MBUNGE CHUMI AITAKA SERIKALI KUSAMBAZA MBOLEA KWA WAKATI

April 09, 2018




Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameitaka Serikali kuhakikisha inasambaza mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

Chumi amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.

'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima hawakupata mbolea'

'Sio hivyo tu, hata hiyo 64% hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa, mkulima wa Itimbo, Kitelewasi, Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia mwezi February wakati uandalizi wa mashamba unaanza mapema Oktoba.'

Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni kuwaonea wakulima

Akizungumzia wakulima kuuza mazao yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani 2.6milioni ya chakula, lakini Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani 26,000(elfu ishirini na sita tu), afu mkulima anazuiwa kuuza mahindi yake, jambo ambalo sio sawa.

Tunawafanya wakulima wa nchi hii kama raia daraja la pili (second citizens) mbolea tuwacheleweshee, ziada ya mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa' alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza kuwa ni vizuri serikali ikaangalia changamoto ilizokutana nazo katika usambazaji wa mbolea mwaka huu na kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima kupata mbolea kwa bei nafuu, kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.

Awataka Wawekezaji Mafinga kuwajali wafanyakazi

Akizungumzia haki za wafanyakazi, Chumi alisema kuwa anapongeza jitihada za Rais John Magufuli kuvutia wawekezaji, lakini akaitaka Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira kutupia jicho haki za wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga.

Uchumi wa Viwanda lazima uendane na welfare ya wafanyakazi, itakuwa haina mana kuwa na viwanda lakini hali za wafanyakazi zinakuwa duni, lazima walipwe vizuri, waangaliwe huduma za afya na kulipiwa nssf , alisisitiza Mbunge huyo.

Akifafanua, alisema sio haki mfanyakazi anatoka Changarawe, anatembea mpaka kilometa nne kwenda kazini, sio haki.ni hatari sana, unakuta mama anaamka saa kumi alfajiri kuwai kazini ambako nako halipwi vizuri, nikuombe mama Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu) na kaka yangu Mavunde (Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Vijana) nadhani ni mdogo wangu kufika Mafinga na kutoa maelekezo.

Apongeza Mhe Rais kukutana na Wafanyabiashara, ashauri akutane nao Kisekta

Tumeona ambavyo Jumuiya ya wafanyabiashara walieleza kero zao na Mhe. Rais na Rais akaagiza Mawaziri wazifanyie kazi, lakini nimuombe Mhe Rais akutane na Wafanyabiashara kisekta mana siku ile wote tuliona muda ulikuwa mdogo kwa mfano anaweza kukutana na sekta ya usafirishaji.

Akizungumza baadae na Mwandishi wetu, Chumi alisema kuwa mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga hayaridhishi na wanapolalamika kwa baadhi ya viongozi taarifa hurejeshwa kwa wenye viwanda kwa siri na matokeo yake mlalamikaji hutafutiwa visa na kufukuzwa kazi.

MKOPO WA DOLA MILIONI 65 WA KAGERA SUGAR WAWEKEZWA NCHINI

April 09, 2018

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Bungeni Mjini Dodoma,  aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kagera, kukopa kiasi  cha dola milioni 65 za Marekani  ambacho amedai kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo  wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.


Na Benny Mwaipaja

Serikali imeeleza kuwa kiasi chote cha dola za Marekani milioni 65 zilizokopwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutoka Benki ya CRDB kwa udhamini wa Serikali mwaka 2004 kimewekezwa nchini na hakijapelekwa kuwekeza katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda hicho kukopa kiasi hicho cha fedha ambacho kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji uliofanywa katika Kiwanda cha Kagera ni wa takribani dola za Marekani milioni 250 hivyo haiwezekani mwekezaji kukopa dola milioni 65 na kuzipeleka Congo ili hali kiwango cha uwekezaji nchini ni kikubwa.

“Mwekezaji wa Kiwanda hicho ni wa ndani na amejitahidi kuajiri watanzania wengi hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kukiwezesha kiwe cha mfano ili kiendelee kuleta matokeo chanya kwa watanzania”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali la msingi la Mbunge huyo, alitaka kujua kiwango cha hisa ambacho Serikali inamiliki katika kiwanda cha Sukari cha Kagera na kiasi cha fedha kilichokopwa na kulipwa na mwekezaji huyo kupitia udhamini huo wa Serikali.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa sasa haimiliki hisa zozote katika kiwanda hicho na kuongeza kuwa hisa zake katika kiwanda hicho ziliuzwa mwaka 2001 baada ya kukibinafsisha kiwanda hicho kwa Kampuni ya Kagera Saw Mills Limited.

Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mwekezaji wa Kiwanda hicho alikopa kiasi cha dola za Maerekani milioni 65 kwa kutumia udhamini wa Serikali mwaka 2004, ikiwa ni udhamini (guarantee) wa kipindi cha miaka 12. Alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho mimerejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 56.88, sawa na asilimia 87.5 ya mkopo wote, na kwamba marejesho ya mkopo uliobaki wa Dola milioni 8.12 yatafikia ukomo wake mwezi Julai, 2019.

JENGO LA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KUWA KIVUTIO CHA KIHISTORIA CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA UTALII JIJINI ARUSHA

April 09, 2018



Na Hamza Temba - WMU
.......................................................
JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa nchini.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla muda mfupi baada ya kukagua jengo hilo ambalo linasemekana kuwa refu kuliko majengo yote jijini Arusha likiwa na jumla ya ghorofa 18.

Alisema jengo hilo ambalo linatizamana na Round About ya AICC katikati ya jiji hilo, limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja (One Stop Centre) cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla.

