MULTICHOICE TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA AFRIKA.

May 26, 2016


Sehemu ya Watendaji wakuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wao, Francis Senguji (wa pili kushoto) wakiwa katika tafrija ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Francis Senguji akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Furaha Samalu.
 Burudani ya Kiafrika ikitolewa.
 Mshehereshaji katika Tafrija hiyo, Masoud Kipaya (kati) pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu, wakimsikiliza Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Shilole wakati akimtangaza mmoja wa washindi wa Dikoda ya DSTV Exprola.
Washindi wa Dikoda za DSTV Exprola kwa usiku huo walikuwa ni Mmiliki Mwendeshaji wa Libeneke la Full Shangwe Blog, John Bukuku na Mwanadada Latoya aliewahi kuwa Mshiriki wa Shindano la Big Brother Afrika miaka ya nyuma.

Sherehe za Kuapishwa Rais Mpya wa COMORO

Sherehe za Kuapishwa Rais Mpya wa COMORO

May 26, 2016

1 
Makamo wa Rais wa Muungano wa Comoro Mhe,Jafar Ahmada Sais wa kisiwa cha Ngazija akiapishwa leo na Jaji wa mahakama ya katiba ya Nchi hiyo Mhe,Loutfi Soulaimane (hayupo pichani ) wakati wa sherehe za kuapishwa Rais kanali Azali na makamo wake 3 iliyofanyika leo baada ya ushindi wa uchaguzi Mkuu uliofanyika Aprili 10 na   marudio ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi mei 11 mwaka huu,hafla ilifanyika uwanja wa mpira mjini Ngazija leo,[Picha na Ikulu.] 26 mey 2016.
9 
Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri akitoa hutuba yake katika sherehe za kuapishwa zilizofanyika  leo kufuatia kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika April Kumi (10) na uchaguzi wa marudio uliofanyika mey 11 mwaka huu,hafla ya sherehe ilifanyika uwanja wa mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
2 
Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri (wa pili kulia) mara baada ya kuapishwa  akiwa na Makamo wake wawili Mhe,Abdullah Said Sharman (kushoto) wa Kisiwa cha Mwali na Mhe,Mustarigan Aboud wa Kisiwa cha Anjouan (wa pili kushoto) katika uwanja wa mpira mjini Ngazija nchini Comoro leo,
3 
Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa katikapicha na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri  mara baada ya kuapishwa  leo baada ya kushinda uchaguzi Mkuu wa April kumi(10) na uchaguzi wa marudio wa mei kumi na moja mwaka huu hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
4 
Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri  akitoa salamu kwa kikosi cha Bendera mara baada ya kuapishwa  leo akiwa mshindi katika   kushinda uchaguzi Mkuu wa April kumi(10) na uchaguzi wa marudio wa mei kumi na moja mwaka huu hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
5 
Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi Comoro  mara baada ya kuapishwa  leo kwa kushinda uchaguzi mkuu wa April 10 na uchaguzi wa Marudio wa Mei 11 mwaka huu  hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
6 
Vikosi vya majeshi ya Ulinzi vya  Comoro vikitoa heshama kwa  Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani  Boinakheri aliyeapishwa leo na jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba Mhe,Loutfi Soulaimane katika sherehe zilizofanyila uwanja wa mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
[Picha na Ikulu.]26 mey 2016.

KATIBU MKUU KIONGOZI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KINONDONI MWANANYAMALA DAR ES SALAAM LEO

May 26, 2016
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akitoa taarifa fupi kabla ya kumribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (katikati), wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala Dar es Salaam leo mchana. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Michael John, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Ali Hapi.
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi.
Mkutano ukiendelea.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Makani ya Pentekosti (MMPT), Askofu Saldonie Sinde (katikati), akimkabidhi Katibu Mkuu magodoro 50 yaliyotolewa na Umoja wa Makanisa hayo kwa ajili ya kusaidia hispitali hiyo.



Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi (katikati), akienda kutembelea hospitali hiyo. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe.



Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia), akiwajulia hali wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika hospitali hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi akizungumza na viongozi mbalimbali katika ziara hiyo.
Hapa Katibu Mkuu Kiongozi akisikiliza malalamiko kutoka kwa wananchi waliofika katika hospitali hiyo kupata huduma (hawapo pichani)

UCHAGUZI YANGA, FOMU KUANZA KUTOLEWA LEO

UCHAGUZI YANGA, FOMU KUANZA KUTOLEWA LEO

May 26, 2016
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza leo Mei 27, 2016 kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika Klabu ya Young Africans ya Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi tarehe 25 Juni mwaka huu.

Nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanane wa Kamati ya Utendaji.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz

Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 31 Mei, 2016.
TBL GROUP YALIPA KODI SHILINGI BILIONI 81

TBL GROUP YALIPA KODI SHILINGI BILIONI 81

May 26, 2016

tb1Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
tb2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
tb3 
Mwandishi wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  (hayupo pichani) kuhusiana na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa mkutano na wandishi wa habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016. \
tb4 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam,  leo  Mei 26 2016.\
tb5 
Mtalamu wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi inavyozalishwa wakati walipotembelea kiwanda hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa  tathmini na waandishi hao
……………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa  taarifa ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi  bilioni165 ikiwa ni kodi ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114   ikiwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo kodi ya PAYE.
TBL Group ni kampuni inayoongoza  kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.
TBL Group inajumuisha  makampuni ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited (TDL)  na  Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na vinywaji vya asili.. 
Jarrin alibainisha hayo wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia ya kisasa
Kampuni inavyo viwanda 10 nchini na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa ubora duniani.
Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza  mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni   – Konyagi, Valuer and Dodoma Wine –  Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba –   Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya  pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni asilimia 50%
 Jarrin aliendelea kueleza kuwa TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya  Bihawana, Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.
Jarrin pia alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na  katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza  kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili  ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha  vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MWANAHABARI MAKONGORO OGING' KUZIKWA MKOANI MARA KESHO KUTWA.

May 26, 2016
 Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging' enzi za uwai wake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging', Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging' wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.
 Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi akitoa heshima za kwa mwili wa marehemu.
 Mhariri wa Habari wa Gazeti la Champion, Salehe Ali akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
 Waombolezaji wakiwa na huzuni wakati wa kuaga mwili wa mpendwa wao Makongoro.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV. Samu Mahela akitoa heshima za mwisho.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akiwa kwenye shughuli hiyo ya kumuaga Makongoro Oging'
 Ndugu yake na Makongoro Oging' akilia wakati wa kumuaga mpendwa wake Makongoro.
 Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye uagaji wa mpendwa wao.
 Uagaji ukiendelea.
 Mtoto wa marehemu akimuaga baba yake 'hakika ni huzuni kubwa'
 Majane wa marehemu akiwa hajiwezi baada ya kumuaga mume wake.
 Mhariri wa habari wa gazeti la Uwazi alilokuwa akiandikia marehemu Oging' Elvan Stambuli akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga Makongoro.
 Baba mlezi wa Makongoro Oging ambaye alimsomesha, akizungumza na wanahabari.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro kulipeleka kwenye gari kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mara.
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari.