WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN

October 11, 2017
 Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy  Mwalimu akizungumza na wananchi wa Tarime mkoani Mara na kutoa miezi sita kwa wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama kwa mtoto kike katika Shule zao.
 Mkuu Wa mkoa wa Mara Mhe. Charles Mlingwa  akihamasisha wananchi wa mkoa wa Mara kuzingatia na kulinda haki za Mtoto katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyofikia kilele chake 11/10/2017.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima". 
 Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
NMB yatoa msaada wa vitanda na magodoro Hosipitali ya Nyamagana

NMB yatoa msaada wa vitanda na magodoro Hosipitali ya Nyamagana

October 11, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa Benki ya NMB wakifungua rasmi tawi jipya la Benki ya NMB Pamba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akizungumza kwenye afla ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB Pamba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda 11 vikiwa na magodoro na mashuka yake katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba) wenye thamani ya Sh Milioni 10 kwa ajili ya akinamama wajawazito na hivyo kupunguza adha ya kukosa malazi. Msaada huo ulitolewa na uongozi wa benki hiyo mara baada ya kukamilika kwa hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMB Pamba katika wilaya ya Nyamagana jijini hapa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa NMB kanda ya ziwa- Abraham Augustino, alisema msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. “Ni utaratibu wa kawaida kwa benki yetu kutoa sehemu ya faida yake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ili nao waweze kunufaika, na kuona umuhimu wa kuwepo kwa NMB katika maeneo yao,” alisema. Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela aliishukuru benki hiyo kwa kuhakikisha kuwa inatoa sehemu ya faida yake katika kuisaidia jamii, hususani kwa kutoa msaada wa vitanda hivyo katika hosipitali ya wilaya ya Nyamagana ( Butimba) Aliipongeza benki hiyo kwa kusogeza huduma za kibenki karibu kwa wananchi, kwa kufungua matawi 32 kwa mikoa ya Kanda ya ziwa na kufanya sasa kuwa na jumla ya matawi 211 kwa nchi nzima. Alisema serikali inaipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo nzuri waliyofikia kwa kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi na kunapunguza umbali na imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma hizo ambao kwa sasa hawafiki asilimia 20 kwa nchi nzima. Aliwataka wakazi wa mkoa wa Mwanza kujiunga na kuitumia benki hiyo ili waweze kuwa na mfumo mzuri wa kuhifadhi fedha utakaowawezesha kupata mikopo kwa ajili ya ustawi wa maisha yao. “Sasa muache tabia ya kuweka fedha nyumbani huduma imekwishaletwa karibu, wekeni fedha zenu benki na hii itasaidia kupunguza kesi za kuvamiwa na kuporwa fedha” alisema. Alisema kuwa, serikali ya awamu ya tano imeweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kwa wananchi wake kwa kutumia fursa zilizopo, na kuwa ndiyo maana imekuwa ikiunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa maendeleo, zikiwamo taasisi za fedha ikiwemo benki hiyo. Aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kubuni huduma mpya na kufungua matawi mapya kwa lengo la kuhakikisha huduma zinakuwa karibu na wananchi, ili kuwaondolea adha ya kufuata huduma hizo mbali na makazi yao. “Napenda kuwapa changamoto kwa ajili ya kusaidia kuendeleza na kukuza uchumi na ajira kwa wananchi, kwa kuendelea kutoa mikopo kwa wakazi wa vitongoji vyote vya mkoa wa Mwanza” alisema. Alisema kuwa, kuwapo kwa huduma za kibenki ni kichocheo madhubuti cha maendeleo ya uchumi, maana sekta ya fedha ndiyo inawezesha shughuli zote za uchumi kama kuwekeza, malipo ya kibiashara na ya binafsi, kuweka amana na mikopo binafsi na ya biashara. Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Tom Borghols alisema kuwa jiji la Mwanza ni jiji linaloendelea kukua kiuchumi, hivyo linahitaji upanuzi wa huduma za kifedha, na ndiyo maana wamekubali maombi ya wananchi ya kuongezewa tawi jingine la benki. “Kufunguliwa kwa tawi hili la NMB Pamba litasaidia kuokoa muda ambao wananchi wamekuwa wakiupoteza kwa kukaa benki kwa muda mrefu kusubiria huduma” alisema. Aidha, alisema kuwa, mbali na kufungua matawi katika maeneo mbalimbali, NMB inazidi kuanzisha huduma mbadala ikiwamo kuweka mawakala, ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wateja, na kwa sasa ina jumla ya mawakala 3,800 nchi nzima. “Tulikuwa na matawi 210 tukiongeza na hili yametimia 211, mawakala wameongezeka sasa ni zaidi ya 3,800, lakini pia tuna mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 700 nchi nzima, na tutaendelea kuboresha huduma zaidi kwa ajili ya wateja wetu” alifafanua.  
Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB, Tom Borghols (aliyesimama) akizungumza katika uzinduzi wa tawi jipya la NMB Pamba katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. 
Burudani za ngoma zikiendelea kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya NMB Pamba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. 
Sehemu ya wananchi wakishughudia uzinduzi huo wa tawi jipya la Benki ya NMB Pamba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com

