SMZ YAIPONGEZA UN KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

SMZ YAIPONGEZA UN KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

October 20, 2015

IMG_9022
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.
Waziri Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi.
Alisema kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja huo na serikali.
IMG_9075
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
“ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri miradi mnayotuunga mkono.

Pia tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.

Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

Bw. Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya nchi.

Alifafanua kuwa katika miradi mbali mbali iliyotekelezwa Zanzibar kupitia mashirika ya Umoja huo hasa UNDP, UN WOMEN na UNESCO miradi hiyo imeweza kufanikiwa zaidi ya asilimia 80 jambo ambalo ni faraja kwa umoja huo.
IMG_9170
Kila mtu alikuwa na tabasamu la furaha....Happy Birthday #UN70
Alieleza kuwa kupitia dhana ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2016 umoja huo umejipanga kusaidia masuala mbali mbali ya haki za binadamu, utawala bora, uwazi na uwajibikaji, afya na vipaumbele vya kisera kwa serikali ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa ni nchi ya kupigiwa mfano kimaendeleo.

“ Tuna kila sababu za kuishukru serikali ushiriki wake katika miradi yetu kwani bila wao kutuunga mkono vizuri leo hii tusingweza kuwepo hapa kusherekea mafanikio tuliyopata ndani ya miaka 70 ya UN hivyo nasi tunaahidi kuenzi mahusiano haya kwa lengo la kujenga jamii bora.”, alisema Bw.Rodriguez.

Aidha aliishauri serikali kuhakikisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia vigezo vya uwazi, uhuru na haki ili kila chama kilichoshiriki katika mchakato huo kinapata haki yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
IMG_9044
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga.

“ Tunawatakieni uchaguzi mwema na wenye mafanikio bila ya kuwepo dalili za uvunjaji wa haki za binadamu ama kiashiria chochote cha vurugu ili muendelee kulinda heshima na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).” alisisitiza Bw. Rodriguez.

Sherehe hizo za kutimiza miaka 70 za UN zilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena Mjini Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa umoja huo wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Zanzibar na kutoa Tuzo na vyeti vya kumbu kumbu kwa taasisi na shule zilizoshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya umoja huo.
IMG_9494
Ofisa anayeshughulikia masuala ya ushirikiano wa WHO Zanzibar, Dkt. Ghirmay Andemichael (kushoto) akibadilishana kadi na mmoja wa wageni waalikwa (ambaye jina lake halikuweza kupatikana kirahisi).
IMG_9166
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kushoto) akifurahi jambo na Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman.
IMG_9314
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakizindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
IMG_9317
IMG_9327
Fataki zikipamba uzinduzi huo, sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_9368
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja huo.
IMG_9352
Baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Dar na Zanzibar wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati akitoa salamu za UN katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9397
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9407
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifanya 'Toast' katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9408
IMG_9418
'Toast' hiyo iliambatana na milipuko ya Fataki kusherehesha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake. 

Rais Kikwete leo akabidhi jeshi la polisi magari 399 mapya kati ya 777 yaliyoagizwa

October 20, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu alipowasili Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 tayari kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi. 
 Wimbo wa Taifa katika sherehe za kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Wimbo wa Taifa katika sherehe za kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Wimbo wa Taifa katika sherehe za kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Sehemu ya magari hayo
 Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisoma risala kwa Rais Kikwete katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
  Sehemu ya maafisa waandamizi wa Polisi katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi
  Maafisa wa Polisi katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi
 Maafisa wa Polisi katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe akimkaribisha Rais Kikwete kuhutubia  katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akihutubia katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akiendelea kuhutubia katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikata utepe katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akimkabidhi IGP Mangu funguo za magari hayo  katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akishukuriwa na IGP Mangu baada ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya magari 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na maafisa na wakufunzi baada ya kukabidhi sehemu ya  magari 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakufunzi baada ya kukabidhi sehemu ya magari  777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya madereva na wakufunzi baada ya kukabidhi sehemu ya magari  777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhi sehemu ya  magari 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Picha ya kumbukumbu na makandarasi walioleta magari hayo
 Naibu IGP akitoa salamu za shukurani kwa Rais Kikwete 
 Rais Kikwete akiongea na IGP Mstaafu Dkt. Saidi Mwema baada ya sherehe hiyo
Sehemu ya magari 399 kati ya 777 yaliyoagizwa. 
PICHA NA IKULU
FUTURE POLICY AWARD 2015: GOLD GOES TO ZANZIBAR’S CHILDREN’S ACT

