SERIKALI YASEMA KERO YA MAJI ITAMALIZIKA MWEZI JUNI MWAKANI

February 01, 2015
NA ELIZABETH KILINDI,MUHEZA.
IMEELEZWA kuwa ifikapo mwezi juni mwakani serikali itakuwa imesaidia kutatua kero ya maji  kwa wakazi milioni saba waishio vijijini.

Kauli hiyo imetolewa na ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu Stephen Wasira wakati wa  ziara yake yakuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Misongeni kilichopo wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Wasira alisema ni  asilimia 57 ya wananchi wa maeneo ya vijijini ambao wanapata huduma ya maji na kwamba lengo la serikali ni kukabiliana na tatizo hilo.

Aidha waziri huyo alisema suala  la ukosefu wa maji katika maeneo ya
vijijini linatatuliwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa ulioanza
kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho akiwemo Amina  Juma alisema walikuwa wakitumia maji ya visima walivyovirithi toka kwa babu zao na kwamba mpango wa TASAF imekuwa msaaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Fatuma  Haruna   Mkazi wa Misongeni alisema walikuwa wakiamka saa nane za usiku kufuata maji kisimani na kwamba tatizo hilo lilikuwa likiwakwamisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji.

"tulikuwa  tunapata shida sana na maji uwezi kuyapata bila ya  kuamka saa nane za usiku tena umbali mrefu mara nyengine  tunakutana hata na wanyama wakali,"alisema fatuma na kuishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »