LAPF NA TAASISI MBALIMBALI ZACHANGIA MIL.172 MAAFA KAGERA

LAPF NA TAASISI MBALIMBALI ZACHANGIA MIL.172 MAAFA KAGERA

September 22, 2016
top1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa Dkt.  Ave Maria Semakafu (kulia), Berious Nyasebwa (wapili kushoto) na Benjamin Thomson wote  kutoka Group la Whats App la Leaders Forum ukiwa ni mchango wa group hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
top2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
top3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani  40 za saruji zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka  kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor (kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a  Advent ukiwa ni mchango kwa waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba  22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
top4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VODACOM TANZANIA, Bw. Ian Ferrao (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake  jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
top5
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Meneja wa Kanda wa LAPF, Amina Kassim (kulia) na  Kafiti Kafiti wa LAPF  ukiwa ni mchango wa Mfuko huo  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo  yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
top6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea sehemu ya  msaada ya vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa viongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Art of Living ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016.  Kutoka kushoto ni Nishitha Kulshreshtha,  Nishit  Patel,  Neha Movaliya,Sharik Choughule ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga  na Neha Movaliaya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………..
TAASISI sita zikiwemo za dini na kijamii zimechanga jumla ya sh. milioni 172.5 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.
Mchango huo umepokelea leo jioni (Alhamisi, Septemba 22, 2016) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Ian Ferrao alisema kiasi cha sh. Milioni 100 kimekusanywa kutoka kwenye mfuko wa Vodacom Foundation pamoja na wadau wao.
Bw. Ferrao amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidiana na Serikali katika uboreshaji wa miradi mbalimbali za kijamii…..
Taasisi nyingine iliyochangia ni Mfuko wa Pensheni wa LAPF  ambapo Meneja wa Kaya ya Dar es Salaam, Amina Kassim amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 20.
Pia Jumuiya ya Kiislam Ahmadiyya imekabidhi msaada wa sh. milioni 10 kati ya hizo sh. milioni nne ni fedha taslimu na zilizobaki ni mabati na mifuko ya saruji.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Advent, Dhruv Jog amemkabidhi Waziri Mkuu msaada wa tani 40 za saruji yenye thamani ya sh. milioni 16.5 na kusema  kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari saruji hiyo imeanza kupelekwa Kagera.
Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya kimataifa ya Art of Living, Neetu Kulshreshtha wametoa msaada wa vyakula mbalimbali pamoja dawa vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.
Dk. Ave Maria Semakafu amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh milioni 16 kwa niaba ya makundi mawili ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Makundi hayo yanaitwa Leaders na Uongozi.
Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Tunashukuru sana kwa michango yote. Tunashukuru na makundi ya WhatsApp ya Leaders na Uongozi ambayo nayo yameamua kuja kutuchangia. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa,” amesema. 
Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.
Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).
Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri. 
Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

MHE. JANUARY MAKAMBA AWATOA WASIWASI WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

September 22, 2016

WN OMR MMZ  Mhe January Makamba akimuangalia mgonjwa Benard Kayumba (60) aliyelala kitandani katika hospital ya Mkoa wa Kagera, akitokea wilayani Karagwe baada ya kuathirika na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera. Aliyesimama n Afisa Muuguzi waHosptal hiyo sr. leonida Lupapilo.
 WN OMR MMZ Mhe. January Makamba akimuangalia motto Asia zuberi aliyhelazwa katika hospital ya Mkoa wa kagera kutokana na homa ya Malaria, Mhe Makamaba alitembelea wahanga wa tetemeko la ardhi hosptalini hapo, alikyekaa ni bibi wa motto huyo Bi Asha Rajabu.
WN OMR MMZ Mhe January Makamba akizungumza na wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, alipotembelea mkoani hapo kuwapa pole wana Kagera na kujionea athari za mazingira zilizosabababishwa na tetemeko hilo. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI WA UJENZI PROFESA MBARAWA ATAKA WADAU WA UJENZI WALA RUSHWA WAFUTIWE LESENI ZAO

September 22, 2016
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa, ameitaka Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuwafutia leseni wadau wa sekta ya ujenzi  watakao bainika kuomba au kupokea rushwa.

Katika hatua nyingine Profesa  Mbarawa ameitaka  Bodi hiyo kuandaa  orodha ya wakadiriaji majenzi na wabunifu  majengo wasiyofuta maadili ya kazi zao ili iwekwe hadharani na wasipate tenda za kufanya kazi popote.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo na kueleza kazi yoyote iwe nzuri na bora ni lazima kuepuka rushwa na kufuata  maadili na kanuni za kazi.

“Napenda niwagize bodi kuanzia sasa nataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo na wadau wote wa sekta ya ujenzi ambao ni wara rushwa muwafutie leseni zao  ili wasiweze kupata tenda au kutoa tenda.Maadili katika kazi zenu ni jambo la msingi na si vinginevyo,”alisema Profesa Mbarawa.

Mbarawa aliigiza bodi hiyo kuandaa orodha ya watakao kuwa  si waadilifu ili kuonyesha katika jamii kuwa hawa hawasitahili kupewa tenda ya aina yoyote. 

Alisema baada ya kuandaa orodha hiyo  ni vizuri ikatangazwe hata katika vyombo vya habari ili iwe fundisho kwa wengine wenye vitendo hivyo.

Mbarawa aliwataka wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo nchini kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika serikali ya Awamu ya Tano ili kuweza kjiongezea mitaji.

“Kuna mradi wa ujenzi wa Reli ya kiwango cha kisasa unakuja na serikali imetenga Sh. Trilioni 1, lazima kutakuwa na ujenzi wa majengo hiyo ni fursa mbayo mnaweza kuitumia kujiongezea uwezo, lakini kama mtafanya kazi kwa kuungana njia hiyo inaweza kuwasaidia kupata tenda hizo.” alisema.

Awali, akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa, alisema semina hizo zimekuwa na faida kwa wakadiriji majenzi na wabunifu, kwani zinawaongezea uwezo wa kujua mambo mbalimbali na kwamba zimekuwa zikifanyika kila mwaka mara mbili na zimewanufaisha wadau wa sekta ya ujenzi 5,328. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

September 22, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kuhusiana na ujenzi wa daraja hilo jipya la Salenda kutoka kwa  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU

Benki ya Barclays yazindua program ya kuwawezesha wahitimu wa vyuo vikuu

September 22, 2016


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed (kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa proram ya ReadytoWork inayolenga kuwapa elimu wanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Elimu
ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Lazaro Malili.
 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa proram ya ReadytoWork inayolenga kuwapa elimu wanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdi Mohamed, Mkuu wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Lazaro Malili na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Junior Achievement, Hamisi Kasongo.
 Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Kilonzo Mringo (kushoto), akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa proram ya ReadytoWork ya Benki ya Barclays inayolenga kuwapa elimu wanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

 Mkuu wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Lazaro Malili (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi waprogram ya ReadytoWork ya Benki ya Barclays inayolenga kuwapa elimuwanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wasanii wa kikundi cha Mama Afrika wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa proram ya ReadytoWork ya Benki ya Barclays inayolenga kuwapa elimu wanafunzi wa elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

MTAA WA MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM WAANZISHA TOVUTI YAKE KWA AJILI YA MAENDELEO

September 22, 2016
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita (kulia), akizungumza katika na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya mtaa huo iliyofanyika Hoteli ya Best Western Plus Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta. 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita, akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya tovuti hiyo.
 Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (katikati), akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, aliyekuwa mgeni rasmi, kuashiria uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta, Mwenyekiti wa mtaa huo, Kimweri Mhita, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Masaki, Richard Mwakyulu na Mjumbe wa Kamati ya Mtaa huo, Rose Mkisi.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea kabla ya uzinduzi huo.
 Wajumbe wa kamati ya mtaa huo wakishiriki kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,  Peter Mkongereze akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
 Mmoja wa waendeshaji wa tovuti hiyo, Benjamin Chaula (kulia), akielezea jinsi itakavyokuwa ikifanya kazi.Kushoto ni Norbert Baranyikwa.
 Makofi yakipigwa baada ya uzinduzi wa tovuti hiyo.
Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.


Na Dotto Mwaibale

SERIKALI ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam imezindua tovuti yake ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo Dar es Salaam leo asubuhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Masaki, Kimweri Mhita alisema tovuti hiyo imeanzishwa kwa lengo la  kuwasiliana na kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo raia wa kigeni wanaoishi katika mtaa huo.

"Kutokana na jiografia ya eneo letu kulikuwa na changamoto kuwa ya kuwashirikisha wenzetu katika masuala mbalimbali kutokana na kutokuwa na mawasiliano tukaona tuanzishe tovuti yetu itakayosaidia kuondoa changamoto hiyo" alisema Mhita.

Alisema kupitia tovuti hiyo itasaidia kuwatambua wafanyabiashara waliopo katika mtaa huo ambao wameanza kujisajili pamoja na wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Tarafa wa Kata ya Magomeni, Fullgence Sakafu alisema kuanzishwa kwa tovuti hiyo katika wilaya hoyo wilaya hiyo mtaa huo umeonesha njia hivyo akaomba mitaa mingine kuiga mfano huo.


Alisema tovuti hiyo itasaidia kuweka wazi mipango ya maendeleo katika mtaa huo pamoja na kuhimizana kwenye kampeni ya kufanya usafi inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuwa.


BODI YA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM YAJIUZULU.

BODI YA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM YAJIUZULU.

September 22, 2016
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo tarehe 22 Septemba 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana. Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.

Bodi ya Uhuru Media Group ndiyo iliyokuwa na majukumu ya kusimamia, kuzielekeza na kuzishauri Menejimenti ya Makampuni hayo na kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa vyombo vya habari vya Chama.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tarehe 22/09/2016.

Kampuni ya Tigo yaendelea na utoaji wa madawati mikoani

September 22, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akimweleza jambo Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya Kaskazini,George Lugata wakati wa hafla ya kukabidhi madawati iliyofanyika katika shule ya msingi Mandela mjini Moshi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Meck Sadiki akiwa ameketi katika Dawati na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini ,George Lugata ,katikati ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Mandela ,Amina Ally ambayo imepata msaada wa Madawati kutoka kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki (katikati) akiwa ameketi pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mandela,Peggy Staki (kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mrumeni Peter Njau ambao shule zao zimepewa msaada wa Madawati 135.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Saidiki akikabidhi Madawati kwa walimu wakuu,Peggy Staki wa shule ya msingi Mandela (kulia) na Peter Njau wa shule ya msingi Mrumeni wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mandela mjini Moshi. 
Baadhi ya Wananfunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiwa wamekaa kwenye Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Tigo ikiwa ni kuiikia wito wa rais John Magufuli katika kutekleza sera ya elimu bure. 
 Baadhi ya wageni waliofika katika hafla hiyo. 
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa kampunu ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (kulia) na Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini ,Henry Kinabo (kushoto). 
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada wa Madawati 135 kutoka kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi yaliyotolewa kwa ajili ya shule za msingi za Mandela iliyopo mjini Moshi pamoja na Mrumeni iliyopo wilaya ya Moshi vijijini. 
 Baadhi ya wananfunzi katika shule ya msingi Mandela wakiwa wameketi katika Madawati mapya yaliyotolea na kampuni ya Mawasiliano ya Tigo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,kanda ya kaskazini ,George Lugata. 
 Sehemu ya Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Tigo. 
 Majengo ya shule ya Msingi Mandela. 
Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Mandela mjini Moshi wakiimba nyimbo za pongezi mara bada ya kupata msaada wa Madawati kutoka kampuni ya Tigo. 
Meza kuu wakifurahia burudani ya nyimbo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mandela mjini Mosi(hawako pichani). 

Picha na Dixon Busagaga.