu kwenye Jamii. Na kwamba ObamaCare inajaribu kutoa majibu yanayolenga kuleta usawa kwa kuwabana wenye kipato cha juu ili kuwahudumia wenye kipato cha chini. Tayari imeonekana kuwa kuna changamoto za kuwakamua zaidi watu wa daraja la kati, badala ya wale wa tabaka la juu kama 'design' na muundo wa awali ulivyolenga, kwa kuwatwisha mzigo wa watu maskini, na kwamba mpango huu kwa baadaye hautohimilika. Bado wanaendelea kubishana! Juzi tumeshuhudia Rais Trump amekwama kwenye jaribio la kuurekebisha. Kazi ya kutatua changamoto ipo na inaendelea kwenye Taifa kubwa la Marekani lenye miaka zaidi ya 200 ya demokrasia. Mfano, tazama changamoto mpya iliyokuja na sera ya CCM kutoa elimu bure mpaka kidato cha nne. Tamko hili la kisera limeleta changamoto nyingi za kiutekelezaji. Kwanza, limeleta urahisi kwa familia nyingi kuona hakuna sababu ya watoto wao, hata mmoja, kukosa elimu hii ya msingi. Wakati tunapitisha sera hii hatukujua kuwa kuna watoto wengi kiasi hiki tunachoshuhudia sasa walikuwa wakikosa fursa (missed opportunity) ya elimu kwa sababu ya vigharama vidogo vidogo.
Rais Dk. Magufuli
Tumeondoa gharama hizi tumekutana na ongezeko kubwa la watoto kuandikishwa shule. Mlipuko wa wanafunzi kuingia darasa la kwanza kwenye shule za msingi kwa wingi umezaa changamoto mpya za upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, idadi ya matundu ya vyoo, idadi ya walimu nk. Wakati tukumbukeni vizuri kuwa juzi tu hapa Serikali ilikuwa inaajiri walimu kwa kipaumbele cha juu kabisa kwa miaka mitano mfululizo, ambapo walimu wote waliohitimu waliajiriwa! Uchumi wetu unakua kwa kasi nzuri, kama ni ndege ndiyo inaongeza spidi ili ipate nguvu ya kupaa; bado uchumi hauna uwezo wa kuhimili mahitaji yetu 'yote' ya matumizi ya kila siku kama tunavyotamani, achilia mbali ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kadri tunavyodiriki kuota ndoto zetu. Mfano: Kwenye ajira bajeti ya watumishi (wage bill) inaongezeka kila siku. Hili tu ni hitajio kubwa na nyeti sana la uchumi wetu. Zamani nilipokuwa Mbunge - bila userikali, kilichokuwa kinanikera ni kwamba, pamoja na changamoto tulizonazo watu wengine walikuwa wanaishi kama wako peponi na wengine wanaishi kama wako motoni, hawa wa peponi walifika huko kwa wizi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma, siyo kwa uchapakazi wala ubunifu. Tena bila huruma kwa waliokuwa wakiishi kama vile wapo motoni. Huku wakiwa na dhamana ya kuwaondoa motoni wananchi wenzetu waliobaki huko! Leo Rais JPM anakosolewa kwa kubana mianya ya rushwa, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na uchumi wa ujanja ujanja, mambo ambayo nakumbuka mimi na wenzangu kwenye bunge la 10 tuliyapigia kelele kwa nguvu sana, tena kwa uzalendo wa hali ya juu na bila hata kuogopa kuwa tunapowashughulikia hawa ndugu wa peponi tunashusha imani ya wananchi kwa chama chetu pia. Sisi tuliamini kwamba hawa ni lazima tushughulike nao. Tuwaondoe ili kukisafisha Chama. Tulikuwa wachache sana. Tulipigana kuwaondoa watu wa aina hiyo na tuliwatoa.
Dk.SHEIN AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA SIMON SIRRO

Dk.SHEIN AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA SIMON SIRRO

June 21, 2017
unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Inspekta Jenerali  wa Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha kwa Rais
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Inspekta Jenerali  wa Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha kwa Rais,[Picha na Ikulu.] 21/06/2017.

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

June 21, 2017
 Afisa Utumishi Mkuu Ally Juma Ally (Kushoto) akisikiliza maswali mbalimbali ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakati wa kikao cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Yamo Wambura



 Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma


Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma

Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO MHE KISARE MAKORI AFUNGUA MAFUNZO KWA WENYEVITI, NA WATENDAJI KATA NA MITAA

June 21, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo sambamba na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa kufungua mafunzo ya siku nne ya kuwajenega uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaakwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg Jmaes Mkumbo akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura (Kulia) sambamba na Hosia Kivulenge wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo