BOHARI YA DAWA (MSD) YAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE YATAMBULIKA KIMATAIFA

March 07, 2018
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana walipotembelea Bohari ya Dawa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula, akitoa maelezo kwa wanahabari jinsi vifaa tiba na dawa zinavyohifadhiwa katika bohari hiyo.
 Muonekano wa maboksi ya dawa jinsi yalivyopangwa ndani ya bohari iliyopo Makao Makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam.
 Dawa na vifaa tiba zikipelekwa kuhifadhiwa ndani ya bohari.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akiwaonesha waandishi wa habari vifaa  mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula na Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia.
  Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia, akiwaonesha wabahabari vifaa vilivyopo kwenye mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Hilda Mhagama kutoka  gazeti la Daily News.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Saum Juma kutoka Kituo cha Televisheni cha TV One.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imezidi kuboresha huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hata kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa na kupata ithibati ya ISO 9001:2015.         

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED ilifanya ukaguzi Makao makuu ya MSD pamoja na Kanda zake nane mwezi Agosti 2017 na MSD ilionekana kufuata miongozo ya juu ya kimataifa na matakwa ya mamlaka za udhibiti ubora nchini.             

Katika mkutano huo, Bwanakunu pia alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu(135)  MSD imeimarika  na kufikia asilimia 90,huku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini hali ya upatikanaji wa dawa ni kati ya asilimia 85 na 98.              

Mkurugenzi Mkuu wa MSD pia aliwaonyesha waandishi wa habari  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000.

Amesihi taasisi, asasi, jumuiya na wananchi kununua mifuko hiyo ya vifaa vya kujifungulia na kutoa msaada kwenye vituo vya afya na hospitali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya nchini .      
                              
Katika mkutano huo Bwanakunu aliwazawadia waandishi wa habari wawili ambao ni wajawazito mfuko huo wa vifaa vya kujifungulia  kwa ajili ya kujiandaa kwenda kujifungua.

WAZIRI UMMY MWALIMU ARIDHISHWA NA UTENGAJI KAZI WA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA ILEJE

March 07, 2018
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi pamoja na mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkudew wakielekea eneo ambalo kituo cha afya kinajengwa kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi na kupokea maelezo ya ujenzi huo na namna pesa za serikali katika sekta ya afya zinavyotumika.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi   pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwa kwenye eneo ambalo kituo hicho kinajengwa.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitenda wakati wa ziara ya waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje

Na Fredy Mgunda,Ileje

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe.
 
Akiwa katika zira hiyo,Waziri Mwalimu alifanikiwa kukagua kituo cha afya cha Lubanda ambacho kilipewa kiasi cha shilingi milioni mia tano(500)  kutoka serikalini kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

“Mimi nimekuja kuangalia utekelezaji wa pesa ambazo serikali tunazileta huku kwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya,maana kumekuwa na watendaji ambao wamekuwa wakizitumia vibaya pesa ambazo tumekuwa tukizileta huku” alisema  Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alisema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa kituo cha afya cha Lubada unaoendelea kwa kasi nzuri na kwa viwango ambavyo serikali inavitaka na kuahidi kuwa ukimalika ujenzi huo utawaletea gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania.

“Kwa hapa mlipofikia nawapongeza sana kwa kuwa kazi nimeiona kwa macho yangu mwenyewe hivyo mkimaliza ujenzi nitakikisha kila kitu kinachotakiwa hapa kitakuwepo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa wilaya ya Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Hata Waziri Mwalimu aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Ileje kwa kufikisha asilimia tisini na moja (91) ya wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambao unarahisisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wanaotumia mfuko huo.

“Niwapongeze tena kwa kazi kubwa mliyofika ya wananchi wengi kukubali kujiunga kwenye mfuko huo,maana kuna halmashauri nyingine zijafgika hata robo yenu hiyo naona utendaji wenu uliotukuka katika kuwatumikia wananchi wa Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alizitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa halmashauri ya ileje kwa namna wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa baina ya mkurungezi mtendaji na mkuu wa wilaya hiyo ndio maana kuna matokeo chanya.

