KOCHA MPYA SIMBA ATANGAZA MAPEMAA VITA NA WENYE TABIA HIZI SIMBA

January 01, 2015


KOPUNOVIC AKIHOJIWA NA WAANDISHI WAHABARI.

Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic ametangaza mapemaa kwa wachezaji kuwa wajue yeye si mtu wa mzaha katika suala la nidhamu.


Kopunovic amesema angependa kufanya vizuri na anategemea ushirikiano wa karibu kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi na wanachama na mashabiki.

Lakini akasisitiza, suala la nidhamu litakuwa namba moja na hatakuwa na mzaha.

“Hakuna kitu kinafanyika kwa ufasaha katika maisha ya mwanadamu kama nidhamu haina uhakika.
“Hili ni sehemu ya misingi bora ya kazi, itakuwa ni muhimu lipewe kipaumbele ni suala muhimu,” alisema.

Rais huyo wa Serbia ametua kuchukua nafasi ya Patrick Phiri baada ya kuingoza Simba katika mechi nane za Ligi Kuu Bara akiwa ameshinda moja, sare sita na kupoteza moja.

SUMATRA TANGA YATOA ONYO KALI KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI MAJINI

January 01, 2015
  Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga,Walukani Luhamba wa kwanza kulia aliyevaa kofia akisisitiza jambo kwa abiria wanaotumia usafiri wa kutoka Korogwe mjini kwenda Bungu juu ya umuhimu wa kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyosimamia sheria pindi wanapobaini magari yanaendeshwa mwendokasi au kuzidishiwa nauli,
Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga,Walukani Luhamba wa kwanza kulia aliyevaa kofia akiwasikiliza abiria wanaotumia magari yanayofanya safari zao kati ya Korogwe mjini hadi Bungu kero wanazokabiliana nazo wakati alipofanya ziara ya kutembelea wilaya ya korogwe kupanga nauli mpya za kutoka mjini kwenye Vijijini,Picha na Oscar Assenga,Korogwe.

Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga,Walukani Luhamba akitangaza viwango vipya kutoka Korogwe mjini kwenda maeneo mbalimbali jana kwenye kikao chake ni wadau wa usafirishaji wilaya ya
Korogwe,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo.
MAMLAKA ya Udhibiti na Usimamizi wa Usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra)Mkoani Tanga umewapa muda wa wiki mbili wamiliki wa vyombo vya usafiri wa majini mkoani hapa kuhakikisha vyombo hivyo vinakaguliwa na kuwa salama kabla ya kuanza kazi zao ili kuweza kupunguza ajali zisizo za lazima.

Wito huo ulitolewa na Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga,
Walukani Luhamba wakati akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema kuwa kwa atakayekaidi agizo hilo atachukulia hatua kali ikiwemo kufutiwa leseni.

Alisema dhamira yao kubwa ya kuhakikisha vyombo hivyo vinakaguliwa ni kupambana na wimbi la ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wananchi ambao hawana hatia kutokana na uchakavu wa baadhi ya vyombo hivyo.

Sambamba na hilo,Afisa huyo alisema kuwa watafanya ukaguzi wa vyombo vidogo vidogo  na vikubwa vinavyotoa huduma za usafiri ndani na nje ya mkoa wa Tanga kwa kuvitaka vijisalimishe vyenyewe kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo alisema kuwa halmashauri mbalimbali mkoani hapa kwa
kushirikiana na wakurugenzi wao hawana budi kuweka utaratibu wa kubandika viwango vya nauli kwenye mabango yaliyopo kwenye stendi za mabasi ili kuweza kuwapunguzia usumbufu wasafiri wao.

    “Hii nadhani ndio njia sahihi ya kuepusha ulanguzi kwa abiria kwa sababu wapo baadhi ya vyombo vya usafiri vyenye kutaka kutoza viwango vikubwa vya nauli kuliko viwango vilivyowekwa na mamlaka husika“Alisema Luhamba.

Akizungumzia suala la baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake mkoani hapa kushindwa kutoa tiketi kwa wasafiri, Afisa huyo alisema kuwa kutokutoa tiketi ni kosa hivyo kwa atakayebainika atatozwa faini ya kuanzia shilingi laki moja.

