DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA

August 24, 2017
 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
 Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga
 mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji

TAASISI YA ESRF NA GRADE WAINGIZA TEKNOLOJIA MPYA YA KUPANGA MAKAZI KUPITIA SIMU

August 24, 2017
TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti lisilo la kiserikali (GRADE) lililopo nchi ya Lima, Peru zimetengeneza program ya simu ya mkononi inayoitwa LOTIZER inayoweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Teknolojia hiyo mpya ya kupanga makazi ilioneshwa kwa viongozi, wananchi na watendaji wa mkoa wa Dar es salaam katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
Programu  hiyo iliyotengenezwa baada ya kufanywa kwa utafiti unaohusu "Upangaji wa Hiari wa Makazi katika Jamii" katika Mkoa wa Dar es Salaam, imefunzwa pia kwa madalali.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida kwenye warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mradi huo wenye lengo la kuimarisha michakato bora zaidi ya kupanga miji katika nchi zinazoendelea, hususani kwenye makazi yasiyo rasmi inaweza kupakuliwa kutoka kwenye tovuti  ya “www.grade.edu.pe/lotizer na kuwekwa kwenye simu ya mkononi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho Profesa  Fortunata Makene ambaye ni mmoja wa watafiti  waliozungumza na wananchi wa maeneo ya holela ya jijini Dar es salaam kama Kivule, Tandika, Tandale na Keko maghurumbasi, Program hii inaweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Profesa Makene alisema kwamba  walifanya utafiti kuelewa sababu za kijamii, kiuchumi na kitamaduni zinazosababisha ukaaji wa watu katika makazi yasiyo rasmi maeneo ya mijini.
Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole akiitambulisha na kuelekeza jinsi ya kupakua LOTIZER programu ya simu bure kabisa ambayo ni teknolojia mpya ya kupanga makazi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AFUNGA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

August 24, 2017
Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano lilodumu kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi wao nchini Tanzania.

Akihutubia mamia ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.

Alisema kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.

Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.

Alisema kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya utambuzi wao.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa ushirikiano huo wa Diaspora kupitia makongamano yote yaliyopita umeimarisha zaidi mahusiano chanya bila kujali dini wala kabila jambo ambalo limeongeza utu, umoja na mshikamano.

Mhe alozi Seif alisema kuwa Diaspora wanatakiwa kuheshimu sheria, taratibu na taratibu za nchi wanazoishi ili kue delea kuipatia sifa chanya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Naomba nikukumbusheni nyote mliohudhuria hapa hii leo kutamnbua kuwa mchumia juani hulia kivulini nanyi kivulini kwenu ni hapa nyumbani hivyo tumie fursa ya uwekezaji vizuri huku mkikumbuka kuwa mkataa kwao ni mtumwa zaidi endelezeni umoja na mshikamano kwani inafahamika kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.” Alisema Balozi Seif Ally Idd

Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.

Kongamano kama hilo linaakisi makongamano matatu ya utangulizi yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam huku kongamano la mwaka 2016 na mwaka huu 2017 yakifanyika visiwani Zanzibar huku likiwa limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Kongamano la watanzania waishio ughaibuni kwa mwaka 2017 limedhaminiwa na PBZ Bank, ZSSF, Idara ya Uhamiaji, Sea Cliff Hotel, CRDB Bank, Mult Colour, Equity Bank, Zanzibar Cable Television, ZBS, Watumishi Housing Cooparation na Petro.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa  kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara. (Picha zote na Mathias Canal)
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa  kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa  kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
TAZAMA PICHA ZAIDI

ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI

August 24, 2017
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .

Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata  maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho

Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia Bella Bird.
Filbert Rweyemamu,Arusha
Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni  ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu.
Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.
Alisema kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.
Bella alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana vyema na serikali .
Makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi  Tanzania (TPSF), Godfrey  Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

August 24, 2017
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini. 
PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO/>BOFYA HAPA -- Best regards Bashir Nkoromo Blogger & Photojournalist UHURU PUBLICATIONS LTD Dar es Salaam, TANZANIA Cell: +255 712 498008, +255 789 498008, BLOG: theNkoromo Blog Email: nkoromo@gmail.com

JANUARY MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

August 24, 2017
Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.
Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.
Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila, Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibarBaadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo

Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi 113 wa Promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi

August 24, 2017


Meneja  Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Ally Mwaisemba,  mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.