“Nichuke nafasi hii kukupongeza sana mkurugezi wangu Haji Mnasi na mkuu wa wilaya Joseph Mkude kwa ushirikiano mnaoushesha katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Ileje,napenda kama halmashauri zote hapa nchini zingekuwa kama halmashauri yetu tungekuwa tumefika mbali kimaendeleo” alisema Waziri Mwalimu

Awali akisoma hotuba kwa waziri, mkurugenzi wa halmashuri hiyo Haji Mnasi alisema kuwa halmashauri imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa afya ya jamii  kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye mfuko huo.

“Tunasheria ya mwaka 2004 ambayo inawataka wananchi wote wajiunge kwenye mfuko huo hivyo tutaitumia vizuri sheria hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajiunga kwenye mfuko huo akiwa tayari amepatiwa elimu ya kutosha na kumfanya ajiunge mwenyewe bila kulazimishwa” alisema Mnasi

Mnasi alisema kuwa huduma za matibabu kwa wazee zinatolewa katika vituo vyote 33 vya huduma za afya na jumla ya wazee 11463 waliotambuliwa na walipewa vitambulisho ni 8954 sawa na asilimia 78 ambapo jumla ya shilingi 7,196,000 zilitumika mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wazee.

“Lakini ukiangalia mwaka 2017/2018 tumetenga kiasi cha shilingi 28,000,000/= ambapo kwa kila zahanati tunapeleka kiasi cha shilingi 1,000,000 na kwenye vituo vya afya tunapeleka 2,000,000 kwa ajili ya huduma ya wazee na kazi ya kuendelea kuwatambua ni endelevu” alisema Mnasi

Mnasi alimuahidi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuwa pesa zote zinazoletwa kutoka kwenye wizara yake zitatumika kama zilivyopangwa na kuhakikisha zinasimamiwa vizuri kama ambavyo wamekuwa wakisimamia pesa zote za serikali zitumike kwa malengo yanayokusudiwa.

SHUWASA YATOA ELIMU YA MAJI KWA WANAWAKE SHINYANGA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

March 07, 2018
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imeendesha semina kwa wanawake wa manispaa ya Shinyanga kuwapa elimu kuhusu utoaji huduma ya maji safi na usafi wa mazingira.

MDAHALO WA KUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV PART ONE

March 07, 2018
Mdahalo wa sehemu ya kwanza wa kugombania kinyang'anyiro cha uongozi wa Waweka Hazina kupitia Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi, Siku ya Jumamosi March 3, 2018 katika ukumbi wa Indiana Springs Terrance Local Park Sliver Spring Maryland Nchini Marekani.

WAJIBU WA WACHIMBAJI WADOGO NI KUFUATA MAELEKEZO YA SERIKALI NA KULIPA KODI KWA UAMINIFU

March 07, 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita juu ya umuhimu wa kufuata taratibu na sheria katika uchimbaji, Jana 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza akisisitiza jambo wakati aliokuwa akihutubia wananchi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu (Kulia) wakisikiliza kero za wananchi wakati wa ziara ya kikazi Wilaa ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Geita

Serikali imesema kuwa imedhamiria kuwanufaisha wananchi wake kupitia rasilimali za nchi hususani sekta ya Madini hivyo jukumu la Wachimbaji hao ni kufuata maelekezo ya serikali ikiwemo taratibu na sheria katika uchimbaji.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa rai hiyo Jana 6 Machi 2018 wakati akizungumza na wachimhaji wadogo katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.

Alisema kuwa Serikali tayari imetenga maeneo maalumu kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Geita na maeneo mengi nchini huku akisisitiza kuwa kuna leseni za utafiti na uchimbaji mdogo 20 ambazo zinaisha muda wake 30 Machi mwaka huu katika Wilaya ya Nyang'wale hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kwani serikali inatazama namna ya kuwapatia wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo hayo.

