President Kikwete receives a rousing welcome in Beijing

President Kikwete receives a rousing welcome in Beijing

October 24, 2014

D92A8241
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping. D92A8392 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit this evening.(photos by Freddy Maro) D92A8416

PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UN)

October 24, 2014
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam leo, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee. 
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu 
maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa 
kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa 
heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni 
wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea
………………………………………………………………………………………………..

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UNTibaijuka alitoa wito huo leo katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Waziri Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi, mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila mmoja kuinusuru dunia.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Katika mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri Tibaijuka alisema.
Hivyo Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio hizo.
Waziri aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha haki za binadamu.
 President Xi Jinping Welcomes President Kikwete in Beijing

President Xi Jinping Welcomes President Kikwete in Beijing

October 24, 2014
China’s President Xi Jinping welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the Great Hall of the People in Beijing this evening during the official formal reception at the climax of the State visit at the invitation of the Chinese leader. D92A8192 D92A8213 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing this evening(photos by Freddy Maro) D92A8224

KAMPENI YA WANAWAKE NA UCHUMI KUNUFAISHA WAJASIRIAMALI 300 MKOANI TANGA

October 24, 2014

KAMPUNI ya Angels Moment ya Jiiji Dar es salaam kuwapatia wanawake wapatao 300 wajasiriamali wa Mkoa wa Tanga elimu ya biashara katika kampeni ya MWANAMKE NA UCHUMI ili kuwajengea uwezo na uelewa utakao ibua hisia chanya kutambua fusa walizonazo kiuchumi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yatagusa masuala ya Ujasiriamali, Utunzaji wa hesabu za Biashara, uwekaji wa Akiba, umuhimu wa rasimali Ardhi na masuala ya Afya bora.

 
Akizungumza kwenye mkutano a waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga, Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi kutoka kampuni ya Angels Moment, Mahada Erick amesema kuna fursa nyingi za utajiri kwa wajasiriamali ambazo wengi wameshindwa kuzitambua kutokana na uelewa mdogo walionao.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Dendego (mwenye nguo ya manjano), pamoja na Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi kutoka kampuni ya Angels Moment, Mahada Erick.




Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Dendego, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi kutoka kampuni ya Angels Moment, Mahada Erick, Donald Lembeli afisa mwandamizi Uendeshaji kutoka NSSF, upande wa kulia ni Baraka Mtoi Afisa Masoko Mkoa wa Tanga, GEPF na Gastory Meneja Mkuu wa Naivera Complex kutoka.




"wanawake wengi wakiwemo wa Mkoa huu wa Tanga, kama mnavyojua wamekuwa wahanga wa kukumbwa na madeni, na kukatiza biashara na ujasiriamali kwa sababu ya kukosa elimu au kukumbwa na changamoto mbalimbali,” alisema Erick na kuongeza.



Moja ya changamoto ni kufanya manunuzi yasiyo yalazima mfano magauni mengi, dhahabu huku wakishindwa kuelewa kuwa hivyo vitu ni mtaji na vinaweza kununulia mashamba na rasilimali nyingine za kuendeleza biashara.



Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga amesema kuwa semina hiyo itakayofanyika Naivera Complex Novemba 5 na 6 mwaka 2014, imekuja kwa wakati muafaka kwa wajasiriamali kujikuza kibiashara na kiuchumi.




 Kwa upande wao afisa mwandamizi Uendeshaji kutoka shirika la hifadhi ya jamii NSSF Donald Lembeli na Baraka Mtoi Afisa Masoko mfuko wa GEPF Mkoa wa Tanga, wamesema kupitia mpango maalumu wa kuwakomboa wanawake wtakuwa bega kwa bega kuendelea kuwahamasisha ili waweze kukopesheka fedha za mashirika kupitia kwenye saccos na kujiwekea akiba.


Kwa upande wao afisa mwandamizi Uendeshaji kutoka shirika la hifadhi ya jamii NSSF Donald Lembeli na Baraka Mtoi Afisa Masoko mfuko wa GEPF Mkoa wa Tanga, wamesema kupitia mpango maalumu wa kuwakomboa wanawake wtakuwa bega kwa bega kuendelea kuwahamasisha ili waweze kukopesheka fedha za mashirika kupitia kwenye saccos na kujiwekea akiba.



Angels Moment wa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsia na watoto pamoja na taasisi ya WAMA imeshanufaisha wanawake 1600. 
Kampeni hii pmoja na Mkoa wa Tanga inatarajia kuwafikia wanawake wa vikundi vya ujasiriamali, SACCOS, VICOBA na makundi mengine ya kijamii kwenye mikoa ya Pwani, Lindi, Ddodoma, Kigoma, na Ruvuma.









Waandishi wa Habari wanaume (waliosimama) katika picha ya pamoja.


Waandishi wa Habari wanawake (waliosimama) nao hawakuwa nyuma.

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE TANGA KUFANYIA USAFI KITUO CHA AFYA PONGWE

October 24, 2014



Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga (TWMO) Bertha Mwambela (wapili kutoka kushoto) na wanachama wa chama hicho kwenye kikao cha maandalizi ya Kufanya usafi, kituo cha afya Pongwe.

CHAMA cha waandishi wa Habari Wanawake Mkoani Hapa, Tanga Women in Organization (TWMO) kesho watafanya usafi katika kituo cha afya Pongwe, tarafa ya Pongwe, kilichopo kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Kituo hicho kilicho chini ya Mganga Mfawidhi, Dk. Faisal Ali, kinapokea mamia ya wagonjwa kwa siku kutoka vijiji mbalimbali wakiwemo wajawazito na watoto.

Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye kikao chao cha maandalizi ya Kufanya usafi, kituo cha afya Pongwe.