Meneja  Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Ally Mwaisemba,  mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA AWAMU YA PILI YA MRADI WA KUWALINDA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI

SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA AWAMU YA PILI YA MRADI WA KUWALINDA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI

August 24, 2017
Shirika la Kutetea Haki na Maslahi ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA lenye makazi yake Jijini Mwanza, limetambulisha awamu ya pili ya mradi wa kuzuia ukatili kwa watoto hao na kulinda haki na maslahi yao. Kabla ya kutambulishwa kwa mradi huo, shirika hilo lilitoa mrejesho wa mradi wa aina hiyo awamu ya kwanza uliokuwa ukiendeshwa kwenye Kata nne Jijini Mwanza, uliodumu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana hadi mwezi Aprili mwaka huu. Akiwasilisha mrejesho huo hii leo Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa shirika la WOTESAWA, Angel Benadicto amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ilifanikiwa vyema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa awamu ya pili ya mradi wa aina hiyo kutoka kwa wafadhiri ambao ni shirika la The Foundation For Civil Society. “Wao wanasema ni muda mwafaka wa kutokomeza ukatili kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo sasa tutakuwa kwenye Kata sita Jijini Mwanza”. Amesema Benedicto. Amesema kwa awamu ya kwanza, watoto wafanyakazi wa nyumbani 154 pamoja na waajiri 199 walifikiwa na kujengewa uelewa ili kuzuia ukatili dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo mafunzo kama hayo pia yaliwafikia wadau mbalimbali kama polisi kupitia dawati la jinsia, vyombo vya habari, watendaji wa serikali wakiwemo madiwani na wenyevyiti wa mitaa. Aidha elimu ya aina hiyo imesambaa zaidi katika jamii kupitia vipindi 15 vilivyorushwa redioni, vipindi saba vilivyorushwa kwenye luninga pamoja na machapicho mbalimbali ambapo wajiri na waajiriwa wao 25 walisaini mikataba ya ajira. Mratibu wa Shirika la Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Nyumbani (Wotesawa) Elisha Daudi, amesema matarajio ya mradi huo ni kuhakikisha ukatili dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani unatokomezwa katika jamii na pia kutoa fursa kwa watoto kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu. Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, Angel Benedicto, akitoa mrejesho wa awamu ya kwanza ya mradi wa kulinda na kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani uliokuwa ukiendeshwa kwenye Kata nne Jijini Mwanza kwa muda wa miezi sita. Awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa vyema na hivyo kufungua milango ya mwendelezo wa mradi wa awamu ya pili utakaodumu kwa miaka miwili kwenye Kata sita Jijini Mwanza. Mmoja wa washiriki akitoa pongezi kwa Shirika la WOTESAWA kwa kazi nzuri ya kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na pia kuuliza maswali na kuchangia mada kwenye semina hiyo.

SBL yawatunuku magari mawili yenye thamani ya 100m/= wasambazaji wake wa juu jijini Mwanza

August 24, 2017



Meneja Masoko Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya Serengeti Patrick Kisaka(kushoto) akimkabidhi funguo za gari mshindi wa usambazaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyi Mkurugenzi wa kampuni ya Gramba Stanslaus Mmbaga, wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vinywaji ya Victoria General Supply Jonathan Karaze akipokea ufunguo wa gari kutoka kwa Meneja Masoko Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya Serengeti Patrick Kisaka(kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana baada ya kushinda usambazaji bora.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vinywaji ya Victoria General Supply Jonathan Karaze, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi.


Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji vinywaji  Gramba Stanslaus Mmbaga, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi.









Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL 
PROF. BRIAN VAN ARKADIE ATOA SOMO MAPINDUZI YA KILIMO MHADHARA WA ESRF

PROF. BRIAN VAN ARKADIE ATOA SOMO MAPINDUZI YA KILIMO MHADHARA WA ESRF

August 24, 2017
TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara. Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo. Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Aidha alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya kukikwamua. Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya wanakijiji. Alisema kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima. Profesa Brian Van Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa. Alisema katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT. Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi. Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu. Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.

MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA SHILINGI MILIONI 80 JIJINI DAR ES SALAAM LEO

August 24, 2017
 Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.