Mhe Biteko alisisitiza hayo wakati akijibu maswali ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara na kuiomba serikali kuwapatia maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji kwani katika kipindi kirefu wamekuwa wakizuiwa kuchimba katika maeneo mbalimbali ambayo yana leseni za uchimbaji.

Alisema kuwa serikali itatoa leseni kwa ajili ya maeneo ya uchimbaji lakini haitatoa leseni hizo kwa mtu mmoja mmoja badala yake amewasihi wachimbaji hao kuanzisha vikundi ili kupatiwa leseni hizo.

Mhe Biteko pia alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wwale Mkoani Geita Mhe Hamim Gwiyama kuitisha kikao ndani ya wiki moja kwa kuwaalika wananchi wote wenyewe vikundi ili kuwaelekeza namna bora ya kufanya kazi za uchimbaji kwa kufuata taratibu na sheria.

Aidha, amewataka Wachimbaji hao Mara baada ya kupewa maeneo ya uchimbaji kuwa waaminifu kwa serikali yao kwa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kuboresha huduma za maendeleo ikiwemo sekta ya Afya, elimu na miundombinu.

UWT YACHARUKA, YAUNGA MKONO UAMUZI WA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) KUWACHUKULIA HATUA WALIOSHINDWA KUREJESHA MIKOP

March 07, 2018
Na Bashir Nkoromo Dar es Salaam
Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) imetaka wateja sugu wanaodaiwa na Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kuhakikisha wanalipa marejesho ya mikopo yao mara moja vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Akizungumza katika Makao Makuu ya UWT  Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Gaudensia Kabaka amesema UWT inaunga mkono Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya wanawake  Tanzania (TWB) Beng'i Issa ya kutaka wadaiwa sugu wa benki hiyo walipe marejesho ya mikopo ndani ya siku saba.

" Sisi Umoja wa Wanawake Tanzania na wanawake wote wa Tanzania kwa ujumla wetu hatutakubali na hatuko tayari kabisa kuona watu wachache wakiwemo hata wanawake wenzetu wakitumia benki hii kwa kujinufaisha wao wenyewe". alisema.

Ameongeza kwamba UWT wanapenda kuona mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati ili wengine pia waendelee kukopa bila matatizo akisisitiza kuwa TWB ndiyo benki pekee inayoweza kunmkopesha mamam mjasiriamali mdogo na pia ni miongoni mwa benki tatu tu zilozopo duniani ambazo ni maalum kwa wajili ya wanawake tu benki hizo zipo Pakistan, India na Tanzania.

"UWT tunatoa rai kwa wakopaji wote na tunatoa tamko kwamba hao ambao wamekopeshwa na hawajarudisha mikopo kwa wakati wachukuliwe hatua za haraka na stahiki ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha wanalipa mikopo yao yote kwa manufaa na uhai wa benki yetu na kwa manufaa ya wanawake wote nchini.

Wadaiwa sugu ni 7065 ambao ni wengi sana hasa kutokana na fedha wanayoihodhi ambazo ni kiasi cha Sh. Bilioni 6.79. Tungependa kuona mikopo hii inarejeshwa kwa wakati" Alisema.

Alisema kuwepo kwa benki ya wanawake nchini ni maombi na kilio cha mda mrefu cha wanawake nchini tangu uhuru kupitia Jumuiya ya CCM kuzaliwa. ni kilio cha Kina bibi Titi Mohammed na mama Sophia Kawawa wakati wa uhao wao wakiwa wenyeviti wa UWT kwa nyakati  tofauti na kilio cha wenyeviti wengine waliofuata hadi sasa.

"Napenda kuwaambia kuwa jambo hili  Kama Mwenyekiti wa UWT nalifuatilia kwa karibu sana kwa kuwa ni miongoni mwa maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wetu, Rais Dk John Magufuli wakati wa Mkutano wetu Mkuu uliofanyika Desemba 8, 2017 mjini Dodoma", alisema

Alisema Uongozi mpya wa UWT umekaa na benki ya wanawake kuangalia namna gani benki itaweza kufikia wananwake wengi na kwa riba nafuu zaidi.