FUTURE POLICY AWARD 2015: GOLD GOES TO ZANZIBAR’S CHILDREN’S ACT

October 20, 2015
22332492835_c6540fb80e_z
Zanzibar’s child rights law is the winner of the 2015 Future Policy Award on securing children’s rights, beating 29 other nominated policies to the prize. The Award will be presented at a ceremony in Geneva today by the World Future Council, the Inter-Parliamentary Union (IPU) and UNICEF during the 133rd IPU Assembly.
The “Children’s Act” is an outstanding piece of legislation. It earned the 2015 Award for its balanced coverage of child abuse and violence against children and for its promotion of child rights – two important topics for children worldwide. Since the enactment of the law Zanzibar has seen favourable and significant shift of social attitudes towards children.
The Act lays the foundation for the establishment of a comprehensive national child protection system to deal with cases of children in need of care and protection and already notable achievements have been recorded in its operationalization. These include the establishment of district child protection committees, the establishment of Children’s Courts, the designation of Police Gender and Children’s Desks in every Police Station in Zanzibar and the roll out of training to social welfare and frontline justice professionals. An exciting feature of this legislation was the child consultation process which provides young people with an understanding of the law and their rights. It gave children a voice in the development of the legislation and resulted in the establishment of over 200 Children’s Councils in the Isles.
21711616543_42e3d29f57_z
On learning about the Gold prize, Asha Abdullah, Principal Secretary of the Zanzibar Ministry of Empowerment, Social, Welfare, Youth, Women and Children said: “This is a great honour. The Award will not only raise global awareness of our model of child rights legislation, but also enhance our commitment to its implementation in Zanzibar.”
UNICEF in Tanzania played a key role in providing the Government of Zanzibar with technical and financial support in the development of the Act and continues to provide assistance, with support from the European Union, in working towards bringing the legislation from paper to practice. Dr. Jama Gulaid, UNICEF Tanzania Country Representative congratulated the Government of Zanzibar on receiving the Future Policy Award 2015 and noted: ‘Hongera Sana, Zanzibar! UNICEF commends the Government and people of Zanzibar for the broad consultation on the Act which heightened public awareness of children’s rights. Child protection is drawing attention from decision makers, media and communities in Zanzibar’.
Birgithe Lund-Henriksen, Chief of Child Protection for UNICEF in Tanzania, added: ‘We are delighted to continue to support the roll out of the Children’s Act 2011 in order to make a meaningful impact on the lives of children in Zanzibar. We are particularly encouraged by the steps that already have already been taken towards implementation and the real ownership the frontline child protection professionals have demonstrated over the new legislation in working to protect children in Zanzibar’.
22145738849_4866c4b32b_z
Jakob von Uexkull, Founder and Chair of the World Future Council, said: “This prize celebrates policies that help us to do the right thing by creating the right rules. Children are among the most vulnerable group facing a host of the world’s emerging challenges. We need more laws that support a just world and protect the rights of future generations.”
IPU Secretary General Martin Chungong said: Parliaments can lead the response against child abuse and violence by ensuring international commitments on children’s rights are adhered to nationally through laws that are effectively implemented and monitored. The winning policies can only inspire parliaments and parliamentarians everywhere on concrete action to take. ”
UNICEF Executive Director Anthony Lake commended the recognition bestowed by the awards: “Children’s rights are brought to life not through pronouncements, but through practical action. Parliamentarians are among UNICEF’s most important partners in driving that action and the results it can achieve in children’s lives. We applaud the World Future Council for spurring more parliamentarians to leverage their powers on behalf of the world’s most disadvantaged and vulnerable children.”
The Future Policy Award is the only award which honours policies rather than people on an international level. The World Future Council will now work to globally raise awareness of the winning model policies and assist policy-makers to develop and implement similar initiatives.