WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAMPA ZAWADI KATIBU MKUU WAO BAADA YA KUTUNIKIWA NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)

WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAMPA ZAWADI KATIBU MKUU WAO BAADA YA KUTUNIKIWA NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)

June 29, 2015


????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Ngao ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hiyo ya kushtukiza iliandaliwa na viongozi hao wa Idara baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na viongozi hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha kutunzia kumbukumbu, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na watendaji hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Mswala wa kuswalia, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na watendaji hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akimshukuru Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa, pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na wakuu hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa wizara hiyo, Martina Nguluma pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na watendaji hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu wa wizara hiyo, Edwin Makene pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na viongozi hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii wa wizara hiyo, Fidelis Mboya pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na viongozi hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
9
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (watatu kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (katikati), Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Haji Janabi (wanne kulia), Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi, Manyama Mapesi (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Marlin Komba (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Jane Massawe (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Edwin Makene (wapili kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Christina Mwangosi. Wakuu wa Idara wa wizara hiyo walimpa zawadi ya kushtukiza Katibu Mkuu wao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).

MKUTANO WA Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii WAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA.

June 29, 2015

 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Ndugu Allan Kijazi akizungumza jambo,wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Wahariri wa Habari Tanzania,mapema leo asubuhi jijini Mwanza.Ndugu Kijazi alisema kuwa Utalii ni sekta mtambuka na inachochea
ukuaji wa sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na
barabara, huduma za fedha, huduma za chakula na malazi kudorora kwa sekta
nyinginezo.  “Hivyo kudorora kwa sekta
hii huchangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa sekta nyingine.  Aidha, hadi sasa, Utalii unaongoza katika
kuingiza fedha za kigeni ikiwa ya kwanza na kufuatiwa na sekta ya madini na
kilimo.
 Kwa  na kwa ujumla unachangia asilimia 17.5 ya Pato
la Taifa lakini tathmini inaonyesha sekta hii inaweza ikachangia zaidi ya 30%
ya pato la Taifa.  Asilimia zaidi ya 80
ya utalii nchini ni utalii wa kutembelea kwenye Hifadhi za Taifa, na hii
inaonyesha kuwa hifadhi hizi ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu.  Ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya
wanaotembelea Hifadhi hizi”,alisema Ndugu Kijazi.
Alisema kuwa  Maeneo yaliyo chini ya Hifadhi za Taifa
yana faida nyingi za kiikolojia (ecosystem services) kama vile kuwa vyanzo vya
maji (mfano; Hifadhi za Kilimanjaro, Arusha na Udzungwa). Maji hayo pia
hutumiwa kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika kwenye gridi ya Taifa. Hivyo
faida za kusimamia Hifadhi hizi haziishii tu kwa watalii kufurahia bali pia
kuna faida nyingine za kiuchumi ambazo sio rahisi sana kuziainisha katika mfumo
wa kifedha
Katika ufunguzi wa Warsha hiyo,Ndugu Kijazi alisema kuwa, Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka
huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. aliongeza kusema kuwa pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA, mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii
na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana na TANAPA katika kuhimiza
uhifadhi na kuendeleza utalii.  “Mada kuu
nne zitawasilishwa na viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd.
Jenerali Ulimwengu na Dkt. Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata
fursa ya kuchangia na mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa
majukumu yetu”,alisema Kijazi.
PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA
 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano.
wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA,aidha imeelezwa katika Warsha hiyo kuwa mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii
na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana nasi katika kuhimiza
uhifadhi na kuendeleza utalii. 
  
 Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi jijini Mwanza
  Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndugu Allan Kijazi pichani kati na Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja

KINANA AITIKISA MWANZA

June 29, 2015
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa
hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya
kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na
kuzitafutia ufumbuzi. 
 