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAOMBWA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA KUNUNULIA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU.

January 01, 2015
SHIRIKISHO la Vyama watu wenye Ulemavu mkoani Tanga (Shivyawata) limeiomba Halmashauri ya Jiji la Tanga kuangalia uwezekano kuwatengea bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa visaidizi kwa jamii hiyo.

Vifaa hivyo ni pamoja na fimbo nyeupe, kiti mwendo (wheelchair) Shime Sikio,(hearing aid) na Mashine ya kuchapia ambapo bila kutegemea msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na Halmashauri hawawezi kuvipata.

Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zuhura Mussa wakati alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema kuwa jamii hiyo imekuwa ikikumbana na changamoto hiyo kutokana na kuwa vifaa hivyo ni ghali hivyo familia nyingi hushindwa kumudu gharama
zake.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo lakini wanaiomba
Halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu iliyopo chini yake inakuwa rafiki kwa jamii hiyo pamoja na kuwapa kipaumbele kwenye masuala ya afya katika vituo vya afya na zahanati.

   “Changamoto zinazoikabili jamii ya watu wenye ulemavu ni nyingi lakini hili la vifaa kwetu ni kubwa hivyo tunaiomba Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo mkoani hapa kuangalia uwezekano wa kutusaidia “Alisema Zuhura.

Alisema kuwa changamoto nyengine ambazo wanakumbana nazo ni kutokuwepo kwa wataalamu wa kutosha katika mashule kwa ajili ya kusaidia na kufundisha watoto wenye ulemavu au kugundua ulemavu wao mapema.

Hata hivyo aliongeza kuwa ufinyu wa bajeti ya kuendesha shughuli zao za kila siku huwalazimu viongozi kufanya kazi za kujitolea na wakati mwengine kushindwa kufikia malengo yao kutokana na uhitaji wa fedha jambo ambalo linachangiwa kwa asilimia kubwa na kukosekana kwa wafadhili na fungu maalumu kutoka halmashauri
.

MANCHESTER UNITED YAHUSISHWA NA USAJILI WA BEKI KISIKI WA ATLETICO MADRID

MANCHESTER UNITED YAHUSISHWA NA USAJILI WA BEKI KISIKI WA ATLETICO MADRID

January 01, 2015

Atletico Madrid itamtoa beki wake kisiki João Miranda kwa moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya England katika dirisha dogo la usajili la Januari, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Star.
Manchester United inatajwa kuwa mlengwa mkuu wa usajili huo ambapo Luis van Gaal anatarajiwa kuongoza mbio za vilabu vya Ligi Kuu katika kuwania saini ya beki huyo wa Kibrazil.
Miranda mwenye umri wa miaka 30, amekuwa nguzo ya Atletico Madrid tangu ilipomsajili Januari 2011, lakini sasa inaonekana wazi kuwa klabu hiyo haina ubavu wa kuendelea kuwa na mchezaji huyo.

ABOOD ATOA WIKI MBILI MTENDAJI WA KATA KURUDISHA FEDHA ZA WANANCHI

January 01, 2015

 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiongea Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani ya Muda wa Wiki Mbili lasivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli Hiyo katiaka ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwajili ya Kusikiliza Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha ia Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2
 Wakazi wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame Kaialiyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za wakulima.

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katibu wa CCM Kata ya Luhungo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akisikiliza kwa makini Kero Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugala Kulia.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akipokea Taarifa za Maendeleo kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Kivuko Kinachounganisaha Mtaa wa Majengo na Mshikamano Eneo la Lukobe Kata Ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wakati wa Mfululizo wa Ziara zake ya Kutembelea Kata Zinazounda Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Mbunge aliahidi Kujenga Kivuko Hicho mara baad ya Kutembelea Eneo Hilo na Ndipo wakati wa Eneo Hilo walipomwomba Mbunge wao Kuwatatulia Kero ya eneo hilo muhimu inayowaunganisha wakazi wa Mitaa hiyo
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Ujenzi wa Kivuko hicho ambapo Mpaka ujenzi utakapokamilika Utagarimu jumla ya Shilingi Million 6.

