RAIS SAMIA NA MGENI WAKE RAIS WA JAMHURI YA GUINEA-BISSAU MHE. EMBALÓ, WASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA MUONGOZO WA USHIRIKIANO

June 22, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akitia saini kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira akitia saini kwa upande wa nchi yake.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira wakati wakionesha Hati ya Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

BODI YA TANESCO YAFURAHISHWA NA KUPONGEZA MAENDELEO YA MRADI WA JULIUs NYERERE

June 22, 2024

 


Na Charles Kombe, Rufiji


Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imefurahishwa na kupongeza wasimamizi wa mradi juu ya hatua za ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Zuhura Bundala walipokua kwenye ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kutembelea mradi huo Juni 19 wakiambatana na kaimu Mkurugenzi wa Shirika upande wa uzalishaji Mha. Abubakar Issa.

"Niwaambie watanzania kujivunia Serikali yao inayopenda nchi na wananchi maana huu mradi ni mkubwa. Naipongeza TANESCO kwa kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huu" amesema Bi. Bundala

Ameongeza kuwa "taarifa tuliyopewa na wataalamu ni kuwa, mradi huu kiujumla wake  umekamilika kwa asilimia 98.01".

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji usambazaji Mha. Abubakar Issa amesema kwa sasa Tanzania hakuna kabisa mgao wa umeme kutokana na kuwa na ziada ya umeme.

"Mwisho wa mwezi huu tunatarajia kuingiza mashine namba saba ambayo itakwenda kuongeza megawati 235 na kupelekea kituo hichi kuwa na uwezo wa kuzalisha  megawati 705" amesema Mha. Issa.

Hii ni ziara ya kwanza ya bodi katika mradi huu ambapo imejionea hatua kubwa ya maendeleo ya ujenzi iliyofikiwa katika mradi huu.