RC SHIGELLA AFUNGUA KIKAO CHA RCC LEO MKOANI TANGA

October 11, 2017
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa huo (RCC) kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika kikao hicho leo
 Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Miundombinu mkoa wa Tanga,Monica Kinala akifafanua jambo kwenye kikao hicho wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akielezea mikakati ya Bandari hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC)
 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga akizungumza katika kikao hicho kuelezea mipango yao
 MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Gabriel Robert
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi katika kikao hicho
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifafanua jambo kwenye kikao hicho kushoto  ni Katibu Tawala wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwenye kikao hicho

 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akichangia kwenye kikao hicho
Mbunge wa Jimbo la Lushoto,Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akiuliza swali kwenye kikao hicho
 Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Miundombinu mkoa wa Tanga,Monica Kinala katikati na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga(RMO) Dkt Asha Mahita wakifuatili kikao hicho
 Mbunge  wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda, Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda akifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaji Mussa Mbaruku akifuatilia kwa umakini kikao hicho
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na PRO wa Bandari hiyo,Moni Jarufu kulia wakati wa kikao cha kamati ya Ushauri wa Mkoa wa Tanga (RCC)
 Meneja wa Shirika la Taifa la  Nyumba (NHC) Mkoani Tanga,Mussa Kamendu na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga,Mhashamu Anthony Banzi akiwa kwenye kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Januari Lugangika kushoto akifuatilia kwa umakini hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017

October 11, 2017
Mkoa wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi Oktoba.

WAFANYAKAZI BENKI YA TPB MKOA WA MBEYA WAUNGANA NA WATEJA WAO KUSHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

October 11, 2017
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika Picha ya pamoja katika sherehe za wiki ya huduma kwa mteja iliyofanyika katika Ofisi Kuu za TPB Mwanjelwa jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wadau mabalimbali wa benki hiyo.

Baadhi ya wateja na wadau mbalimbali waliohudhuria kilele cha wiki ya huduma kwa mteja benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika Ofisi za kuu Tpb Mwanjelwa.


Wateja na wadau wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya wakikata keki katika sherehe za kilele cha wiki ya huduma kwa mteja iiliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu za TPB Mwanjelwa .

Meneja wa Benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Ndugu Humphrey Julius (kulia ) akilishwa keki na mteja wa TPB  katika kilele cha wiki ya huduma kwa mteja iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu za benki hiyo Mwanjelwa jijini Mbeya

Wafanyakazi wa benki ya TPB Mkoa wa Mbeya katika nyuso za furaha siku ya sherehe za wiki ya huduma kwa mteja ambayo imefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za TPB Mwanjelwa jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali. .

