TAMASHA LA KUSAKA VIPAJI VYA UTANGAZAJI LA "HHC ALIVE TALENT SEARCH" JIJINI MWANZA LAIBUA VIPAJI VIPYA

May 22, 2016
Kushoto ni Meneja wa kituo cha Radio cha 91.9 HHC ALIVE cha Jijini Mwanza, Maganga James Gwensaga, akizungumza katika tamasha la kusaka Vipaji vya Utangazaji (HHC ALIVE TALENT SEARCH 2016) lilizofanyika katika Kanisa la HHC Cathedral, Ilemela Mkoani Mwanza.

Watangazaji chipukizi, Hellen Jerome, Ibrahim Mgaya pamoja na Deophinius Salvatory, wameibuka kidedea katika tamasha la kusaka Vipaji vya Utangazaji lililoandaliwa na kituo cha redio cha 91.9 HHC Alive cha Jijini Mwanza.
Picha zaidi BONYEZA HAPA

KAMPUNI YA MABIBO BEER YAENDELEA KUDHAMINI TAMASHA LA WAZI LA BURE LA MICHEZO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM

May 22, 2016
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Abdallah Ngoma akizungumza na wanahabari kuhusu bia ya windhoek na tamasha hilo kwa ujumla.
Mdau wa Windhoek, Kasano Jonathan akizungumzia ubora wa bia ya Windhoek.
Mkufunzi Mkuu wa Kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es Salaam Sas Sangandele akizungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi.
Wadau wakipata chakula katika tamasha hilo.
Mazoezi yakiendelea.
Hapa sebene na mazoezi kwa kwenda mbele.
Hapa ni mazoezi tu kwa kusonga mbele.
Hapa ni mpango mzima wa midundo ya kamatia chini.
Wadau wa windhoek wakiwa kwenye tamasha hilo.
Hapa ni furaha tu katika tamasha hilo.
Mwonekano wa kivingine wa bia ya Windhoek katika chupa mpya.

Mazoezi yakiwa yamepamba moto.

Na Dotto Mwaibale

WADAU wa mchezo zaidi 150 wameendelea kunufaika na mazoezi ya bure ya viungo kutoka kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits  Ltd.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika tamasha la michezo ya wazi kupitia kituo hicho, Mkufunzi Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema mazoezi ni muhimu sana kwa kila mtu kwani yanajenga afya na kupunguza magonjwa mwilini.

Alisema kituo hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo kupitia kinywaji cha Windhoek wamekuwa wakifanya mazoezi ya wazi kwa wananchi wote bure katika viwanja vya Leaders katika wakati unaopangwa.

Alitaja michezo inayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, kufukuza kuku na mingineo mingi ambayo inafanyika katika jimu mbalimbali.

Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Abdallah Ngoma alisema wanajisikia fahari pale wanaoona wadau wa bia ya windhoek na wananchi kwa ujumla wanaimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi na baada ya mazoezi wanaburudika na bia ya windhoek iliyopo sokoni kwa muonekano mpya wa chupa yake huku kinywaji kikiwa kilekile.

Alisema kampuni hiyo imedhamini tamasha hilo  kupitia kinywaji hicho baada ya kuona kunamuitikio mkubwa wa wananchi kwa kufanyamazoezi jambo linalowasaidia wawe na afya bora na kupoza koo kwa bia hiyo ambayo inakubalika na wengi nchini kutokana na ubora wake.

JUMA ABDUL MCHEZAJI BORA APRILI VPL

JUMA ABDUL MCHEZAJI BORA APRILI VPL

May 22, 2016
Beki wa kulia wa timu ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma Abdul ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya kura zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye pia anakipiga Young Africans na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani.

Katika rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) iliyoketi Jumamosi Iliyopita, imeonesha kwamba Abdul alicheza mechi zote tano za Ligi Kuu kwa mwezi Aprili ambapo pia aliifungia timu yake bao katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16.


Rekodi hizo pia zinaonyesha kwamba beki huyo hakuonyeshwa kadi hata moja katika michezo hiyo mitano sambamba na kutoa mchango mkubwa katika michezo aliyoshiriki kwa mwezi Aprili, 2016. Abdul atazawadiwa fedha Sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya mahiri ya simu za mkononi ya Vodacom.

Uwezo aliouonyesha Abdul ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ kumjumuisha katika kikosi chake kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya kadhalika Mapharao wa Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.

Wachezaji bora wa miezi minne iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Young Africans (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016), Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016) na Shiza Ramadhani Kichuya wa Mtibwa Sugar
RAIS FIFA GIANNI INFANTINO AIPONGEZA YOUNG AFRICANS

RAIS FIFA GIANNI INFANTINO AIPONGEZA YOUNG AFRICANS

May 22, 2016
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.
Young Africans imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.


Katika salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa wa Young Africans kwamba umetokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.

“Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa. Taji la Young Africans ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Young Africans.

Amesema pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Young Africans.

“Kwa niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Young Africans na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.

Tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya fedha Sh 81,345,723.

TANGAZO MUHIMU LA BIASHARA JENGO LA MAJESTIC

May 22, 2016


JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) MKOA WA TANGA INAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI WOTE KUWA WANAKODISHA JENGO LAO LILILOPO ENEO LA MAJESTIC KARIBU NA SHULE YA SEKONDARI OLD TANGA JIJINI TANGA.
JENGO HILO NI NZURI LINAFAA KWA BIASHARA MBALIM BALI KWA AJILI YA KUPATA WATEJA KUTOKANA NA KUWEPO KATIKATI YA MJI.
KWA MAWASILIANO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA +225714113900.
NYOTA MNAKARIBISHWA !

NHIF TANGA YAWAPIGA MSASA WARATIBU WA CHIF MKOA WA TANGA.

May 22, 2016
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akisisitiza jambo wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo

Mratibu wa GIZ Mkoa wa Tanga,Apolinary Primus Rutakuburwa ambao wanasapoti huduma za afya na matibabu kulia akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akifuatilia kwa umakini

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga,Miraji Msile akiwaelekeza jambo waratibu wa CHF wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo

Maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Dr.Sana kulia wakifuatilia semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Mratibu wa CHF Mkoa wa Tanga,Apolinary Primus Rutakuburwa kulia akisisitiza  jambo kwa waratibu wa CHF mkoa wa Tangawakati wa semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo.
 
Waratibu wa CHF Mkoa wa Tanga wakinakili maelezo kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo waratibu wa mkoa mzima