Showing posts with label TANGA. Show all posts
Showing posts with label TANGA. Show all posts

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KWA TANROAD KUWASIMAMIA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI NCHINI

November 22, 2023 Add Comment
WAZIRI wa Ujenzi Inocent Bashungwa akikagua barabara inayotoka Kwamsisi kuelekea Pangani mkoa ni Tanga wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Albart Msando

Waziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa akizungumza mara baada ya kuikagua barabara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Albarto Msando
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni Saitoti Zelothe akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia  ni Waziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa





 Na Oscar Assenga,HANDENI




WAZIRI wa Ujenzi Inocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara nchini kutokana na kusuasua na serikali kutoridhishwa na kasi ya ujenzi.



Sanjari na agizo hilo pia amesema iwapo miradi hiyo ya barabara itaendelea kusuasua atalazimika kumshauri Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambadilishe Mtendaji Mkuu wa Tanroad nchini Mohamed Besta kama ataendelea kucheka na wakandarasi hao bila ya kuwachukulia hatua.



Bashungwa aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Handeni na Pangani ambapo alikagua barabara ya kutoka Tanga-Pangani hadi Bagamoyo ambayo inatekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya Kichina ya Railway 15, hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.



Alisema kwamba kuna miradi mingi imekuwa ikisuasa suasua lakini bado wanaendelea kuiangalia bila kuchukua hatua jambo ambalo linakwamisha juhudi kubwa za Serikali kuifungua nchi kupitia miradi ya barabara ya kimkakati.



“Barabara hii nikuambie Mkurugenzi Mkuu wa Tanroad, kama hatutachukua hatua kwa muda unaotakiwa miradi kama hii inayoendelea kusuasua nitamshauri rais akubdilishe hatuwezi kuendelea namna hii”Alisema Waziri Bashungwa.



“Lakini pia Kaimu Mkurugenzi wa Miradi Tanroad tumemuamini tumekukaimisha ili usimamie hayo tumekuwa na wewe uone, Boniface Mkumbo yule aliyekuwa kabla yako nilipokuja kumtoa ilikuwa mbinde kwa sababu ya kulindana sasa Mkurugenzi Mtendaji baada ya wao utakuwa wewe kama usipobadilika”Alisema



Waziri huyo alisema haiwezekani anapokwenda kila kipande cha barabara nchini niwaamshe nyie hapana lazima mbadilike kama sijawaamsha na ile mipango mlioniambia naenda kukagua barabara lakini sitaki wakandarasi wa aina hii kule yule CR 7 hawa ni CR 15 wanaweza kukuta mtu na binadamu yake.



“Lakini yule CR 7 ni shida kwani miradi kama sita imesimama kwa sababu ya kurundikiwa miradi na nyie mnajiita CR 15 nyie mnauhusiana na C7 hii ni tatizo kila mradi mnaoufanya hii barabara wananchi mmesikia mipango ya Serikali ninakwenda kuikagua”Alisema



Aliwaambie wananchi tayari Serikali imeshaleta fedha lakini mkandarasi anawachelewesha wameona ni kwanini wanawachelewesha Mkurugenzi wa barabara hautakiwa kuwa ofisini unapaswa uzungumze maeneo mbalimbali nchini ili uweze kuona changamoto



Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Tanroad alimueleza Waziri Bashungwa kwamba hatua ambazo wamechukua ni kumuelekeza mkandarasi aongeze vifaa na awe na mpango kazi ambao unaendana na wakati.



Alisema kwa sababu kwa sasa yupo nyuma ya asilimia 19 ya mpango wake ya kazi na Novemba 14 waliwaita makao makuu na kukaa kikao nao na baadae Novemba 28 wamewaita tena ili kuona kama yale maelekezo yametekelezwa.



Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando alisema kwamba wananchi wa eneo la Kwamsisi wameandika Historia kwa kuwa Waziri wa kwanza kufikia na kuzungumza nao na kutembelea barabara hii na wananchi walikuwa wamekata tamaa.