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA AFRICAID KUPITIA MRADI WA KISA LAWAKUTANISHA WASICHANA WA KIDATO CHA TANO NA SITA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOANI KILIMANJARO

October 11, 2017
Muwasilishaji wa mada katika kongamano lililowajumuisha Wasichana wanaosoma kidato cha tano na sita katika shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro,Nyamagesa Laban akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Wanyamapori Mweka. 
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa karibu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Nyamagesa ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.
Baadhi ya wananfunzi walioshiriki kongamano hilo wakiuliza maswali kwa Nyamagesa mara baada ya kumaliza kutoa ujumbe kwa wanafunzi hao.
Muwasilishaji wa mada katika kongamano la Wasichana wa Shule za Sekondari mkoni Kilimanjaro,Stumai Simba akizungumza katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia Mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya Wanafunzi wakimuuiza maswali Muwasilishaji wa mada katika ongamano hilo.

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

WASICHANA walioko shuleni  wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.

Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.

Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400 kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .

Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.

Msimamizi wa Mradi wa KISA mkoa wa Kilimanjaro ,Devota Mlay amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa kike wanaosoma kidato cha tano na sita ni kuwaandaa kwenda kutoa elimu kwa mtoto wa kike katika jamii pindi wamalizapo masomo .

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki kongamano hilo wameeleza mambo wanayojifunza kupitia makongamano huku wakifurahishwa na namna ambavyo wawasilishaji wa mada walivyofanikiwa bila ya kungojea kupata ajira serikalini.

Kongamano hilo ambalo limejumisha shule za 11 kutoka wilaya za Mwanga,Rombo,Same,Siha ,Hai  na Moshi mjini linatarajia pia kufanyika katika mkoa wa Arusha na kuhusisha wanafunzi wa kidadto cha tatno na sita katika shule za mkoa wa Arusha.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB,MATAWI YA MAWENZI NA MBUYUNI MJINI MOSHI WAFANYA USAFI NA KUTOA ZAWADI KWA WAGONJWA ,HOSPITALI YA ST JOSEPH

October 11, 2017
Wafanyakazi wa Benki ya NMB ,Matawi ya Mawenzi na Mbuyuni wakiwa katika Hospitali ya St,Joseph mjini Moshi kwa ajili ya zoezi la usafi pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni muendelezo a wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja wa watumishi wa Hosptali ya St Joseph akimvisha kizuia vumbi ,mfanyakazi wa Benki ya NMB walipofika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya usafi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya St Joseph Sista,Ubanus Lyimo akimvisha kofia maalumu Menenja wa Benki ya NMB,tawi la Mawenzi kabla ya kuanza zoezi la Usafi katika Hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Maeenzi na Mbuyuni mjini Moshi wakishiriki zoezi la usafi eneo la nje ya Hospitali ya St Joseph ikiwa ni sehemu ya kuendelea na maadhimisho ya wiki ya huduma kwa watena.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakichoma moto taka mara baada ya kuhitimisha zoezi la usafi katika Hospitali hiyo
Wafanyakazi wa NMB,matawi ya Mawenzi na Mbuyuni mjini Moshi ,wakiwa wameshikilia Fagio mara baada ya kuhitimisha zoezi la usafi katika Hospitali ya St Joseph.
Afisa Mikopo katika Benki ya NMB,tawi la Mawenzi mjini Moshi,Elikana Boyi akikabidhi mche wa sabani kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya St Joseph Mjini Moshi.
Meneja wa NMB,tawi la Mawenzi ,Johnson Urasa akiweka mche wa sababuni mbele ya mtoto aliyelazwa katika hospitali ya St Joseph ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya huduma kwa wateja.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Mbuyuni ,Rose Manyoni (katikati) akisaidiana na mwenzake kumuinua mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya St Joseph walipofika kuwajulia hali pamoja na kutoa zawadi. 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi,Sista Ubanus Lyimo akizungumza mara baada ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Mawenzi na Mbuyuni kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwakatika hospitali hiyo.
Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Mawenzi ,Johnson Urasa akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la kufanya usafi pamoja na utoaji wa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Mawenzi na Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha zoezi la kufanya usafi na utoaji wa zawadi kwa wagonjwa waliolazwakatika Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.