Mkutano
huo umefanyika kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza jana jioni. Ndugu Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, tayari wamesafiri umbali wa Km
193,537, kwa kufika katika Wilaya 163, majimbo 239, nusu ya vijiji na
kata 1938 za Tanzania. Pia msafara wake ulitumia jumla ya saa 84
kuzunguka mikoa yote hiyo, na kusafiri kwa mitumbwi katika visiwa 16.
Amehutubia jumla ya mikutano ya ndani/hadhara 1918 na kujikusanyia
wanachama wapya 284300 ambapo kutoka upinzani 38984.
Aliyekuwa
mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita,
Twalib Ngika, akikabidhi Kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana  baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa
hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini
Mwanza jana.
 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa
hadhara kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana jioni, ambapo amewataka
viongozi wa chama na Serikali kutoka maofisini kwenda kwa wananchi
kuzitafutia ufumbuzi kero zao.
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua jambo mbele ya wakazi
wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,alipokuwa akiwahutubia katika
mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31
nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za
wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 
 
 Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza
kuwahutubia kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jioni ya leo,Kinana
aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM,
litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali
kuhusu utendaji wake.
Ndugu
Kinana akiwapungia mkono wananchi alipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa
Furahisha jijini Mwanza, ambapo aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa
bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa
kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CCM kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.
 Katibu  Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapigia saluti, maelfu ya wananchi, alipowasili kuhutubia  mkutano wake wa hadhara aliofanya leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwahamasisha maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo katika Vianja vya Furahisha Jijini Mwanza.
“‘SAFI SANA”Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aonyesha dole gumba ambayo ni ishara ya CCM na kuonyesha kuwa mambo safi, alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Malikia wa taarab, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM, wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhmn Kinana uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Furahiha jijini Mwanza
 Mashabiki wakimg’amg’ania Khadija Kopa wakati akiimba wimbo maalum mbele ya mashabiki hao wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wake wa hadhara aliofanya katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana
 Maelfu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana
 Maelfu wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja hivyo jana
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi y Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akitangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi y Chadema, katika uchaguzi mkuu
uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi yadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinna  baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa
hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja
vya Furahisha jijini Mwanza jana

 Kinana akisindikizwa na maelfu ya wananchi alipokuwa akiingia kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo. Pmoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo n Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, akihutubia mkutano huo
Mmoja wa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, akiwa na mtoto wake aliyeshika kipeperushi cha CCM
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo akihutubia kwenye mkutano huo
 Meya wa Jiji la Mwanza,  Stanslaus Mabula akihutubia kwenye mkutano huo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihitimisha kwa hotuba katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Furahisha jijini wanza leo. PIcha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
MAABARA YA MAFUNZO ITEMBEAYO YAZINDULIWA RASMI