HERI YA MWAKA MPYA 2015...SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA RAIS KIKWETE

January 01, 2015


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa katika Salamu zake za Mwaka mpya wa 2015 kwa Watanzania.
Elimu

Jambo jipya sana na la kihistoria katika Sera mpya ya Elimu ni dhamira ya Serikali ya kuondoa ada katika elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016. Mpaka sasa hatuna ada kwenye shule za msingi, sasa wakati umefika kufanya hivyo pia kwa elimu ya sekondari.

Ujenzi wa Maabara


Ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia katika shule za sekondari za Kata 3,463 umekwenda vizuri kiasi. Kwa idadi hiyo ya shule inatakiwa zijengwe maabara 10,389 ilipofika Novemba, 2014. Hadi kufikia Desemba 29, 2014, maabara 4,207 sawa na asilimia 40.5 zilikuwa zimekamilika, maabara 5,688 sawa na asilimia 54.8 zilikuwa katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji, na maabara 494 sawa na asilimia 4. zilikuwa katika hatua za awali za ujenzi.
Umeme


Hivi sasa wananchi milioni 17.3 nchi nzima sawa asilimia 36 wamefikiwa na huduma ya umeme ikilinganishwa na watu milioni 8.1 sawa na asilimia 18.4 waliokuwa wamefikiwa na huduma hiyo mwaka 2012. Mwaka 2015 tunatarajia watu milioni 18.2 sawa na asilimia 38 watafikiwa na umeme.
Chakula


Mwaka 2014 ulikuwa mzuri sana kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini. Uzalishaji ulikuwa tani milioni 16.02 ukilinganisha na uzalishaji wa tani milioni 14.38 mwaka wa jana 2013. Hili ni ongezeko la tani milioni 1.64. Kwa mujibu wa mahitaji yetu ya chakula nchini kuna ziada ya tani milioni 3.25.
Mfumuko wa Bei


Mfumuko wa bei uliendelea kushuka na kufikia asilimia 5.8 Novemba, 2014 ukilinganisha na Januari 2014 ulipokuwa asilimia 6.0. Ni matumaini yangu kuwa mfumuko wa bei utaendelea kushuka na kufikia asilimia 5 ifikapo Juni, 2015.
Ujangili


Kwa ujumla kasi ya ujangili imeendelea kupungua. Katika mwaka 2014 ndovu 114 waliuawa ikilinganishwa na ndovu 219 waliouawa mwaka 2013 au ndovu 473 mwaka 2012. Aidha, majangili 1,354 wamekamatwa na pembe za ndovu 542 na silaha mbalimbali 184 nazo zilikamatwa.

Dawa za Kulevya


Mwaka huu watuhumiwa 935 wakiwemo vigogo wa biashara hii haramu duniani wamekamatwa. Jumla ya kesi 19 zimefunguliwa Mahakamani. Aidha, kiasi cha kilo 400 za heroine, kilo 45 za cocaine na kilo 81,318 za bangi zimekamatwa.
Mapato ya Serikali


Makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwezi, kati ya Julai hadi Novemba, 2014 yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 3,555.5 kipindi kama hicho mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 3,924.1 mwaka huu. Hata hivyo, makusanyo hayo yalikuwa asilimia 90 ya lengo tulilojiwekea la kukusanya shilingi bilioni 4,459.7.

SIKU YA PILI ILIVYOKUWA KWA MABALOZI WAKATI WAKIPANDA MLIMA KILIMANJARO.

January 01, 2015


Majira ya saa moja asubuhi katika kituo cha Mandara ikiwa ni siku ya pili ya safari ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro maandalizi ya muendelezo wa safari hiyo yanaanza.
Balozi wa Tanzania katika falme za nchi za kiarabu,Mbarouk N. Mbarouk akiongoza msafara wa Mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
Sfarai inaendelea.
Balozi Adadi Rajab anayeiakilisha Tanzania nchini  Zimbabwe na Mauritius akitafakari safari ya kuelekea kituo cha Horombo.
Mabalozi Patrick Tsere (Malawi) na Balozi Batilda Burian wakivuta pumzi kwanza kabla ya kuendelea na safari.
Balozi Grace Mujuma (Zambia) akiongozana na Balozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Balozi Charles Sanga wakienda na mwendo wa Mdogo mdogo.
Muongoza watalii mkuu msaidizi wa kampuni ya Zara Tour ,Theofiri(mwenye miwani) akiwaongoza mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
Mabalozi ,Waandishi pamoja na waongoza watalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea kwa umbali mrefu kueleka Horombo.
Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikaendelea kwa pamoja bila ya kuacahana.
Mahala pengine Mabalozi walilazimika kutumia fimbo maalumu kupanda maeneo ambayo yalkuwa na vipando vikali.
Mabalozi ,Shamim Nyanduga( Msumbiji) na Radhia Msuya (Afrika Kusini) walilazimika kupaka mafuta mgando katika nyuso zao ili kuzuia kubabuka na jua.
Balozo Tsere akipatiwa huduma ya kwanza ya kuchuwa mguu wake ili aweze kuendelea na safari ,kulia ni balozi Batilida Buriani.
Balozi Mwinyi aliamua kupoza koo huku akitafakari safari hiyo.
Kila mmoja aliamua kupumzika ili kuvuta nguvu ya kumalizia kipande kilichokuwa kimebakia.
Maeneo mengine mabalozi walifanya mazungumzo na wageni waliokuwa wakishuka toka kileleni.
Hatimaye Mabalozi wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula .
Wale waliokuwa wamepungukiwa maji waliongezewa kwa kuwa ndio dawa pekee ili kufanikisha kuwez kupanda Mlima Kilimanjaro.
Safari ikaendelea.
Hataimaye kituo cha Horombo kikaonekana kwa mbali na mabalozi walitembea na kupumzika hapo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini aliyekuwa katika msafara wa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mwakyembe atimua watumishi 6, TRL

Mwakyembe atimua watumishi 6, TRL

January 01, 2015
Waziri wa Uchukuzi nchini Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi wafanyakazi 6 wa Shirika la Reli nchini (TRL) kwa makosa ya wizi wa fedha na ameamuru wakamatwe kuanzia leo na wafunguliwe mashtaka mara moja.

Akiongea Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo yake na wafanyakazi wa TRL waliopeleka malalamiko ofisini kwake kuhusiana na uonevu wanaofanyiwa, Dkt. Mwakyembe amesema waliofukuzwa kazi ni pamoja na kiongozi anayehusika na kukata tiketi pamoja na wafanyakazi wa kawaida watano kwa makosa ya kukatisha tiketi feki.
Dkt. Mwakyembe amesema uchunguzi bado unaendelea kubaini wafanyakzi wengine wanaokiuka sheria na taratibu za kazi zinazopelekea kudhoofisha ufanisi wa shirika hilo linalotoa huduma ya usafiri wa reli ya Kati nchini.
Lakini kufuatia uamuzi huo wa waziri wa uchukuzi, Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa Reli Tanzania TRAU Erasto John Kiwele amesema kwamba hawajaridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa na waziri kwa sababu watuhumiwa wakuu wameachwa na kukandamizwa wadogo.
Wakati huo huo, Wizara ya Uchukuzi imetolea ufafanuzi tukio la kuvunja kwa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kulikosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha juzi katika jiji hilo.
Akitolea ufafanuzi suala hilo katika mahojiano maalum na Hotmix, waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe amekiri kutokea kwa hali hiyo na kusema kuwa serikali ina mpango wa kulibomoa jengo, na tayari ujenzi wa jengo jipya litakalokuwa likitumika kwa kazi hiyo umekamilika.
Akizungumzia tatizo la usafiri wa majini kati ya miji ya Mwanza na Bukoba baada ya kuisimamisha meli ya MV Victoria, Dkt Mwakyembe amesema Meli ya MV Serengeti yenye uwezo wa kubeba abiria 500 na mizigo tani 385 itachukua nafasi ya MV Victoria iliyokuwa ikibeba abiria 1200, ambayo imesimamishwa kwa ajili ya matengenezo.