DAWASCO YANASA NYUMBA TANO KWA WIZI WA MAJI TABATA

February 26, 2016

Na Mwandishi wetu,

Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (Dawasco), imenasa wizi mkubwa wa Maji katika nyumba tano ambazo zimeunganishiwa huduma ya majisafi kinyume cha utaratibu maeneo ya Tabata Magengeni, nyumba hizo zinamilikiwa na mfanyabiashara mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, nyumba hizo zimepangishwa kwa familia tano tofauti (Apartments).


Akizungumzia tukio hilo katika operesheni ya mtaa kwa mtaa ya kuhakiki matumizi sahihi ya Maji kwa wateja wa majumbani, Meneja wa Dawasco Tabata, Bi. Victoria Masele, alisema kuwa amebaini wizi huo baada ya kuona bili ya mwezi inayokuja haiendani na matumizi halisi ya Maji, hivyo wakaamua kufanya uchunguzi na kubaini kuwa mteja alikuwa amejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha taratibu.


Msoma mita wetu alikuwa na wasiwasi sana na matumizi ya Maji ya hizi nyumba, kwa sababu bili ilikuwa ndogo ukilinganisha na idadi ya familia zinazoishi kwenye hizi nyumba, ndipo tukaamua kufanya uchunguzi wa kina na kukuta mteja amejiunganishia laini 3 za Maji, laini 1 ikiwa imepita kwenye mita, 2 hazijapita kwenye mita, zimeelekezwa kwenye kisima na baadaye Maji yanasukumwa na kujaza matenki 5 ya lita 10,000, na lingine la lita 6000


Baada kunasa wizi huo, tuliwasiliana na meneja wa nyumba hizo ambaye hakuwepo eneo la tukio, na kudai kuwa hajui chochote kuhusiana na wizi huo wa Maji kutokana na kuishi mbali na nyumba hizo na kwamba wizi huo inawezekana wa wapangaji wenyewe, lakini aliahidi kufika katika ofisi zetu za Dawasco kumaliza tatizo baada ya wapangaji kushindwa kutupa ushirikiano alisema Bi. Masele


Hadi taarifa hizi zinakwenda mtamboni, meneja wa nyumba hizo alifika katika ofisi za Dawasco Tabata na kufanya mazungumzo na Meneja wa kituo, na kutakiwa kulipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 5.3.


DAWASCO inaendelea kutoa rai kwa wananchi wote kuwafichua wezi wa Maji kwa kuwa wanasababisha wateja halali kukosa huduma ya Maji kwa wachache kujiunganishia huduma kinyume na taratibu, hivyo mwananchi yeyote ambaye amejiunganishia Maji kinyume cha taratibu na ambaye hana huduma ya Maji afike katika ofisi yoyote ya Dawasco iliyopo karibu yake ili aunganishiwe huduma ya Maji kihalali.

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI CHAFANYIKA LEO.

February 26, 2016
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jesh Lupembe akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halamshauri hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashari ya Manispaa ya Moshi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo .
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa  katika kikao cha baraza hilo.
Diwani wa kata ya Ngangamfumuni ,Anthony .......akichangia hoja katika kikao cha bajeti cha Halmashauri ya manispaa ya Moshi .
Diwani wa kata ya Ng'ambo ,Genesis Kihwelu akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akifuatlia hoja katika kikao hicho.
Msathiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jesh Lupembe.
Diwani wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo akichangia hoja katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia michango ya madiwani wenzao katika kikao hicho.
i Diwani wa kata ya Miembeni,Mbonea Mshana akichangia hoja katika kikao hicho.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiwa katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Bondeni Masiu Kilusu akifuatilia hoja za madiwani wenzake.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael pia laikuwa ni miongoni mwa madiwani waliohudhuria kikao hicho.

Na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.
RAIS MHE.DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MHE.BENJAMIN MKAPA PAMOJA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA GUINEA BISAU FEBRUARI 25,2016

RAIS MHE.DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MHE.BENJAMIN MKAPA PAMOJA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA GUINEA BISAU FEBRUARI 25,2016

February 26, 2016



1wdfdvgfdv Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 25,2016
6be4d8af-3789-4718-9cd6-3cea233acf6c 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
86ef9304-4088-4daf-91c2-36d3da94bc67 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Genarali Omar Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz Ikulu jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mjumbe huyo alileta salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Guinea Bisau.
7b43ac9e-5731-47e8-8a95-8052a96d306eRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua kutoka Genarali Omar Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz.
7140a43f-ddcd-430a-a8a1-ad242342715a
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau mara baada ya kupokea barua ya Salamu na pongezi.
63f0b3cb-c17f-4ff0-9cf0-5173772db23b
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Genarali Omar Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz Ikulu jijini Dar es Salaam
Chanzo:Blog Rasmi ya Ofisi ya Rais
Serikali yawakutanisha vijana kuunda kanuni za uendeshaji Baraza la Vijana Taifa