HABARI KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akifafanua zaidi kwa nini UWT ipo bega kwa bega na beki ya Wanawake Tanzania, wakat akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Baadhi ya maofisa wa UWT wakiwa kwenye kikao hicho
Waandishi wa habari wakimsikiliza Gaudensia Kabaka
Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi akifunga Mkutano huo na Waandishi wa Habari baada ya Mwenyekiti wake Gaudensia Kabaka (katikati) kumaliza kutoa taarifa nzito ya UWT. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara Eva Kihwelo Mwingizi.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO


--

Best regards


Bashir Nkoromo
Blogger & Photojournalist
UHURU PUBLICATIONS LTD
Dar es Salaam, TANZANIA
         +255 789 498008,
BLOG: theNkoromo Blog  
Email: nkoromo@gmail.com  

MADINI NI MALI YA WATANZANIA SIO WAWEKEZAJI WA KIGENI-BITEKO

March 07, 2018

Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya watendaji katika Wilaya ya Nyang'wale mara baada ya kuzuru wilayani Nang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama ikimsikiliza kwa makini Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (aliyesimama) akielezea mikakati ya wizara hiyo wakati alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu, na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mhe Hamim Gwiyama

Na Mathias Canal, Geita

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tangu ianze utendaji wake imejipambanua wazi kuwa rasilimali zote za nchi ikiwemo madini ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni Mali ya watanzania wenyewe sio wawekezaji wa kigeni.

Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa katika rasilimali Madini Taifa halipaswi kukurupuka kuyachimba kwa kuwa uwezo wa kitaaluma na kiteknolojia kuwezesha kuyachimba na kuyafaidi kama Taifa ulikuwa mdogo kwa mantiki hiyo, Baba wa Taifa akaenda mbali zaidi kwa kuagiza madini yasichimbwe hadi hapo Taifa litakapokuwa na uwezo wa kuyachimba ili watanzania waweze kunufaika ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 6 Machi 2018 wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.

Mhe Biteko alisema kuwa Mwalimu kwa wakati huo alijua fika kuwa Tanzani a ikifungua milango ya kuchimba madini bila Taifa  kujenga uwezo imara wa kufanikisha lengo hilo ipasavyo, wataalamu na wafanyabiashara au wale wanaoitwa wawekezaji kutoka nje, ilimradi wanazo fedha nyingi; watalilalia Taifa na kuwadanganya watanzania na hatimaye kuweza kufaidika zaidi kutokana na rasilimali madini.

Alisema kuwa Kwa mtazamo huo Rais Magufuli, aliamua kuweka mbele utaifa kuliko maslahi binafsi kwa kuifufua sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2017 ili kuiyafanya rasilimali Madini kuwa na manufaa kwa watanzania wenyewe kuliko ilivyokuwa awali.

"Mimi nataka niwaambie kuwa rasilimali madini ni mali ya Taifa letu au kwa maneno mengine ni mali ya Watanzania; na viongozi (kwa ngazi zote) tumepewa dhamana tu ya kusimamia na kuhakikisha Taifa letu linanufaika kutokana na uchimbaji madini, na si vinginevyo" Alisema Biteko

Aliongeza kuwa Taifa linaweza kuendelea zaidi endapo kwa wachimbaji kwa pamoja watakubali kufuata sheria na taratibu za uchimbaji huku wakiunga mkono juhudi za serikali kwa kulipa kodi ili kuwa na mafanikio wezeshi kwa watanzania wote.

Kwa upande wake Mbunge Wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassoro Amari Kasu alisema kuwa Katika Wilaya hivyo serikali bado inapoteza kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya kutowarasimisha na kuwapa leseni Wachimbaji wadogo.

Aidha, aliiomba serikali kuwapatia leseni Wachimbaji wadogo kupitia vikundi vyao walivyovianzisha ili kurahisisha ukusanyaji Wa mapato sambamba na mafanikio ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.