Alisema kwamba wanawaomba wanapokwenda kwa maofisi ya wakuu wa wilaya wasije na kuondoka na waache kujifungia ofisini wabadilike watumie ofisi zilizopo katika maeneo wanayotekeleza miradi.



“Mh Waziri sisi hapa leo tunapoteza tuna mazao mengi tunalima unaweza kukaa wiki nzima hautaja toa mazao na hivyo kupoteza mapato mengi ambayo serikali yangepatikana kwamsisi jana na juzi wamekusanya 0 hakuna gari zinaingia shambani kwa sababu ya ubovu wa barabara”Alisema



Alisema kwa sababu wao ni wazalishaji wengi ya muhogo barabara hii itakuwa mkombozi na wananchi hao watakukuyumbisha hivyo Tanroad lazima waangalie mahitaji ya wananchi na fedha imetengwa haenda hatua moja mbele.






DKT SIMEO: MICHEZO NI NGUZO MUHIMU YA UTULIVU NA USALAMA KWENYE NCHI

August 06, 2023 Add Comment
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Tanga Edgar Mdime akizungumza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo
MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Sinde Mtobu akieleza umuhimu wa uchangiaji damu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime

Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime akichangia damu



Na Oscar Assenga, TANGA.

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Japhet Simeo leo amezindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga huku akieleza kwamba michezo ni moja ya nguzo muhimu katika utulivu na usalama kwenye nchi.

Simeo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kwenye uzinduzi huo alisema kwamba michezo ina tija sana katika maisha ya binadamu ikiwemo kuwaunganisha jamii na kutengeneza undugu.

Alisema kwamba uchangiaji wa damu ni muhimu ili kuokoa maisha ya wagojwa wahitaji wa damu wakiwemo waluopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto waliopo katika hospital mbalimbali mkoani Tanga.

Mganga Mkuu huyo aliwapongeza wanachama hao kwa utayari wao wa kuona umuhimu wa kuchangia damu ambayo itakwenda kusaidia jamii yenye uhitaji huku akizitaka Taasisi, Vikundi na watu binafsi kuendelea kuwa na utamaduni huo ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofika hospital kupata huduma hiyo.

"Nawapongeza mashabiki wa timu ya Simba SC kwa utayari wenu kuja kuchangia damu mimi nawaambia hii ni sadaka na thawabu kubwa sana mliyoitoa kwa wenzenu wenye uhitaji wa damu " Alisema Simeo.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya Simba SC Edgar Mdime alisema kwamba zoezi la uchangiaji wa damu imekuwa ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wahitaji.

Alisema bado wanasukumwa kuchangia damu katika hospitali wakitambua kuwa uhitaji wa damu ni mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu hivyo licha ya kushiriki siku hiyo adhimu kwao bado wanaendelea kuhamasishana kujitoa kwa pamoja katika zoezi hilo.

Aidha alisema walianza na zoezi la usafi kubwa zaidi ilikuwa ni kuchangia damu na hamasa kubwa sana ambayo imetokea kwa mkoa huo kwa wana Simba na matawi yote wameungana kwa pamoja kwa ajili ya zoezi hili la kuchangia damu

Hata hivyo alisema kwamba wanajua damu ni muhimu sana kwa kila mmoja hasa ukizingatia wapo wakina mama wanaojifungua katika hospitali ikiwemo ajali zinatokea watu wanahitaji kuwekewa damu kwa hiyo wao wamehamasika kama wanajamii ukiachana na suala la michezo.

Tambo 

Mwenyekiti huyo alisema kwamba dhamira yao kubwa msimu huu lazima timu yao ichukue Ubingwa kutokana na uwepo wa kikosi kipana kulingana na usajili mkubwa uliofanyika wakiamini lazima timu hiyo ifanye makubwa katika mashindano ya ndani na hata kimataifa pia.

Katika hatua nyengine, Mdime alituma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.

Mchezo huo unatarajiwa kucheza Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024 .