Serikali yawakutanisha vijana kuunda kanuni za uendeshaji Baraza la Vijana Taifa

February 26, 2016

vio1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi akizungumza na vijana (hawapo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
vio2
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
vio3
Mwezeshaji Bw. Patrick Kipangula (aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
vio4
Mjumbe  wa maendeleo ya vijana akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
vio5
Wawakilishi kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa, Taasisi za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za sekondari na Shule za msingi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
vio6
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi (watatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na vijana wenye ulemavu wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia (waliokaa) ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi, wapili kushoto ni Mwenyekiti wa kikao Bw. Godwin Kunambi, na wanne kulia (waliosimama) ni Mkurugenzi msaidizi Vijana Bibi. Ester Riwa
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na; Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na chombo chao chenye kujali utaifa, uzalendo na maslai bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, rangi, hali za kiuchumi, jinsia na maumbile kwa kuandaa kanuni zitakazolifanya Baraza la Vijana Taifa kuwa huru na lenye haki.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleeo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
“Nimuhimu kuunda Baraza kisheria litakalokuwa na uwakilishi wa vijana wa makundi yote ili liweze kutumika katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa” alisema Bw. Shitindi
Aidha Bw. Shitindi amelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutunga sheria Na. 12 ya mwaka 2015 ya Baraza la Vijana Taifa ambalo litaleta maendeleo ya vijana na nchi kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti aliyeteuliwa kuongoza mjadala huo Bw. Godwin Kunambi amesema kuwa Vijana takribani 120 wamepata fursa adhimu ya kushiriki katika uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa hivyo kuwataka vijana hao kujadili mambo ya msingi yatakayowawezesha wananchi wa Tanzania hususani vijana kutatua kero zao kupitia Baraza hilo.
Naye mwakilishi kutoka kundi la watu wenye ulemavu Bw. Gaston Hemed Mcheka ameipongeza Serikali kutoa nafasi kwa kundi la watu wenye ulemavu kuwa na uwakilishi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa pindi Baraza la Vijana Taifa litakapoanza ambapo kundi hilo litatumia nafasi hiyo kutatua changamoto zinazowakabili.
Kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa kimeshirikisha takribani vijana 120 kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi  za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za Sekondari pamoja na Shule za msingi.
MAWAZIRI WAPEWA MWISHO LEO KUJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI, HATI YA UADILIFU

MAWAZIRI WAPEWA MWISHO LEO KUJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI, HATI YA UADILIFU

February 26, 2016

kas1
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa  ofisi ya Waziri Mkuu wakati alipotoa maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusu  mawaziri ambao bado hawajajaza fomu za  Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni (Ijumaa, Februari 26, 2016).(PICHA NA JOHN BUKUKU- WA FULLSHANGWEDAR ES SALAAM)
kas2
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akiendelea kufafanua mambo kadhaa kwa wanahabari katika mkutano huo kushoto ni WAZIRI wa nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora, Mh Angella Kairuki
…………………………………………………………………………………………………………………
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni (Ijumaa, Februari 26, 2016).
Agizo hilo la Rais limetolewa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam.
“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.
Amewataja mawaziri wanaotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa  Nchi (OMR – Mazingira), Bw. Luhaga Mpina anatakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

WAZIRI NAPE AAHIDI UPATIKANAJI WA SERA YA FILAMU NCHINI.

February 26, 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akihojiwa na na Wanahabari pamoja na baadhi ya Wasanii mara baada ya kuwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo (kushoto) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa Uchaguzi wakitoa maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

ZANZIBAR KUANZISHA KITUO CHA MTANDAO WA MAENEO YAKE.

February 26, 2016

 Mkurugenzi wa Mipango miji na Vijiji Zanzibar Dkt. Mohammed Juma akizungumza kando ya Warsha ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya Zanzibar huko Shangani mjini Zanzibar.
  Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Taasisi ya Mazingira ya Finland Bi Riihz Teinirants akielezea hatua mbalimbali za kufuatwa kwa maafisa mbalimbali walioshiriki mafunzo ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya Zanzibar huko Shangani mjini Zanzibar.  
 Picha no - 0707 na 0710 Baadhi ya Maafisa kutoka Zanzibar na wenzao wa Finland wakijadiliana namna ya bora ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru Shangani mjini Zanzibar.
Picha no - 0687 Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali za Zanzibar wakisikiliza mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Maafisa kutoka Finland juu namna ya bora ya kuanzisha kituo cha Mtandao wa Maeneo na mazingira ya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru Shangani mjini Zanzibar. 
Picha na Makame Mshenga

Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
IDARA ya Mipango miji na Vijiji Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Zanzibar wanatarajia kuanzisha Kituo cha Mtandao wa Taarifa za Maeneo na mazingira ya Zanzibar ambapo Wananchi watalazimika kupata taarifa kupitia kituo hicho.
Taarifa hizo zitawekwa katika mfumo wa kidigitali na kuwekwa katika Mtandao huo ili kuepusha upotoshaji wa taarifa na pia zipatikane kwa wakati bila ya usumbufu.
Mkurugenzi wa Mipango miji na Vijiji Zanzibar Dkt. Mohammed Juma ameyasema hayo wakati wa warsha ya kuandaa utaratibu wa kuanzisha kituo hicho cha Mtandao Shangani mjini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa kutokana na kuwepo kwa Vyanzo vingi vya Taarifa zinazohusu Maeneo ya Zanzibar kunapelekea baadhi ya Taarifa hizo kutokuwa sahihi na kupelekea mkanyiko katika jamii.
“Kwa sasa kuna Vyanzo vingi vya kujua maeneo na mazingira ya Zanzibar..kwa mfano ukienda kutaka taarifa juu ya eneo fulani inawezekana taarifa hiyo ikatofautiana na Vyanzo vingine lakini tutakapokuwa na Chanzo kimoja taarifa zitakuwa moja na sahihi”Alisema Dkt Mohamed.
Ametaja faida zitakazopatikana kupitia Mtandao huo kuwa nipamoja na kuwarahisishia Wananchi kupata taarifa popote walipo na kwa wakati kinyume na ilivyo sasa ambapo hulazimka kwenda katika Taaisi husika jambo ambalo huwaletea usumbufu.
Aidha amesema pia itakuwa ni sehemu ya uwazi kwa Serikali kupitia Taasisi zake ambapo kila kitu kitawekwa wazi na kupatikana kirahisi kupitia Mtandao huo.
“Mtandao huo utaweka wazi maeneo yote yakiwemo,Makaazi,maeneo ya uwekezaji..isipokuwa yale yakiusalama ili kumrahisishia mwananchi kuweza kupata Taarifa bila kuhangaishwa huku na kule” alibainisha Dkt Mohammed.
Aidha amebainisha kuwa katika Warsha ya kuandaa Mtandao huo Taasisi nane zimeshiriki ili kuwa na sauti moja juu ya maeneo na mazingira ya Zanzibar.
Amezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa ardhi, Idara ya Mazingira, Idara ya Misitu na maliasili zisizorejesheka na idara ya maendeleo ya uvuvi.
Taasisi zingine ni pamoja na Idara ya Rasilimali za baharini, Chuo kikuu cha taifa SUZA na Mamlaka ya Mazingira Zanzibar (ZEMA) ambazo zote zimeshiriki katika Mpango huo wa kuandaa Taarifa za pamoja.
Jumla ya shilingi Milion 140 zitatumika kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao ambazo ni msaada kutoka Serikali ya Finland.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Taasisi ya Mazingira ya Finland Bi Riihz Teinirants amesema Taasisi watendaji wa Taasisi hizo walioshiriki mafunzo wanajukumu la kuwafahamisha wenzao ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Aidha bi Riihz amesema mbali na kutoa mafunzo ya kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao wataisaidia Zanzibar kutafuta taarifa za maeneo yake na kuziweka katika Kituo hicho hasa zile za mwambao wa bahari ili kuleta ufanisi unaohitajika.
Kunzishwa kwa kituo hicho cha Mtandao wa Taarifa za maeneo ya Zanzibar ni matokeo ya kukamilika kwa Mradi wa kutunza mazingira Zanzibar (SMOLE) uliofadhiliwa na Serikali ya Finland katika kuisaidia Zanzibar ambapo Mradi huo ulipata mafanikio makubwa.

ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WASHIRIKI WA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHONI LAANZA KATIKA HOTEL YA KEYS MJINI MOSHI.

February 26, 2016
Muonekano wa vipita shoto katika mji wa Moshi unavyoonekana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni zitakazofanyika Jumapili hii.
Baadhi ya wajasiriamali wakiwa wameweka bidhaa zao nje ya Hotel ya Keys kunako fanyika zoezi la uandikishaji wa washiriki wa mbio hizo.
Baadhi ya washiriki wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni wakijiandikisha katika moja ya banda yaliyopo Hotel ya Keys.
Raia wa kigeni pia wamejitokeza kujiandikisha kushiriki mbio hizo.
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Km 42 zinazodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakijaza fomu wakiti wakijiandikisha katika Hotel ya Keys.
Wakimbiaji wa Mbio za KM 21 zinazodhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo wakijiandikisha katika Hotel ya Keys mjini Moshi.
Zoezi la uandikishaji likeindelea katika Hotel ya Keys.
Washiriki wa Mbio za walemavu zinazodhaminiwa na kampuni ya GAPCO wakijiandikisha katika banda lililopo katika Hotel ya Keys mjini Moshi.
Hotel ya Keys ambako zoezi la uandikishaji wa washiriki wa mbio za Kimataifa za Kiliamanjaro Marathoni unafanyika.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.