MWENYEKITI WA VIJANA KKKT (KDMs) USHARIKA WA MAKORORA ATOA NENO KWA WAHITIMU WA CHUO CHA AFYA TANGA

July 25, 2023




Mwenyekiti wa Vijana KKKT (KDMs) Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani Steven Mduma amewataka wahitimu Chuo cha Afya –Bombo kuzingatia upendo na uaminifu kufikia malengo yao waliojiwekea.



Mduma aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa akizungumza katika mahafali ya Umoja wa Wanafunzi Wakristo katika chuo hicho ambapo alisema kwamba hayo ndio mambo muhimu ya msingi ya kuzingatia baada ya kumaliza chuo ili waweze kufikia ndoto zao walizojiwekea wanapokuwa kazini.



Mduma aliwataka pia wahitimu hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vinakwamisha juhudi za kimaendeleo na kupelekea kushindwa kutimiza malengo yao hivyo wahakikishe wanaachana navyo.



“Ndugu zangu leo hii mnatarajiwa kumaliza hapa chuoni na kwenda kwa jamii hivyo niwaase mhakikishe mnakwenda kuishi kwa, uaminifu, upendo mkiwa kama vijana leo mnahitimu kutoka hatua moja kwenda nyengine”Alisema



Hata hivyo aliwataka pia wanaohitimu kwenda kufanya kazi kwa ujasiri, nguvu na uaminifu ambao utakuwa chachu yao kuweza kufikia mafanikio.



Aidha katika Halfa hiyo Mwenyekiti huyo alihaidi kutoa laki tano kwa ajili ya kuchangia vyombo vya mziki na kutunisha mfuko wa umoja huo ili kuhakikisha wanapiga hatua ,kubwa za kimaendeleo

JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA TANGA YAHIMIZA JAMII KUTUNZA MAZINGIRA

July 25, 2023


KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Urassa Nanyaro kulia akipokea miti kwa ajili ya kuupanda wakati Jumuiya hiyo iliposhiriki kwenye kampeni inayoendeshwa na Taasisi ya Tea inayojishughulisha na mazingira ikiwemo upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo ambapo miti hiyo ilipandwa kituo cha Afya Mwakidila
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Urassa Nanyaro kulia akipanda miti  wakati Jumuiya hiyo iliposhiriki kwenye kampeni inayoendeshwa na Taasisi ya Tea inayojishughulisha na mazingira ikiwemo upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo ambapo miti hiyo ilipandwa kituo cha Afya Mwakidila


Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye picha ya pamoja  mara baada ya kumalizika zoezi la kupanda miti wa pili kutoka kulia ni Mjumbe wa Wazazi wilaya ya Tanga Pamela Chaula


Na Oscar Assenga,TANGA.


KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Urassa Nanyaro ameshiriki kwenye kampeni ya upandaji wa miti katika kituo cha Afya Mwakidila Jijiji Tanga huku akiitaka jamii kuendelea kutunza mazingira.

Nanyaro aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati Jumuiya hiyo iliposhiriki kwenye kampeni inayoendeshwa na Taasisi ya Tea inayojishughulisha na mazingira ikiwemo upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo.

Alisema kwamba wananchi na jamii kwa ujumla wanapaswa kutunza mazingira kwa mustakabvali wa kuimarisha vyanzo vya maji na uchumi wa Taifa letu kwa sababu maji ndio chanzo kikubwa cha nishati ya umeme.

Aidha alisema na nishati ya umeme inapatikana kutokana na utunzaji mazingira na unapandwaji wa miti na hivyo kupatikana mvua za kutosha zinazopelekea mitambo ya kuzalisha umeme kutokana na uwepo wa mvua za kutosha.

“Niipongeze taasisi ya Tea kwa kuendesha kampeni hii kwani miti inapopandwa inasaidia kupata lishe,kivuli na matunda na kuwasaidia kuwezesha kupata mvua ya kutosha itakayowezesha kuendesha mitambo na kuzalisha nishati ya umeme inayotumika hospital viwanda na kuinua uchumi wa Taifa letu”Alisema Nanyaro.

Akiwa katika shule ya Msingi Mwakidila Katibu huyo aliwapongeza walimu wa shule hiyo kutokana na utunzaji wa mazingira na wana hifadhi ya mazingira ambayo ndio chanzo za utunzaji huo

“Sisi Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga majukumu yetu ni kushrikiana na shule za msingi ,awali,sekondari vyuo Lengo kuhamasisha vijana wapate malezi bora kulingana na tamaduni ya kitanzania tupo hapo leo wanapoanda miti ya matunda na kwa hali hiyo tuliokuta tunaamini miti itakuwa kwa muslakabali wa viumbe hali na kutunza vyanzo vyetu na vya maji “Alisema

Hata hivyo alisema licha ya utunzaji wa vyanzo vya maji lakini pia mwisho wa siku kupitia mazingira mazuri Taifa liweze kusonga mbele kiuchumi likiwa na watu wenye afya na siha njema.