Alisema jengo hilo litatoa fursa kwa wadau mbalimbali wanaotoa huduma za utalii kuweka ofisi zao ikiwemo mabenki, watoa huduma za usafiri, mashirika ya ndege, mawakala wa safari za utalii na huduma, maduka ya bidhaa za utalii na mahoteli.

"Tutapamba pia jengo hili na" live screen" (Mabango ya Video Mubashara) za vivutio, hivyo wanyama wakiwa wanapita huko porini watakuwa wanaonekana "LIVE" (Mubashara) kwenye jengo hili kupitia LED Screen ambazo zitakuwa zimezunguka jengo hili" alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema huduma nyingine zitakazotolewa katika Jengo hilo ni pamoja na zile za kuangalia jiji la Arusha kupitia darubini, huduma za burudani ikiwemo kumbi za starehe na migahawa.

Kwa upande wake Mkandarasi wa jengo hilo, Mhandisi Bismas Meela wa Kampuni ya Inter-Consult limited alisema ujenzi wa jengo hilo ambalo ulianza mwezi Novemba, 2013 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.

Alisema jengo hilo ambalo lina uwezo wa kupaki magari 67 kwa wakati mmoja katika ghorofa za chini linagharimu shilingi za Kitanzania bilioni 45.

Katika ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa jengo hilo, Dk. Kigwangalla aliongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi na Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu kuhusu jengo la kitega uchumi la mamlaka hiyo lililopo katikati ya Jiji la Arusha ambalo limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Jiji la Arusha akiwa juu ya Jengo la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kutoka kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi.

Dk. Kigwangalla akiendelea kupata maelezo kuhusu jengo hilo kutoka kwa Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa mamlaka hiyo, Asangye Bangu.
Dk. Kigwangalla na msafara wake wakiangalia umbo la uso wa simba uliotengengenezwa katika moja lango la kuingilia kwenye lift ndani ya jengo hilo. Milango yote ya kuingilia kwenye lift ndani ya jengo hilo itapambwa kwa taswira mbalimbali za wanyamapori.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ngazi maalum zinazotumia nishati ya umeme ndani ya Jengo hilo. Kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu na nyuma yake ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi. \
Waziri Kigwangalla akikagua kabati la kuhifadhia vitu katika moja ya Hotel Aprtment ndani ya jengo hilo. Kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu.

Muonekano wa jengo hilo kutokea barabara ya Makongoro Jijini Arusha.

KINANA AONGOZA VIONGOZI WA CCM MAOMBOLEZO YA WINNIE MADIKIZELA MANDELA

April 09, 2018


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dkt Gaudensia Kabaka (MCC) akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg.Shaka Hamdu Shaka akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana akiagana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.


(Picha zote na Fahadi Siraji CCM BLOG)

NAIBU SPIKA TULIA AWAASA WATANZANIA KUILINDA NA KUITUNZA AMANI YA NCHI TAMASHA LA PASAKA MJINI DODOMA

April 09, 2018


Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akikata utepe kuashiria uzinduzi wa albamu mpya ya Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili. Rose Muhando ijulikanayo kwa jina la 'Usife Moyo'wakati wa kilele cha tamasha la pasaka katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana jioni.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na mwandaaji wa tamasha hilo Alex Msama.

Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson kwa pamoja na viongozi wengine wakifurahia jambo mara baada ya uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando ijulikanayo kwa jina la 'Usife Moyo',.

Mgeni rasmi katika tamasha la pasaka 2018,Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akizungumza mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),waliofika kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili wakitumbuiza katika tamasha hilo mapema jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Dkt Tulia aliwaasa Watanzania kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa gharama yoyote,kwani wakiichezea amani waliyonayo kuipata tena haitakuwa rahisi,hivyo akaongeza kwa kuwaomba Watanzania waishi kwa upendo,kushirikiana kwa namna moja ama nyinine na pia kushiriki katika suala zima la kujenga uchumi wa nchi yao na hatimae kupiga hatua katia suala zima la maendeleo.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini,Mh.Anthony Mavunde akitoa neno la shukurani kwa kampuni ya Msama Promotions Ltd kwa kuandaa tamasha la pasaka 2018 mjini humo na kuwakusanya Wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake,kuja kujionea waimbaji mahiri wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa Jamhuri.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Alex Msama ambaye ndiye Muaandaji wa tamasha la pasaka 2018 akiwashukuru wakazi wa Dodoma na Vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi katika tamasha la pasaka ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson,Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwajelwa pamoja na Rose Muhando.

Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akicheza na Mwimbaji Rose Muhando, Mwimbaji Bonny Mwaiteje na Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwajelwa na baadhi ya wabunge mara baada ya kuzindua albam yake inayoitwa “Usife Moyo” kwenye tamasha la pasaka lililofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana jioni.Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na mwandaaji wa tamasha hilo Bw. Alex Msama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Mh. Kapteni George Mkuchika akizungumza katika tamasha hilo huku Naibu Spika Dk.Tulia Ackson na baadhi ya viongozi wengine wakimsikiliza.

Sehemu ya Meza kuu,ikifurahi yaliyokuwa yakijiri uwanjani huku waimbaji wakiendelea kuimba kwa zamu ndani ya tamasha la Pasaka jana jioni mjini Dodoma.


Sehemu ya Meza kuu ilipoamua kushuka na kwenda jukwaani kuunga mkono na kutoa neno la shukurani kufuatia kufanyika tamasha la Pasaka jana jioni mjini Dodoma.

HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.