MAABARA YA MAFUNZO ITEMBEAYO YAZINDULIWA RASMI

June 29, 2015
DSC_0080
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando akisoma hotuba ya uzinduzi wa maabara itembeayo kwa ajili ya mafunzo ya upasuaji. Kulia ni Naibu Balozi wa Ireland nchini, Maire Matthews na kushoto ni Mkurugenzi wa ECSA anayeshughulikia Afya ya jamii Prof Yoswa Dambisya.
Na Mwandishi wetu
Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Magreth Mhando mwishoni mwa juma alizindua maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.
Alifanyakazi hivyo kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Seif Rashid.
Maabara hiyo ambayo ni mradi wa majaribio wa chuo hicho wenye lengo la kufundisha wapasuaji pale walipo imegharimu dola za Marekani 100,000.
Kwa mujibu wa taarifa za COSECSA maabara hiyo itakuwa nchini kwa miezi kama mitatu kabla ya kwenda Kenya na baadae Malawi.
Mradi huo wenye lengo la kufundisha wapasuaji zaidi kwa kufika eneo ambalo wanafanyia kazi, ni moja ya miradi ya chuo kitembeacho ambacho toka kimeanzishwa mwaka 1990 kimeshatoa wapasuaji 200.
Hafla ya uzinduzi wa maabara hiyo yenye vifaa vya kisasa vya kufundishia na kufanyia upasuaji ikiwamo ya upasuaji kwa kutumia darubini ulifanyika katika hospitali ya kumbukumbu ya Hubert Kairuki.
DSC_0053
Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kabla ya uzinduzi.
Akizindua maabara hiyo Dk. Mhando alisema kwamba ni matumaini yake italeta mabadiliko makubwa katika kuwezesha taifa kuwa na wataalamu wengi wa upasuaji.
Aidha alisema changamoto ya kutosajiliwa kama chuo kamili wakati mataifa mengine yamefanya atayafuatilia ili kuweza kuona ya kukiwezesha chuo hicho kutambuliwa rasmi nchini Tanzania.
Maabara hiyo mali ya College of Surgeons of East Central and Southern Africa (COSECSA) iliwasili mapema mwezi huu na jana ndio ilikuwa uzinduzi rasmi ambao ulishuhudiwa na wanafunzi wa upasuaji, wataalamu na maofisa mbalimbali wa afya wakiwemo watu wa Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kaimu mkurugenzi wa Mfuko huo Michael Mhando alisema kwamba wamefurahishwa na juhudi za wadau wao katika kuimarisha vifaa tiba na utoaji wa wataalamu.
Alisema anaamini kwamba maabara hiyo ni moja ya mambo muhimu yanayotakiwa kufanywa na wadau ili kuimarisha tiba nchini.
Alisema kwamba wataangalia namna ya kufanya ili kusaidia huduma hiyo kwani inahitajika sana vijijini ambako wengi wa watu hawapati fursa ya kufanyiwa upasuaji hata ule mdogo.
DSC_0130
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.
Maabara hiyo yenye uzito wa tani 30 inatarajia kufanya mafunzo ya upasuaji katika hospitali zenye uhusiano na COSECSA.
Aidha maabara hiyo inaweza kufunza wapasuaji 10 kwa mkupuo mmoja.
Kuletwa kwa maabara hiyo kutoka Ireland ambako kuna uzoefu wa miaka mingi wa kutumia maabara zitembeazo za upasuaji kumefanikishwa na mahusiano yaliyopo kati ya Royal College of Surgeons in Ireland (RCSI), Shirika la misaada la Ireland (Irish Aid) na College of Surgeons of East, Central and Southern Africa (COSECSA).
Maabara ya mafunzo ya upasuaji itembeayo ilianzishwa na RCSI kwa mara ya kwanza duniani mwaka 2006 na kwa uzinduzi uliofanyika dare s Salaam jana umedhihirisha dhamira njema ya COSECSA na RCSI ya kutoa mafunzo bora kwa lengo la kuimarisha afya za wanadamu.
Akizungumza kwenye tukio hilo Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo alisema kwamba kuwepo kwa maabara hiyo kutasababisha mabadiliko makubwa katika utoaji mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki, kati na Kusini ( ECSA).
Alisema kwamba kutokana na uasili wa maabara hiyo wanafunzi hawatakuwa wanalazimika kufuata kituo cha mafunzo na badala yake kituo hicho kitawafuata pale walipo.
Aidha alisema kwamba muundo na mfumo wa ufundishaji umeshatengenezwa kwa ajili ya kusaidia mafunzo hayo kwa nchi wanachama.
DSC_0023
Naye Mkurugenzi wa ECSA anayeshughulikia Afya ya jamii Prof Yoswa Dambisya alisema kwamba wataendelea kuwa mstari wa mbele kufundisha wataalamu wa afya kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisasa na zenye kutoa tija kama kuwepo kwa mabara hiyo.
Alisema kutokana na haja kubwa ya wataalamu wa upasuaji kuwepo kwa maabara hiyo itembeayo kutasaidia kufunza wanafunzi wengi katika eneo ambalo uwiano wa wataalamu na wagonjwa ni mtaalamu mmoja kwa wagonjwa 190,000 ukilinganisha na Uingereza ambako uwiano ni mtaalamu mmoja kwa wagonjwa 2,800.
Alisema raslimali kama ya maabara itasaidia kufunza watu wengi zaidi ili kuendelea kupunguza pengo la wataalamu wa upasuaji.
Alisema pia kwamba takwimu za dunia zinaonesha kuwa asilimia 6.5 ya magonjwa yanatokana na kukosekana kwa huduma za upasuaji.
Alisema vifo vingi vinatokana na kukosekana kwa huduma za upasuaji kuliko Malaria, Ukimwi na kifua kikuu kwa pamoja.
COSECSA ambayo ilianzishwa mwaka 1999 kwa malengo ya kutoa elimu ya upasuaji ilianzishwa na shirikisho la wapasuaji Afrika Mashariki ambalo lina miaka takaribani 60.
DSC_0087
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando akikata utepe kuzindua maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.
DSC_0097
Mmoja wa walimu ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando aliyemwakilisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu Balozi wa Ireland nchini, Maire Matthews.
DSC_0146
Wageni mbalimbali wakiangalia namna maabara hiyo inavyofanyakazi.
IMG_2862
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando (kulia) akishuhudia zoezi la upasuaji kwa vitendo ndani ya maabara hiyo.
DSC_0151
Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukagua maabara hiyo katika uzinduzi huo.
DSC_0090
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
DSC_0047
Maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.