RAIS KIKWETE ATENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI WAKE WANNE NI KATIKA SAKATA LA OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI

December 20, 2013

Rais Jakaya Kikwete ametengua rasmi uteuzi wa Mawaziri wa nne waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za kiraia wakati wa Oparesheni Tokomeza Ujangili iliyokuwa ikiendeshwa na Serikali.
Akisoma Bungeni mjini Dodoma leo jioni, Taarifa hiyo ya Rais, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Bungeni mjini Dodoma kuwa Rais ameridhia maoni ya Wabunge wakati wa kujadili ripoti ya Kamati iliyoundwa na kuongozwa na Mbunge James Lembeli kuwa Mawaziri waliotuhumiwa waondoke.
 
CHANZO  mrokim.blogspot.com

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA (TFF)

December 20, 2013
Release No. 211
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 20, 2013

AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.

TFF tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi.

Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari  25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

ANGALIA KAZI YA KWANZA YA OKWI MAZOEZINI, AZIDI KUMUUMBUA RAGE

December 20, 2013



im
OKWI MAZOEZINI NA YANGA LEO ASUBUHI

Baada ya hadithi nyingi za Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage, Okwi ameweka tayari rekodi mbili na Yanga.

Moja ilikuwa jana alipovaa kwa mara ya kwanza jezi ya Yanga na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo.

Lakini leo, ameweka nyingine baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo akiwa chini ya Kocha Mholanzi, Ernie Brandts.

KAGERA SUGAR KUCHEZA MECHI 4 ZA KIRAFIKI UGANDA

December 20, 2013


imewekwa Desemba 20 saa 05:51 Jioni.
Timu ya ya Kagera Sugar inatarajia kucheza mechi nne za kirafiki na timu za Sports Club Villa, Express, URA na Bunamwaya kutoka Uganda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Januari, mwakani.

SIMBA SC KAMILI YAREJEA DAR LEO TAYARI KUIONYESHA YANGA SC ‘CHA MDOLI MILELE’

December 20, 2013
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIKOSI kizima cha Simba SC kinarejea leo Dar es Salaam kwa ndege kutoka Zanzibar walipokuwa wameweka kambi wiki yote hii kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe kesho dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Simba watakwenda kambini katika hoteli ya Spice, Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho.
Wanarejea leo; Simba SC wanatua kwa ndege leo kutoka kambini Zanzibar

Taarifa zinasema hakuna majeruhi na wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa kesho, unaoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro.  

TCRA YAWAFUNDA WAANDAAJI WA VIPINDI NA WATANGAZAJI WA REDIO KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

December 20, 2013

Imewekwa Desemba 20 saa 05:07 Jioni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Tcra ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi, Magreth Mnyagi amesema lengo la washa hiyo ni kuwakumbusha watangazaji kuhusu kufuata maudhui yaliyokusudiwa yanayoelimisha na kuburudisha jamii na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Mgeni rasmi wa Washa hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amesema kukiuka kwa maadili katika baadhi ya vituo vya utangazaji kunatokana na wamiliki kuwaajiri wafanyakazi wasiokuwa na taaluma ya Utangazaji.

KIMBUNGA KILICHOAMBATANA NA MVUA KALI CHAUA WAWILI NA KUHARIBU NYUMBA ZAIDI YA 183 MBARALI MBEYA

December 20, 2013

IMEWEKWA DESEMBA 20 SAA 12:58 MCHANA.

Mkuu wa mkoa Mbeya Abas akielezewa jinsi kimbunga hicho kilivyo haribu nyumba za wananchi wa kata tatu Mbarali


RAGE: WALIOMUUZA OKWI NI SC VILLA YA UGANDA LAKINI PIA NI HUJUMA KUTOKA NDANI YA KLABU YA SIMBA

RAGE: WALIOMUUZA OKWI NI SC VILLA YA UGANDA LAKINI PIA NI HUJUMA KUTOKA NDANI YA KLABU YA SIMBA

December 20, 2013

Emmanuel Okwi.

imewekwa Desemba 20 saa 12:51
Na Nicodemus Jonas

MWENYEKITI aliyesimamishwa wa Simba, Ismail Rage, amefanya kikao na baadhi ya wanachama wa timu hiyo na kutoa siri kwamba waliomuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa Yanga ni Waganda, SC Villa, lakini akasisitiza ni hujuma kutoka ndani ya klabu hiyo.

Championi Jumatano lilikuwa likipata ‘live’ kila kinachoendelea ndani ya kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya klabu ya Simba, barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam, juzi.

Akionyesha mwenye masikitiko, Rage alisema kuna baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wanahusika katika usajili wa Okwi aliyetua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

RUBANI WA NDEGE YA ETHIOPIA ILIYOTUA ARUSHA KWA DHARURA ALIUCHANGANYA UWANJA HUO NA WA KIA

December 20, 2013



Imewekwa Desemba 20,2013 saa 12:40.
Rubani wa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines iliyotua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Arusha, alitua kwenye uwanja huo baada ya kudhania ni ule wa Kilimanjaro International Airport (KIA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, (TCAA) imesema.
Badala yake rubani huyo alitua kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wenye njia ya kutua iliyo na urefu wa meta 1,640 ambayo ni fupi mno kwa ndege hiyo aina ya Boeing 767-300ER kutua. Ndege hiyo inahitaji walau njia ya kutua yenye urefu wa meta 1,798.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhil Manongi, alisema kwenye maelezo yake kuwa pamoja na kwamba kulikuwa na ndege mbovu kwenye njia ya kutua ndege ya KIA, uwanja huo una njia yenye urefu wa meta  3,600 na kusema kuwa bado kulikuwa na meta 3,200 zilizotosha kwa ndege No. ET-815 kutua.

Amesema tayari wataalam wapo uwanjani hapo kufanya uchunguzi.Meneja wa Uwanja wa Ndenge wa Arusha, Ester Dede alisema baada ya abiria wote 213 waliokuwa katika ndege hiyo kusaidiwa na kuendelea na safari zao, uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha tukio hilo.
SOURCE: TIMES FM