BENKI YA CRDB YAZIDI KUMWAGA PASSO KWA WATEJA WAKE

July 09, 2015

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari mshindi wa Promosheni ya 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo’, Peter Fundi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa Promosheni ya ‘Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo’, Peter Fundi. Kushoto ni Meneja wa benki hiyo Tawi la Mzumbe, Jane Maganga.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Promosheni ya 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo’, Peter Fundi. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mzumbe, Jane Maganga na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Godwin Semunyu (kulia). 
 Peter Fundi akiwa katika gari lake aina ya Passo.

WAZIRI MEMBE ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA NCHINI

July 09, 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akiongea kwenye muhadhara kabla ya Mtoa mada mkuu Prof. Justin Yifu Lin hajaongea katika muadhara uliokuwa unazungumzia umuhimu wa viwanda nchini ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya (Kulia), na kushoto ni Balozi Mstaafu Mhe. Elly Mtango wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Lin (hayupo pichani).
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza kwa makini Prof. Lin (hayupo pichani), Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Nigel Msangi, Kushoto ni Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Mambo ya Nje Bw. Ally Mkumbwa nao wakifuatilia kwa makini Muhadhara uliokuwa ukiendelea
Balozi Simba akichangia mada katika muadhara uliokuwa ukiendelea
Muhadhiri Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akiuliza swali

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU WIKI YA USALAMA BARABARANI YA UMOJA WA MATAIFA DAR ES SALAAM LEO

July 09, 2015

 Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi.
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia), akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo. 

 Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mkaguzi wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Mossi Ndozero (kulia), akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry
 Bantu akizungumza kwenye semina hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi akitoa mada kuhusu sekta ya Afya inavyokabiliana na changamoto za utoaji huduma kwa wagonjwa wanaopata ajali.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikifunguliwa.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
semina hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.


Dotto Mwaibale

WATOTO 1, 86, 300 wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za magari duniani hivyo kuwa changamoto kubwa ya usalama barabarani.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy wakati akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina ya siku moja ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani iliyofanyika Dar es Salaam leo.

"Hii ni changamoto kubwa duniani na hapa nchini kwani kati ya watoto hao idadi kubwa ya wanaopoteza maisha katika ajali hizo ni watoto wa kiume" alisema Kessy.

Mkaguzi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero alisema kumekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na masuala ya usalama barabarani ikiwemo ukiukwaji wa sheria za barabarani unaosababishwa na binadamu.

Ndozero aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria jambo litakalo saidia kupunguza changamoto hiyo ya ajali kama sio kuisha kabisa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema maendeleo ya dunia yamesababisha ongezeko la magari barabarani hususan nchini Tanzania hivyo kuongeza ajali za barabarani.

Bantu aliwataka watanzania kujenga utamaduni wa usalama barabara ambao hatuna jambo litakalo saidia kupunguza ajali kwa kusaidiana na wadau wengine.


Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi alisema ajali zinazotokea nchini zimechangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa hivyo kuwa changamoto katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na wodi kutokidhi ongezeko la wagonjwa na vifaa tiba.

Alisema kilele cha maadhimisho ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani yatafanyika Julai 15 mwezi huu Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AFUNGUA UKUMBI MPYA WA MIKUTANO WA CCM, MJINI DODOMA LEO

July 09, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyeza kitufe cha kengere kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM unaofahamika kwa jina la Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, baada ya kuufungua rasmi ukumbi huo leo Julai 9, 2015 mjini Dodoma.
Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.


















IGP MANGU AZINDUA NA KUKAGUA MIRADI YA POLISI TABORA, TANGA NA SINGIDA

IGP MANGU AZINDUA NA KUKAGUA MIRADI YA POLISI TABORA, TANGA NA SINGIDA

July 09, 2015

7
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Ludovick Mwananzila na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe.Suleiman Kumchaya.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora.IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Polisi Dkt.Nyanda wakitoka kukagua Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora baada ya kuizindua wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo..IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
4
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiweka jiwe la msingi katika jengo la Kikosi cha usalama barabarani mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.Kulia ni Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna msaidizi wa Polisi, Juma Bwire.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikagua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Polisi na Makazi ya Askari Wilayani Ikungi mkoani Singida wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni ni kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi Thobias Sedoyeka na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ikungi.
6
Kamanda wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, Richard Malika akimtembeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kuangalia ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.